Tujikumbushe ILBORU

Duh, mkuu Kwetuni..... yaani hapo mpaka mbavu zimekaribia kunivunjika manake mambo ya magazeti na ukiweza daka "TOP LAYER" siku za nyama basi hata "DH" hakuna tena faida ya kwenda...........

Shule yangu Ilboru inasifika sana....................

Hivi kuna mtu anamkumbuka yule mzee Alfayo wa jikoni nilimuacha miaka ya mwanzo ya tisini?
 
Hivi kuna mtu anamkumbuka yule mzee Alfayo wa jikoni nilimuacha miaka ya mwanzo ya tisini?

Mkuu MTM, Mzee Alfayo..... na yule tulikuwa tunamuita "NALABUK" manake alikuwa mnoko kinoma unamkumbuka??? Hawa wazee nadhani watakuwa wamesha retire manake sisi tuliwaacha miaka ya mwanzo 90 na walikuwa tayari mvi zimeanza kuwatoka si unajua tena na mambo ya kupikia kule old kitchen, sio kule kwenye gesi!!!
 
Wale wazee waliwa-time sana kuiba maji ya kuoga saa kumi na moja asubuhi... ni mbinde pale ilikuwa mida hiyo
 
mumezungumzia ilboru mumenikumbusha mbali sana na mimi nilikuwa shule ya jirani pale Ekenywa nimepiga mwaka pale,si vumbi hilo kupandisha kutoka mjini,nilitokea Enaboishu baada ya kupewa suspesion ndo nikapiga mwaka pale kumalizia o'lever,mwaka 98.MTM ulikua mwaka gani ilbori?maana hata ile disco tushatembeleana sana michezo.ilikuwa ni shule yenye vipaji maalum ilboru
 
Mwanzoni mwa miaka ya tisini... enzi za medukenya na yule mchanga aliyekuja kumpokea vijiti Bino

Naskia yule mchagga watu walimtandika na kumvamia nyumbani kwa kuzidi unoko
 
Tunapokumbuka Enzi zetu Ilboru tuchukue nafasi hii kuwakumbumba Dr. Mujuni Mutabuzi na Dr. Allute ambao wametutoka siku ya tarehe11/04/2009 kwa kuzama Majini huko Udzungwa Morogoro, Hawa jamaa ni Ex- Ilborians ( Alumni).
Mwanga wa Milele uwape ee bwana na Raha ya Milele uwaangazie wapumzike kwa Amani. Amina
 
Mwanzoni mwa miaka ya tisini... enzi za medukenya na yule mchanga aliyekuja kumpokea vijiti Bino

Naskia yule mchagga watu walimtandika na kumvamia nyumbani kwa kuzidi unoko

Huyu alikuwa K.J.J.J. MTUI aka Kubwa Jinga Mtui. Duh umenikumbusha mbali sana mzee!!!! Jamaa alitulisha maharage yanateleza kama mlenda yakiwa hayana mafuta wala chumvi kwa siku mbili mfululizo. Siku ya pili mchana watu wakagoma kula, akaja Medukenya akajaribu kubembeleza watu wakakubali kula ugali kwa spinach mchana huo.

Then ilipofika jioni ngoma ikarudi kwenye lile lile arage linalotereza. Basi waungwana tukashawishika kupanda juu (upper pitch). Viranja njaa wakawa wanajaribu kuzuia watu, akatokea mbunifu mmoja akazima main switch shule yote ikawa giza. Basi watu wakapanda kuelekea upper pitch. Tulipofika karibu na nyumba ya second master Medukenya (Mzulu) akaja barabarani akawa anawaomba watu wasiende kufanya fujo bali warudi shuleni tukaongee.

Kwa vile Mzulu alikuwa mtata kwenye kutambua watu wale ambao alibahatika kuwataja kwa majina wakarudi, wengine tukasonga mbele mpaka upper pitch. So ndio likaanzia hapo, watu wakaanza kurusha mawe kwenye nyumba yake, gari yake pickup ikaletwa uwanjani ikapigwa mawe vya kutosha then ikasukumwa kuelekea korongoni, lakini kwa vile mteremko haukuwa mkali haikufika mbali.

Nakumbuka shule ilifungwa na tuliporudi kila mtu alitakiwa kuleta sh elfu moja kufidia uharibifu uliofanyika, ingawa ndio tukasaidia kumstaafisha kubwa jinga Mtui
 
Wakuu, kuna jamaa mmoja miaka ya 94...alikuwa mtaalamu sana. Arnold Swai-kuna mtu anajua yuko wapi siku hizi?
 
Tunapokumbuka Enzi zetu Ilboru tuchukue nafasi hii kuwakumbumba Dr. Mujuni Mutabuzi na Dr. Allute ambao wametutoka siku ya tarehe11/04/2009 kwa kuzama Majini huko Udzungwa Morogoro, Hawa jamaa ni Ex- Ilborians ( Alumni).
Mwanga wa Milele uwape ee bwana na Raha ya Milele uwaangazie wapumzike kwa Amani. Amina

Ndege ya Uchumi, naomba niungane na wote kuwapa pole familia, jamaa na marafiki waliowapoteza ndugu zetu hawa.... On a second note, huyu Mutabuzi ni related na Mama Mutabuzi (RIP) aliyekuwa mwalimu Ilboru??

By the way, KJ Mtui nilipata habari mwaka flani kwamba ametangulia kwenye haki... Sikuweza kuhakiki habari ile lakini kama ndivyo Mwenyenzi Mungu amlaze pema!!!
Kikubwa mimi nakumbuka alipoingia Ilbrou mwanzoni kabisa alileta mapishi mapya ya "SUMU", hili la kwake lilikuwa linachanganywa na maji kisha linaachwa lilale mpaka alfjiri ndipo wapishi walikuwa wanalichemsha, mwanangu si utani lilikuwa linalaza watu klasi kinoma, tulikuwa tunaliita "Fermented Sumu"
 
Tunapokumbuka Enzi zetu Ilboru tuchukue nafasi hii kuwakumbumba Dr. Mujuni Mutabuzi na Dr. Allute ambao wametutoka siku ya tarehe11/04/2009 kwa kuzama Majini huko Udzungwa Morogoro, Hawa jamaa ni Ex- Ilborians ( Alumni).
Mwanga wa Milele uwape ee bwana na Raha ya Milele uwaangazie wapumzike kwa Amani. Amina

Mungu awalaze mahali pema peponi, AMEN
 
Wazee idea ya Alumni imetulia sana, sasa inafanyikaje????
That place has contibuted to make us who we are today. Tujitahidi kuhakikisha jina la Ilboru halisahauliki....
 
Jamani wakuu wa mti safi mnamkumbuka mtu Lobilo? hivi huyu jamaaa yupo hai? maana dua zilikuwa nyingi saaaaana..

Sitaki kusema maeneno ya MAPUTO...... naskia kuna jamaa aliwahi kuibiwa trouser yake....
 
Nyie washkaji wa Ilboru mlikuwa mnatuchukulia mademu zetu wa Enaboishu Secondary School!! Tulikuwa tunawamind nyie!!! Anyway yalikuwa mambo ya shule very interesting ukiyakumbuka leo!!!
 
mumezungumzia ilboru mumenikumbusha mbali sana na mimi nilikuwa shule ya jirani pale Ekenywa nimepiga mwaka pale,si vumbi hilo kupandisha kutoka mjini,nilitokea Enaboishu baada ya kupewa suspesion ndo nikapiga mwaka pale kumalizia o'lever,mwaka 98.MTM ulikua mwaka gani ilbori?maana hata ile disco tushatembeleana sana michezo.ilikuwa ni shule yenye vipaji maalum ilboru

Tabu, mambo ya discipline master Mshanga nini? ndo yaliyokufanya ukatimkia Ekenywa!!! Nani aliyesoma Enaboishu hasiyemjua Mshanga na ubabe wake!!!
 
Hakika mmenikumbusha mbali sana hapa ILBORU. mimi nilipita pale 1985 -87 form five na six HGL. nilipangiwa kukaa bweni la hanang lakini mimi nilikaa MERU.

Nilikuwa mwenyekiti wa waislamu na mwenyekiti wa ulinzi

Nimewakumbuka sana waalimu wangu Kwanza BINO( Head master) Mzava ( maarufu kama Mapambano), Medukenya (Mzuru) mwl wangu Mzava Kapombe, Mwl Mushi (Mke wa capt), Mwl Jumaa (Bwana kaka) na wengine wengi.

naukumbuka kwa mbali sana wimbo wa shule especially wakati wa MZEE BANGO.

Shule yangu Ilboru inasifika sana.
Popote ninapokenda Inasifika sana.
Kwa usafi na ......, Inasifika sana,

Walimu wafanyakazi, wasifika sana.
......
...
Shule yangu nakupeenda.

Hakika hii ilikuwa ni shule best katika Tanzania. jamani nipeni habari za waalimu hawa BINO, KAPOMBE na Mwl JUMA wapo. naomba mawasiliano nao.

Show Ilboru personality

Dr Hamza Yousuf Al Naamani
Doha
 
n1246250343_30239290_1020.jpg

i remember how i used to pray in this chapel. UKWATA! morning, evenin and night, i saw God there
 
Back
Top Bottom