Tujikumbushe ya Adam Malima na ulimbukeni wa madaraka

Malima akamdanganye mtoto wa chekechea kuwa hakuwa na changudoa siku alipoibiwa

chumba cha 400,000 , hotel ya hadhi hii ina vibakaa??? kibaka asingeiacha bastola hata iweje...
watu wamenunuliwa , watu wamebambikiziwa kesi
 
Mi nilishasema hapa kuwa, lazima aliondoka na kahaba. Kama sio Kahumba night club basi Makuti bar.
 
Ha ha haaaa... Hivi hao walugaluga wameachiwa kweli??? Hii nchi kuna siku tutadai uhuru toka kwa hawa wakoloni weusi kwa jinsi mambo yanavyoenda na unyanyasaji kukithiri plus dhuluma na kubambikizia kesi wanyonge.

Wanaogopa kumkamata huyo dada kwa vile naye atamwaga mboga kuharibu ndoa na kazi ya Malima
 
Malima akamdanganye mtoto wa chekechea kuwa hakuwa na changudoa siku alipoibiwa

chumba cha 400,000 , hotel ya hadhi hii ina vibakaa??? kibaka asingeiacha bastola hata iweje...
watu wamenunuliwa , watu wamebambikiziwa kesi

Hao walalahoi wameshavuta mpango kumsetri Mh. Naibu waziri Adam Malima.

Bongo jinsi maisha yalivyokuwa magumu kuna watu wanajitolea kufungwa gerezani kwaajili ya watu wengine. Wewe kama umefungwa una pesa zako wasela wako kibao wa kutumikia kifungo badala yako, wewe una sepa nchi za ng'ambo hadi kifungo chako kitakapokwisha ndiyo unatia nanga tena Tanzania as if umetoka kifungoni. CCM imeifanya nchi hii kama Banana republic
 
Haya sasa mambo yaanza kuanikwa hadharani ili naye mke wa Malima aone jinsi anavyofuga kumbakumba hapo nyumbani kwake asiyetishwa na maradhi hatari ya siku hizi.

JF Morogoro tupeni taarifa zaidi juu ya afya ya hao walalahoi wenzetu walioswekwa rumande ili kumkinga Malima na aibu ya Morogoro.
 
eti jambazi likutane uso kwa uso na smg halafu liiache?!?



kwa kweli hii nchi ni ya ajabu sana.. mtu kaibiwa katika starehe zake za ufuska, haya leo wanaenda kuwa kamata washikaji hao na dada yetu huyo sijui kwa lipi.. kweli jambazi gani akuvamia aache kuchukua silaha kweli?? Aisee inaniuma sana hii serikali imejaa udharimu wa hali ya juu yaleyale ya babu seya.. halafu wanajifanya ooh ni nchi ya sheria.. wewe waziri kama ulienda kihali morogoro kwanini hukutembea na walinzi wako? masilaha yotee hayo ni ya nini.. huyo alienda kwenye dili zake feki na ndio maan ahakuwa na walinzi.. Pole vijan wenzagu dunia ni hamna haki..haki iko kwa Mungu tu.. na inchi hii sheria zipo na zinatumika kuwaangamiza wanyonge, yatima na maskini tu.. ila inapokuja kwa kizito fulani hakuna sheria hapo. Poleni Muombeni Mungu afanye maajabu other wise mtaenda kunyea debe tu Mkono wamara au moro town pale, au kule mbigili. Mungu awape nguvu
 
Unajua nilishawahi kumwambia nikiwa songea siku moja malaya ni malaya tu adam usipobadilika hiko cheo kitakutokea puani na hata kilichofanywa si o yeye ni game ya wabaya wake ambao wako nyuma yake
 
Sijui ni mimi peke yangu au kuna mtu mwingine hapa jamvini anayehisi kuwa huyo mama aliyeko kwenye landrover hausiki! Kama Malima anasoma huu uzi au kama kuna mtu wake wa karibu basi nashauri akae chini na ajiridhishe kweli kama huyo mama anahusika. Machozi ya mtu hayapotei bure, na haki ya mtu haidhulumiwi.

Ni hisia zangu pengine Malima ndiye mwenye kujua ukweli ni upi lakini huyo mama kweli kamuibia Mheshimiwa laptop tatu? na pete?
 
Sijui ni mimi peke yangu au kuna mtu mwingine hapa jamvini anayehisi kuwa huyo mama aliyeko kwenye landrover hausiki! Kama Malima anasoma huu uzi au kama kuna mtu wake wa karibu basi nashauri akae chini na ajiridhishe kweli kama huyo mama anahusika. Machozi ya mtu hayapotei bure, na haki ya mtu haidhulumiwi.

Ni hisia zangu pengine Malima ndiye mwenye kujua ukweli ni upi lakini huyo mama kweli kamuibia Mheshimiwa laptop tatu? na pete?

Machozi ya huyo mama yatamuandama hadi kaburini na vitu kuu vyake. Chezeya natural justice !
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hebu ngoja kidogo mkuu,

Hapo kwenye wino mwekundu uliokolea namba moja; inamaana hili la ADAM MALIMA DAM DAM NA mabinti wala si jambo lililotokea tu kibahati mbaya kule Morogoro bali ni jambo la siku nyingi tu linalojulikana ka kilema chake kiasi cha wewe kuwahi kumhofia huenda ikamvurugia kazi?

Je, hapo namba mbi mbona mkuu unaleta habari nusu nusu hivi; wabaya wa Malima wanaomfanya atamani kusafiri na kifaru cha jeshi letu sehemu zote kiasi kwamba hata SMG na Pistol zote zaonekana kwake zana dhaifu ni akina nani hao na ni juu ya mstari kama huo huo ulioelezea kwa ufasaha hapo juu au ni juu ya kuzidiana ujanja kwenye mgao wa kitenesi cha ufisadi wa mikataba mbali mbali ya rasilmali zetu?


Unajua ((1) nilishawahi kumwambia nikiwa songea siku moja malaya ni malaya tu adam usipobadilika hiko cheo kitakutokea puani na hata kilichofanywa si o yeye (2) ni game ya wabaya wake ambao wako nyuma yake
 
Wana JF, mnakumbuka ile mechi ya Malima vs Mengi? Kugombea kombe la nani apewe 'air time' kubwa kati ya JK au Mengi. Ukilaza wa Malima Kithembe niliuona kuanzia hapo.
 
Nimeipenda sana hii anaysis. Laptop tatu ni ulimbukeni tu, watu wanafanya kazi za kutosha kabisa na mini laptop moja. Blackberry ya hiyo bei, sijawahi sikia, ina nini?
Dola za Marekani, huzihitaji kwa safari ya Morogoro. Kuwa na SMG guest house ni kashfa ya kumfanya aondolewe huo uwaziri mara moja. Na hawa watu wanohusika na kutoa vibali vya mtu kumiliki silaha tunahitaji watueleze inakuwaje mtu anamiliki SMG.
Mwisho, siku niliyomsikia Malima akielezea alivyoibiwa nilitamani nijifiche kwa aibu, sikuamini huyo aliyekuwa anaongea ni waziri katika nji hii
 
Mzee Regnald Mengi,

kama mtoto wa Kigoma Malima aliyekuwa anajaribu kukuonyesha ubabe wa kuwa mwandani serikalini kwenye vyombo vyako vya habari ndiye huyu huyu aliyelewa madaraka na kuzunguka ovyo na midola za Kimarekani na kuweka pajani kwake silaha hatari za kivita na hafanywi lolote na serikali ya Kikwete mpaka sasa, mzee Mengi Watanzania leo hii tunakuomba radhi kwa ufedhuli wa huyu kijana wetu.

Tafadhali endelea na kazi kwenye vyombo vyako ila ukakatae chombo chochote kati ya vyombo hivo kutumika kiupendeleo kwa chama chochote kile. Mzee Mengi chonde pole sana na ulevi wa madaraka wa huyu Malima miaka ile. Si kipindi kirefu sana wataanza kuingia disko na SMG na mi-lapto 20 kidogo hawa.


Wana JF, mnakumbuka ile mechi ya Malima vs Mengi? Kugombea kombe la nani apewe 'air time' kubwa kati ya JK au Mengi. Ukilaza wa Malima Kithembe niliuona kuanzia hapo.
 
Tangu sasa nimeanza kujifunza kwamba hata sakata la 'air time' aliyoshupalia Malima yote ilikua ni kujipendekeza akapewe uwaziri ambao hivi sasa unaelekea kumpeleka kaburini baada ya utamu wake kuzidi sukari kule Morogoro.
 
Back
Top Bottom