songea-dar kulikuwa na kiswele --hakuna basi lingine lililotia mguu njia ile miak nenda miaka rudi
baba umenitoa machozi, ile kiswele haitatokea tena, kule nyuma imeandikwa iga ufe supu ya mawe, halafu umkute dereva mwenyewe marehemu wiligisi, haha wanatoka songea saa kumi na mbili asubuhi wanafika dar saa kumi na moja jioni wakati mabasi mengine yanafika saa mbili usiku, mbaya zaidi wakitoka dar saa kumi na mbili nilishudia mwenyewe saa kumi basi linafika bombambili wanasimama pale saa nzima wanaogopa kukamatwa na trafiki. Ile ilikuwa mashine kubwa
Dah.. mimi nilikuona tuu naona hizo daladala nikenda shule nikiwa ndani ya Cidiz la baba !.. haswa hasa Mbibi, kabibi - Posta - Masaki.
We kilichokuudhi ni nini? Jamani matatizo yako na mkeo usiturushie janvini!I hate you!
Leo nimekumbuka sana zile enzi za madalada zenye majina maarufu ....wakati tukiwa madenti yaani ujanja ni kuwa 'staff' kwenye daladala maana yake haulipi nauli sababu makonda au dereva ni washkaji..ilikuwa raha kwelikweli.....kama konda hakujui akikuomba nauli unamwambia mi staff...muulize dereva..dah ...
Temeke Posta - Dunia Hadaa( hizi zilikuwa za mwanzo kabisa-Temeke/Tandika Posta),Riziki kwa mungu ,Golo, Kainkwa,Kita Ngoma nk.....Kwa upande wa Ubungo posta kulikuwa na yakle marefu makubwa ..nakumbuka Matema Beach....tukumbushane wadau......
mbeya kulikua na mwailubi,urassa,sokolo,mbembela,double coaster ya kwanza mbeya nzima el_kibo,karanja ilikua inapiga tripu tukuyu-mbeya mjini,wengine wataongezea.
na kuna goma lilikuja lilikua linaitwa MGANGALUMA mnalikumbuka?Bakukijana, kumbuka Ile maneno inaitwa MBOGO'ULENJE pale Mbeya, kipiga ruti za Igoma Tunduma. Ile kitu ilikuwa haina mfano wake, Leyland Albion, ikipiga ile kinanda yake inasikika umbali wa kilometa kadhaa! Gia yake ndefu kama fimbo ya kuchezea pool!
Maisha haya bana!
ndio halafu kuna scania moja nimesahau kidogo jina ila ni southern cross au????Kyela-mbeya ilikuwepo LEA WATOTO, HUDUMA (la mwenye lift valey hotel), NTAHENA, UPENDO, KARANJA. humo ni kupakia mikungu ya ndizi na mafuta ya mawese. Tehlikumbuka?, teh,