Tujadili mila, jadi na desturi za wachagga

wachagga mpo, nawapa na zawadi yenu hii hapa

banana.jpg

ndizi mshare.jpg
 
Mkuu kwa kiswahili anaitwa komba...
sidhani, komba kichaga chake ni "ngaawa"

Tena hiyo avatar yako Lady N imenikumbusha siku nilipo goma kwenda shamba nikapanda kujificha juu ya kai huku nikizishambulia hizo ndizi hadi nikalala huko kiruu !!! waliporudi shamba c wakawa wanapika hapo kwa chini sasa shida ni ule moshi uliokua unapanda kule aisee nilijikabidhi polepole tu walinipa kichapo mbaya jamaangu.
pole sana sana, na ivi wanaweka mashiwa hapo chini ya dari kabisa ili ndizi iive haraka, "nulela kura mtsu?"

hivi kisusio cha kitimoto kinaitwaje?
na kukaa kwangu kote moshi sijaona kula kisusio cha nguruwe
 
Ukimpiga mkeo usiku akapiga yowe basi wazee wanakuja wanakamata ng'ombe au mbuzi wanachinja usiku huo huo na kumla. Kama huna basi ujue utapigwa au utoe pesa watu wakaburudike. Infact hairuhusiwi kupiga mkeo usiku.
Baadhi ya vyakula vya asili:-
-kiburu(kiumbo)
-machalari(ndizi)
-kitawa(ndizi zilizopikwa zikasongwa na kuchanganywa na maziwa mgando)
-kimamtine(damu iliyochanganywa na maziwa mgando)
-ngararimo(mahindi yaliyopikwa bila kukobolewa yakachanganywa na maharage)
hapo kwenye red napinga kwa nguvu zote, kimamtune kinapikwa kama kiburu(kyumbo) tofauti yake ni kwamba hakima maharage hichi na huwa wanapewa sana watoto

hivi pia ni baadhi tu ya vyakula vya uchagani
meeba tsa mmbala
somi
malopa
nb vyakula vyote hivyo vinawekwa magadi
 
Naombeni kujua maeneo mazuri Moshi ya kwenda kupumzika na watoto.
 
wachaga maarufu na sehemu walizotoka

kibosho - alex masawe, babu sambeke
vunjo - agustino mrema
machame - r. Mengi, f. Mbowe
marangu - +kibo and other marealles
rombo - b mramba
old moshi - mama mkapa
uru - :eek:

wana jf ongezeeni hapa.
Aina ya watu inaweza kutupa tabia za wastani za watu wa sehemu fulani

michael ngaleku shirima- precision air
 
Wakiruai na Wamwika wanakuwa kwenye kundi lipi la wachaga?

a.Wakibosho b.Wahuru c.Wamachame d.Wamarangu e.Warombo f.Wasiha
 
-kimamtine(damu iliyochanganywa na maziwa mgando)

kimamtune = kinapikwa kama kiburu (kiumbo) ila hakina marahage (soko)

mlaso = damu iliyochangaywa na maziwa mgando na mafuta = maalum kwa mama aliyetoka kupata mtoto.
 
Naombeni kujua maeneo mazuri Moshi ya kwenda kupumzika na watoto.

tumwombee buji arudi salama atakuambia mahali pazuri pa kuipumzisha mwili/roho yako, vipi kule arusha haukufanikiwa au walikurusha.
 
yule aliyekua mke wa Dkt salmin Amour si mu Uru? na Hugo kissima ni mu uru
 
unajua ni kwanini???
ukimfanyia mtu ubaya kuna dua fulani wanaombaga wanaita (kupiga NUNGU) wakishapiga hiyo kama familia wanakufa wote basi yule wa nje ndo atasalia

Very good strategy
 
Mkuu unaweza kunieleza kwa nini wakibosho,wanarumu,wa-uru,na warombo walinyimwa elimu?
nikiangalia hayo maeneo roman catholic wamejikita sana,
lakini ukija machame na marangu kuna lutheran ambayo imejenga shule nyingi,

mbona mimi mrombo af nna bonge la elimu!!! vp ww?
 
Jaman wapi Susuviri na ndokororo?
hon'ga=kumbikumbi
mang'arwa=mchwa wakubwa waishio kwenye kichuguu..hawa viumbe wamentesa sana enzi zangu za kutafuta kumbikumbi miaka hiyooooo.
 
Back
Top Bottom