Tujikumbushe mambo Enzi za Mwalimu

Tarehe 26 Februari,1982 Ndege ya Tanzania,Boeing 737,ikiongozwa na rubani Kapteni Deo Mazula ilipaa angani saa 11:20 kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza kuelekea Dar es Salaam (takribani 90dk,maili 500),ilitekwa na vijana waliojiita ni wanaharakati wa ukombozi ikiwa ni njia ya kumshinikiza Mwalimu Nyerere ajiuzulu,ikaishia kutua Uingereza baada ya kusafiri kwa maili 9500.
Nawatakia mlo mwema wakuu
 
Mbona thread haina mshiko ndugu! Sasa kama vijana waliiteka ilikuwa huko huko angani au ilikuwa imetua Dar? Na kama waliiteka ilituaje uingereza tena?
 
Mbona thread haina mshiko ndugu! Sasa kama vijana waliiteka ilikuwa huko huko angani au ilikuwa imetua Dar? Na kama waliiteka ilituaje uingereza tena?

Ingekuwa vema sana ungeuliza kwa busara,kuliko kusema thread haina mashiko, watu wa aina yao ambao hawapendi kujufunza ni wengi,asante ndugu
 
Nachokumbuka ni kuwa mwal aling'atuka na kuiacha nchi haina kitu, sukari, sabuni ,unga wa yanga kwa foleni. Neno ulanguzi lilianzia hapo. Viwanda vilikufa vyote. Pia kingine ni kuwa aliwatelekeza wapigania uhuru wenzake ambapo waliishi maisha ya dhiki. Hayo ndo nayokumbuka kipindi hicho
 
059.jpg
 
Hii imenifurahisha zaidi!
Ananikumbusha uchekibob wa vijijini enzi hizo!
Ukimwangalia hizo nywele alikuwa anazichana kwa kutumia kwaruzo lile la kizamani ambapo waya zinagongewa kwenye kibao na linakuwa chanuo.
 

Duh hii Landrover 109 aka Mandolini siku hizi hata OCD haipandi hakuna tofauti ya gari anayotembelea mkuu wa nchi na gari anayotembelea RPC !.



059.jpg
 
Karume alikuwa mtemi ?.Hicho kijibwa kilikuwa kinafanya nini kimekosa adabu.


10952_106310996048396_100000084877856_180070_5956175_n.jpg
 
Halafu sijui huyo Man Bestfriend katikati ya Mwalimu na Mengistu alikua ni wa Mwalimu au?
 
Duh hii Landrover 109 aka Mandolini siku hizi hata OCD haipandi hakuna tofauti ya gari anayotembelea mkuu wa nchi na gari anayotembelea RPC !.
059.jpg
natamani hili ndo lingekuwa gari la wabunge watz..
 
Halafu nimeifuraia hii picha Mwalimu kapiga Kipepsi au Kishoka kwenye hiyo Mandolini!
 
mzee hii link yako imenikumbusha mbali sana, i can recall a lot of things kutokea hapa
 
Back
Top Bottom