Tujikumbushe jinsi TUNDU LISSU alivyowachana MAGAMBA na hatimaye MAGAMBA yakapandisha Mori

Chenge

JF-Expert Member
Oct 5, 2011
1,073
377
MWENYEKITI: Namwita Mheshimiwa Tundu Lissu na badala ya Mheshimiwa Mnyaa,
Mheshimiwa Amina Amour na Mheshimiwa Kafulila na Murtaza Magungu wajiandae.
MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kunipatia nafasi hii
kujadili hoja hii ya bajeti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hiki ni kipindi kingine tena ambacho wengine wanakiita silly
season. Silly season, muda wa mambo ya kipuuzi, silly season.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kila mwaka, tunakutana katika Bunge hili kuzungumza na
kupitisha mambo ambayo tunajua hayatekelezeki. Serikali inakuja na bajeti, inakuja na ahadi
ambapo yenyewe inajua hazitekelezeki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wabunge wanasimama, wanasema wanaunga mkono mia kwa
mia, kinachofuata ni kuponda hicho walichokiunga mkono mia kwa mia kwa sababu wanajua
deep down ni uwongo, hakitekelezeki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, this is another silly season. This is another season to lie to
ourselves, to lie to our children, to lie to our country. We should be ashamed of ourselves. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana tulikuja tena kwenye silly season ya mwaka jana,
tukaambiwa na Serikali inayojua kwamba haya mambo hayatekelezeki, tukaletewa Mpango wa
Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano. Serikali inayojua kwamba haya mambo hayatekelezeki,
ikatuambia kwamba kwa maneno yao, kwa maneno ya Mpango wenyewe, kuanzia sasa
tutatenga shilingi trilioni 8.6 ya mapato ya ndani kwa ajili ya Bajeti ya Maendeleo. Asilimia 35
Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano, trilioni 43 approximately, tukaambiwa kwamba
tutatenga kila mwaka shilingi trilioni 8.6 ili kutekeleza mpango huu, another silly season. Tukaitwa St.
Gasper na Mheshimiwa Rais, tukalishwa, tukanyweshwa, tukapiga makofi, mwaka huohuo mwaka
jana, badala ya kutenga shilingi trilioni 8.6, wakatenga trilioni 4.9, silly season. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukahoji hapa, tukahoji kwamba mbona mmesema mtatenga
shilingi trilioni 8.6, mbona mmetenga shilingi trilioni 4.9? Wakasema huu ni mwaka wa mpito. Sasa
leo, tunakutana hapa kujadiliana juu ya Mpango wa Maendelo na bajeti ambayo imetenga
shilingi trilioni 4.5 kwa ajili ya bajeti ya maendeleo, tuliambiwa, tutatenga kila mwaka shilingi trilioni
8.6, they knew they were lying, we knew they were lying; we should be ashamed of ourselves.
(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, we should be ashamed of this Government, we should be
ashamed of this party, and we should be ashamed of these Members of Parliament wanaopitisha
this kind of silly thing. (Makofi)


KUHUSU UTARATIBU
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa
Mwenyekiti!
MWENYEKITI: Mheshimiwa Lissu naomba ukae. Mheshimiwa Lukuvi?
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa
Mwenyekiti, kuhusu utaratibu tu, namkumbusha uncle wangu, lugha hizi za kuudhi haziruhusiwi
humu Bungeni, tafadhali sana. Naomba tu aendelee na mchango wake, lakini lugha za kuudhi,
Kanuni zetu zinakataza, Kanuni ya 64.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Lissu, ninaamini una hoja nyingi nzuri, unaweza kuwasilisha vizuri
na kila mmoja akaelewa, Kanuni ya 64 inatufunga kutumia maneno ya kuudhi wengine, naomba
uchangie hoja zako kwa uzuri, Serikali inakusikia, naomba uendelee.
MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Katika Mpango wa mwaka
jana tuliambiwa kwamba, Serikali itaziba mianya ya ukwepaji kodi, itapunguza misamaha ya kodi.
Hii lugha ni ya miaka mingi sana. Leo hii, mwezi huu, viongozi wetu wa kidini wa Baraza la
Maaskofu Tanzania wa Christian Council of Tanzania na wa BAKWATA, wametoa ripoti wanaiita
The One Billion Dolar Question; jinsi ambavyo Tanzania inapoteza fedha kutokana na mianya,
ukwepaji na misamaha ya kodi ambayo imepitishwa na Bunge hili na kila mwaka tunaambiwa
itashughulikiwa, lakini Serikali haifanyi hivyo, Wabunge wa Chama kinachotawala hawafanyi hivyo
na wao ndio wenye responsibility kwa sababu, wao ndio wengi. Kwa hiyo, this One Billion Dollar
Question, this One Billion Dollar Disaster ni disaster ya CCM and nobody else. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa wasiofahamu historia ya mambo haya, mwaka 1998,
Mheshimiwa Dkt. Abdallah Kigoda, alikuwa Waziri wa Madini, ndiye aliyeleta Muswada wa Sheria
ya Madini hapa. Mimi sikuwepo hapa, Mzee Cheyo, alikuwepo na kwenye Muswada, kwenye
mjadala wa kupitisha Sheria ya Madini ya Mwaka 1998, Hansard za wakati huo, Mheshimiwa Dkt.
Abdallah Kigoda na Mawaziri wenzake wakati huo waliliambia Bunge hili kwamba, sekta ya
madini italiingizia Taifa hili 52% ya revenue yote inayotokana na madini; we were told,
walituambia, walituahidi, leo hii viongozi wetu wa kidini wanatuambia katika mabilioni
yanayotokana na madini yetu, tunapata an average dola milioni 100 kama kodi na mirahaba na
vitu vinginevyo na wanasema kitu kingine kwamba, 65% ya hizo dola milioni 100 zinatokana na
kodi za wafanyakazi. Shame on this Government, shame on this party, shame on this people.
(Makofi)
MWENYEKITI: Samahani. Waheshimiwa ambao mnashabikia kwa kuongea, Kanuni
zinatuzuia. Huruhusiwi kuongea, isipokuwa kwa idhini ya Mwenyekiti au Spika. Muacheni achangie
vizuri, mtamshangilia huko nje.
Mheshimiwa Tundu Lissu, tafadhali!
MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tumekuwa na dini mpya Bunge hili
na kwa Serikali hii, tuna Miungu wapya na hawa Miungu wanaitwa wawekezaji. They are our new
Gods, they are untouchable; kila kitu ukifanya, eeh, wawekezaji, eeh, wawekezaji, don't touch
them. Hawa ndio Miungu wetu wapya, what have they done for us out of other? No! Madini
wanatuambia, ni product inayoingiza more foreign exchange than any other. Hizo fedha
mlizotuambia zitakuja ziko wapi,? We have struck up and immerse riches off our cost. Natural gas,
kwa utaratibu wa hawahawa, wa chama hikihiki, wa Serikali hiihii, natural gas ambayo
imegunduliwa off our cost itakwenda njia ileile ya dhahabu na tanzanite. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi I have lost faith completely na Serikali hii. I have lost
faith na chama hiki. I have lost faith na watu hawa. Nawaomba Watanzania, watuunge mkono
katika hili. There is obsolutely no future kama nchi yetu itaendelea kuwa chini ya watu wenye
rekodi ya aina hii. (Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimalizie maana wengine wanataka kuzungumza.
Mwalimu Nyerere kwenye kitabu chake cha ‘Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania', alisema na
wala hatuwajibiki kuendelea na chama na Serikali hii na kama tukiendeleanayo, mbele ni giza
tupu, majuto ni mjukuu. Watanzania wenzangu hatuhitaji kuendelea na chama hiki, hatuendelei,
hatuhitaji kuendelea na this kind of silly na vitu ambavyo ni vya uongo, havitekelezeki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)
MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii sio kampeni.


MWIGULU

MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana kwa kunipa
nafasi hii ili nizungumze na Watanzania. Awali ya yote, Watanzania wanatakiwa wawe makini
sana na waigizaji. Ukimpata mwigizaji mzuri, unaweza ukalia, kumbe mwenzio anaigiza na hiki
ndicho ambacho kimetokea muda mfupi uliopita hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa...
MWENYEKITI: Mheshimiwa, nakuomba ufute neno uigizaji.
WABUNGE FULANI: Aaah!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafuta kama kuna waigizaji hapa.
MWENYEKITI: Naomba ufute neno uigizaji.


MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafuta neno uigizaji kama kuna
waigizaji, lakini maana ya kusema hivi ilikuwa ni hii, tatizo linalojitokeza hapa ni kwamba, bajeti
imeandaliwa na wataalam, lakini watu badala ya kuuliza wajue undani wa bajeti, aliyesomea
Sheria za Mambo ya Kichawi na yeye anakuwa mchambuzi wa uchumi, mwenye uzoefu wa
kuendesha disko anakuwa mchambuzi wa uchumi, unawachanganya Watanzania. Sasa uhalisia
ndio huu, mimi ni Mchumi wa Daraja la Kwanza na Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, ngojeni
niwaambie uhalisia wa bajeti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kwenye Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano,
tunapoongelea 35%, tunajumuisha pamoja na uwekezaji kwenye sekta ya elimu lakini
tunapozungumzia bajeti hii ya leo, sekta ya elimu iko pembeni, fedha zake zimewekwa pembeni,
zile za maendeleo zimewekwa pembeni. Watanzania tuulizane, hivi kweli tunaposomesha
wanafunzi vyuo vikuu, hatuwekezi? Hivi kweli tunapojenga maabara, hatuwekezi? Hivi ni kweli
tunaposomesha vyuo, tunapoandaa Wataalam wa Ugani, tunapoandaa Madaktari, hatuwekezi?
Tulisoma wapi? Hiyo Sheria iliyokuwa inatenga investiment on human capital, ilikuwa ni ya miaka
ya 50 na 60 lakini ukisoma David Roma, ukasoma Waive, ukasoma Mankyu, miaka ya 90, Cop
Douglas Production Function, inatambua human capital kama investiment. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Mpango wa Maendeleo huu tunaojadili, umejumuisha
investiment on human capital ndio ukapata 35%. Ukienda kwenye bajeti ya mwaka huu,
ukichukua investiment kwenye elimu, uwekezaji tuliouweka kwenye elimu, bajeti ya maendeleo
inaenda 39% kwenda 40%. Mmesoma wapi nyie? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, ukiingalia kiutaalamu tu bajeti yenyewe, kiutaalamu
tu, dependency ratio, utegemezi bajeti imepungua. Ukiweka na ile mikopo kwa sababu mikopo
nayo ni fedha yetu tutalipa, ukiondoa na ile ya mikopo, utegemezi kwenye bajeti imebaki 6.5%.
Sifa nyingine ya bajeti, ukienda zile fedha zinazoenda kwenye kulipa mishahara, hamna hata senti
moja inayoenda kwenye mishahara, mishahara inalipwa na fedha za ndani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu muone sasa hili nililolisema ambalo mmesema nilifute, hebu
oneni sasa Bajeti ya Kivuli, wameandika kwamba, kima cha chini kitakuwa 315,000/= hawajui
wanaolipwa kima cha chini ni wangapi, zidisheni mpate hesabu, mimi nitawaambia mwishoni.
Halafu chukueni Walimu muwapandishie mishahara mara 50, chukua Madaktari uwapandishie
mara 50, chukua Manesi uwapandishie mara 50, tafuta jumla yake. Halafu chukua walewale,
makundi matatu haya, uwapandishie mara moja na nusu, bajeti ya matumizi inaenda zaidi ya hii
shilingi bilioni tisa waliyoandika wao. Hii waliyoandika kwenye matumizi ya kawaida inazidi,
ukijumlisha na ile wanayosema kwamba watalipa pensheni kwa wazee, hawajui idadi ya wazee,
ukijumlisha inakuwa zaidi ya shilingi trilioni 15, mmnatumia bajeti ya wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu wanasema...
MBUNGE FULANI: Silly thinking.
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi hili nitalirudia tu, halafu
wanasema kujenga, wanasema kupunguza mzigo wa matumizi ya magari. Mwaka jana
Mwenyekiti wao, Mheshimiwa Mbowe, alirudisha gari akisema kwamba, kupunguza matumizi,
akawahadaa Watanzania. Baada ya muda fulani, kumbe alilikataa lile gari kwa sababu
limechakaa, lilikuwa linatumiwa na Kiongozi aliyepita, baada ya muda fulani kachukua
kimyakimya gari lingine analitumia. Amelirudisha kimyakimya hajawaambia Watanzania kama
ameshalichukua. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa watu wanatakiwa kwa kweli Wachamungu wote, mimi
tangia nizaliwe sijawahi kuona Kambi ya Upinzani yenye pepo mtaka vyeo kama hawa hapa.
(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanatakiwa waombewe, watalipeleka Taifa pabaya, mimi
nawaambia Watanzania mkiendelea kushabikia watu ambao haijulikani kama wako normal au
wanatakiwa wawe Mirembe mtapata kiongozi kama Iddi Amini hapa.


MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!
MBUNGE FULANI: Mwehu huyu!
MBUNGE FULANI: Mwongozo! Anatutukana huyu!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Nimesema niseme na Watanzania, ngojeni niwaambie,
jambo lingine ambalo wanalolikataa hapa, ngojeni mjue unafiki uko wapi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine wanalolikataa wanaongelea OC kama vile ni
dhambi kubwa kwelikweli, angalieni OC kuna nini, OC Serikali imetenga shilingi bilioni 140 kupeleka
vijana JKT, hivi kweli hiyo ni dhambi kupeleka vijana JKT. (Makofi)
MBUNGE FULANI: Waambie!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Serikali imetenga OC kwenda kwenye Tume ikakusanye
maoni ya Katiba Mpya, mnataka Katiba Mpya hamtaki tuweke bajeti, mnataka Katiba mpya kwa
kutumia fedha gani.
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Serikali imetenga fedha kwenye OC kwa ajili ya sensa,
mnataka sense, hamtaki tuweke bajeti. Serikali imetenga fedha kwenye OC kwa ajili ya fidia za
watu wanaondolewa kwenye maeneo kupisha miradi ya maendeleo, mnataka zisiwekwe, wale
watu mtawapatia hela gani mnapowaondoa pale? Serikali imetenga fedha kwenye OC kwa ajili
ya chakula, wanafunzi, wafungwa, wagonjwa mnataka ziondoke mtawapa nini? (Makofi)
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mimi sijawahi kuona Bajeti Kivuli ya aina hii, this is concisely
and precisely rubbish. (Makofi)
MWENYEKITI: Samahani kaa chini, Mheshimiwa naomba ukae.
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
(Kicheko/Makofi/Vigelegele)
MWENYEKITI: Ngojea Mheshimiwa Mwigulu, order in the House, Mheshimiwa Mwigulu
naomba ufute neno pepo kwa sababu ni kinyume…
(Hapa baadhi ya Wabunge walizomea)
MWENYEKITI: Order in the House.
MBUNGE FULANI: Mbona walipotaja Mungu mpya hukusema?
MWENYEKITI: Order in the House.
MBUNGE FULANI: Afute.
MWENYEKITI: Order in the House, naomba ufute neno pepo halafu tuendelee.
MBUNGE FULANI: Mwongozo!
MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwigulu futa neno pepo tuendelee.
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!


MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa humu ndani nafuta lakini watu
wa aina hiyo wakaombewe, nafuta neno hilo. (Makofi)
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.
MWENYEKITI: Naomba tuendelee.
MBUNGE FULANI: Kuhusu utaratibu!
MWENYEKITI: Naomba tuendelee, sasa namwita Mheshimiwa Ahmed Ally Salum na
Mheshimiwa Amina Clement ajiandae na atafuatia Mheshimiwa Komba. Yupo au hayupo?
MBUNGE FULANI: Yupo!




KOMBA


MWENYEKITI: Ahsante, namwita sasa Mheshimiwa Amina Clement na wa mwisho atakuwa
Mheshimiwa Capt. John Komba.
MHE. CAPT. JOHN D. KOMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nishukuru kwa kunipa nafasi
nichangia bajeti hii.
Kwanza nikuambie mimi nafikiri moja ya masharti ya kuingia humu ndani tuwe tunapimwa
akili kama wote tuna akili sawasawa au namna gani, inawezekana watu waliambiwa waende
Mirembe halafu waje humu, wameanzia humu kabla ya kwenda Mirembe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo hili litajirudia sana maana huwezi kusema kila mwaka
tunashuhudia upuuzi humu ndani, tunapanga bajeti ya upuuzi humu ndani, mwaka jana upuuzi,
mwaka huu upuuzi na yeye yumo humuhumu ndani, anakaa humu, huu ni wendawazimu kabisa.
Ni vizuri tukapimana akili kidogo wa Mirembe wakaenda Mirembe, halafu wakarudishwa hapa
wakawa wamesharekebishwa katika ugonjwa.
MBUNGE FULANI: Tuanze na wewe.
MHE. CAPT. JOHN D. KOMBA: Maana yake inapotukanwa, hapa hakitukanwi chama
chochote hapa, lakini mtu anaposimama anazungumza habari jamani wananchi acheni CCM,
hii siyo kampeni humu ndani, humu tujadili habari ya bajeti hii. Kama ulishindwa kupata watu
wengi huko ulikotoka miaka miwili iliyopita wananchi wale ndiyo wameipa CCM ridhaa ya
kutawala miaka mitano, sasa unapowatukana wananchi wale mimi ndiyo nauita ukichaa. Kwa
hiyo, ni vizuri watu wakapimwa kwanza kabla hawajaingia humu ndani. (Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naangalia sana hizi TV za nje, UBC ya Uganda, KBC ya
Kenya, naangalia Wabunge wa Uganda na wa Kenya wanaisifu bajeti yetu tumejali wanafunzi,
tumejali barabara, tumeleta matrekta wanayaona na wanaizungumza kila siku lakini sisi
tunaiponda hiyo bajeti halafu tunasema bajeti yetu ni kujirudia mwaka hadi mwaka. Ni lazima
irudiwe kwa sababu sisi kazi yetu ni kusaidia wananchi lazima tuwasemee wananchi jana, kesho,
kesho kutwa tutawazungumza tu, wanafunzi watazungumzwa mwaka jana, mwaka huu, mwakani
kwa sababu ndiyo lengo la kuwakomboa wanafunzi na wakulima. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu nimeitwa ghafula niende kwenye Jimbo langu,
Jimbo langu ni maskini...
WABUNGE FULANI: Ohoo! Hapohapo.
MHE. CAPT. JOHN D. KOMBA: Jimbo langu ni maskini, katika Wilaya ya Mbinga, lile Jimbo
ambalo limetengwa ndiyo Jimbo maskini, lakini bahati mbaya sana wenzetu wanaofanana na sisi
wa Malawi ndiyo wanaozalisha samaki kupeleka nje, ziwa lilelile huku hakuna samaki lakini
upande ule wanazalisha samaki, wanapaki kwenye makopo wanapeleka nje. Mimi silaumu sana
Serikali yangu kwa sababu Malawi ni nchi ndogo sana, Malawi inaingia kwenye nchi yetu zaidi ya
mara kumi, kwa hiyo, katika nchi wengine walipendelewa mapema, watu wa Kaskazini walipata,
watu wa katikati walipata, mashariki walipata sasa bajeti hii ilenge sisi watu wa pembezoni kama
ambavyo Mheshimiwa Rais amekuwa akizungumza siku zote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi watu wa kule Mbinga Magharibi kule ama kule Nyasa
tunategemea bandari ya Bambabay, lakini ukiangalia bandari ya Bambabay haijapewa pesa
hata senti tano sasa maendeleo yatakujaje? Kama unatengeneza bandari ya Mtwara unataka
bidhaa ziende Malawi, Zimbambwe, Botswana, Namibia, South Afrika, Kongo, zitakwendaje kama
bandari ya Bambabay haiwezi kupitisha mizigo hiyo? Kwa hiyo, naomba sana bandari yetu ya
Bambabay ipewe umuhimu wa kwanza kama zilivyo bandari zingine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ziwa letu la Nyasa, ni Ziwa ambalo vifaa vyake ni duni na kwa vile
sisi tulikubali kuwasaidia watu wa Kaskazini tulikuwa tunawalimia mashamba, maana tunalima
mahindi wanakula wao, tunalima maharage wanakula wao, tunalima mchele wanakula wao,
sasa ni wakati wa kusaidia watu wale waweze kuvua vizuri samaki ili wale vizuri, tena na hao
tunawapelekea maana samaki wako, vyombo vya kuvulia ni duni, teknolojia ni duni. Tunaomba
sana bajeti hii ilenge kuwasaidia wavuvi wadogo wadogo wanaokaa kandokando ya Ziwa Nyasa
na pia na maziwa mengine kwa mfano Rukwa, Tanganyika, Nyumba ya Mungu wapi wasaidiwe
hao, maana tumeshawasaidia sana Ziwa Victoria, kila siku, maana hata siku hizi nikiangalia
wanavyotoa habari ya hali ya hewa wanazungumza halafu wanasema Ukanda wa Ziwa, hivi sisi
Tanzania tuna Kanda moja tu maana yake ni Ziwa Victoria basi uko Ukanda wa Ziwa Victoria,
Ukanda wa Ziwa Nyasa, Rukwa haya maziwa haya nayo yana ukanda wa ziwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba sana kutukanana tukuache, maana yake
tumeshaona huko katika Mabunge mengine watu wanapigana ngumi, sasa huku tunakoenda
tutapigana ngumi na ngumi zilizo upande huu ni nyingi kuliko za upande huu mtakufa. Kwa hiyo,
naomba sana heshimu chama cha wenzako, heshimu chama kilicho madarakani, heshimu
wananchi waliotoa madaraka hayo, changia hoja yako, vunja hoja iliyoko siyo kutakana Chama
cha Mapinduzi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na uwe unaangalia pande zote wanaotukana
sana hawa uwaambie ndiyo watoe maneno, lakini yule uliyemwambia atoe neno lile neno halina
sababu ya kulitoa. Wanaotukana hawa ndiyo uwaambie, naunga mkono hoja mia kwa mia.



MSIGWA



Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi.Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuanza kwa nukuuambayo naipenda sana inayosema:-


"Insanity is keeping doing the same thing in the same way and expecting different result"

ambazo zinalikabili taifa lakini kwa bahati mbaya nimeona yaani uwendawazimu nikufanya jambo lilelile kwa njia ileile huku ukitegemea matokeo tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanafalsafa Albert Einstein anasema:-"Problems can not be solved by the same level of thinking that creates them". Ndugu zangu, kabla sijawa Mbunge kama alivyosema kaka yangu Mheshimiwa Akunaay, nilikuwa nawa-admire sana Wabunge wanavyokuwa Bungeni, wakivaa suti, nilikuwa naona hapa ni mahali ambapo tuna reason, mahali ambapo tuna question na mahali ambapo tunatoka na solutions


is the opposite, binafsi najisikia vibaya sana. Kama taifa tupohapa, we are dealing na future ya taifa hili, tunashughulika namamia ya maskini wa Tanzania, tunashughulika na barabarambovu za Watanzania, tunashughulika na hospitali mbovu zaWatanzania, halafu tunakuja hapa tunaongea mambo yakhanga!

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma historia, nchi za Ulayakarne ya 14, Marekani na Ulaya na nchi zilizoendelea, zilikuwana fikra na mawazo kama tunavyofanya sasa hivi lakini ilipofikakarne ya 18, inaitwa age of enlightenment, reasoning age, walianza kufikiri, kuhoji na kudadisi. Tunapofika katika karne hiikatika Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania,tunapojadili bajeti maana yake tunazo changamotozinazotukabili kama taifa.

Badala ya kukaa na kujiuliza kwa ninitupo hapa, tunatokaje hapa tulipo, tunaanza kuongeangonjera na maneno ya uswahiliuswahili yaani unafiki, woga,kujipendekeza na kutokujadili mambo ya msingi.


(Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, najisikia uchungu sana mamiaya wananchi wametuamini tuje tujadili vitu vya maana hapalakini tunakubaliana akili ndogo itawale akili kubwa. JamesMadison mwaka 1822 alisema, "
knowledge forever will governignorance".

Tumekubali Bunge hili knowledge ndogo i-governknowledge kubwa, tumekubali ignorance i-govern knowledge,tunalipeleka wapi taifa? Akichangia professor hapa hanatofauti na mtu wa darasa la pili. Huwezi kutofautisha mtumwenye masters na mtu wa darasa la pili, where are we takingthis nation? Watu wametupa kura, tunapoteza fedha zaWatanzania, tumekaa hapa tunaacha kujadili mambo yamsingi kwamba tunawezaje kutoka kwenye matope haya? Karne hiyo ya 18 ninayoisema walipoanza kuhoji, walipoanzakudadisi ndipo mapinduzi ya viwanda yalivyojitokeza, no wonder watu wanaosema ni wataalamu wa uchumi wametufikisha hapa tulipo, if that is the case, haya ndiyo masuala ambayo tunapaswa tuyajadili kama taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti inaonyesha hapa, kitabu cha uchumi cha Mheshimiwa Wassira kwamba deni limekuwa shilingi trilioni 20. Ukigawanya ni kama karibu kila Mtanzania anadaiwa shilingi laki nne na themanini na zaidi, hata mimba inadaiwa, ndiyo taifa tulipofika hapa sasa hivi.

Pianinashangaa katika mpango wake wa bajeti taifa hili kamatunafuatilia na tunakwenda na takwimu, mdogo wangu amezungumza hapa kwamba tunatumia takwimu za nyuma, unawezaje kupanga mambo na takwimu za nyuma?

Leo hii katika taifa hili 44.2% ni watoto walio chini ya miaka 15 maanayake hawa ni consumers, wanakula zaidi hawa-produce, wakoshuleni na wanao-produce katika nchi hii ni wachache sanakuliko wanaokula ukijumlisha na wazee tuna mzigo mkubwasana. (Makofi)



Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa utaratibu wabajeti tulio nao hapa,
there is no way kama tunaweza tukafanya maendeleo, it will take ages kubadilisha taifa hili kama tunaendelea na ngonjera za namna hii na kuruhusu akili ndogo itawale akili kubwa.

Watu wenye akili kubwawanaweka akili zao mfukoni kwa sababu ya ushabiki wakivyama badala ya kukaa tuka-discuss namna ya kutatuamatatizo yetu.Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama wanao-consume niwengi na wanao-produce ni wachache maana yake nini?

Tutaendelea kuomba fedha nje na kukopa fedha nje ilituwalishe kwa sababu ni wajibu wa Serikali kusomesha watoto,ni wajibu wa Taifa kuhakikisha watoto wanavaa na kusomashule nzuri lakini mpango mzima wa uchumi uko kimya,hauzungumzi.

Hapa watu wasomi ambao tupo 350 taifalimetuamini tukae hapa tunatakiwa tujihoji, ndiyo maananimesema problems can not be solved by the same level ofthinking that created them, you guys you are tired!

Kwasababu hamuwezi kutetea matatizo haya, mmetuwekakwenye mess ninyi wenyewe, ni lazima akili ya juu zaidi iwezekutatua, ni principle hii yaani huwezi kubadilisha that is theprinciple, iwe ni mwanamahesabu na nikiunganisha na insanityis keeping doing the same thing in the same way andexpecting different results and this is what we are doing.



Tunafanya hayohayo kila mwaka bajeti ya namna hiyohiyo.Ukienda kwenye elimu ni matatizo, ukienda kwenye kilimo nimatatizo, ukienda kwenye afya ni matatizo mwaka baada yamwaka ni matatizo yaleyale,
why can't we think a little bitmore?

We can't stretch our brain a little bit more kama taifa?(Makofi)



Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeongea na watu wengineambao ni ma-professor wanasema mara nyingi wakitoaushauri wa kitaalamu, Serikali hamsikilizi na inawezekanawanakaa watu wachache, wanajifungia halafu wanatoamaamuzi kwa sababu wanajua mambo ni yaleyale, business asusual. Ndugu zangu, where are we going? Where are weheading?



Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaonyesha tenakaribu 42% ya watoto wanaozaliwa wanadumaa,


they can notthink properly, they can not question, they can not ask.

Ubongo aliotupa Mungu ni lazima uwestretched ili uwezekuchambua kwani tumeumbwa ili tutatue matatizo hapaduniani na siyo tu-create matatizo. Tulipokuja hapa Bungenitunatakiwa tu-solve problems, Bunge hili naliomba liwe Bungela kimapinduzi, tu-change namna ya kufikiri na tu-change


namna ya kufanya vitu na wengine wanapata taabu hapakwa sababu tumezoea Bunge la chama kimoja.

Tuna mfumona traditional ya chama kimoja cha zamani, ulimwengu umechange
halafu tumesimama mahali pamoja hatuendi naulimwengu unavyokwenda. Maendeleo duniani yamekuja kwakuwa na mawazo tofauti yanayopingana, badala yakutuzomea mtusikilize, huu ndiyo wajibu wetu. Mimi kama opposition

siwezi kusifia bali nakukosoa ili ufanye kazi yako vizuriili na wewe utimize wajibu wako. (Makofi)



Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa deni kama hili kila mwakalinaongezeka halafu tunakaa hapa tunasema Serikali ya CCMitaendelea kutawala, so what? Ili iweje? Kwa sababu lengo laSerikali kuwepo ni kutatua matatizo ili tuhakikishe tuna-improve maisha ya watu lakini watu kwa sababu wanalinda vyeo, kunammoja amesema Mchungaji, lakini nitasema tu hata kamamtasema au kunitoa nje ya Bunge lakini kama ukweli unakosewa


I will speak out kwa sababu hiyo ndiyo kazi ya Wachungaji vilevile. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mbunge mmoja alishaurihapa tuombewe lakini sioni hata theory ya uchumi inayosemakama unataka kutatua matatizo ya uchumi eti ufanyemaombi, ninashangaa huyu amepata wapi hilo?

As aTheologians hata Paul anasema asiyefanya kazi na asile siyo aombewe, unamnyima chakula lakini yeye anasema watu waombewe. Mimi kama Mchungaji naombea wazinzi, wanaofumaniwa na wake za watu, ndiyo tunawaombea, mimi kama Mchungaji tunawaombea wenye mapepo na hii ni
principle tuna apply,una-consumers wengi lakini producers wachache maana yake you have to produce more tafuta njiaza ku-produce zaidi, we don't pray for this, we don't have topray for this. (Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu tumekaa hapatumezalisha taifa la watu waoga, wanafiki nawanajipendekezapendekeza, mimi sijaja hapa kwa kupewafedha bali wananchi wa Iringawamenichangua, wananiaminina ninajua wananiunga mkono, wananisikiliza. Sasa sihitajikujipendekeza nitaeleza ukweli as a nation tupo kwenyematatizo. Wehave to address this problems lakini siyo tunakujahapa tunaweka ngonjera maneno ya khanga halafu watumnawapigia makofi, tunalipeleka wapi taifa hili? (Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, ninajisikia uchungu, naomba

niachie hapo. Ahsante sana. (Makofi)
 
MH! magamba yanachemsha sana.hayana hoja. ahsante kwa thread hii.nimeipenda.nilikuwa naihitaji sana.
 
Good extract! Sasa mwigulu anataja habari ya uchawi; ivi ni chama gani chenye wataalam wa uchawi? Majimarefu - profesa wa uchawi yuko chama gani?
 
Hapa huyu mwenyekiti naona ansindiketi na CCM! Mbona Mwongozo wa Spika au Utaratibu unapoombwa Mbunge wa CCM anapochangia Mwongoza kikao anaangalia tu? Hapa naanza kumwelewa Dkt. Masaburi! Kuna siku Mabumba alimkatalia Mwongozo Mnyika baada ya kumtukana kuwa Anawashwawashwa! Je, hii ni Demokrasia? Na baadae Anne Makinda anawataka wabunge Wasiongee kama wako Kariakoo! Anayeongea hivyo si Afukuzwe? Kanuni zasemaje? Mie naona Mwongoza kikao akiwabeba CCM na Kuwagaya Washindani anaharibu na analea Utamaduni mbaya!
 
Ungeiunganisha au ukaiongezea na ile ya Mhe Peter Msingwa (MB) Iringa Mjini. Itakuwa imetupa mwendelezo mzuri sana wa pumba na mchele. We can finally make a book!! Tutauza sana, au siyo mwanzisha uzi?
 
They are our new
Gods, they are untouchable; kila kitu ukifanya, eeh, wawekezaji, eeh, wawekezaji, don't touch
them. Hawa ndio Miungu wetu wapya, what have they done for us out of other? No!

ukitaka kuhakikisha hili ingia kwenye 18 za Barrik..
 
Ungeiunganisha au ukaiongezea na ile ya Mhe Peter Msingwa (MB) Iringa Mjini. Itakuwa imetupa mwendelezo mzuri sana wa pumba na mchele. We can finally make a book!! Tutauza sana, au siyo mwanzisha uzi?

Tayari imeunganishwa Mkuu
 
Tayari imeunganishwa Mkuu
Thanks mkuu, inabidi mkuu tuandae kitabu cha haya mambo!! Tutakiweka sawa kwa kuongeza watu wengine wanaotoa michao yao katika kuhakikisha taifa linabadilika, iwe nje au ndani ya bunge.
 
Inasikitisha na inatisha. Hawa ni watu ambao wanalipwa kwa kodi zetu lakini ufanisi wao ni wa kutiliwa mashaka sana. Wanaambiwa waache upuuzi Bungeni kakini hawaelewi. Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom