Theodora
JF-Expert Member
- Dec 20, 2009
- 802
- 570
Wakuu asalaam aleykum;
Jana katika pitapita yangu nikatua kwenye nyumba ya ibada ili kujiandaa vyema kwa ajili ya hiki kipindi cha kwaresma
wakati wote huo akili yangu ilikua fast iki-reflect jinsi maisha yanavyoenda, kazini, starehe, michezo (kidogo) na more important loved ones. Baada ya muda, (kwakweli ilifika wakati nikawa navusha hadi kupoteza kabisa ibada yenyewe); nikaona ngoja nijaribu kuweka mbili tatu ziwe agenda japo kwa siku kadhaa.
hivyo basi, naomba ndugu za ngu tuwe pamoja kwenye hili na tujitahidi (kwa wale wanaoweza) kuboresha imani na matendo japo kwa mwezi tu ili tuanze maisha matamu zaidi
- kupunguza tungi kwa zaidi ya 50% maana kwa sasa hazipiti siku mbili mtu lazma ushtue tena si kidogo
- kuwahi hom ili kujiweka vizuri na kamanda
- kuanza mazoezi ya nguvu ili kuondoa hizi love handles ambazo kwa jinzi zinavyokuwa kubwa mtu unaweza hata kuanikia combat la jeshi
- kubadili kidogo mlo ili kusafisha ini na viungo vingine
- kuepuka kabisa mazingira hatarishi yanaweza kuchochea kale kamchezo
Its all about love, au sio?
Maoni na ushauri mzuri. Lkn naona labda isiwe tu kwa ajili ya kwaresma iwe siku zote. Ikiwa tu kwa ajili hii to me it sounds like pretence....Lets be real, maana haya ni maisha not a rehearsal.
Mungu hadanganyiki.