ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Mie natafuta nyimbo za TOM MALANGA:
1.AMIGO
2.AFRO
3.BARUA.
Na pia natafuta nyimbo za yule mwanamziki mkongwe(marehemu kwa sasa)ni msambaa wa VUGA Lushoto na kwa jinsi nilivyokua nampenda mwaka 2010 nilisafiri mpaka kijijini kwao nikaliona kaburi lake.
wimbo wake ninao upenda zaidi unaitwa Mwisho wa mwezi.Hapa namuongerea EDDY SHEGGY.

Eddie Sheggy: Wimbo- Hakuweza ulezi. Bonge la nyimbo!

Pia: Julie, Shakaza, Penzi la Ulaghai, na Ukewenza( kulala sebuleni). Hizi aliziimba akiwa na Washirika Tanzania Stars.

Mwisho wa mwezi, ogopa tapeli, kapu la mjanja, wivu hizi na zingine aliziimba akiwa na Vijana Jazz.

Milima ya Kwetu- Huu aliuimba akiwa na super rainbow!
 
Hizo nyimbo zote na nyingine nyiiingi mimi ninazo ila nauza.
Una pakee mfukoni ni PM ili nikuite sehemu na kukuchomea kwenye CD...
Napatikana Dar kwa sasa, lakini mwezi ujao ntakwenda home Baidoa.
acha roho mbaya mpe tu mwenzio
 
Msaada wenu wana jf msaada wa rekodi ya nyimbo hizi za zilipendwa online 1. DALILI-MSONDO NGOMA 2. CHEUSI MAGALA NO.1-OTTU JAZZ 3. MALARIA-MSONDO NGOMA 4. NIPELEKE KWA BABA NO.2-OTTU JAZZ 5. SI WAZURI BINADAMU-MLIMANI PARK ORCHESTRA Kama kuna mdau ataweza kuniaploadia online au anafahamu link ambayo nitaweza kuzipata nyimbo hizi, nitashukuru sana

Kama hujazipata na upo dar, nitafute mimi nitakupatia bure ninazo zote kwenye flash yangu lakini audio tu. Nipo Open university ukitaka njoo hapo chuoni
 
wadau wengine wawasiliane nami ninazao zilipendwa kwa wale watakaohitaji..... nami natafuta hizi .......
1. nalila masumanda- hamza kalala
2. fransisca----- ukimuona huko aliko,mwambie kuwa nateseka sana,nafasi yake bado ipo moyoni mwangu....
 
Ningependa wale wanaopenda nyimbo za bendi zetu wasifanye uvivu wa kupata collection ambayo wataifurahia
 
kama hajazipata hizi hapa
zilipendwa jf request

na wengine pia ambao wanahitaji nami pia nina kaaalibrary kangu ningependa kuka test mapungufu yake kwa kuombwa nyimbo mbali mbali ambazo upatkanaji wake ni wa shinda
 
Eddie Sheggy: Wimbo- Hakuweza ulezi. Bonge la nyimbo!

Pia: Julie, Shakaza, Penzi la Ulaghai, na Ukewenza( kulala sebuleni). Hizi aliziimba akiwa na Washirika Tanzania Stars.

Mwisho wa mwezi, ogopa tapeli, kapu la mjanja, wivu hizi na zingine aliziimba akiwa na Vijana Jazz.

Milima ya Kwetu- Huu aliuimba akiwa na super rainbow!



huuo wimbo wa mwisho wa mwizi uliupata??? ninao kama bado sema urushiwe
 
ZILIZOVUMA Non stop 4 Hrs 28 minutes by Richman K of Youtube:

Gonga hapa : https://www.youtube.com/watch?v=Kc9LDuFOmUA

1. Pitie. 2. Nadina. 3. Kasongo. 4. Shauri Yako. 5. Vunja Mifupa. 6. African Typic Collection. 8. Afro.
9. Ba Gerants Ya Mabala. 10. Barua yako. 11. Beyanga. 12. Boyaye. 13. Cadence Mudanda. 14. Charonyi ni wasi. 15. Che.
16. Dracula. 17. Embakasi. 18. Halleluya. 19. Kalala Mbwebwe. 20. Kasuku. 21. Kwanza jiulize. 22. Marie.
23. Marina. 24. Mobali Na Ngai Wana. 25. Msichana wa elimu. 26. Napika. 27. Naza. 28. Nimaru. 29. Nyako Konya.
30. Pamela. 31. Paulina. 32. Rebecca. 33. Shida. 34. Sina makosa. 35. Stella. 36. Wendenda.
 
