Tujikumbushe wana Azania

Nipo bongo nakimbizana na life, we wapi? Lunya namkumbuka, mi nilikua na kina Dickson, Frank Lyatuu,RIP. Mussa Sechonge, Kaseja, na bounser wetu Salanga. Jeremiah sijui yuko wapi sasa. Man it was fun when i think of it now. Mwalimu Moland wa english na yule wa chemistry alikua kituko kweli. Bila kumsahau Mapimpi wa Siasa enzi hile alikua anavuta fegi class alafu hana habari.

Mzee kweli una memory nzuri umenikumbusha Mapimpi sina hamu jamaa alikuwa kachoka akiingia class ,class yote inanuka kachaso na yeye ndio anaikolezea na fegi sijuikama atakuwa hai sasa hivi.Ila kwa siasa na history alikuwa mzima.Mwalimu Moland sitamsahau siku moja kaniuliza kwa nini umechelewa shule ile nataka kumjibu tu master huyu katokea kwenye kile kikorido kati ya IV-E na IV-F Moland si akabadilisha kibao kanishtaki kwa master anasema jamaa kanigomea wacha mchaga anirukie nisingekuwa na mbio naona angeua:lol: .Mimi sasa hivi niko Netherlands mwanangu bado tunasaka mautaalam na kuumia na winta.
 
Mazee mnanikumbusha Azaboy kuna siku moja kulikuwa na mkutano wa madent na mateacher khs library na maabara,akasimama denti mmoja simkumbuki jina Mchwampaka aka mruhusu,jamaa akaanza tuna library nzuri sana LKN VITABU VIMEACHWA VIMELIWA MCHWA........MPAKA sasa kuisema ile mchwa mpaaka ilisikika kama Mchwampaka...madent hapo wote lete vitabu vyetu weeeeeee...hapo ndo ukawa mwisho wa mkutano lkn kesho yake MCHWAMPAKA alimtafuta yule dogo acha...AZABOY for real..
 
Nadhani alikuwa anaitwa Bob Leo ,ni mwana harakati wa kitu kama haki za binadamu alisoma sheria nadhani baadae.
Jamaa alikuwa kiongozi fulani ,yah mwaka ule waziri wetu wastarehe alijiua tetesi kwa penzi la binti jangwani ilishangaza maana hatukuwa ma lover kivile.
 
Paka Mweusi, wewe ni ndugu yake Paka Jimmy? Karibu ukumbini!

A kuu mie Paka Jimmy wala thimjui Paka Mweuthi mie nilidhaliwa peke yangu.Nashukuru kunikaribisha ingawa nimeshafika na nimepata marafiki na maadui mwendo mdundo kama nnaria vile
 
Mjomba wewe wa wapi lakini maana unarukia topic bila kuzielewa.Kule kwa wazanzibari umejidai kuchokoza umenikimbia sasa na huku tena na kwa taarifa tu huyu tunayemsema alikuwa mwalimu wetu na sio mwanafunzi kama unavyofikiri wewe na alikuwa havuti bangi elewa mjomba hapa watu unaoongea nao si kama unavyofikiria wale wa skuli ya kiembe samaki.Hapa ni vichwa makini toka Azania boys
Ona sasa unavopoteza!! wa pugu boys watasemaje!.. ?? BTW sirukii thread ni kawaida yangu kuchangia thread yoyote.
 
hahahaaaa wa zenji wanaita shule BANDA.
 
Mzee kweli una memory nzuri umenikumbusha Mapimpi sina hamu jamaa alikuwa kachoka akiingia class ,class yote inanuka kachaso na yeye ndio anaikolezea na fegi sijuikama atakuwa hai sasa hivi.Ila kwa siasa na history alikuwa mzima.Mwalimu Moland sitamsahau siku moja kaniuliza kwa nini umechelewa shule ile nataka kumjibu tu master huyu katokea kwenye kile kikorido kati ya IV-E na IV-F Moland si akabadilisha kibao kanishtaki kwa master anasema jamaa kanigomea wacha mchaga anirukie nisingekuwa na mbio naona angeua:lol: .Mimi sasa hivi niko Netherlands mwanangu bado tunasaka mautaalam na kuumia na winta.

Ebwana imekaa sawa mwendo mdundo, pole na winter, unajua Mapimpi alikua mwalimu wa a-level ila nadhani baada ya Meja kuhamia moshi ikabidi aje kuendeleza darasa la siasa.
 
mazee mnanikumbusha azaboy kuna siku moja kulikuwa na mkutano wa madent na mateacher khs library na maabara,akasimama denti mmoja simkumbuki jina mchwampaka aka mruhusu,jamaa akaanza tuna library nzuri sana lkn vitabu vimeachwa vimeliwa mchwa........mpaka sasa kuisema ile mchwa mpaaka ilisikika kama mchwampaka...madent hapo wote lete vitabu vyetu weeeeeee...hapo ndo ukawa mwisho wa mkutano lkn kesho yake mchwampaka alimtafuta yule dogo acha...azaboy for real..

lol
 
Ona sasa unavopoteza!! wa pugu boys watasemaje!.. ?? BTW sirukii thread ni kawaida yangu kuchangia thread yoyote.

Mjomba kwani na wewe ni wa pugu boys mbona unawasemea si uwaache wajisemee wenyewe.Mbona unataka kutuletea shule za maporini wakati wewe ulisomea skuli ya Langoni.Na naomba unitajie kabila lako waweza kuwa mtani wangu ili nikutanie vizuri
 
Hata wewe Bulesi bado dogo saana. Sisi ndio vikongwe wakati Headmaster alikuwa Mr. K.R. Jones(British), halafu akaja Mr. Abdirahaman Mwalongo (mjalukolo) akafuatwa Joshua Mwambungu (mwanafiale).

Enzi hizo tulipiga kitabu kama vile hatuna akili nzuri na mitihani ya University of Cambridge kwa ajili ya Form 4 na 6 ilitukoma. Kwa taarifa yako Gavana/Professor Benno Ndulu ni product ya Azania enzi hizo. Vijana walikuwa hawachakachu vitabu bali walikuwa nyomi kwa sana.
Hivi kwa tanzania ni shule gani imeshawahi kutoa viongozi wengi wa nchi?..tathimini za haraka yaonekana Zamani pugu ndo ilikuwa shule special ...je azania kuna historia yoyote?..Kuna kipindi azania ilitisha kwa matokeo ya O level vijana walikuwa wanaweka mabanda mpaka mzuka..ila A level walikuwa kichochoro tu !!
 
Poa mwana ! enzi hizo Mchwampaka ! aliwakamata madogo wamewasha moto kiwanjani saa sita mchana wanaota! kumbe walikuwa wanakamua jani kiulaini walipomuona wakatupa vipisi kwenye moto!

:confused2:Hii ilikua kali sana, inaelekea alietoa ushauri wa kuwasha moto wa kuzugia mchana alikua keshabembea. LOL.
 
Heri hao wana busara. Kuna wale waliokuwa wanakaa kwenye yale mapango kule mpakani na Jangwani. Hawa walimwambia Mchwa arudi alikotoka tena kinyumenyume. Hiyo kwata iliyotokea hapa ilikuwa ya aina yake. Hebu fikiria mzee mzima Mchwa akipiga ligwaride kinyumenyume mpaka maeneo ya bweni!Hii sidhani kama alimhadithia kaka!Hivi nani anaikumbuka na ile stori ya Mchwa kumwambia kaka kuwa ameriona rianafunzi rinatishia kumpiga kaka na bastora?

Sawasawa man, yale tulikua tunayaita matembe na tulienda kule kwenye shamba la minazi la Jangwani kukimbia wanoko ila tulikua tunapiga buku kama kawa kwa uhuru wetu. Mchwa sifa zake baada ya kutonywa na viranja wake wanoko akajipendekeza kibao kikamgeukia alitegemea watu wangemkimbia wakimwona. madafu ya Jangwani yalikua full limited.
 
Ha ha haaa...

Huwa kuna walimu wawili nawakumbuka sana:

1)Mwalimu Mosha - Huyu mwanzoni alijaribu kufundisha physics. Basi huwa alikuwa anauliza swali hilo hilo kila mwanzoni mwa kipindi "hivi mnajua kwa nini shillingi inazama lakini meli inaelea (lafidhi za kichaga)?" ...Halafu anafungua briefcase yake na kuanza kuuza pastpapers kwa muda wote wa kipindi uliobaki. Mwishowe walikuja kumbadilisha na kuanza kuanza kufundisha Civics. Yaani huko ndio ilikuwa mambo ya kuuza papers toka mwanzo mpaka mwisho wa kipindi.

2) Huyu mwalimu jina lake limenitoka kidogo. Alikuwa anafundisha physics. Yeye alikuwa akiingia darasani anakuja na sauti kali sana ya mkwara "Father = mother!".... akimaanisha F = MA (Force = Mass x Acceleration). Halafu anatoa mfano "mko kwenye basi mnakwenda temeke, dereva anafunga breki ya ghafla, na abiria wote wanasukumana kwenda mbele. Dereva anasimama, nyinyi mnang'ang'ania kutaka kuendelea na safari.".... halafu kwa sauti kubwa anasema "FORCE....FATHER = MOTHER"... anafunga Aboti lake....huyo anachukua zake time....kipindi kimeisha. ha ha ha

By the way, Mwl Mitimingi alipata nafasi ya kwenda kujiendeleza UDSM. Baada ya hapo sidhani kama alirudi kuendelea na ualimu.

Mwalimu Mosha alikuja kua mlevi kweli na mfanya biashara mzuri wa pamphlets, na huyo wa physics ni mwalimu John ana kamwili kadogo na funny kichwa machachari kwa mikwala na alikua anakufanyia kweli ukimletea uchale ila alikua na watu wake washkaji.
 
Azania imechanganyika na mademu? Hii kweli balaa! Yani hamna hata fleva tena ya chama letu!! Mimi nakumbuka kiunganishi mashuhuri cha mwalimu Mitimingi hasa, akiongea kiingereza. Badala ya kusema kiufasaha 'another thing' alikuwa akitumia sana neno 'anaza sing' , basi kwetu ikawa kila akija skuli balaza inakuwa tunamwita anaza sing.

Halafu kulikuwa na nunda fulani pale shule linaitwa "batman", sijui bado lipo maana nakumbuka kuna siku lilimzaba Mchwa bonge la kofi kwenye school baraza.I wonder litakuwa lina shughuli gani siku hizi.

Mwalimu Kijazi wa Biolojia sijui bado yuko au vipi. NIlikuwa nammaindi sana, sema basi tu!

Mwalimu Dathi yule mhindi, sijui bado yuko hai, alikuwa mzuri sana wa Chemistry. NIkimuona tena lazima nimpe zawadi.

"Azania, Azania, Azania our school, we look at you with pride, you are known far and wide, you are always our best, we will never forget you",
Wana wa Azania mnakumbuka hii school anthem??

BIla kumsahau Mheshimiwa sana, mwalimu Kente mzee wa Mabuga!!

Uko mulemule mwana kuna yule mama alikua amejazia alifundisha kiswahili kwa muda flani, mpole kweli siku moja Moland alifumwa na mumewe mjeshi anaimbisha pale kwenye hall akaingia mitini, Isaya wa hesabu alikua makini sana, na yule mwalimu mchizi wa chemistry mlvi wa pombe chafu alikua na tuiton jumamosi ya sh 50 masaa mawili palepale azania, alikua anameno machafu kweli alafu anakuambia baada ya ile tuition akishakusanya chake anaenda kula romance na mpenzi wake. LOL.
 
Hapo Mama Idi tu ndo umenikumbusha mbali,,mwalimu wangu wa geography huyo..
utamsikia kila mara "are we together on that?"
 
Nakumbuka nikiwa form 4 tulimpiga chabo patron Yengela akiwa anado......dah!Hostel hakukuwa na adabu hata kidogo.
 
Mjomba wewe wa wapi lakini maana unarukia topic bila kuzielewa.Kule kwa wazanzibari umejidai kuchokoza umenikimbia sasa na huku tena na kwa taarifa tu huyu tunayemsema alikuwa mwalimu wetu na sio mwanafunzi kama unavyofikiri wewe na alikuwa havuti bangi elewa mjomba hapa watu unaoongea nao si kama unavyofikiria wale wa skuli ya kiembe samaki.Hapa ni vichwa makini toka Azania boys

Mwambie hyo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom