Tujifunze nini kutoka wa Wachaga?

tujifunze kutoishi mbali na kwetu,ili iwe rahisi kurudi kutembea na kusalimia.
wachaga hawaendi mikoa ya mbali na moshi huwa wapo jirani kama dar ambako nauli ya chini inaanzia elfu 15 au 20.huwezi kukuta mchaga anaishi bukoba,kigoma au tabora akaenda uchagani kila mwisho wa mwaka.na ni wachache wanaoishi huko.
 
Kwenda moshi ni sawa lakini kupandisha nauli holela si sawa, na kukubali nauli hizo kupandishwa hovyo kisa mmevuna sana huku dar ni makosa lazima muende moshi kwa kiwango kilekile kilichowekwa na mamlaka husika...kwasababu mnakuwa na shauku ya kuhesabiwa mpaka ukitajiwa elfu 40 au 50 mnalipa...aisee babaangu nitalipa we nipe tu hiyo tiketi msee....
 
Kurudi home kwa kipindi cha mwisho wa mwaka ni jambo zuri sana. Si Wachagga tu hata WAZUNGU PIA. Kuna wakati Easter ilinikuta Norway na watu wa kule walituonyesha kuwa ni zaidi ya Wachagga. Ofisi zote za Norway zinafungwa wanaanchwa walinzi na baadhi wa watoa huduma wa lazima tu. Wengine wote wanakwenda nyumba za milimani ambazo ziko huko vijijini kwao. Wao tofauti na wa Wachagga, familia zote zinatoka mjini na wanaenda kukutana huko shamba. Nilipenda ile style maana hakuna kutoa sababu hapo familia nzima inakutana kwa kipindi cha kuanzia wiki moja hadi mbili. Niliipenda sana ile. Chaggas stand up and rush Migombani!!
 
Hapa sasa Wachaga ndio wanendeleza Sikukuu huko sidhani kama hii migomba ni ya Bagamoyo
 
tujifunze kutoishi mbali na kwetu,ili iwe rahisi kurudi kutembea na kusalimia.
wachaga hawaendi mikoa ya mbali na moshi huwa wapo jirani kama dar ambako nauli ya chini inaanzia elfu 15 au 20.huwezi kukuta mchaga anaishi bukoba,kigoma au tabora akaenda uchagani kila mwisho wa mwaka.na ni wachache wanaoishi huko.
una uhakika?Kuna mahali hakuna wachagga? Nenda hata Msumbiji walikokataliwa na marehemu Samora Machel utawakuta wamejaa tele... nenda Sumbawanga -Nkasi ..nenda Chunya utawakuta... wao riziki ni popote.
 
Sijawahi kwenda kijiji nisikute mchaga kama anabisha na hilo ataje hichokijiji twende tukaulizie .....
una uhakika?Kuna mahali hakuna wachagga? Nenda hata Msumbiji walikokataliwa na marehemu Samora Machel utawakuta wamejaa tele... nenda Sumbawanga -Nkasi ..nenda Chunya utawakuta... wao riziki ni popote.
 
Upendo, Umoja, Bidii katika kazi, Pia hawa jamaa huwa wanapenda kumsaidia mtu namna ya kutafuta na kufanikiwa. (Hawakupi samaki ila wanakufundisha na kukuwezesha kuvua)
 
Kutambika kunamaana nyingi.But wachagga wanaenda kutumia na familia zao, ukoo wao kile walichokichuma mjini.Bible say: Utachumia ugenini utalia nyumbani,Pia Mithali imesisitiza umuhimu wa kurudi na kukaa katika ardhi ya mababu kani huko ndiko baraka ziliko na katika udongo wa ardhi ya babu zenu ndiko baraka itakapoandikwa kwa wale wakristo mnaweza soma biblia kitabu cha mithali utakuta mambo mengi ambayo wachaga wanayazingatia...na ukifuatilia mahubiri ya Mwakasege utaona jinsi gani amewazungumzia wachaga kuhusu ardhi na uzao wa kwanza.
MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU WACHAGA
-Hawauzi ardhi ya urithi ni mwiko kufanya ivyo tapoteza utajiri na baraka zote
-Hautakiwi kuwa nje ya ukoo na unashiriki kikamilifu shughuli za ukoo hata kama unakaa mjini.
-Mgeni hapewi jina la ukoo pindi anapoomba kuwa mwana ukoo, kwani kufanya hivyo ni sawa kuuza thamani ya wazawa wakwanza
-Unapomaliza std 7 unaanza kujitegemea kuanzaia malazi na makazi
-Usipo jenga nyumba yako pindi unapofariki au mtoto wako anapofariki utazikwa ktk shamba lako hata kama ni pori na maiti haitaingia katika nyumba ya mtu mwingine hata kama ni kaka yako au mwanao isipokuwa yule ambae hajawa na familia bado.
-kama mzazi hana shamba au mali nyingi za urith mtoto wa mwisho wa kiume ndiye atakae rithi mali zilizopo na atapewa jukumu la kuwaangalia wazee nyie wengine mtaenda kujitafutia chenu na familia zenu. Mtasaidia wazee pale inapolazimu na kama shukrani kwa mzazi lakini yule mdogo ndiye mwangalizi wa wazazi kwa asilimia kubwa labda tu awe mzembe.
-Hutakiwi kuogopa kuishi katika mazingira tofauti ivyo lazima utoke siokukaa kijijini,ila sharti mwezi wa kumi na mbili urudi ukakutane na ndugu zako mjadiliane na kushukuru pamoja
-MWEZI WA KUMI NA MBILI NI MWEZI WA KWENDA KUTOA MICHANGO MBALIMBALI KANISANI NA KWENYE UKOO
-
-
 
Nimegundua wote mnaochangia hii kitu ni wachaga, hamna hata mmoja anaponda!
Anyway,let's stay positive, kwanza christmas kinapatikana Kilimanjaro kwani hata waliopo Arusha nauli ilikua Tsh.5000 kwenda hapo Moshi
Pili, wanaenda kufanya evaluation ya mwaka mzima, mazungumzo kama haya huwa yanakuwepo katika familia "hivi wewe Rafaelii umekaa daslam mwaka mzima hata kiwanja haunaa, unafanya nini? si bora urudi kijijini kumsaidia mzee kulima mashamba" hii huwa inawapa vijana changamoto na kurudi kupambana hadi wakamilishe hiyo target.
Mind you, that is from experience!
 
