Tujikumbushe Mabasi ya abiria ya zamani tokea tupate uhuru

VICTORIA TOURS - Mbeya to Iringa, mnaondoka Mby saa 2 usiku halafu mnaingia Iringa saa 12 asb.
 
Mmmh,
nakumbuka Ngorika (1970), Kizota (AR -TA) TTBS, Comfort, Lang'ata Bus Service.
Wa Moshi, mnaikumbuka Maranzana Bus? KIDECO je, mlipanda?
 
Wale wa Rombo kulikuwa na Rombo Investment, Rombo Tulia,.....
 
Manyani wee, twa mbombo? hivi mzee Karanja yupo tky bado?

Viva Karanja, Ni super sonic, Arawa hii ni kiboko yake nduli!
Haya ni maneno yaliyo kwenye basi la Karanja.
Amejaa tele pale Kiwira road Tukuyu.
Nilisoma na mtoto wake, Fred Karanja.
Ni miongoni mwa wachaga waliolowea Tukuyu.
Kuna wakati alikuwa akituhumiwa kuua watu katika zile zama za wanyonya damu!
 
Kitu Wifi Naye njia ya Mtwara inapoingia Dar tairi zake utadhani za udongo kumbe zilizama kwenye tope njiani
 
KINDOKYAKOMBE hiyo leyland ilikuwa Moshi - Marangu - Kilema. Hilo jina ni vifupisho vya majina ya vijiji.
 
dah..., kwa sisi wa nyumbi hii, bombi hii..., kiswele ilikua noma aisee,, ila miaka ya kati hapo ikaja ruvuma tours.., na chiku express.., hizi bus ilikua ukipanda, roho mkononi, dereva anakula bia huku anaendesha na hamna anayelalamika

r.i.p kiswele, nakumbuka mwaka wa ‘96 kiswele ya kutoka dar iliingia songea saa kumi jion, three hour ahead of schedule, ilikua balaa, maana dereva anapaki na gofu mbili zimemfuata kwenda mahabusu
 
Arusha - singida kitu SAHIBU, Singida dar kitu ELIABRY, SHA-ALLY, Singida dodoma MORNING STAR, Dar. DMT became uda, USAI, YELLOW LINE. KAMATA. . . . . . . . .
 
Kulikuwa na basi moja linaenda mbeya miaka ya 90, dereva wake alikuwa anaitwa Giriki.Hilo basi bwana ni mwendo mwendo

huyu jamaa alivuma sana hasa mitaa ya iringa maana akat anaendesha kiswele injin nyuma kakonga sana wabeba ulanzi kwa baiskeli mitaa ya tanangozi, hii basi ilikua ukiisikia ujue imepita.
kaendesha pia tawaqal, mwana-apa ambayo baada ya kupata ajal mbaya itabadilishwa jina na kuwa m-sleeping coach.
watu tulikua tunauliza giriki anaondoka lini?
ndo tunakata tiket.
 
Wadau haswa lale lalioenda umri kidogo, hebu tukumbushane mabasi yetu ya zamani. Mengi yalikuwa ni Leyland.
Nakumbuka Njuweni, Masama Clif na Masama Safari, Yarabi Salama na Yarabi Toba,

Unania Mabasi ya zamani au Kampuni za Mabasi za zamani zilizofirisika Mkuu?Fafanua kiunagaubaga Mtu.
 
Back
Top Bottom