Tujadili ifm sasa.......

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
353
Zimekatwa sana issue za UDSM na Mzumbe hapa lakini naona tumekasahau haka ka institute kalikopo mtaa wa Shaaban Robert. Nimeskia mengi sana kuhusu hiki chuo yakiwemo ya walimu kufanya biashara ya kuuza mitihani esp. supplimentaries, na walimu haohao kuonyesha udhaifu wa kutisha kwa mabinti wanaosoma hapo.

Wafanyakazi vilaza wa BOT na TRA ndio wana reputations kwenye suala la kununua mitihani, jambo ambalo linawakera wanafunzi wengine ambao wanakesha usiku kucha wakisoma wakati wenzao wanakunywa bia. Na kwa kuwa masista duu wengi wanauelewa udhaifu wa walimu wao, wamekuwa wakitumia mwanya huo kujipata vyeti kiulaini na kuendelea kujaza maofisi yetu kwa diploma na advanced diploma za chupi.

Uozo huu na mingine mingi inayoendelea kwenye kachuo hako ulipelekea Mkuu wa Chuo hicho kuondolewa, inaeleweka pia kwamba Bw Madofe naye alikuwa ni mtu wa kuendekeza sana sketi chuoni hapo. Je Principal mpya- Prof Doriye atamudu kusafisha uchafu ambao umelundikana chuoni hapo kwa muda mrefu?
 
Je Principal mpya- Prof Doriye atamudu kusafisha uchafu ambao umelundikana chuoni hapo kwa muda mrefu?

Prof Doriye sio Principal mpya pale IFM, ni wa zamani na muda wake uliisha mwaka jana. Sasa hivi bado yupo pale kwasababu anamalizia Project zake za kutengeneza majengo ambazo hazijaisha (as if hakuna wengine wanaoweza).
 
Nawakumbushia si unajua shuleni unafundishwa darasani halafu halafu unajisomea, inakiuja TEST1, TEST2 halafu final Exam una-supp unarudia mtihani una-supp sup halafu una-carry mzunguko unajirudia tena. Ukizubaa unadisco.
Anamaliza project kuwa-carrisha tu kozi.

Conlusion: Repeatition allowed.
 
kusafisha uchafu ambao umelundikana chuoni hapo kwa muda mrefu?

Be specific bas.
Muda mrefu ni muda gani na Uchafu ni uchafu gani. kama ni ishu za kuuza mitihani ni ujinga na uzembe wa lecturer. Kila jamii ina kasoro zake. Huwezi kuondoa zote.
 
Back
Top Bottom