Tujikumbushe enzi za madaladala maarufu

Ubungo -Posta, 'dau la mnyonge...' Basi yakati zile (1983) kuna mwalimu alitoa mtihani wa muhula wa kiswahili akiandika methali, 'dau la mnyonge...' Mwanafunzi akamalizia ... ubungo mpaka posta
 
Leo nimekumbuka sana zile enzi za madalada zenye majina maarufu ....wakati tukiwa madenti yaani ujanja ni kuwa 'staff' kwenye daladala maana yake haulipi nauli sababu makonda au dereva ni washkaji..ilikuwa raha kwelikweli.....kama konda hakujui akikuomba nauli unamwambia mi staff...muulize dereva..dah ...
Temeke Posta - Dunia Hadaa( hizi zilikuwa za mwanzo kabisa-Temeke/Tandika Posta),Riziki kwa mungu ,Golo, Kainkwa,Kita Ngoma nk.....Kwa upande wa Ubungo posta kulikuwa na yakle marefu makubwa ..nakumbuka Matema Beach....tukumbushane wadau......

Hizi zilikuwa gari za rafiki yangu suchak.

Riziki ( nyuma iliandikwa golo yuleee ( ilikuwa inatoka Mwenge - Posta.
Na Golo (nyuma iliandikwa Riziki yule) hii ilikuwa inatoka Temeke- Posta. zote hizi zilikuwa scania za mizigo vikavishwa bodi ya kubeba abiria
 
Back
Top Bottom