Tujihadhari na mahouse girl

Kweli dunia inabadilika . Miaka 10, 15, 20 iliyopita mambo hayakuwa hivi. Mi nakumbuka nimelelewa na HG bila matatizo. Though kwa wastani kila baada ya miaka miwili ilibidi wazazi waagize HG kutoka kijijini.

Wakati kukiwa hakuna taasisi za kidali za watu hawa nawashauri wanaolazimika kuwa nao option ya kwanza watafute wahusika kutoka vijini kwao. Ukweli kila mtu kijijini au origin yake kuna familia/watu walio kwenye mazingira magumu. Bibi babu wa kijijini wakipewa kazi ya kukutafutia msaididi utapata msaididi ambaye japo unayo historia yake fupi.

Ingawa gharama ya mwenyeji wa kagera au Tabora kuleta mfanyakazi wa ndani inaweza kuwa kubwa san lakini kuna RISK kubwa utakuwa umepunguza.

Sio Vizuri nani kuwa na HG analea wewe hujui wala ndugu zako hawajui japo wazazi wake, mjomba wake ,shangazi yake nk ? Njia hii ina usalama kiasi fulani.

 
Sawa unaweza kuwa na ndugu yako akakulelea mtoto. Lakinimimi nimewahi kuwa naye wa jinsi hiyo. Alikuja mjini hata kiswahili hajui sawasawa, lakini baada ya kumsoapsoap alianza kiburi ajabu! Fikiria wageni wakifika ukimtuma kununua soda umbali wa mita mia moja anachukuwa masaa matatu, ukimuuliza anavimba utadhani tkiti maji. Baadaye nikatambua kwamba ameanza kusifiwa na wanaume majirani kwamba hajambojambo. NIlianza kupata salaam "hajambo fulani?" Nikabaki najiuliza salam hizo ni za namna gani. Siku moja nikasikia anaimba wimbo wa tangazo la kutumia condom kwenye corridor kwa sauti huku akicheza, vijana wakawa wanamshangilia naye anapandisha midadi "Tumia salama condom"

Nilitumia janja kumrudisha nyumbani, lakini wazazi wake kumbe walitarajia pesa nyingi za mshahara. Niliwapa pesa ya kuanzia mtaji kijijini, wazazi wake wakailamba yote, lakini kwa kuwa alikuwa ameiva kisawasawa kila idara ikijinadi, vijana wakampokea kijijini kiutamu, akapata mimba within the same yea. Vijana walitambua kwamba hata kiswahili chake sasa ni bomba, wale waomisomi wakawa ndio wa kupiga stori naye kijijini, mikesha ya Krismas yeye akawa ndiye mjanja zaidi ya wenzake wa kuwafundisha namna ya kuongea na wanaume kiswahili cha mjini. Nikashukuru bora nilimwahisha, maana alianza kuniringia hata mimi mwenyewe. Unaweza kumwita akanyamaza kimya akihesabu unamwita mara ngapi. Mtoto wakati huo tkiwa na mmoja tu hakutaka hata kumlisha. Alikuunywa mwenyewe uji akasingizia mtoto hataki.

Hiyo ya hse grl kufundisha watoto tabia mbaya niliwahi kuipata pia. Mke wangu alimfuma hse grl mmoja wa Morogoro ambaye alitudanganya kwamba hakuwahi kuolewa kumbe kakimbia mume, akiwa na umri wa miaka 23, alikuwa anamfundisha binti yetu jinsi ya kumfurahisha bwana. Binti yetu akakutwa anafurahi sana na kuahidi amalize darasa la saba upesi ili naye akamfurahishe bwana. Wageni wakifika pale nyumbani wakitaka kumwona Mrs Lekanjobe aliitika yeye mwenyewe akijitambulisha kwamba ndiye yeye. Tulipotambua hilo nikajua hapa shetani amekalia kiti cha nyumbani. Nikajiuliza ingekuwa vipi kama ningekuwa nimewahi kutanua naye. Maana endapo nilimweka mbali nami lakini bado alijiita mrs na kuwajibu watu maswali kibao kama mama mwenye mji ilikuwa ni hatari. Siku moja tukaambiwa mbona tulimkuta mrs wako mwingine, kwani unao wawili? Tuliacha midomo wazi na mke wangu.

Hse grl huwezi kuachana nao kwa sababu bora mfanya kazi kuliko nduguyo. Mama mdogo naye anazo hatari zake, kwani atakuwa mtu mzima siku moja naye mazoea ya nyumbani yanaweza kukuhatarishia ndoa yako. Namfahamu mtu mmoja ambaye alilazimika kuendelea kuzaa na shemeji yake kwa sababu mama alienda safari akawaacha mr na mdogo wake mtu mzima nyumbani, uvumilivu ukawashinda na ikawa hiyo ndiyo habari. Bahati nzuri mama alipokujatambua kuwa mdogo ana mimba ya mumewe alifurahia sana kwa kuwa yeye mwenyewe hakujaliwa kupata mimba, watoro mpaka leo wanadhani mama yao ni yule mkubwa na aliye mama yao hasa wanamwita dada kwa heshima ya dada mkubwa. Ni wachache wenye bahati hiyo.
 
https://www.jamiiforums.com/members/lekanjobe-kubinika.html Kila option ina risk zake. lakini risk kubwa ni kutokuwa na correct info na background za huyo HG. kuwa na HG ambaye hajui japo kidogo culture, cutom, beliefs za origin yako tena aje kulea mtoto mchanga ni big risk. Mke au mume inabidi 1ja achukue wajibu huo.

The best way to me siku ikilazimika kuwa na House girl ni mimi au mke wangu kuwatumia wakubwa wetu wa kijijini wanitafutie msichana aliye tayari katika familia yoyote kijijini. sio lazima we ndugu.

Sometime naona serikali inakurupuka kusema watoto wa under 18 wasiajiriwe. village kwetu kuna shule darasa la saba wakichaguliwa wanafunzi wengi ni wa3. wanaobaki wachache wanaendelea na private. watoto wa kike hapo kinachobaki ni kuolewa na kutumiwa tu na kupewa mimba.

serikali ilitakiwa kuweka sheria za kuwafanya watoto wa aina hii wanaokuja mjini kufanya kazi hawanyanyaswi. May be kungekuwa na Register ya familia zenye ma HG wenye wasichanawavulana ambao ni btn 14-19. Nasema 14 sababu na aasume by 14 amemaliza la saba si mototo asiyweza kufanya kazi.
 
Ndg zangu.mie ushauri wangu ni huu, Tumtangulize Mungu ktk kila jambo_Omba Mungu akupe watu wazuri wa kufanyanao kazi, kwani tatizo sio mahausi geri tu, hata watumishi wengine baadhi yao ni balaa kabisa.Hebu tuwemakini lakini cha zaidi Tumuombe Mungu sana,ili atuepushe la mabalaa mbalimbali.
 
Ndg zangu.mie ushauri wangu ni huu, Tumtangulize Mungu ktk kila jambo_Omba Mungu akupe watu wazuri wa kufanyanao kazi, kwani tatizo sio mahausi geri tu, hata watumishi wengine baadhi yao ni balaa kabisa.Hebu tuwemakini lakini cha zaidi Tumuombe Mungu sana,ili atuepushe la mabalaa mbalimbali.

:clap2::amen:

Lakini mbona unajitia kiberiti... vp?
 
Back
Top Bottom