Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,476
- 4,752
- Thread starter
- #61
Chaaz Nyangi tupo naye hapa jijini, anaishi Sinza kwa Remmy. So ulimaliza na kina shanel?, sie tulimuachia dorm 5 mwaka 2000.
Mkuu Shonge,,,angalia PM yako
Chaaz Nyangi tupo naye hapa jijini, anaishi Sinza kwa Remmy. So ulimaliza na kina shanel?, sie tulimuachia dorm 5 mwaka 2000.
Hiki ndicho kikosi cha Jimbo la Ei Wani (A One) 2001-2003 waanzilishi wa Mikondo miwili ya ECA. Pamoja na kuongeza mkondo lakini bado tulikuwa wachache sana enzi hizo tuliokuwa tukisoma ECA Mafuta.
Nakumbuka tulipiga ucheche wa nguvu kiasi kwamba tulianza kukokotoa yumkini (probability) ya kutopata wani na kuona kwamba ilikuwa hakuna. Hivi ndivyo tulivyokuwa tukikokotoa. Kwa vile tulikuwa hatuna mwalimu wa Uchumi kwa muda mrefu tukawa tunaasume kwamba tutapata mswaki wa Uchumi ambayo ni pointi 5; ukija kwenye uhasibu na biashara hakukuwa na dalili za mtu kupata pointi zaidi ya nne yaani A moja na C moja. Ukizingatia kwamba wakati ule bado kanuni ya matokeo ya umbwe ilikuwa inahold; niwakumbushe kanuni yenyewe ilikuwa inasema hivi: Ukichaguliwa tu kujiunga na Umbwe Sekondari tayari una Divisheni IV; ukisafiri na kufika getini Umbwe una Divisheni III; ukiingia darasani una Divisheni II; ukiandika notice una Divisheni I; namna gani utachechelaiz ndiyo ditaminant fakta ya kupata wani ya pointi ngapi. Kanuni hii ilichafuliwa na jamaa mmoja ambaye alimaliza 2004 na kuzungusha. Huyu jamaa aliyekuwa na china la chombo kimojawapo cha kutilia chakula alikuwa mwanasoka mzuri kweli. Laiti angekulia nyakati hizi za udhamini wa NMB na Senge angeshakuwa juu sana.
Nakumbuka tulitembelea UDSM FCM tukawa tunaulizia vigezo vya kuingia Mlimani, manake tulikuwa tukihofia BAM na siasa (BAM alianza kutufundisha Savimbi lakini baada ya mgomo wa Novemba 2001, tulivyorudishwa shule akasusa kutufundisha, badala yake tukawa tunafundishwa na Protas Mwalimu wa Olevel. Bw. Protas naye siku moja akatuletea zake tukamkoromea naye akazira, ikabidi tuanze kufundishana wenyewe. Siku moja Mw. Protas akawa anapita nje ya darasa la V ATwo, akaona kwa dirishani intergration inashushwa na jamaa mmoja aliyejulikana kama Martin Chanila-Vijana waliokuwa wamesoma additional Math-. Hapo ndipo alipogundua kuwa hakuwa ametukomoa, na hivyo kuona soo na kuamua kurejea mwenyewe kutufundisha). Yule Lecturer wa UDSM ambaye tulikuwa tunamwuliza mahitaji ya kufaulu ili kuingia UDSM, yeye akatwambia msihangaike kuulizia habari hizo nendeni mkasome kwa bidii kwanza. Tukamwambia hivi pale tulivyokuwa kila mtu alikuwa na uhakika wa kupata wani ila pointi tu ndo tulikuwa hatuzijui. Kwahiyo ndo akatuambia kwamba iwapo utapata mswaki wa BAM au Siasa lakini kwenye kombi umefanya vema, wataangalia Form IV kama ulipata C na kwenda juu basi watakuchukuwa. Ungejuwa tulivyofurahia maelezo hayo huwezi pima, maana tulikuwa ha uhakika kwamba hata kama Vibaraka wa Savimbi wakiamua kutofundisha BAM au Siasa hakuna noma kwani kila mwanafunzi alikuwa na akiba ya form IV
Kichankuli naona unapotosha ukweli katika post yako. Mikondo miwili ya ECA pale MTI SAFI haikuanza 2001 kama unavyosema. Sie tumemaliza hapo kabla wewe hujaanza na ilikuwa miwili. In fact sidhani kama iliwahi kuwa mkondo mmoja tangu a-LEVEL ya ECA ilipoanzishwa Umbwe, kwenye mid 1980's. Halafu ni vema pia tukarekebishana kimahesabu kuwa Mswaki 'F' ya form 6 ni point 7, na sio point 5, so ili upate Div ONE kama una F ya Economics huna choice zaidi ya kupata A in both Commerce and Accountancy.
Kesho yake HP Kisare Makori akaenda kushtaki kwa Baba yake Savimbi, naye Savimbi hakusita kutufanyia kweli, na hivi ndivyo alivyotuambia, nanukuu ".....sasa nasema kweli kwa jina la Mungu, kwa vile nyinyi mmeamua kummwagia kinyesi HP Kisare, hakika na nyinyi mtalazimika kukigusa kinyesi hicho. kwa hiyo kila darasa litachagua mwakilishi ambaye atakwenda kukigusa (kudeki) kinyesi hicho kwenye chumba cha HP" mwisho wa kunukuu. Shughuli ilikuwa kwenye kuchagua nani wa kwenda kuwakilisha kugusa hicho kinyesi, sikumbuki kwenye Jimbo la Ei wani ni nani ambaye alidondokewa na kura hiyo.
Kitendo hiki hakikuwa cha kiungwana lakini kwa Mtu kama Kisare Makori ililazimu kufanya hivyo. Sijui siku hizi huyu jamaa yuko wapi, maana nakumbuka mwaka 1999 alitaka kugombea Urais wa DARUSO, tukalazimika kumchimba mkwara kwamba yatamtokea kama ya Mti safi. Huyu jamaa alikuwa hafai kabisa kwani mwishoni mwa mwaka 1991 wakati tukiwa kwenye mgomo pale Umbwe, yeye alighairi kuendelea na mgomo na kwenda kumweleza Savimbi mikakati yetu ya kuandamana hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimakyaro (wakati ule alikuwa Samwel Sitta) kwenye kuhoji kwanini alikuwa amekaa na fedha zetu (kama walivyosema walimu) wakati akijua kuwa tulikuwa karibu kufunga shule na tulizihitaji fedha hizo. Baada ya jamaa kutangaza kujitoa kwenye mgomo na kwenda kumweleza Savimbi juu ya mpango wetu wa kuandamana, kesho yake tukaanza kulipwa fedha. Na baada ya hapo tukafukuzwa shule; nakumbuka tukio hili lilienda sambamba na lile la Matusi ya nguoni aliyoyapata Mheshimiwa Rais Ally Hasan Mwinyi toka kwa wanafunzi wa UDSM; kwani yalitangazwa kwa pamoja kwenye taarifa ya habari.
Mkuu naona unachanganya mambo kwa kiasi fulani....
- Mwaka 1999 Kisare hakuwepo UDSM, hivyo hawezi kuwa alitaka kugombea urais wa Daruso.
- Mwishoni wa mwaka 1991 (wakati wa mgomo wa kudai kurudishiwa fedha za nauli wakati wa likizo), head prefect alikua sio Kisare Makori.
- Hiyo nukuu yako toka kwa Shayo (Savimbi) inatia mashaka sana....siikumbuki. Unakumbuka baada ya tukio lile, pia alitishiwa kuchomwa kwa petroli? Hadi ikabidi aje mkuu wa wilaya?
- Kisare kwa sasa ni mwajiriwa wa Ikulu (nilishawahi kumwona akiongea kama kaimu mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu - ile nafasi ya Salva).
- Mbona unaongelea matukio ya 2001 na 1991 kwa wakati mmoja, sidhani kama unaweza kuwa ulisoma mti safi miaka yote hiyo.
Kichankuli naona unapotosha ukweli katika post yako. Mikondo miwili ya ECA pale MTI SAFI haikuanza 2001 kama unavyosema. Sie tumemaliza hapo kabla wewe hujaanza na ilikuwa miwili. In fact sidhani kama iliwahi kuwa mkondo mmoja tangu a-LEVEL ya ECA ilipoanzishwa Umbwe, kwenye mid 1980's. Halafu ni vema pia tukarekebishana kimahesabu kuwa Mswaki 'F' ya form 6 ni point 7, na sio point 5, so ili upate Div ONE kama una F ya Economics huna choice zaidi ya kupata A in both Commerce and Accountancy.
Shonge nianze kwa kukiri kosa la kiuandishi la mwaka nilimaanisha 1991 badala ya 2001; vivyo hivyo 2001-2003 siyo sahihi bali sahihi ni 1991-1993. Kuna uwezekano basi awali ilikuwa mikondo miwili ya ECA halafu mmoja ukajapunguzwa kwasababu ECA iliyomaliza 1991 na 1992 ilikuwa na mkondo mmoja tu
Msele aliondoka nadhani around 2003. He was a nice headmasterSamahani kuchelewa kujibu mkuu, nimemaliza mwaka 1997, nahisi ulikuwa hujaingia bado, -so mimi mzee kidogo.
Huyu jamaa ALEX MSELLE ALITOKEA Old Moshi, alitukuta pale.
Alikuwa mnoko kishenzi, ila nasikia akirudi home mke wake anamtuliza, ''yaani mama anatawala nyumba''
Aisee jamaa sura yake tu akikuangalia adhabu tosha!
May be mpaka leo bado yeye, una taarifa zozote?
Huo mgomo ulikuwa 1998 na sio 1997. Ni katika maswala ya kuweka rekodi sawa tu.mimi nilimaliza 1999 nakumbuka mambo mengi ila kati ya yote sita msahau braza karua alinipokea mwaka 1996 na kuwa kaka yangu.zaidi ya yote sitaisahau tarehe 28/1/1996 kwani siku hiyo ndio form two walifungua shule na kutukuta form one nakumbuka ilikuwa ni pata shika nguo kuchanika kwanza ilikuwa form one (njuka)huruhusiwi kulala bwenini nakumbuka siku hiyo mida ya saa nne usiku nilikutwa na braza mmja wa form two akaniomba shilingi 100 nikamuambia sina nilipigwa vibao viwili nikapewa kiatu kinacho nuka sana nikaambiwa nipige simu nyumbani niwaeleze wazazi wangu kuwa sina hela kile kiatu kilikuwa kinanuka sana kweli kwa form one ilikuwa ni mateso
nakumbuka wakati tukiwa njuka tulikuwa tunaambiwa tudeki madom bila kuwasha taa ili tusiwasumbue kaka zetu hio ilikuwa mwaka 1996
msele alikuja mwaka 1996 katikati akataka kubadili utaratibu uliozoeleka
form one(njuka) kudeki madom
form two kudeki vyoo
form three kufeka viwanja
form four sikumbumbuki walikuwa wanafanya nini
form wani tikasema tutadeki tumalizie mwaka akatukubalia tulipofika form two akataka akachange akasema wote tudeki na form two ndio mgomo ulipo tokea mnaukumbuka mgomo wa umbwe mwaaka 1997 ulianza ijumaa siku ya general clean wakina kinabo wakiwa vinara namkumbuka kichalechale john,ayubu marehemu shida