Kutambika kunamaana nyingi.But wachagga wanaenda kutumia na familia zao, ukoo wao kile walichokichuma mjini.Bible say: Utachumia ugenini utalia nyumbani,Pia Mithali imesisitiza umuhimu wa kurudi na kukaa katika ardhi ya mababu kani huko ndiko baraka ziliko na katika udongo wa ardhi ya babu zenu ndiko baraka itakapoandikwa kwa wale wakristo mnaweza soma biblia kitabu cha mithali utakuta mambo mengi ambayo wachaga wanayazingatia...na ukifuatilia mahubiri ya Mwakasege utaona jinsi gani amewazungumzia wachaga kuhusu ardhi na uzao wa kwanza.
MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU WACHAGA
-Hawauzi ardhi ya urithi ni mwiko kufanya ivyo tapoteza utajiri na baraka zote
-Hautakiwi kuwa nje ya ukoo na unashiriki kikamilifu shughuli za ukoo hata kama unakaa mjini.
-Mgeni hapewi jina la ukoo pindi anapoomba kuwa mwana ukoo, kwani kufanya hivyo ni sawa kuuza thamani ya wazawa wakwanza
-Unapomaliza std 7 unaanza kujitegemea kuanzaia malazi na makazi
-Usipo jenga nyumba yako pindi unapofariki au mtoto wako anapofariki utazikwa ktk shamba lako hata kama ni pori na maiti haitaingia katika nyumba ya mtu mwingine hata kama ni kaka yako au mwanao isipokuwa yule ambae hajawa na familia bado.
-kama mzazi hana shamba au mali nyingi za urith mtoto wa mwisho wa kiume ndiye atakae rithi mali zilizopo na atapewa jukumu la kuwaangalia wazee nyie wengine mtaenda kujitafutia chenu na familia zenu. Mtasaidia wazee pale inapolazimu na kama shukrani kwa mzazi lakini yule mdogo ndiye mwangalizi wa wazazi kwa asilimia kubwa labda tu awe mzembe.
-Hutakiwi kuogopa kuishi katika mazingira tofauti ivyo lazima utoke siokukaa kijijini,ila sharti mwezi wa kumi na mbili urudi ukakutane na ndugu zako mjadiliane na kushukuru pamoja
-MWEZI WA KUMI NA MBILI NI MWEZI WA KWENDA KUTOA MICHANGO MBALIMBALI KANISANI NA KWENYE UKOO
-
-

Chechekali hapa umenikuna kabs!!

Kwa kweli yako ya muhimu hapa kama kwenda kuona wenzako wanafanya nini, kupata baraka za wazee! kumbuka msahau kwao anakuwa mtumwa katika nchi ya watu!!
 
Kwa ushauri wangu, usijifunze toka kwa wachaga in general, utapotea!!!
Iga tabia ulizoona nzuri kutoka kwa watu unaokutana nao WEWE, achana na sifa na maneno ya magazeti, mengi ni uzushi tu.
Ila kama una mtu unayemjua jifunze kwa kumuuliza alianzia wapi, anafanyaje, ana sacrifice nini, uangalie kama kuna relationship na jinsi maisha yako yalivyo sasa.
Mfano,
-kwenda Kwao mwisho wa mwaka- je umeacha ndugu muhimu kwenu, kama hakuna sasa utaenda kufanya nini? wengine wamezaliwa mijini toka enzi na enzi.
Kuna mila fulani kwetu inayokataza mtu kuchinja bila kaka zake kuwapo, hii mwanzo ilikuwa ni kwa matambiko, ila kwa sasa naona wanataka kuhakikisha kila mtu anakuwapo, muda mzuri ni Xmas, hata kama huchinji kwa kuwa huna sababu mfano kupata mtoto, labda kipaimara au kupeleka mke au kumbukumbu ya harusi, basi lazima ufanye heshima yakwenda kwenye shughuli ya kaka zako.
In short ni kama lazima fulani hivi au uwe mbishi tu, au uwe na dharau kwa ndugu zako au uwe na sababu ya kazi au kipato. Wengine hawapendi ila wanalazimika kwa ajili ya kuheshimu ndugu zao tu.

hii nayo imekaa vizuri
 
daah hii thread ilivyoanza nilifikiria tunatafuana maneno, lakini this i very serious busness to learn!! big up it has reminded me alot
 
Kwenda moshi ni sawa lakini kupandisha nauli holela si sawa, na kukubali nauli hizo kupandishwa hovyo kisa mmevuna sana huku dar ni makosa lazima muende moshi kwa kiwango kilekile kilichowekwa na mamlaka husika...kwasababu mnakuwa na shauku ya kuhesabiwa mpaka ukitajiwa elfu 40 au 50 mnalipa...aisee babaangu nitalipa we nipe tu hiyo tiketi msee....
mchezo mchafu sana pale unachezekaga, ticket zinanunuliwa na mtu mmoja kwa bei ya kawaida then yeye anaanza kuuza kwa bei yake anayoitaka, mie wananiudhi kweli, ukienda oficin gari imeaja, kwenye gari ticket zinauzwa!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom