Tujikumbushe sakata la Rada

Huu ni Wembe mkali (PEMASHAPU) juu ya mwili laini wa konokono.

Konokono wetu akijitikisa,akienda mbele,akirudi nyuma, pia akikaa pale palealipo, Wembe wetu unajisindiria ndani ya mwili wake na kuupasua vipande bila huruma.
Hatuna haja ya kuukandamiza wembe wetu mwilini mwake konokono, kwani kazi ya kujikata vipande vipande ni yake mwenyewe konokono.

Patamu ni pale tukichomoa wembe wetu na kuweka mseto wa Pilipili Mbuzi,chumvi na tui la mbilimbi.

Safari hii haokoki mtu ndani ya CCM wala serikali yake hatulali mpaka wote waibusu ardhi kwa ndimi zao.

Si mawe tu, hata kokoto moja haitaachwa imesimama juu ya kokoto.
 
sasa nimegundua kwanini Pinda amesema watachunguza tuhuma zote zinazolalamikiwa..... mpaka WAZUNGU waanze.... what a shame
 
Huu ni Wembe mkali (PEMASHAPU) juu ya mwili laini wa konokono.

Konokono wetu akijitikisa,akienda mbele,akirudi nyuma, pia akikaa pale palealipo, Wembe wetu unajisindiria ndani ya mwili wake na kuupasua vipande bila huruma.
Hatuna haja ya kuukandamiza wembe wetu mwilini mwake konokono, kwani kazi ya kujikata vipande vipande ni yake mwenyewe konokono.

Patamu ni pale tukichomoa wembe wetu na kuweka mseto wa Pilipili Mbuzi,chumvi na tui la mbilimbi.

Safari hii haokoki mtu ndani ya CCM wala serikali yake hatulali mpaka wote waibusu ardhi kwa ndimi zao.

Si mawe tu, hata kokoto moja haitaachwa imesimama juu ya kokoto.

halafu akisha jikatakata unammwagia chumvi....aaaahhhh... anayeyukaaa kabisa basi unabaki unachekelea tuu ushindi
 
Katika watu wanaotakiwa kuchunguzwa ni pamoja na prof. Mwandosya.

Pamoja na kwamba mipango ya ununuzi wa radar ilianza mapema lakini ununuzi
nafikiri ulifanywa 2001 wakati ambapo yeye alikuwa ni waziri wa mawasiliano na uchukuzi.

Je huyu prof. wetu hakukatiwa kitu kwenye hilo deal? Thisday itabidi mutusaidia kujua huyu prof. alifaidika vipi na hiyo miradi?

Ni muhimu kwa Prof. Mwandosya kuchunguzwa ipasavyo hasa kwenye hiyo radar na ndege ya rais. Ni kweli kununua hivyo vifaa ulikuwa ni uamuzi wa serikali nzima, lakini je hao wahusika hawakufaidika na pesa za rushwa kwenye hiyo miradi?

Hivi ni nani alikuwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi kwa kipindi cha 1995 mpaka 2000?

Hivi pesa za kununua radar zililipwa lini (mimi naamini zililipwa 2001)?

Nafikiri ilipofikia TZ sasa ni kutokumwamini mtu yeyote mpaka pale uchunguzi ukituambia tofauti.
 
Na ndo alipata Vijisenti....uu..mm...... sorry......ubavu wa kutaka kugomea uraisis
 
....duuh, Mtanzania, naona usemi 'sheria ni msumeno' umeamua kuutumia ipasavyo.

...."have got nothing, have got nothing to hide or fear"?!............is a tough precept.

SteveD.
 
Huu ni Wembe mkali (PEMASHAPU) juu ya mwili laini wa konokono.

Konokono wetu akijitikisa,akienda mbele,akirudi nyuma, pia akikaa pale palealipo, Wembe wetu unajisindiria ndani ya mwili wake na kuupasua vipande bila huruma.
Hatuna haja ya kuukandamiza wembe wetu mwilini mwake konokono, kwani kazi ya kujikata vipande vipande ni yake mwenyewe konokono.

Patamu ni pale tukichomoa wembe wetu na kuweka mseto wa Pilipili Mbuzi,chumvi na tui la mbilimbi.

Safari hii haokoki mtu ndani ya CCM wala serikali yake hatulali mpaka wote waibusu ardhi kwa ndimi zao.

Si mawe tu, hata kokoto moja haitaachwa imesimama juu ya kokoto.

Madela hii kauli na mifano yako pamoja na profile picture yako kwa kweli vinaonyesha usanii wa hali ya juu na nimeuzimia kiaina!Kama vile unaposema konokono na wembe pemashapu together na profile picture yako huyo jamaa anonekana kama anamwangalia konokono halisi hapo chini!safi sana!Halafu wembe pia ni something huyo bushman lazima atakuwa nao!
 
Huu ni Wembe mkali (PEMASHAPU) juu ya mwili laini wa konokono.

Konokono wetu akijitikisa,akienda mbele,akirudi nyuma, pia akikaa pale palealipo, Wembe wetu unajisindiria ndani ya mwili wake na kuupasua vipande bila huruma.
Hatuna haja ya kuukandamiza wembe wetu mwilini mwake konokono, kwani kazi ya kujikata vipande vipande ni yake mwenyewe konokono.

Patamu ni pale tukichomoa wembe wetu na kuweka mseto wa Pilipili Mbuzi,chumvi na tui la mbilimbi.

Safari hii haokoki mtu ndani ya CCM wala serikali yake hatulali mpaka wote waibusu ardhi kwa ndimi zao.

Si mawe tu, hata kokoto moja haitaachwa imesimama juu ya kokoto.

MADELA:
Aste...Aste.

Not so fast my friend.

Mimi naogopa kuwa 'disappointed' baada ya kufurahia tukidhani kuwa sasa kweli mafisadi wamekabwa koo kisawasawa.

Tunaweza kujikuta tunakuwa 'disappointed' ile mbaya mafisadi yakiamua kusikiliza ushauri wa Pinda!

I keep hopping this is for real!
 
Katika watu wanaotakiwa kuchunguzwa ni pamoja na prof. Mwandosya.

Pamoja na kwamba mipango ya ununuzi wa radar ilianza mapema lakini ununuzi
nafikiri ulifanywa 2001 wakati ambapo yeye alikuwa ni waziri wa mawasiliano na uchukuzi.

Je huyu prof. wetu hakukatiwa kitu kwenye hilo deal? Thisday itabidi mutusaidia kujua huyu prof. alifaidika vipi na hiyo miradi?

Ni muhimu kwa Prof. Mwandosya kuchunguzwa ipasavyo hasa kwenye hiyo radar na ndege ya rais. Ni kweli kununua hivyo vifaa ulikuwa ni uamuzi wa serikali nzima, lakini je hao wahusika hawakufaidika na pesa za rushwa kwenye hiyo miradi?

Hivi ni nani alikuwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi kwa kipindi cha 1995 mpaka 2000?

Hivi pesa za kununua radar zililipwa lini (mimi naamini zililipwa 2001)?

Nafikiri ilipofikia TZ sasa ni kutokumwamini mtu yeyote mpaka pale uchunguzi ukituambia tofauti.

Wote wachunguzwe, Ununuzi wa rada malipo yalishaanza kutolewa 1998 kwa rada.....hawatapata kitu maana paper trail ipo ya huyu jamaa ndo maana anapeta tu kila saa. walijaribu sana wakina rostam kumchafua Prof kwa kujaribu kumhusisha na rada ila wapi yanawarudia maana hakuhusika kabisa, yeye alivyoingia dili tayari lilipigwa akafanya formalities tu za kutoa speech bungeni, soma speech za bunge hata yeye anakupa timeline. kuhusu ndege, hamna kitu

Ila I agree with you Ni vizuri wachunguze. Na Prof mwenyewe welcomes that.
 
Amini usiamini.

Hofu yetu Watanzania juu ya nguvu za Mafisadi wa CCM haitokani na nguvu walizo nazo bali mazoea yetu yakuhofia Vingunge tuliyoijenga vichwani mwetu siku nyingi.

Kam kuna pingamizi kubwa la kutuzuia kwenda mbele na kuwapa kibano cha mwisho, pingamizi hilo ni HOFU TULIYOIJENGA KUTOKANA NA HOFU.

Viongozi wetu wanatumia vizuri sana weakness yetu ya kuwaogopa hasa pale watumiapo madaraka yao kutuadabaisha kwa vyombo vya kulinda usalama wa Raia.

Mmekwisha kuona jinsi viongozi wetu wanavyonywea na kushindwa kudinda mbele za halaiki ya wananchi wanaowazomea.

Silaha kubwa wanayojivunia kuendeleza ubabe si VIJISENTI walivyoweka huko Jersey, silaha yao kubwa ni kutupa kajihofu ili kuamsha Hofu kuu iliyolalavichwani mwetu tangu tuijue serikali ya CCM.

Nguvu yetu kama wananchi imo ndani ya unyonge na udhaifu na mazoea yetu ya kuhofia hofu.

Hakuna kinachotisha kutoka kwa Mafisadi.

Tunatishika kutokana na Hofu itokayo ndani ya akili na mfumo wetu wa kufikiri.
 
