Tujadili mechi ya Simba Vs Yanga leo

bado tutawanyonga tu. subiri dakika zisogee litarudi na tunaongeza
 
njama tuu hizo...from prev records he is always red carded against yanga...
Ufisadi wa manji hizo...ushindi unakwenda msimbazi tuu na huyo refa lazima achapwe bakora tuu leo..tunamsubiri baada ya mechi maana tulishasema ujinga wa refa hatutavumilia

Refa angekuwa na njama si angewanyima penati? na gemu lingekuwa limekwisha. Sema anawabeba lakini hambebeki, inabidi tu afanye kazi aliyotumwa. Simba nje tu leo.
 
Refa Katubeba tumeshindwa kubebeka nipo uwanjani ......Boban bado mshamba saaana ana mambo ya kitabora mpaka leo mpira utamshinda hata huko ulaya aaaaache bangii bao la ngasa pia lilikuwa zuri tuwache unazi leo jamaa walitukamata siku yao
 
lile la ngasa refa kalikata lakini pia halikuwa na matatizo nadhani kuna haja ya kuangalia wa kumpata kiungo mwingine tafouti na jerry santo
 
Kama Yanga kashinda wataweza kupita msimbazi? Maana tetesi zinasema watapigwa mawe! Mipira ndiyo hiyo ya Bongoland. Tunasubiri ma-pundit walioshuhudia mpambano huu.
 
Sasa tunawataka hao mapaka wanaokaa kwenye masofa. Wamezoea kutoa dozi, wacha sisi tuwaonyeshe soka la bongo.
 
oyaaa waganga wa kienyeji uchwara mliotabiri mechi itaisha ndani ya dkk 90, mmenoa. 1-1, na sasa zinaongezwa 30 min.
 
siku za karibu na sikukuu huwa ni mbaya kwa wanyama
huwa wanachinjwa
siku za karibu na sikukuu huwa ni nzuri kwa kandambili
huwa hazivaliwi
(badala yake vinavaliwa viatu)


YANGA HOYEEE!
 
Back
Top Bottom