Tujifunze kupitia kisa cha ''mtego wa panya" anaandika Amani Msumari

Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,830
976
Ndugu zangu wasomaji ni ukweli usiopingika kuwa hadithi zinakuwa na malengo ya kuonya, kufundisha na kuburudisha. Wazee wetu walitunga hadithi hizi ili ziweze kusaidia vizazi vilivyopo na vijavyo. Twende pamoja kwenye hadithi hii ya zamani kabisa iitwayo mtego wa panya.

Siku moja mwenye nyumba alirudi nyumbani na kutega mtego wa panya kwa lengo la kukamata panya ili aondoe kadhia hiyo nyumbaani kwake. Kwa bahati nzuri kabisa Bwana Panya alikuwa amejificha sehemu fulani huku akishuhudia tukio zima la utegaji wa mtego ule. Basi mara baada ya mtego kutegwa Bwana Panya huku akitetwa alikimbia huku na huko akitafuta msaada wa jamaa zake ili kwa pamoja waweze kuutegua mtego ule.

Bwana Panya akimfuata ndugu jogoo ili wasaidiane, jogoo akacheka sana na kumwambia Panya kuwa hilo ni tatizo lake na yeye halimhusu. Panya hakuchoka akmfuata anko Mbuzi a.k.a kaka beberu ambaye naye kama jogoo alisema hahusiki na matatizo ya ndani ya nyumba, hilo ni tatizo la panya na ahangaike mwenyewe kulitatua. Kutokana na kuiona hatari hiyo, Panyaa akapiga hodi hadi kwenye zizi la bradha Moo a.k.a Ng'ombe. Ng'ombe aliposikiliza habari hiyo alikasirika sana na kumfukuza panya kwa kumpotezea muda kumueleza vitu visivyomuhusu. Basi panya akaondoka na kwenda kujitafutia riziki yake maporini.

Muda si muda shangazi nyoka akaingia ndani ya nyumba na kuja kutahamaki mtego umemnasa mkiani. Nyoka akahangaika wee kujiokoa ila wapi akashindwa hivyo akabaki amevimba kwa hasira na uchungu wa maumivu. Mida ya jioni mwenye nyumba akarudi. Alipofika eneola mtego hamadi nyoka akamuuma. Sumu kali ya nyoka ikamfanya apige kelele na kupoteza fahamu. Majirani wakaja, wakamuua nyoka na kumchukua mgonjwa na kumpeleka hospitalini.

Baada ya muda mgonjwa akapata nafuu na kuagizia aletewe supu ya kuku. Jogoo akchinjwa na supu akaletwa. Baada ya muda hali ya mgonjwa ikabadilika na hatimaye akafariki dunia. Maiti ikiwa chamba cha kuhifadhia maiti waombolezaji wachache wakafika msibani na hivyo kutokana na idadi yao ikabidi wachinjiwe mbuzi. Siku ya msiba watu walikuwa ni wengi sana hivyo ng'ombe akachinjwa. Bwana Panya alikuwa akifuatilia matukio yote kwa mbali huku akiwasikitikia jamaa zake.

SOMO:
1. Wema hauozi, wema ni akiba
2. Mwenzako akinyolewa zako tia maji
3. Maisha ni kutegemeana

JE, WEWE UMEJIFUNZA NINI?
 
Back
Top Bottom