ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Kitu Tupa Tupa kutoka kwao JUWATA Jazz Band wana Msondo ngoma 'magoma kita kita' a.k.a Baba ya muziki.....

(Wote)
Usiku umekucha na jua limechomoza, mwili umechoka kwa shida nilizonazo,
Pesa ni maua na tena inaua,walimwengu walisema na leo nimeyaona,walimwengu walisema na nimeyaona...

Pesa ni maua na tena inaua,walimwengu walisema na leo nimeyaona,walimwengu walisema na nimeyaona...
Nilikuwa naitwa Tupatupa kwa pesa za urithi sikujua ya baadae pesa zitaniishia,
Nilikuwa naitwa Tupatupa kwa pesa za urithi sikujua ya baadae pesa zitaniishia,
Nakumbuka pesa nyingi nilizorithi kwa baba yangu,watarithi nini wanangu kama mimi nilivyorithi,
Wakale waliyasema bora uwe fukara upate akili,wakale waliyasema bora uwe fukara upate akili....

(Wote)
Nilikuwa naitwa Tupatupa kwa pesa za urithi sikujua ya baadae pesa zitaniishia,
Nilikuwa naitwa Tupatupa kwa pesa za urithi sikujua ya baadae pesa zitaniishia,
Nakumbuka pesa nyingi nilizorithi kwa baba yangu,watarithi nini wanangu kama mimi nilivyorithi,
Wakale waliyasema bora uwe fukara upate akili,wakale waliyasema bora uwe fukara upate akili....

(Wote)Eee jamani nawausia walimwengu msifuate anasa mtapotea,kama jama aa yamenikuta...kama jama aa yamenikuta..

(TX Moshi) Nipitapo mitaani Tupatupa kapita,nikiingia kwenye baa Tupatupa kaingia...

(Wote) Eee jamani nawausia walimwengu msifuate anasa mtapotea,kama jama aa yamenikuta...kama jama aa yamenikuta..

(TX Moshi) Yapata wiki mbili sijawaona mke na wanangu,imebaki shida na huzuni moyoni....

(Wote) Eee jamani nawausia walimwengu msifuate anasa mtapotea,kama jama aa yamenikuta...kama jama aa yamenikuta..

(TX Moshi) Yapata wiki mbili sijawaona mke na wanangu,imebaki shida na huzuni moyoni....

Enjoy...
 
Nimeipenda sana makala hii niliyoikuta kwenye gazeti la Tanzania Daima iliyochapishwa mwaka jana mwishoni...

UVCCM Vijana Jazz imewakosea nini?

Juma Kasesa

KARIBU mpenzi msomaji wa Jamvi la Kulonga nikitumaini mkononi mwako umelishika gazeti hili kwa lengo la kutaka kusoma yale niliyokuandalia kutoka katika anga za burudani na sanaa.

Katika Jamvi letu la leo ningependa kuizungumzia bendi kongwe ya muziki wa dansi nchini Vijana Jazz ‘Sagha Rhumba’ kutokana na jinsi ilivyotelekezwa na wamiliki wake ambao ni Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM); tuanze na historia yake fupi.

Bendi ya Vijana Jazz ‘Sagha Rhumba’ ni moja kati ya bendi ambazo zina mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza muziki wa dansi nchini ikiwa imepitia mabonde na milima.

Bendi hii ilianzishwa miaka 40 iliyopita ikiwa inamilikiwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha TANU-TANU Youth League-( sasa CCM-UVCCM) chini ya waasisi John Ondoro, Abdalah Kwesa, Isach Chakupele, Hussen Stima, Hassan Dalali, Ramadhan Mtoro, Akili Ismail, Hamza Kalala, Manitu Musa ‘Baba Watoto’ na Waziri Omary ambaye alikuwa akipiga tumba.

Ilianza kupata mafanikio mwanzoni mwa miaka ya 1972-74 ikiwa inatumia mtindo wa Kokakoka na kufanikiwa kutunga nyimbo kadhaa kama ‘Magdalena’ ‘Kuruka Ukuta’ ‘Uhuru wa Mapenzi’, ambapo nyimbo nyingi zilikuwa zikipigwa solo na Hamza Kalala.

Ilipotoa nyimbo hizo Hayati Hemedi Maneti ‘Sauti ya Chiriku’ alikuwa ameshajiunga na bendi hiyo akitokea TK Lumpopo iliyokuwa chini ya Juma Kilaza kwa ushawishi wa Kalala ‘Mzee wa Madongo’ ambaye alikuwa kiongozi kwa wakati huo ambapo baadaye alijing’atua na kwenda kuasisi bendi ya Uda Jazz na kumuachia uongozi Dalali (aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba) kabla ya kurudi tena kundini.

Kutokana na kipindi hicho kutokuwepo kwa mfumo wa kutoa albamu, ilikuwa ikipiga nyimbo hizo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za chama na serikali.

Nyota ya bendi hii iliwika zaidi baada ya Maneti kutua ambapo mwaka 1978 alitunga wimbo wa ‘Belibe’ na Kalala akafyatua ‘Pili Nihurumie’ nyimbo ambazo zilitikisa anga ya muziki wa dansi wakati ule wa kipindi cha michakato kilichokuwa kikiendeshwa na Redio Tanzania (RTD).

Iliendelea kutamba katika anga ya muziki wa dansi na kutoa upinzani kwa bendi kama Juwata Jazz, DDC Mlimani Park Orchestra Sikinde ‘Ngoma ya Ukae’, Dar International, Dar Jazz ‘Majini wa Bahari’ na Uda Jazz.

Wakati huo iliamua kubadilisha mtindo kutoka ‘Kokakoka’ na kutumia ‘Hekaheka’ ambapo walitoa nyimbo za ‘Stela’, ‘Leila’ ambapo mwaka 1982 walitikisa zaidi kwa nyimbo za ‘Maisha ya Amba’, ‘Madaraka Ulevini’ ‘Chiku Mwanamama’, na ‘Masaki’ kabla ya baadaye kutumia mtindo wa ‘Takatuka’ na ‘Sagha Rhumba’ wakiburudisha katika ukumbi wao wa Vijana Social bila kulisahau bonanza lao la kila wiki la Vijana Day.

Miaka yote hiyo bendi hii ilikuwa ikipata ufadhili wa vyombo na mishahara kutoka UVCCM ikiwa ni agizo la Makamu wa Kwanza wa Rais Mzee Rashidi Mfaume Kawawa ‘Simba wa Vita’ ambaye alivutiwa na uwezo wa Vijana Jazz ilipokwenda kushiriki maadhimisho ya mwaka wa kwanza ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Zanzibar Abeid Aman Karume.

Baada ya Dalali kuondoka uongozi ulikamatwa na Maneti na baadaye Kalala alirudi toka Matimila Jazz na kushirikiana kutoa vibao kadhaa kama ‘Bujumbura’, ‘Mundinde’ ‘Ilikuwa Lifti’ ‘Ogopa Tapeli’ ‘Chaurembo’, ‘Azza’ ‘Maria’ ‘Ngapulila’ ‘Wifi’ ‘Mwisho wa Mwezi’ na nyinginezo.

Miongoni mwa wanamuziki walioshiriki na Vijana Jazz ni Cosmas Chidumule, Benno Vila Anthony, Saidi Khamis, Jery Nashon ‘Dudumizi’ Abdala Mgonanzeru, Kurwa Milonge, Eddy Sheggy, Abdalah Chomachoma, Adam Bakari, Shaban Yohana ‘Wanted’, Shabani Dogodogo, Mohamed Gotagota, Suleimani Mbwembwe, Jimmy Mensah, Athuman Momba, Aggrey Ndumbaro, Rashid Pembe, Miraji Shakashia, Shomary Ally, Abuu Semhando, Bakari Semhando Kida Waziri, Hamis Juma, Rahma Shaly, Mhina Panduka John Kitime na Nuru Baby White.

Msomaji wangu wa Jamvi la Kulonga nilitaka kwanza uifahamu kwa muhtasari Vijana Jazz wapi ilikotoka na wapi ilipo kwa sasa lakini kubwa ambalo ndiyo hoja yangu ya leo ni kuitazama bendi hiyo kwa namna ilivyotelekezwa na wamiliki wake UVCCM ambapo imebakia kama mtoto yatima asiye na wazazi ikiwa dhoofu kiutendaji kwa kukosa zana za kazi.


Kwa muda mrefu sasa bendi imekuwa ikifanya maonyesho katika hali ngumu kutokana na kutumia vyombo chakavu ambavyo vimeipoteza katika medani ya muziki wa dansi huku wamiliki wake wakitoa ahadi za ‘acha kulia mwanangu nikirudi kazini ntakuletea pipi’ ambazo wazazi hutumia kuwalaghai watoto pale wanapokuwa wakilia.

Ahadi za kupewa vyombo vipya ni zaidi ya miaka 10 sasa ambapo mara ya mwisho ilikuwa wapewe vyombo hivyo kabla ya kampeni za uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu.

Jamvi la Kulonga lilikuwa likifuatilia kwa umakini ahadi za viongozi wa UVCCM na wa kitaifa juu ya kuiwezesha Sagha Rhumba iweze kurudi katika hadhi yake, lakini hali hiyo inaonekana ni tofauti na matumaini yamepotea kwa wanamuziki na uongozi wa bendi hiyo.

Kibaya ambacho Jamvi hili linashangazwa nacho ni kuona viongozi wa UVCCM na CCM kwa ujumla wakitoa misaada mingi ya vyombo na mishahara minono kwa bendi nyingine ambayo inamilikiwa na chama hicho ya Tanzania One Theatre (TOT) chini ya Kepteni John Komba huku wakiitenga Shagha Rhumba kama mtoto ya yatima.

Swali ambalo Jamvi hili linawauliza UVCCM, Vijana Jazz imewakosea nini mpaka kuitelekeza? Sipendi kuwa mtetezi wa bendi hiyo kwa kusukumwa nyuma ya pazia lakini nitaitetea iendelee kuwepo na kupata sapoti kwa kuwa inahitajika kuendelea kuwepo katika kukuza na kuutangaza muziki wa Tanzania.

Lakini pia imeitangaza Tanzania kimataifa p​ale ilipofanya ziara nchini Burundi ambapo kutokana na mapokezi mazuri waliyoyapata kutoka kwa wakazi wa jiji la Bujumbura waliamua kutunga wimbo wa Bujumbura ukiwa umetungwa naye ‘Chiriku’ Hemedi Maneti.

Kiongozi mkuu wa bendi hiyo Mbunge wa viti Maalumu kupitia (CCM) ambaye pia Katibu Uhamasishaji Chipukizi Taifa, Esther Bulaya, kulikoni mama unawaacha wanao kizani? Shime mama Jamvi hili linakupa ushauri wa bure uweze kupitisha harambee kwa wadau wa muziki huo na wanachama wa chama hicho kwa ujumla waweze kuichangia Vijana Jazz ili iweze kurudi katika hadhi yake.

Pia kumbuka wahenga walisema kuwa mchelea mwana kulia hulia yeye kadhalika kumbuka kwamba kwa kupitia tiketi yao ndiyo sababu uko mjengoni kama msemaji wao.

Kwa leo nalikunja Jamvi langu msomaji wangu hadi wiki ijayo nikikutakia afya njema katika shamrashamra za miaka 49 ya Uhuru wa Tanganyika.




 
Kaka asante sana kwa muktasari wa hizi bendi....mimi ni mdau mkubwa wa SIKINDE na TINGISHA ila Niko Zengekala alinikuna moyo sana na Jakii na Solemba.....
 
Majumba na maeneo ambayo vijana wa zamani, nikimaanisha wale wa miaka ya 80's na 90's walikuwa na maeneo yao ya kujidai, haswa wale watoto wa mjini. Kulikuwa na majumba kadhaa ya kucheza disco.

Sea View (Sansui) = DJ Seydou (Afro 70, Safari Trippers wakipiga hapo)

Africana = DJ Mehboob

Motel Agip na New Africa hotel ghorofa ya saba = DJ Emperor (Joseph Kusaga wa Clouds fm), Boniface kilosa alias Bonny Love na DJ Jesse Malongo.

Rungwe Oceanic Beach Resort kwa Mzee Mwakitwange = DJ Ngomely, DJ Pop Juice

Silver Sands = John Peter Pantalakis, Mzee mzima Choggy Sly na Kalikali baadaye alihamia YMCA.

New Space 1900, Mbowe hoteli = Chriss Phabby

New Vision = DJ Super Deo, DJ Paul MacGhee na Joe Johnson Holela, DJ Young

RSVP Discotheque = Saidi Mkandara a.k.a DJ Seydou na DJ Gerry Kotto.

Keys Hotel = DJ Eddy Sally na DJ Sweet Francis

Ukienda kwenye hayo madisco, wapiga picha maarufu walikuwa Bob Spear narafiki yake, kisha akaja Issa Michuzi.

Style kubwa za uchezaji disco zilikuwa Robot, Breakdance, Reggae, Rhumba na Chachacha.


Nyimbo kama hizi zilitamba sana.

Easy - Commodores


Endless Love - Diana Ross & Lionel Richie


I'm Coming Out - Diana Ross


Midas Touch - Midnight Star


Forget Me Nots - Patrice Rushen


Let The Music Play - Shannon


Don’t StopTill you Get Enough - Michael Jackson


Master Blaster Jammin - Stevie Wonder


A Night To Remember - Shalamar


Ukienda kule kwenye madisco ya Uswahili haswa madisco ya Jeshini utakutana na ngoma za bakurutu kina TP Ok Jazz na Franco, Tabu Ley, kwenye majumba ya disco ukitaka kuwaudhi basi piga hizi nyimbo tukizita nyimbo za Bolingo.

Le T.P. O.K. Jazz Mzee Franco


Massu


Maze - Tabu Ley Rochereau



Ukitaka kuzifaidi nyimbo hizi, basi tulizifaidi sana kule viwanja vya sabasaba, kwenye banda la Yahaya Hussein.
 
Last edited by a moderator:
Diamond Sound Band 'wana Dar es salaam Ikibinda Nkoi'.

Kwa vile tunazungumzia Bendi zilizotamba miaka ya 80 na 90 si vibaya tukaiangalia na kuizungumzia pia Bendi ya Diamond Sound maarufu kama 'wana Dar es salaam Ikibinda Nkoi' ambayo iliundwa mwishoni mwa mwaka 1996 na baadae kuwa tishio katika jiji la Dar es salaam hususan maeneo ya Mwenge katika ukumbi wao wa New Silent Clu ambapo sasa hivi pamebadilishwa na kuwa kanisa baada ya mmiliki wake Papaa Fred Rwegasira kuokoka....

Bendi hii ililishika hasa Jiji la Dar es salaam kiasi kwamba ilikuwa ni kosa kwa mjanja wa jijini Dar kukosa maonesho ya wana Dar es salaam Ikibinda Nkoi siku za Jumatano,Alhamis, Ijumaa,Jumamosi na Jumapili....Kila mtu alikuwa anataka kuingia ukumbini hapo Silent Club na ilifikia kipindi wamiliki waliongeza kiwango cha kiingilio ili kuzuia watu kuingia ukumbini lakini hii nayo haikufua dafu.....Kila wikiend ilikuwa ni nyomi ya kufa mtu....

Kulikuwa na Usiku maalum wa wanavyuo kila siku ya Ijumaa ambapo wanavyuo wa Vyuo vya UDSM, Dar Tech, IFM, MUCHS(sasa MUHAS) na vingine walijazana ukumbini hapo kwa kiingilio cha bei chee huku wakionesha vitambulisho vyao getini....Ilikuwa ni raha mpaka basi,mambo yote yalikuwa ni Dar es salaam Ikibinda Nkoi.....

Bendi hii ilitamba na nyimbo kama Neema, Kimalumalu, Jetou, Kazi bila mshahara, Valentines Day, weekend,

Bendi hii iliundwa na wanamuziki hawa wafuatao:

Waimbaji walikuwa ni Ibonga Katumbi 'Jesus', Liva Hassan 'Sultani', Allain Mulumba Kashama 'Mstahiki Meya wa Jiji' , Richard Mangustino, Aniceth Petero 'Mukombozi', Wayne Zola Ndonga, Roger Muzungu...Drums zilipigwa na Marehemu Abuu Semhando, na Marehemu Gabby Katanga...Gitaa la Solo lilipigwa na Adolph Mbinga ,Elly Chinyama na Ellystone Angai,Al , Gitaa la besi lilipigwa na Jojoo Jumanne, Gitaa la Rhythm lilipigwa na Adolph Mbinga na Elly Chinyama, Kinanda kilipigwa na Andrew Sekidia, Tumba zilipigwa na Soud MCD na Mzee Moto...Pia alikuwepo German Kissa na wengine wengi.....Kwa ujumla hawa jamaa walikuwa wanatisha...

Bendi hii ilikuwa na safu ya wadada wanenguaji ambao walikuwa ni moto wa kuotea mbali,walikuwa wanatisha si kawaida katika kunyonganyonga viuno,wanenguaji hao ni pamoja na Salma Abeid 'Mama Lao', Marehemu Elly Longomba, Lilian Tungaraza 'Internet', Janeth 'Jackson' Isinika, Lilian Kinondoni, Modester 'Scud' Chengo na Kamuke Sukari......

Bendi hii ilianza kusambaratika mwaka 2000 baada ya mmiliki wa bendi hiyo Papaa Fred Rwegasira kushindwa kuwalipa wanamuziki wa bendi hiyo na baadae kuokoka...Hali hii ilipelekea wanamuziki wa bendi hii kutunga wimbo wa 'Kazi bila mshahara' kikiwa ni kijembe kwa Rwegasira...Baadae baadhi ya wanamuziki wa Bendi hiyo wakiongozwa na Ellystone Angai, Liva Hassan Sultan na Allain Mulumba Kashama waliondoka na kuelekea nchini Zimbabwe na kuanzisha bendi ya Diamond Sounds(sasa hivi ipo nchini ikijulikana kama Diamond Musica International)....Wanamuziki waliobaki wakiongozwa na Ibonga Katumbi Jesus na Richard Mangustino waliungana na vijana wageni akina Totoo Ze Bingwa na Donat Zinga Nkuvu na kuanzisha bendi ya Beta Musica.....

Hao ndio walikuwa Diamondo soundo the besto of the besto wana Dar es salaam Ikibinda Nkoi.....

Mambo yote kipindi hicho yalikuwa ni New Silent Club(zamani Silent Inn) pale Mwenge....
 
Nani anaikumbuka bendi inaitwa Tanga international wakipiga wimbo unaitwa mpenzi roza miaka ya 80. Sina uhakika kama nimekosea majina. Nautafuta sana wimbo huo.
 
eeh elly longomba marehemu??? mkuu unawakumbuka beta musica/ pia walitingisha kidogo
 
eeh elly longomba marehemu??? mkuu unawakumbuka beta musica/ pia walitingisha kidogo
Yap....Elly Longomba alifariki siku nyingi, tena alikufa baada tu ya kutoa/kuurudia upya wimbo wa baba yake Lovy Longomba wimbo wa 'Elly wangu' ambao alimshirikisha Papy Nguza 'Papy Kocha'...

Nakikumbuka sana kibao cha Bana Beta cha Beta Musica......Hii bendi ilitamba na kupotea ghafla...Wanamuziki waliounda bendi hii Ibonga Katumbi Jesus, Richard Mangustino, Totoo Ze Bingwa na Donat Zinga Nkuvu na mcheza shoo mahiri mwanama Salm Abeid 'Mama lao',,,
 
ngoja niendeleze hapo ulipo ishia kwa kumbu kumbu za wana dukuduku

..nimekuja kucheza ..nimekuja kufurahisha mwili wangu bwana weee mimi ni muke wa watu
..na mume wangu yupo hapa hapaa ..ameniruhusu kucheza muziki wa kwetu
..tafadhali bwana duku duku ni wasiwasi wao jamanii eehe mziki wetu unatia fora
..wasiwasi wao ..sisi wao baridi kwetu hakuna shida ooho wache wasemee

bala utafute kwa marefu ingawa najua ulikuwa na ubeti mmoja au mbili then wakawa wanarudia kibwagizo hizo..

Huu wimbo hawa jamaa waliyacopy mashairi yake mwanzo mpaka mwisho kutoka kwenye wimbo BINA NANGAI NA RESPECT-Cheza na mimi kwa adabu/heshima wa FRANCO na TP OK JAZZ yake...



Live yake hii hapa.....


 
Last edited by a moderator:
kaka kuna viba vya zamani 2 navitafuta kwa udi na uvumba, nio tayari utoa 40,000tsh kwa yeyote ataenitaftia.
1. kivumbi kimenizonga (ioss ya Ndala kasheba) na tucheze sote tukunyema ( Mk beats ya shem karenga)
 
kaka kuna viba vya zamani 2 navitafuta kwa udi na uvumba, nio tayari utoa 40,000tsh kwa yeyote ataenitaftia. 1. kivumbi kimenizonga (ioss ya Ndala kasheba) na tucheze sote tukunyema ( Mk beats ya shem karenga)
TehTeh....Ngoja nizichangamkie buku 40 aisee....Naziangalia kunako kalibrary kangu mkuu...Nikizipata nitaziweka hapa ASAP....
 
Wakuu tukitaja zamani na Tanzania na wanamuziki wetu..., Hii sentensi itakuwa haijakamilika bila kumtaja Jabali la Muziki...

Wadau naomba mtu anitafutia link au attachment niweze kudownload ya wimbo Dunia Sasa Imani Imekwisha - Marijani Rajabu... will greatly appreciate
 
Wakuu tukitaja zamani na Tanzania na wanamuziki wetu..., Hii sentensi itakuwa haijakamilika bila kumtaja Jabali la Muziki...

Wadau naomba mtu anitafutia link au attachment niweze kudownload ya wimbo Dunia Sasa Imani Imekwisha - Marijani Rajabu... will greatly appreciate

Heshima yako mkuu....

Fanya upitie thread nzima utakutana na post namba 59 ambayo inasema hivi:

Huyo ndio Jabali la muziki Marijan Rajab na Dar International mkuu...

Marijan Rajab kabla hajahamia Dar International alikuwa katika bendi ya Safari Trippers ambayo ilisambaratika mwaka 1977......Baada ya Safari Trippers kufa nini kilifuata?.....Mwaka huohuo 1977 mwanamuziki mwingine Nguli chini Abel Barthazar alianzisha bendi ya Dar Internatinal ambayo pamoja naye(Balthazar) pia walikuwepo Joseph Mulenga,Abdallah Gama,Cosmas Thobias Chidumule,ALi Rajab,Belesa Kakere,Marijan Rajab,Machaku Salum,King Michael Enock,Joseph(Yusuph) Bernard na Habib Jeff.......

Bendi hii ilianza kwa kutoka na vibao kama Nyerere mwanamapinduzi,Rufaa ya kifo,Mwana uoe,Betty,Margreth na Sikitiko,....Vibao hiivi vilitamba hasa na bendi ilianza kushika chati ya juu katika medani za muziki wa Dansi Tanzania.....Bendi hii ilikuwa maarufu ghafla na kwa kupitia Marijan Rajab ilipiga muziki wenye mahadhi kama ya ule muziki uliokuwa ukipigwa na Safari Trippers hivyo kuzidi kumletea umaarufu Marijan Rajab kitu ambacho inadaiwa hakikupendezwa sana na wanamuziki wengine akiwemo Abel Barthazar ambao waliona kwamba watu wanaichukulia Dar International kama Safari Trippers....Walianza kumpiga vita Marijan Rajab ambaye hakupendezwa na hali hiyo hivyo kuamua kujitoa katika bendi hiyo(miezi 9 tu baada ya bendi kuanzishwa).....Mwaka 1978 baada ya Marijan Rajab kujiondoa bendi haikudumu sana kwani ilisambaratika baada ya wanamuziki nane(08) tegemeo wa bendi hiyo Abel Barthzar(aliondoka kabla ya wenzie),King MichaelEnock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum na Habib Jef waliondoka na kwenda kuanzisha bendi ya Mlimani Park Orchestra(baadae DDC Mlimani Park Orchestra).....

Baada ya bendi kusambaratika,mmiliki wa Dar International Zachariah Ndebame alimuomba Marijan Rajab arudi kwa ajili ya kuisuka upya bendi hiyo ambapo alikubali na kurudi rasmi kwenye bendi,hapo akakutana na mpiga solo Hamza Kasongo ambaye kwa kushirikiana waliiongoza bendi hiyo kutoa vibao vitamu kama Zuwena,Vick na Mayasa......Vibao hivi viliurudisha umaarufu wa bendi hii kiasi cha kuzitisha bendi ilizozikuta zikitamba wakati huo kama Vijana Jazz,Juwata Jazz,Mlimani Park,Marquiz na Biashara Jazz.....Hali hii ilileta ushindani mkubwa miongoni mwa bendi hizo.....Baadae bendi hii ilipata wanamuziki chipukizi kama Fresh Jumbe ,Tino Masinge 'Arawa', Mohammed Mwinyikondo na wengine na kurekodi vibao vitamu kama Mzee Said,Baba Anna,Masudi amekuwa jambazi,Bwana Mashaka,Pondamali kufa kwaja, Mwajuma, Pendo si kulazimishana, Usimtese Mwana, Chakubanga na nyingine nyingi zilizotamba na kufunika ile mbaya enzi hizo.....

Bendi hii ilikuwa ikitumia mtindo wa Super Bomboka.......Nyimbo nyingine zilizotamba za bendi hii ni pamoja na Mwanameka, Ukewenza, Sababu ya Mapendo, Usia wa Baba, Aisha Mtoto wa Mwanza, Siwema, Mama Maria, Paulina, Mateso ya ndoa, Ponda Mali Kufa Kwaja, Amekosa Nini Mama, Pesa Sabuni ya Roho, Ukatili Ni Unyama, Siwema No. 2, Mwana Acha Kidomo Domo, Mpenzi Christina, Uzuri wa Asali, Ninamsaka Mbaya Wangu, Emmy, Umevunga Ahadi, Alinacha, Nitajirekebisha, Ndugu Umepotea, Baba Anita, Ndugu umepotea No. 2, Pendo, Pombe si chai, Esther, Baruti, Vicky, Uzuri wa asili, Mapambano yanaendelea, Mwana mpotevu na nyingine nyingi...........

Hao ndio Dar International Orchestra wana Super bomboka chini yake Jabali la muziki Hayati Marijan Rajab(R.I.P)......
 
Heshima yako mkuu....

Fanya upitie thread nzima utakutana na post namba 59 ambayo inasema hivi:

Asante mkuu, kweli umeonyesha kwamba knowledge si haba kwenye nyanja hii ya wanamuziki na bendi za tz enzi hizo., sasa mkuu naomba kama unaweza kunitafutia Dunia Sasa imani imekwisha (sababu nimesearch pote online sijapata) vile vile kama unaweza kupata wimbo wa super rainbow (milima ya kwetu No 2) yaani yule dada anavyomjibu yule kaka baada ya kumsema kwenye milima ya kwetu No 1... "Machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo, tulitoka wawili ninarudi peke yangu, wazazi wangu wataniuliza bibi yako yupo wapi.....)
I hope nimekupa info za kutosha kuweza kuniangusha ka-link au download
 
Asante mkuu, kweli umeonyesha kwamba knowledge si haba kwenye nyanja hii ya wanamuziki na bendi za tz enzi hizo., sasa mkuu naomba kama unaweza kunitafutia Dunia Sasa imani imekwisha (sababu nimesearch pote online sijapata)
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom