Tujihadhari na wagombea ubunge wa aina hii

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
[FONT=ArialMT, sans-serif]Machi 2 na 3 wiki iliyopita, nilibahatika kushiriki kwenye warsha iliyoandaliwa na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata), pale mjini Mbeya. Warsha hii ililenga kubadilishana mawazo baina ya wadau mbalimbali kuhusu ujenzi wa masoko katika wilaya za Mbarali (Mbeya) na Sumbawanga (vijijini) mkoani Rukwa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mapema, nilielezwa kwamba Mviwata, kupitia uhamasishaji wa wanachama wake, wadau na wafadhili mbalimbali, imeshajenga masoko yanayofanya vyema katika wilaya za Kongwa (Kibaigwa), Njombe (Igagala), Handeni (Mkata), Mvomero (Nyandira) na Morogoro vijijini katika maeneo ya Tawa na Tandai.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Niligundua kwamba Mviwata, kama kauli mbiu yake inavyosema ni sauti ya wakulima kweli kwani imewasaidia wakulima wengi kujua habari mbalimbali za masoko, kuboresha kilimo chao na hata masuala ya mipaka.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mapema nilidokezwa kwamba warsha hiyo ingehudhuriwa na mkuu wa Mkoa wa Rukwa, wakuu wa wilaya husika, wabunge, madiwani, wakulima na wadau wengine muhimu, hususan wanachama wa Mviwata waliotapakaa nchi nzima. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika warsha hiyo iliyofunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Daniel Ole Njoolay, niligundua kwamba wakati wa utambulisho wa warsha hiyo muhimu kwa maendeleo ya wakulima na wafanyabishara wa mazao ya wakulima, hakukuwa na mbunge hata mmoja![/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Japo mbunge wa Mbarali kunakotarajiwa kujengwa soko kwa juhudi za Mviwata alituma mwakilishi, mbunge wa Sumbawanbga vijijini ambako wananchi wake pia wanapelekewa soko na Mviwata, wala hakujali hata kutuma mwakilishi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Nilimuuliza ofisa habari wa Mviwata, Susuma Susuma, kama mbunge wa Sumbawanga vijijini alipata mwaliko, akanijibu kwamba wabunge wote walipelekewa mwaliko kwa kuzingatia umuhimu wao.[/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Wote tuliwapa mwaliko na kuwaeleza umuhimu wa kufika lakini hata sisi tunashangaa. Yule wa Sumbawanga vijijini hatukumuona kabisa, hakutuma mwakilishi wala kutuambia tu kwambna ana udhuru,” aliniambia Susuma.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Nilimuuliza Susuma kuhusu masoko mengine waliojenga kwa mikakati yao katika maeneo mbali mbali ya nchi yetu kama huwa wanapata ushirikiano kwa wabunge wa maeneo hayo. Yeye alinijibu kwamba mara nyingi hawapati ushirikiano mzuri wa wabunge isipokuwa akamtaja Mbunge mmoja wa Kibakwe, George Simbachawene kwamba ndiye amekuwa akishirikiana nao kwa karibu muda wote.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kilichonifanya niandike makala haya ni kuwataka wapiga kura wenzangu mwaka huu tunavyoelekea kwenye uchaguzi kujihadhari na wagombea ubunge, hususan wale wanaotaka kugombea tena mwaka huu, watakaokuwa wanapita na kuoredhesha mambo lukuki wakidai wameyaleta wao, wakati yamefanywa na watu wengine na ushiriki wao ulikuwa ziro![/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Yamekuwepo madai ya muda mrefu kwamba baadhi ya wabunge wamekuwa na kawaida ya kusoma taarifa za halmashauri za miji na wilaya zinazoonyesha mambo yaliyofanya kwa mwaka na halmashauri hizo, kisha wabunge hao kuyachukua kama yao na kuwadanganya wapiga kura kwamba mambo hayo yametokana na wao wakati hawakusaidia lolote![/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hili la Mviwata, linathibitisha kwamba kumbe si halmashauri pekee bali hata asasi na taasisi za kiraia zimekuwa zikifanya mambo makubwa katika kusaidia wananchi kwenye maeneo mbalimbali ya nchi huku wabunge ambao walitakiwa kuwa karibu nazo sana wakiwa mbali kabisa, pengine kwa vile warsha za asasi hizi hazina ‘mibahasha mikubwa mikubwa’ ambayo nasikia wabunge wamezoea kupewa![/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Lakini mwisho wa siku maendeleo yakipatikana wanawahadaa wananchi kwamba yametokana na wao.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Nimegusia suala la bahasha kubwa kwani niliwahi kuumwa sikio pale Dodoma wakati fulani nilipokuwa Bungeni kwamba kama ukiandaa warsha unayotaka wabunge washiriki, kama hakuna bahasha iliyononana, bila kujali semina hiyo bila kujali ina umuhimu kiasi gani, sahau kupata idadi ya washiriki wa kutosha. Nasema niliumwa sikio na mtu, pengine ni kweli ama si kweli.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ninaamini kabisa kama soko la Kasanga, Sumbawanga vijijini, litajengwa kabla ya uchaguzi wa baadaye Oktoba mwaka huu, litamnufaisha mbunge wa sasa kama atagombea tena akidai ni moja ya maendeleo aliyoyaleta![/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Linaweza kutumiwa tena na mgombea uchaguzi ujao kama ‘moja ya miradi yake’ ingawa alipewa mwaliko na hakufika bila hata kutoa udhuru![/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa msingi huo, nilikuwa ninawaomba wapiga kura wenzangu tuwapime kwa makini wagombea wanaporukia maendeleo yaliyofanywa na wengine na kudai ni wao wameleta. Ikiwezekane, tusiwe tunaishia kuamini maneno yao bila kutafiti na kisha kuwasuta.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika muendelezo wa uongo ambao bila shaka mwaka huu tutalishwa kwa wingi, tulianza kuona baadhi ya wagombea wakitumia majina makubwa hadi Rais Jakaya Kikwete kuwa ndiye kawatuma kugombea ubunge![/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa vile makala haya leo sipendi kutajana majina, ninashukuru Rais Kikwete kututahadharisha wananchi kujihadhari na waongo hao wa mchana kwa sababu yeye hajatuma mtu kugombea.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Isitoshe Rais alisema yeye anazo nafasi 10 za kuteua wabunge na hivyo kama kuna mtu anamtaka anatumia nafasi hizo kumteua.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kundi lingine la wagombea hatari ninalowashauri wapiga kura wenzangu kujitenga nalo ni wale wenye ajenda ya kujadili wenzao ama matukio.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mgombea anayekuja, na hususan wakati huu wa kuelekea kwenye kura za maoni, tusimruhusu kumpikia majungu ama kukalia kumsema mbunge aliyetangulia kuwa alikuwa hivi ama hajatekeleza kile. Yeye atueleze anachotaka kutufanyia kwa kushirikiana na sisi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Pia ipo aina ya wagombea wanaopenda kujisifia mambo ya nyuma ambayo ilikuwa majukumu yao ya msingi badala ya kutuambia mikakati yao ya sasa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Sisi tumtake mgombea, cha kwanza zaidi, ajadili masuala ya msingi na kero ambazo amezigundua katika jamii husika kama vile elimu, barabara, umeme, maatibabu, maji, huduma za kilimo na kadhalika na si kujadili historia.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Tusimwache akaishia kutaja kero pekee bali na mkakati wake kama anao wa kuzitatua.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kikubwa cha kumpima mgombea hapa ni kama ana uwezo wa kuhamasisha raslimali zilizopo katika kutatua kero zetu na pia kama ana ushawishi wa kutosha dhidi ya serikali katika kuleta raslimali chache za nchi katika eneo letu ili kututatulia kero mbalimbali zinazotukabili.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mgombea mwingine wa kuogopa kama zimwi ni anayepita sasa akimwaga pesa au kujenga vijimradi hivi na vile kwa kutumia senti zake za watoto nyumbani, yaani anayenunua uongozi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ndugu zangu, kama kuna mgombea hatari ni huyu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati fulani, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alisema lazima mgombea anayetumwagia ‘vijisenti’ tujiulize kwamba huyu bwana atazirudishaje hizo senti zake za mboga ya watoto?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Jibu liko wazi kwamba mgombea wa aina hiyo, haumwi na kero za wananchi isipokuwa anachokifanya sasa ni danganya toto. Anautaka ubunge kwa maslahi yake binafsi na akishauoata anajichimbia katika kutumia nafasi hiyo kurejesha gharama zake, bila shaka kwa njia ya kifisadi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Haya mambo yamesemwa sana na mifano tunayo lukuki lakini tatizo letu wapiga kura ni kuendekeza njaa ya muda mfupi kwa kuchagua mtu anayenunua kura zetu ili tupate mlo wa leo na kusahau kauli ya wahenga kwamba ‘kesho ndiyo kubwa na muhumu.’[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mambo ya kuzingatia kwa wagombea yako mengi, lakini kwa hayo machache niliyojadili hapo juu kulingana na ufahamu wangu mdogo, nilipenda kuhitimisha makala haya kwa kuwataka wapiga kura wenzangu kuzingatia kwamba kama tunataka maendeleo ya majimbo yetu na nchi kwa ujumla, wakati wa uchaguzi tuweke kando kabisa ushabiki wa vyama kwani hautatusaidia abadani.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Tuchague mgombea mwenye uwezo wa kujenga hoja na mikakati thabiti ya kutatua kero zetu na si chama chake, utajiri wake, ama sura yake. Pengine cha kuangalia, kwa mtazamo wangu, ingawa si muhimu sana ni elimu yake.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wiki iliyopita, nilibahatika kuandika makala nyingine kuhusu uchaguzi ambapo nilivitaka vyama vya upinzani kujipanga sasa ili kufanikisha kuongeza idadi yao bungeni.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Sipendi kurudia nilichosema lakini nilielezee tu kwa kifupi kwamba uzoefu unaonyesha kuwa uwepo wa wabunge wengi wa upinzani bungeni wanasaidia kuibana serikali itekeleze majukumu yake kuliko Bunge linapotawaliwa na idadi kubwa ya wabunge wa chama tawala ambao wakati mwingine hulazimishwa kupitisha mambo ambayo si maslahi ya umma mpana, isipokuwa genge la watawala wachache.[/FONT]



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom