Tujadili mechi ya Simba Vs Yanga leo

INASIKITISHA: Baada ya mechi nilikua napita maskani flan hivi. Nkaskia washkaj wakiskitika kumpoteza rafiki yao mshabiki wa Yanga.
Marehemu alikua akichek game uwanja wa Taifa. Alianguka ghafla baada ya mpira kuisha. Jamaa wanahisi marehemu hakutegemea YANGA kuibuka na ushindi. Plus na matitizo yake ya Low blood pressure, basi huduma ya kwanza waliompa wale marafiki zake pale uwanjan wala haikuzaa matunda. Mauti yakamkuta pale pale.
Namwombea Marehemu a-rest in peace. Mara ya mwishokusikia m2 kufa kwa upenzi wa timu ni yule jamaa wa Nairob shabiki wa Arsenal kujinyonga baada ya th gunnerz kutolewa champs league na liva if am nat mistaken. Jaman 2sishabikie timu ze2 kupita kiac. 2naweza hatajitaftia magonjwa ya pressure bureee!
Asanten
 
12_09_t6jwrm.jpg


















12_09_8htjf2.jpg










TEAMS:
Yanga: Yaw Berko/Obren Curkovic, Nsajigwa Shadrack, Amir Maftah, Bakari Mohamed, Nadir Haroub, Athumani Idd, Nurdin Bakari, Abdi Kassim/ Shamte Alli, Jerryson Tegete, Mrisho Ngassa, Kigi Makassy/ Godfrey Bonny.

Simba: Juma Kaseja, Salum Kanoni, Juma Jabu, Kelvin Yondan, Joseph Owino, Jery Santos/ Ramadhan Chombo, Hilary Echessa, Mohamed Banka, Mussa Hassan/ Mike Baraza, Emmanuel Okwi/ Mohamed Kijuso, Haruna Moshi.


Wacha1
Asante sana mkuu, nakupa tano kwa tano!
 
Hongereni watani zetu yanga kwa kupata ushindi mliostahili!!! Mlicheza mpira mzuri na hii itatufungua macho wanasimba kujipanga zaidi kwenye ligi
 
Ni muda mrefu nilikuwa siangalii mpira wa Simba na Yanga lakini kiwango kilichonyeshwa na timu hizi juzi kimenifanya nibadili mawazo. Kwa sasa hizi timu zinacheza mpira wa kisasa ,wachezaji wanatoa pasi za uhakika nathubutu kusema Simba na Yanga wanacheza vizuri kuliko hata TAIFA STARS. Nawapa hongera makocha wa timu hizi Patrick Phiri na Kostadin Papic , namshauri MAXIMO awe anashirikiana na noa watamsaidia sana.Kuhusu mechi ya juzi
SIMBA
Walicheza kwa kujiamini sana wakijua Yanga ni vibonde wao,kuingia kwa Redondo kulileta matumaini kwenye safu ya kiungo.
Haruna Moshi anatakiwa apewe ushauri aache mambo ya kijinga yatamuaharibia future yake kwenye soka
YANGA
Pongezi ziende kwa magolikipa na Nadir Haroub Canavaro-huyu jamaa alivyoondoka kweli aliacha pengo.Ngasa alikuwa anapiga krosi nyingi sana zinaenda nje nafikiri bado kuna tatizo la maelewano ya viungo na washambuliaji
Pongezi kwa PAPIC kuchezesha wachezaji wa nyumbani
 
Wakuu naomba nitoe assessment yangu ya mpira wa jana, naona wengi wetu tunapelekwa zaidi na ushabiki kidogo kuliko upenzi wa mpira wa miguu, na kwa bahati mbaya siku hizi hata waandishi wa habari hawatoi in depth analysis ya mpira kama ilivyokuwa zamani. Ntaanza kama ifuatavyo;
1. Yanga.
Walionekana kucheza mpira ambao sijawahi kuona wakiucheza, naweza kusema sio 'culture' ya Yanga kucheza a passing football. Hayo ni mabadiliko makubwa sana niliyoyaona kwa Yanga. Pia walikuwa wanakaba sana meaning kwamba walikuwa hawaachi nafasi kwa wachezaji wa Simba kucheza na mpira, na huo ndo mpira wa kisasa, unapokuwa na possession unacreate a lot of space to pass the ball around na unapopoteza you close all spaces ili mpinzani wako ashindwe kuuchezea mpira. Tatizo ambalo nililiona kwa Yanga ni kuwa wachezaji wa mbele walikuwa wanashindwa kupata ujanja wa kuipenya ngome ya Simba na hivyo kuishia kupiga mashuti ya mbali ambayo mengi yalikuwa yanatoka nje. Kwa hiyo kwa ujumla Yanga walikitawala vizuri kipindi cha kwanza.
2. Simba
Walikuwa surprised kidogo na kiwango cha Yanga na kidogo hasa katika kipindi cha kwanza wakashindwa kucheza mpira mzuri wa pasi. Mara nyingi walikuwa wanakosa nafasi za kupasiana kutokana na style ya Yanga ya kukaba sana. Katikati walipwaya sana katika kipindi cha kwanza. Katika kipindi cha pili ndo tuliiona Simba yenyewe ikicheza mpira wa kasi na wa pasi ambazo ziliwachanganya kabisa Yanga. Na natofautiana na mwana JF mmoja aliyesema kuwa Redondo ndiye aliyebadilisha mpira wa Simba, hapana, ni Mike Barasa ndiye aliyebadilisha kabisa midfield ya Simba, na nadhani pia Kocha Phiri alikosea kumtoa Mgosi labda kama alikuwa ameumia, lakini kwa uchezaji ule wa kipindi cha pili kama Mgosi angekuwepo angeleta shida sana langoni kwa Simba.
Conclusion:
Kwa jinsi timu zilivyocheza nadhani timu yoyote ilikuwa na haki ya kushinda ile mechi, nadhani Simba watabidi wajilaumu sana kwa kuwa na mchezaji mzuri lakini muhuni na selfish ambaye hajui maana ya team work na ushindi ni nini, huyu ni Haruna Moshi. With all respect to Haruna Moshi i think huwa anawapa wakati mgumu sana wachezaji wenzake kukabiliana na pressure baada ya yeye kutolewa kwa utovu wa nidhamu. Kwa Simba itakuwa si busara kuendelea kumtetea Haruna, ni lazima akubali kuwa professional vinginevyo hata future yake hulo Ulaya siioni kwa tabia hii. Kama mechi ya Simba na Yanga inamshinda atawezaje kucheza mpira sehemu ambayo anaweza kuitwa nyani tangu mpira unaanza mpaka unaisha? Namshauri abadilike vinginevyo he is gone...otherwise credit kwa Yanga kushinda na credit pia kwa kocha wao kuwaeza kubadilisha mpira wao wa kupiga na kukimbia, kama wataendelea hivi basi tutakuwa tunaona mpira safi kati ya Yanga na Simba cos Simba kupasiana is part of their culture. Ni hayo tu wakuu.
 
Chesty nakubaliana kabisa na wewe, Phiri alikosea kumuanzisha Jerry Santo na akagundua mapema na kumuingiza Kanoni.Kweli Baraza alibadilisha timu ya Simba jamaa ana-control na ana-confedence.Haruna Moshi hakuna haja ya kumtetea
 
Back
Top Bottom