Amen mhubiri, Amen!
 
Wote wachunguzwe, Ununuzi wa rada malipo yalishaanza kutolewa 1998 kwa rada.....hawatapata kitu maana paper trail ipo ya huyu jamaa ndo maana anapeta tu kila saa. walijaribu sana wakina rostam kumchafua Prof kwa kujaribu kumhusisha na rada ila wapi yanawarudia maana hakuhusika kabisa, yeye alivyoingia dili tayari lilipigwa akafanya formalities tu za kutoa speech bungeni, soma speech za bunge hata yeye anakupa timeline. kuhusu ndege, hamna kitu

Ila I agree with you Ni vizuri wachunguze. Na Prof mwenyewe welcomes that.

Hana sehemu ya kukimbilia kwani hata ubinafishaji wa TTCL utamkumba akipona kwenye deal la rada, maana safari hii tutafunua each and everything na wao wakitusaidia kurushiana vijembe.
 
Orodha ya MAFISADI WALIOKUBUHU

1. Zakhia Meghji:-

(A) aligawa holela vitalu vya uwindaji akaipotezea Tanzania Tsh 3,304, 903,050/- akiwa waziri wa Mali Asili na Utalii.Ovyo zaidi hata wanafamilia wake walijiingiza katika ufisadi huo kwa kumiliki baadhi ya vitalu kibadhilifu

(B) Alipotosha ripoti ya mkaguzi wa BOT mwaka 2005/2006

(C) Kuchonga bajeti angamizi ya mwaka 2007/2008

(D) Kuidhinisha matumizi mabovu zaidi ya millioni 143 kwa mawaziri mafisadi kwenda kuifagilia bajeti ya kihuni ya 2007/2008 mikoani. Mafisadi hao hawakusita kukomba millioni 143 Tsh kwenda kuzomewa mikoani.

(E) Kufumbia macho shughuli fisadi na za kitaprli za BOT ambayo iliipatia Tangold ltd Kampuni feki kiasi zaidi ya Sh 37.7 billioni ambayo haikuwa na usajiri wowote, akidanganya kuwa ni matumizi nyeti ya serikali kumbe ni ulaji wake na vigogo wenzake

(F) Kubarikli uporaji wa fedha BOT tsh 18,465,755,495.39/- zilizopelekwa kwenye makampuni mbalimbali feki kuanzia decemba 2005 hadi 2007.

2. Benjamini Mkapa:

(A) Kufanya biashara akiwa ikulu ambacho ni kinyume kabisa na katiba ya nchi yetu

(B) Kuanzisha makampuni mufilisi akiwa ikulu ambayo yamelipora taifa zaidi ya Tsh 908,798,045,050/- akiwa ikulu hadi leo kwa makampuni ya kihuni kama ANBEN ltd, Fosnik ltd na Tanpower

(C) Wizi wa zaidi ya Tsh Trillioni 8,86 BOT kwenye kampeini za uraisi na ubunge zilizotuwekea rais mufilisi. Mkapa anatakiwa asimame kuelekea kizimbani na kujibu wizi huo ulioifilisi nchi ikawa kama dampo la umasikini

(D) Uporaji fedha za taia hili kupitia ununuzi wa rada feki Tsh 50 billioni ambayo aliishupalia kama ruba

(E) Uuzwaji angamizi wa mashirika ya umma na viwanda kwa hila zote, kwani hata yale yaliyokuwa yakijiendesha kwa faida kubwa yaliuzwa kwa bei ya tupatupa (throw away prices)

(F) Kushiriki mikataba mibovu ya madini alilipotezea taifa zaidi ya Tsh 959,588,789,005/- kwa kipindi chote Hivyo huyu ni fisadi lililokubuhu.

3. Edward Lowassa

(A) Anahusika moja kwa moja na ufisadi kupitia kampuni haramu ya RICHMOND na shoga wake DOWANS ambao wamelipora taifa zaidi y ash billioni 273/- kwa umeme hewa

(B) Upotevu wa sh millioni 12.5 /- kupitia kampuni feki ya Water City ambayo aliibariki licha ya kuambiwa kuwa ilikuwa haifai, lakini E.L. aliingilia kama alimasi

(C) Kuliingiza taifa kwenye mkataba mufilisi ,fisadi na angamizi wa Buzwagi . E.L. alikuwa pamoja na fisadi kuu Karamagi kusaini mkataba angamizi na filisi hotelini uingereza. Hivyo analipotezea taifa zaidi ya billioni 3,895/- kila mwaka kwa muda wa miaka 25 kama ulivyo mkataba

(D) Kujiingiza kwenye uporaji kwa kutumia ujenzi wa mahekalu ya hoteli ambayo hayalingani na kipato chake, akibisha data hallisi tutazianika hadharani.

4. David Ballali

(A) Amelipotezea taifa kifisadi zaidi ya sh 693,795,398,805.39/- kupitia BOT kwa malipo hewa kwa makampuni hewa ya kitapeli ya EPA, Jeetu P.ltd, Alex Stewart, Tangold ltd, Mwananchi gold co.ltd, Green F. Co.ltd na mengine mengi,

(B)Kulipotezea taifa matrillioni ya fedha kwa kukwamisha ukaguzi halisi wa BOT

(C) Trillioni 5.3 alizochota kwa ajiri ya kampeini haramu za urais za mwaka 2005 zilizozaa rais mlea mafisadi. The breeder of corrupt leaders at all level

5. Basil Pesambili Mramba

(A)Alibarikina kuhusika na uporaji wa sh 17,697,556,594.85/- kutoka BOT akiwa waziri wa fedha kwenda kwa makampuni mbalimbali feki na watu binafsi hasa magabacholi wa kihindi na kiarabu

(B) ununuzi wa ndegefeki ya rais, rada feki ya rais. Alitangaza Watanzania hata wakila majani ndege feki ya rais lazima ingenunuliwa. Je, mr.. Mrmba, uliona Watanzania ni mbuzi hata wale majani?

(C) Uuzaji feki wa Air Tanzania kwa makaburu. Asingeiingilia kikwete Hapa Mrambaji angetajirika ukomo.

(D) Ubinafisaji holela na kwa kiburi na uhujumu wa rasilimali za tiafa kwa masilahi yake akiwa waziri wa fedha , walishirikiana na fisadi ambaye ni rafiki wake wa damu -Abdallah Kigoda

6. Andrew Chenge

(A) Kalipotezea taifa zaidi ya sh 17,857,616,400/- zilizoporwa na Tangold ltd kutoka BOT . Chenge hili hawezi kukwepa kwani alikuwa mkurugenzi wa Tangold ltd at the same time akiwa mkurugenzi wa BOT

(B) Kulipotezea taifa mabillioni ya fedha kwa kuridhia mikataba mibovu/feki/angamizi ya madini akiwa mwanasheria mkuu wa serikali. Takribani zilipotea zaidi y ash 2,890,687,084,573/- kwa kipindi chake chote. Kama anabisha tutazitoa kwa unyambulisho wake.

(C) Zaidi ya billioni 800 zianpotea kwa mwaka kwa mikataba mibovu ya ujenzi wa barabara ama kwa kuweka makampuni feki ambayo huishia kuchota fedha na kutoroaka nchini na vitita vya fedha. Ana kurugenzi wezi wizarani kwake lakini amefumbia macho kwa manufaa yake binafisi. Chenge unasubiri nini kungCcā,?ā"catuka?

7. Gray Mgonja

(A) Alibariki na kuhisika na uporaji wa sh 17,857,616,400/- BOT kwenda kampuni yao ya tangold ltd akiwa mkurugenzi wa BOT pia hapo hapo akiwa mkurugenzi wa Tangold ltd kampuni ambyo hikuwa na usajili.

(B) Kunyamazia ufisadi wa uporaji wa trillioni za fedha BOT kenda kwenye makampuni hewa akiwa mkurugenzi BOT

8. Peter Msolla

(A) Uporaji wa sh billioni 5 zilizokuwa zimetolewa na EUROPEAN OVERSEAS AGENTS miaka ya 90 akiwa makamu mkuu wa SUA. Fedha hiyo ilikuwa imetolewa kukiendeleza chuo(SUA) kitaaluma, miundo mbinu kama barabara za ndani , tafiti mbalimbali na kuwa dila ya maendeleo ya kanda ya mashariki mwa Tanzania (Morogoro, Pwani, Tanga, Dar-es salaam). Cha ajabu fedha hiyo iliishia kwenye midomo ya mamba mafisadi (Prof Msolla, Prof Ishengoma, Mr A.. Magoma (Mhasibu wa kufoji ), keshia Prof Mgongo na maswahiba wao.. Planner mkuu wa wizi huo alikuwa Magoma wakisaidiana na Msolla. Wakaamua kununua magari ya kifahali na kujenga majumba ya kifahari yakiwapo magesti house kwa siri.

(B)Uporaji wa fedha za DANIDA millioni 490 zilizokuwa zimetolewa kwa ajili ya mradi wa OTAITISI (OTITIS) .Fedha hiyo iligawanywa hapo vet SUA na kunguru mafisadi wachache. Msola akachukua 80% ya fedha hiyo na kujenga majumba makubwa ya kifahali . Ngombe wa Mradi huo wakaishia kulala kwenye matope yafikayo kwenye kimo cha tumbo lao wakiwa wamesimama.. Wafadhili walikasirika kupita upeo, wakajitoa. Ukweli huu hauhitaji hata kupeleleza pale VET-SUA.

(C) Hujuma ya fedha ya punguzo la wafanyakazi SUA Tsh 2,245,045,000/- ilyotolewa na benki ya dunia 30/6/1996. Ilipangwa kwamba mtu mwenye mshahara mdogo kabisa apewe Tsh millioni 8. Jambo la kushangaza ni kwamba kila mtu aliyepunguzwa kazi alipewa asilimia kumi tu (10%) ya malipo yake. Hivyo mwenye mshahara mdogo alipewa sh 300,000/- tu. Aliyekuwa anatakiwa kulipwa millioni 20/- alipewa millioni tatu tu. Yeye Msolla na mafisadi wenzie (A.Magoma, Prof Luoga akiwa VC-SUA, Prof Mgongo, keshia na maswahiba wao waligawana 90% ya fedha yote iliyotolewa na benki ya dunia... Mafisadi hawa wakawa wanaishi kama wapo peponi. Wakanunua magari ya kifahali na kujenga majumba ya KUFURU yakiwamo magesti house bubu (kwa siri) na kununua mashamba kila kona Mkoani Morogoro.

(D) Wizi wa millioni 442 SUA kuamkia tarehe 22/4/2006.Yaani, Kati ya shs 442, shs millioni 400/- zilikuwa peti keshi zilizokusanywa kwa miaka miwili . Hivyo Msolla, Keshia, Prof Luoga na Magoma waliziiba zile millioni 400/- mchana kweupe tarehe 21/4/2006 kutoka kwenye sefu, baadaye wakaingiza sh millioni 42/- za malipo ya wafanya kazi SUA, ndipo kesho yake tarehe 22/4/2006 wakatangaza kuwa sh millioni 42/- za malipo ya wafanyakazi SUA ziliibiwa. Kwa uhakika zilizohamishwa kiporaji zilikuwa sh millioni 442(millioni 42 zikiwa malipo ya wafanyakazi SUA na millioni 400 zikiwa peti keshi ) . Sababu ya uporaji huo wa kifisadi ni: (i) kujiandaa kwa kustaafu kwa prof. Luoga, Mr Magoma na Msolla (ii) Kutokuwa na imani na Kikwete kwani SUA walitegemea Sumaye ndiye angekuwa rais ambaye ni fisadi mwenzao. Hata hivyo hawakujua kuwa hata Kikwete ni mama na mlezi wa mafisadi (iii) Kupata fedha lukuki za kufanyia kampeni za ubunge kwa Msolla na hatimaye uwaziri. Hivyo kesi hiyo aliisimamia Prof Monera kwa ahadi kwamba kama angefanikiwa kuivunja kesi hiyo angekuwa VC. Monera alifanikiwa kuizima kesi hiyo, Prof Luoga na Msolla wakampendekeza kwa rais awe VC ili siri hii isifichuke. Kikwete akaingia kwa jeuri yake kichwakichwa akaweka fisadi pandikizi kuwa VC- la SUA ambalo linakomba fedha ya SUA na ya wafadhili likishirikiana na Mufilisi mwenzie Prof Msolla kiasi kwamba, fedha ya wafadhili inayopitia Wizarani (Sayansi na Elimu ya juu) kwenda SUA igawanwe na kukombwa vizuri.

9. Joseph Mungai

(A) Aliingiza silabasi feki kuanzia chekechea hadi elimu ya sekondari kwa Watanzania wa kawaida huku watoto wao wanasoma nje ya nchi.Watoto hapa nchini hawakujua walichokuwa wanasoma, si jogg ama mchemsho. Akaua elimu kupindukia. Alifanya hivyo ili fedha nyingi zibaki wizarani ili azitumie na mafisadi wenzie kwa masilahi binafsi. Zaidi ya billioni 300 zilikuwa zinaliwa wizarani kwa ufisadi huu.

(B) Alikula takribani sh millioni 8/- za bima na likizo za waalimu na mapunjo mbalimbali ya waalimu yakiwamo ya mishahara ya walimu wa shule za msingi na sekondari.Waalimu wakapiga kelele kudai haki zao wakaonekana kutimiza usemi kwamba KELELE ZA MLANGO HAZIMKOSESHI USINGIZI MWENYE NYUMBA.

(C) Kupora fedha inayobaki wizarani mwisho mwa mwaka. Kapuya alichagua baadhi ya maofisa wa elimu wa mikoa/wilaya na mahedimasta wa shule za sekondari ambako alikuwa akituma fedha mwishoni mwa mwaka (mwezi wa 5) na baadaye kutuma wahasibu mafisadi kuifuata fedha hiyo. Alikuwa akipora kati ya sh billioni 3-4 kwa mtindo huo kila mwaka alitafuna na maswahiba wake

10. Juma Ngasongwa

(A) Kalipotezea taifa zaidi ya sh Billioni 9,845/- kwa kipindi akiwa waziri wa Mali Asili na Utalii kwa kupewa pipi kidogo na kuachia uwindaji haramu na angamizi kwa rasilimali na uchumi wa nchi. Ufisadi huu ulimfanya afukuzwe uwaziri wakati wa MZEE RUKSA kwani mzee ruksa alikuwa makini. Hakuwa kama Kikwete ambaye amefunga ndoa na mafisadi kama Kapuya, Ngasongwa, Meghji, Ballali, Msolla, Diallo, Benno Ndullu nk.

(B) Kuchochea vurugu SUA... Yeye alipoona kuwa wanafunzi wa SUA wamemkataa kwa kuwa alikuwa haeleweki anachofundisha , si DS ama DESKI CHAFU, alianza vurugu zilizomfanya afukuzwe kazi SUA katika miaka ya 90. akakimbilia siasa. Vilevile mzee ruksa akamfukuza kazi Mali asili na utalii katika miaka ya 90. Bwege Mkapa akamrudisha kuhujumu, pia Kikwete akameza matapishi hayo hayo.

11. Stephan Wasira

Mamillioni ya fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kupunguza makali ya mbolea ameyakomba.. Yaani, fedha ya sabsidi ya mbolea zaidi ya sh billioni 12,5 ameifagia na kufanya bei ya mbolea kuanza kupaa juu kama kunguru kila kukicha katika mikoa ya nyanda za juu kusini The big four (Mbeya, Iringa, Ruvuma na Rukwa). Kilimo katika mikoa hiyo hutegemea mbolea asilimia mia moja(100%).

Sasa mbolea haishikiki kwa wakulima wengi (90%) kwani ni kati ya sh 40,000/-sh 55,000/- kwenye mfuko wa kilo 50. Kwa ekari moja inahitajika mifuko 4-5 kutegemea na hali ya udongo husika. Mbaya zaidi , si Kikwete wala Wasira anayetembelea mikoa ya Mbeya, Iringa ama Rukwa tangu wawahadae wananchi kuwaletea maisha mazuri. Huu ni utapeli wa unaotakiwa ulaaniwe na kila mpenda haki. Kila leo utamwona Kikwete akitembelea KWA WASUKUMA (MWANZA NA SHINYANGA), BUKOBA NA MUSOMA, PWANI NA MOROGORO MAANA AMEYAONA MAJITU HAYO ZUMBUKUKU.

11. Nazir Karamagi

(A) Kufanya ufisadi wa kusaini mikataba angamizi ya madini kama ya Buzwagi nje ya nchi hotelini!!!!!!!!!!!! Uliolikosesha taifa sh 9,239,389,394.25/- kwa kipindi chote

(B) Kuligharimu taifa zaidi ya billioni 173 kutokana na uroho wa kujitumbukiza kwenye sakata la kampuni tapeli ya RICHMOND na binti yake DOWANS

(C) Kunyamazia kupanda kwa umeme kwa walipa kodi maskini ili kufidia gharama angamizi za TANESCO zinazotokana na mafisadi vigogo kutolipa gharama za umeme.

12. Ibrahim Msabaha

(A) Kulipotezea taifa zaidi ya sh billioni 174 kutokana na kufunga ndoa na kampuni mufilisi , feki na tapeli ya RICHMOND . Anatakiwa akamatwe atiwe ndani na alipe deni hilo .

13. Benno Ndullu

(A) Kabariki ufisadi na uharamia wa sh 693,795,398,800/- zilizohamishwa kijambazi na kaka zake (Ballali, Mramba, Zakhia M) akiwa naibu gavana wa BOT. Hili halikwepi. Tunajua amewekwa pale na Kikwete ili kuficha ushahidi wa mafisadi wenzie wakiwemo watoto wa vigogo. Hapa tayari anaingia kwenye kundi la mafisadi.

(B) Kutomshauri Kikwete avunje bodi inayoshughulikia kutafuta kiini cha ufisadi BOT, kwani bodi hiyo imejaa mafisadi kama G. Mgonja, Zakhia Meghji nk Hivyo hakuna chochote kitakachofanyika zaidi ya kwenda kuficha ushahidi.

14. Edward Hosea

(A): Amekomba zaidi ya billioni 65 kwa kupokea rushwa nene na kutoa taarifa feki kwenye uchunguzi wa RICHMOND , sakata la Buzwagi, mikataba mibovu ya madini, sakata na hujuma za wahindi kupanga kwenye nyumba nzuri za National Housing kuliko wazawa, Sakata la DOWANS na hujuma nyingine nyingi... Ni fisadi anayetakiwa ajiuzuru mara moja.

USHAURI KWA WAPINZANI

(1) Shinikizeni kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi itakayochaguliwa na wabunge mseto. Yaani wabunge 2 CCM, 2 CHADEMA, 2 CUF, I TLP, I UDP na isiwajibike kwa kingunge yoyote bali kwa maslahi ya kitaifa. Msipofanya hivyo, mtakuwa wasindikizaji watindikiwa katika uchaguzi wa mwaka 2010. Hata taahira huwa hashiki moto.

(2) Tembeleeni vijijini mkawaelimishe watu wanaodanganywa na CCM kila kukicha, kwani huko ndiko kuna zaidi ya 85% ya wapiga kura nchini..Wanaishi maisha magumu kama wako mahabusu ya uhaini ndani ya nchi yao lakini hakuna wa kuwaelimisha Kikwete ndio amewasusa watu wa Mbeya, Iringa, Rukwa na Ruvuma huku akiita mikoa hiyo THE BIG FOUR na kunadi kuwa kilimo ni uti wa mgongo na kuwasuta akisema kuwa mbolea ya ruzuku haipo , wasibweteke, watainunua tu hata kama bei yake inapaa kama tai kila kukicha.. Kwa akili finyu ya watanzania, mwaka 2010 atajipitisha kwao na kuwafanya wasahau kuwa aliwahi kudondoka chini akiwahadaa maisha bora katika kura za mwaka 2005. Hivyo wapinzani tembeleeni vijijini maana mjini watu wanawaelewa.

(3) Piteni mkiwaambia watanzania kuwa MAFIGA MATATU YA KIKWETE ni kurudisha utawala wa chama kimoja wenye kubariki kila ufisadi na mafisadi wa uchumi wetu na rasilimali za taifa. Utawala wa kidikiteta na mufilisi bila kuhojiwa na mtu yeyote kwani bunge linakuwa na mafisadi wanaotetea mafisadi , ufisadi na hujuma ya kila aina kwa Watanzania ili mradi tu yapore utajiri wa taifa hili.

USHAURI KWA JK

(1) Wale wote wanaohusika na ufisadi usiwarudishe madarakani (uwaziri ama ukatibu mkuu ama ukurugenzi, kwa mfano:

(A)WIZARA YA MIFUGO IMEOZA TANGU WAZIRI WAKE,MAKATIBU WAKUU NA KURUGENZI ZAKE NDIYO MAANA HAIPAFOMU CHOCHOTE. FEDHA ZAIDI YA MILLIONI 600 ZIMEKUWA ZIKITUMWA KWENYE RANCHI ZA KUZALISHA MITAMBA NA KWENDA KUCHUKULIWA BILA KUFANYA KAZI ILIYOKUSUDIWA

(B) WIZARA YA KILIMO OVYO M KWANI MBOLEA ZIMEPANDA NA ZINAPANDA KILA KUKICHA, WASIRA AMEKOMBA FUNGU LA MBOLEA ZA RUZUKU TAKRIBANI BILLIONI 12.5... DATA TUNAZO.

(2) ACHANA NA KUCHAGUA WATU KWA KUFUATA URAFIKI, UKOO, NAFIKIRI UMEYAONA MWENYEWE
 
Hana sehemu ya kukimbilia kwani hata ubinafishaji wa TTCL utamkumba akipona kwenye deal la rada, maana safari hii tutafunua each and everything na wao wakitusaidia kurushiana vijembe.

Hata TTCL wachunguze tu, hamna kitu watapata kwa huyu Mwandosya zaidi ya majungu tu na hayo majungu yatajibiwa ki-elimu kwasababu ushahidi mkubwa anao kutohusika na mambo ya ajabu tunayoyaona leo...vizuri wachunguze wananchi angalau waone nini kilitendeka
 
Mwanahabari,

Wanaanza kupaka matope na kinyesi wale wote ambao wanaonekana wanaweza kuwa tishio 2010 au 2015!
 
Mwanahabari,

Wanaanza kupaka matope na kinyesi wale wote ambao wanaonekana wanaweza kuwa tishio 2010 au 2015!

Hivi hawa walioangushwa na Scandals wanadhani watafanya comeback kweli 2010 au 2015?

Labda watu wawe vipofu kweli kuruhusu hiyo
 
Mwanahabari,

Wanaanza kupaka matope na kinyesi wale wote ambao wanaonekana wanaweza kuwa tishio 2010 au 2015!

Rev. Kishoka,

Nafikiri ilipofikia kwa nchi yetu ni kutokumwamini mtu mpaka imeonekana wazi hana madhambi.

Kwa muda mrefu nimekuwa mtetezi wa prof. Mwandosya kwa kutumia knowledge ndogo niliyo nayo juu yake. Lakini baada ya kushuhudia yale yanayojitokeza juu ya madhambi ya serikali ya awamu ya tatu, naanza kuwa na wasiwasi na watu wote waliokuwa na nafasi muhimu kwenye hiyo serikali.

Njia pekee ya kurudisha imani kwa sisi wananchi ni kwa wahusika wote kuchunguzwa ipasavyo ili wale wazuri wawe cleared.

Mwanahabari anasema deal la radar lilifanyika wakati prof hayuko madarakani, hiyo ni kweli, lakini pesa zililipwa wakati yeye yuko madarakani. Pia yule Mhindi alilipwa commission yake mwaka 2001 wakati prof. Mwandosya ni waziri. Je wakati anatoa mgawo, yeye prof. hakuambulia kitu?

Kwenye suala la TTCL, mimi niliwahi kufuatilia karatasi kwa karatasi. Kule timeline inakataa na nina uhakika kwamba uhusika wake ulikuwa wa kubambikiziwa zaidi ya ukweli.

Ununuzi wa ndege ya rais ulikuwa chini yake, je huyo Mhindi hakumkatia kitu?
 
Kaka yangu Mtanzania,

Mwandosya alipopigana kumbo na Kikwete nishati, alifanya vyema. Inawezekana kabisa yeye alikuwa mzee wa Mikasi kwenda chukua Radar na Ndege, lakini najiuliza, kwa nini yeye, Marmo, Shein na wengine ambao inasadikika ni wasafi wanaendelea kula sahani moja na wale kina "Paulo usije kucheza na sisi una mikono michafu"?

This does not make sense at all! Sitting with most corrupt faces earth could ever breed, na anaendelea kutingisha kicha na kusema yes, yes yes?

Hivi hawa hawana wapambe ambao wako UWT au mitaa mingine wawape kweli kuwa whumo waliko kumeoza?

Au ni ile Collectivelly Responsibility? Kiapo cha kulindana?
 
Rev. Kishoka,

Nafikiri ilipofikia kwa nchi yetu ni kutokumwamini mtu mpaka imeonekana wazi hana madhambi.

Kwa muda mrefu nimekuwa mtetezi wa prof. Mwandosya kwa kutumia knowledge ndogo niliyo nayo juu yake. Lakini baada ya kushuhudia yale yanayojitokeza juu ya madhambi ya serikali ya awamu ya tatu, naanza kuwa na wasiwasi na watu wote waliokuwa na nafasi muhimu kwenye hiyo serikali.

Njia pekee ya kurudisha imani kwa sisi wananchi ni kwa wahusika wote kuchunguzwa ipasavyo ili wale wazuri wawe cleared.

Mwanahabari anasema deal la radar lilifanyika wakati prof hayuko madarakani, hiyo ni kweli, lakini pesa zililipwa wakati yeye yuko madarakani. Pia yule Mhindi alilipwa commission yake mwaka 2001 wakati prof. Mwandosya ni waziri. Je wakati anatoa mgawo, yeye prof. hakuambulia kitu?

Kwenye suala la TTCL, mimi niliwahi kufuatilia karatasi kwa karatasi. Kule timeline inakataa na nina uhakika kwamba uhusika wake ulikuwa wa kubambikiziwa zaidi ya ukweli.

Ununuzi wa ndege ya rais ulikuwa chini yake, je huyo Mhindi hakumkatia kitu?

Nakuunga mkono 100% na ni vizuri tuone nini kilitendeka, maana haya mambo yanayotoka sasa, bora wote wachunguzwe ili watu wawe na imani ya hao ambao hawakuhusika. Wajue nini kilitendeka na lini.
 
Kuna watu wanafikiri tuko kwenye state ya Paranoia kwa kuhisi na kushuku kila kitu!

No we have a right to suspect everything at this day and age. Ndio maana hakieleweki kusikia kuwa Shein ni Safi.

Maokola Majogo tulijua ni safi mpaka alipokamatwa na Bunduki, tukahoji kulikoni.

Sasa sifa zote za Mwakyembe zimeingia mchanga kisa kajitobolea bomba la maji bila kufuata kanuni!

Hatutafuti masihi, bali tunataka watendaji ambao ni wafuata Sheria, wapenda haki na wachapa kazi!
 
Back
Top Bottom