Nafarijika nikisoma comments za wadau hapo juu, kweli mUZIKI huunganisha watu. mwenye nyimbo za NUTA Jazz na Jamhuri Jazz atuwekee hapa
 
  1. FM ACADEMIA na kitu MAPENZI YA KISASA : https://www.youtube.com/watch?v=gB-eu4Rl0RA
  2. FM ACADEMIA na kitu NEEMA : https://www.youtube.com/watch?v=vQ0vT56qbps


Source: Video zote kwa hisani kubwa ya FM ACADEMIA Wazee wa Ngwasuma wa YouTube
Thanks kwa post mdau...

Ingawa unaenda tofauti na lengo la thread hii ambayo heading yake ni : "Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake..."..

Hawa Ngwasuma ni wa juzi tu mkuu...Hawana sifa ya kuwepo katika thread hii...
 
Heri ya Mwaka mpya 2015 wadau...

Mkuu Balantanda heri ya mwaka Mpya pia....

Kuna hii band inaitwa Serengeti band wamerudia nyimbo nyingi za Zamani.Hivi unaweza ukatupa taarifa zao kidogo na kama bado wanapiga wanapatikana wapi?
 
Dahh! Asante sana Balantanda na wengine wote kwa kazi nzuri. Naumba kuuliza kuna mtu aliimbwa na vijana jazz. Wimbo unahusu sherehe ya kuuaga umasikini mtu huyo aliitwa Joseph Pauline unao kwenye maktaba yako . Tafadhali naomba niwekee Kama upo
 
Dahh! Asante sana Balantanda na wengine wote kwa kazi nzuri. Naumba kuuliza kuna mtu aliimbwa na vijana jazz. Wimbo unahusu sherehe ya kuuaga umasikini mtu huyo aliitwa Joseph Pauline unao kwenye maktaba yako . Tafadhali naomba niwekee Kama upo

Yote aliyofanya ndugu yangu Joseph Pauline ni sawaa au amekosea eeeh ni sawa au amekosea a eeeh .

Pauline kafanya mambo katuacha kwenye mataa ee Pauline .....
Katuacha tumeduwaa eeh
Vyombo......

Chorus. ......Jambo la kushangaza Pauline kafanya party la kuuga umasikini eeeh, Pauline oooh oohh laa la la laaa la.

Tumesukuma nae mikokoteni maskani ooohh oohh jama aa Pauline rafiki yetu la la la la

Chorus repeats!

Watu wengi walihudhuria pati hilo ooo

Fred Benjamini alikuwepo
Toto Tundu alikuwepo

Shomari Ally akikuwepo

Shakashia alikuwepo

Suleiman Mbwembwe alikuwepoooo

Mkuu nimekumbuka mistari hiyo japo kwa kujivuruga. Majina ya wanamuziki waliotajwa kwenye wimbo huu walikuwa mahiri sana wakati ule. Na ni katika Album hii Vijana Jazz ilianza kufifia. Wengi waliondoka na wengine walishatangulia mbele ya haki. Ni Album ya msimu wa 1996/97. Baada ya hapo Vijana haikutoa Album iliyohit kwani ilitoa I love you Mpiga debe miaka ya 1999 na Mabaa Maid miaka hiyo ya 1999/2000.

Sababu kubwa ni viongoz wa bendi yaani UVCCM kuipa sapoti kubwa TOT Band.
Album hiyo yenye wimbo ulioutaja ndo ya mwisho katika mtiririko wa Pure Vijana Jazz Air Pamba moto, Saga Rhumba! Ukiondoa wimbo huo, nyimbo zingine nzuri kabisa katka album hiyo ni Mama Samia, Mbuzi yake kamba nk. Naitafuta hii Album katika CD ila naikosa. Ninayo kwenye tape, bahati mbaya vifaa vyangu siyo rafiki tena kwa tape.

Ila Bantalanda ninashida sana na wimbo Kapu la Mjanja na Janja ya Nyani pamoja na Visa vya Mume.

Wimbo huu visa vya mume naupenda sana hasa pale wanaposema- Nikipika wali unasema una mawe e , nikipika ugali unasema una mabuja sema kinachokukera bwana eeeh. Ilikuwa ni combination ya hatari wakina Adam Bakari( sauti ya zege). Daa zaman kulikuwa na Muziki na Vijana Jazz ilikuwa ni noma. Ila nayo ilipata Upinzani mkali kutoka Washirika Tanzania Stars(Watu Njatanjata) na Bimalee.
 
Nakushukulu Sana chaza tupo pamoja.ukianza mwanzo mwa ukurasa huu utakutana na kapu la mjanja. Mimi nakumbuka kidogo

Uliona wapii bundi kwenye kun Ia njiwa eeee.x2
Elewa kapu la mjanja mjinga Haiti mkono
 
Back
Top Bottom