Tujadili huu mpango biashara (business plan) wa kuku wa kienyeji

Pawaga

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
1,330
966
Mapambano bado yanaendelea wakuu,
ninajishughulisha na ufugaji wa kuku kwa kipindi kirefu sasa. Nimeamua sasa kufanya shughuli hii kitaalam ndipo nikachanganya madesa tofauti tofauti na kupata mpango biashara huu,tafadhari naomba tujadili kwa wale wataalam watoe mapungufu na marekebisho muhim.
karibuni sana nipo tayari kupokea changamoto
nimeattach file katika format mbili yaan word dic na PDF uchague inayokufaa
 
Attachments

  • poultry.docx
    32.1 KB · Views: 819
  • poul pdf.pdf
    103.6 KB · Views: 801
umejitahidi sana ila bado haujakaa vizuri kuwa na section ya Uzalishaji uanze na kusema sehemu ya mradi ni muhimu kujua sehemu ili kuona aina ya mabanda (sehemu za joto vs baridi) n.k sema aina ya kuku (breeds) na sifa zake ili uweze kusema kila mzao atataga mayai mangapi, ataangua mangapi na watafikia maturity wangapi (mortality rates), hujasema wakianguliwa watalelelwaje waatachwa na mama zao ama watanyanganywa na kulelelwa tofauti.

kuku wengi wanapoteza sifa ya ubora kwa sababu ya in breeding yaani baba anazaa na mtoto, mama anazaa na mtoto etc mpango wa kubadili majogoo na majike unakuaje,

kuhusu mpango wa chanjo na kinga je utakuaje (kila eneo lina mlipuko kipindi fulani), je madawa hayo ni yapi na yanapatikana wapi au karibu na mradi?

Pia kuku unawafuga kwa style gani (utawafungia ndani muda wote na kuwalisha ama utawaachia na kuwapa supplementary feeding) etc

Gharama za uendeshaji
  • gharama za chakula ni kiasi gani kwa jumla na kuku mmoja kwa umri tofauti
  • gharama za madawa
  • gharama za wafanyakazi
  • Gharama za umeme, maji, ulinzi, stationery, simu etc
  • ghrama za mikopo (riba) na assets (depreciation)

Mpango wa Fedha:

Thamani ya uwekezaji (ardhi, mabanda, nyumba za wahudumu, fence, vifaa vya kulishia, magari etc)
mapato na matumizi (unatakiwa uandae Profit and loss account), Cash Flow and Balance sheet

mazingira

Utatunzaje mazingira? kama unafuga maeneo ya mjini utakabilianaje na suala la harufu mbaya, utupaji wa taka, zitokanazo na mradi wako etc

ukiboresha hayo utakuwa na mpango mzuri sana wa biashara
 
Chakula unaweza kuwanunulia mahindu ukayabaraza (kuyavunjanja) kisha ukachanganya na pumba, mashudu,chumvi,pumba lainina ya mpunga na vinginevyo kwani mahindi ni bei rahisi hasa kwa eneo utalofanyi mradi.
 
umejitahidi sana ila bado haujakaa vizuri kuwa na section ya Uzalishaji uanze na kusema sehemu ya mradi ni muhimu kujua sehemu ili kuona aina ya mabanda (sehemu za joto vs baridi) n.k sema aina ya kuku (breeds) na sifa zake ili uweze kusema kila mzao atataga mayai mangapi, ataangua mangapi na watafikia maturity wangapi (mortality rates), hujasema wakianguliwa watalelelwaje waatachwa na mama zao ama watanyanganywa na kulelelwa tofauti.

kuku wengi wanapoteza sifa ya ubora kwa sababu ya in breeding yaani baba anazaa na mtoto, mama anazaa na mtoto etc mpango wa kubadili majogoo na majike unakuaje,

kuhusu mpango wa chanjo na kinga je utakuaje (kila eneo lina mlipuko kipindi fulani), je madawa hayo ni yapi na yanapatikana wapi au karibu na mradi?

Pia kuku unawafuga kwa style gani (utawafungia ndani muda wote na kuwalisha ama utawaachia na kuwapa supplementary feeding) etc

Gharama za uendeshaji
  • gharama za chakula ni kiasi gani kwa jumla na kuku mmoja kwa umri tofauti
  • gharama za madawa
  • gharama za wafanyakazi
  • Gharama za umeme, maji, ulinzi, stationery, simu etc
  • ghrama za mikopo (riba) na assets (depreciation)

Mpango wa Fedha:

Thamani ya uwekezaji (ardhi, mabanda, nyumba za wahudumu, fence, vifaa vya kulishia, magari etc)
mapato na matumizi (unatakiwa uandae Profit and loss account), Cash Flow and Balance sheet

mazingira

Utatunzaje mazingira? kama unafuga maeneo ya mjini utakabilianaje na suala la harufu mbaya, utupaji wa taka, zitokanazo na mradi wako etc

ukiboresha hayo utakuwa na mpango mzuri sana wa biashara
asante sana mkuu Mungu akubariki kwa constructive ideas ulizotoa hapo,ntalifanyia kazi
 
unatakiwa uwe na makadirio ya miaka mitano sio mwaka mmoja kama ulivyofanya ili iwe strategic
 
Back
Top Bottom