Tujadili hoja na sio jaziba na chuki, Mh. MSIGWA

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,878
5,424
IMG_1923.JPG

Tunamshukuru Mungu kwa kutuweka hai. Wiki iliyopita swali langu limeleta gumzo na maneno ya jaziba na matusi dhidi yangu kwa baadhi ya watu waliodhani kuwa Mimi ni mpinzani wa dini ya kiislamu.

Niwashukuru wote miliotoa maoni yenu kwenye ukurasa huu, mazuri na mabaya, kutoka wa marafiki na maadui, kwani wote mmetoa. Lakini jambo moja ndugu zangu wantazania naomba tujifunze kujadili hoja sio jaziba na chuki.

Naomba tujifunze kuangalia mambo katika usahihi sio jaziba udini na itikadi, tujaribu kufanya observation iliyo sahihi kisha tufanye
interpretation sahihi inayotokana na observation kisha unajua kipi cha kufanya ambayo ni application itakayokuongoza kwenye
implementation.

Dini isitufanye Tusiwe na uwezo wa kufikiri, kuhoji au kudadisi, kwa wale wanoweza futilia historia someni reason age, philosophers wangi pamoja na wa kiislamu ambao walipinga kanisa lilipokuwa linalzimisha watu kutii bila kuhoji hiyo likuwa karne ya 18'ni ajabu tunataka turudi nyuma.

Ni uvivu wa kufikiri na Kuniita mdini eti kwa sababu imehoji mamlaka ya katiba na kuwa katiba imevunjwa kule Zanzibar na waziri
mkuu ameunga mkono uvunjaji wa katiba ambayo wote pamoja na yeye tuliapa kuilinda.

Siwezi ogopa kusema ukweli eti kwa sababu nitawaudhi watu Flani au dini Flani, swala la nguo sio ajenda hapa, hiyo ni zile tunaita cheap politics.

Ndugu zangu waislamu kawasomeni wale wanaoitwa Muslim modern philosophers, ambao walitoa mchango mkubwa sana katika
kipindi hiki kinachoitwa enlighment age au reason age

SOURCE: MH. PETER MSIGWA BLOG
 
Usinichukie kwa sababu ya dini yangu,timu yangu ya mpira,kabila langu,rangi yangu,chama changu cha kisiasa.
 
Zanzibar ni nchi ya Waislaam kwa asilimia zaidi ya 98 (98%).
 
Hii ndio taabu ya kuwa na mapadri, wachungaji na makatekista kwenye chama. Akili zao ni kupambana na uislamu.
 
Ni nchi iliyo na Waislam wengi wala si nchi yenye Kutawaliwa na Waislam. Acha Udini wewe angalia Reality

Udini uko wapi hapo? au ni uongo Zanzibar sio zaidi ya 98% Waislaam? mseme nyinyi tukisema sisi udini, wakati nyinyi ndio wadini wakubwa na mnachuki kila mnapoona neno Uislaam au Waislaam roho zenu zinawauma. Zanzibar 98% ni Waislaam kwa hiyo huwezi kwenda wewe na uchungaji wako ukawapangie wafunguwe hoteli za mitaani mwezi wa Ramadhan. Waislaam wana vigezo vyao vya Hoteli na Restaurants zipi zifunguliwe mwezi wa Ramadhan na kwa namna gani, kwani katika Uislaam kuna vigezo vya wasioweza kufunga kwa wakati huo, kama wagonjwa, wazee, watoto, wasafiri, wanawake walio kwenye siku zao. Wote hao wana ruksa ya kula mchana lakini kwa vigezo vyake, sio kwa kuwa wameruhusiwa basi wakae nje wale waziwazi.

Usomeni Uislaam muuelewe, umekuja kuwaokoa katika kufuru za kuabudu binaadam wenzenu kwa kuwafanya ndio miungu yenu. Uislaam haukulazimishi wewe uyafate mambo ya Waislaam na wala wewe usiwalazimishe Waislaam wafate utakavyo wewe.

Wacha kumsikiliza huyo mchungaji aliyekosa umaarufu kwa siasa safi anarukia kujitafutia umaarufu dini ya Wazanzibari, zote chuki kwa kuwa chadema hawana kiti hata ch akuombea maji Zanzibar.

Anajuwa akiuleta udini kwa Wazanzibari Waislaam wote wa bara na pwani hatutakaa kimya na ndicho anachokitaka kujitafutia umaarufu lakini hajui kuwa anazidi kukishindilia msumari chama chake kinachofata siasa za Kikristo kikisaidiwa na CDU ya Ujerumani.

Kaona Zitto hampati ki udini sasa anawachokoza Waislaam wa Zanzibar, asiwachezee Waislaam, akichokoza Muislaam mmoja ajuwe kachokoza Waislaam wote, amuulize Mwinyi, alizabwa kibao hadharani kwa kushadidia zinaa na kondom.

Na yeye asituletee udini wake. Atuwache Waislaam kama tulivyo. Amuulize Zena Kawawa, umesahau au hujui yaliyomkuta au Mrema, mpaka leo hana hamu ya kuwataja Waislaam. Acheze na kanisa na Wakristo asicheze na Muislaam au Uislaam, hatutamvumilia.

Hivi mna wabunge wangapi kutoka Zanzibar? kwi kwi kwi teh teh teh!
 
Hii ndio taabu ya kuwa na mapadri, wachungaji na makatekista kwenye chama. Akili zao ni kupambana na uislamu.
.

"...kazi yake , kama Makureshi wengine...kazi yake kubwa ilikuwa ktunga mashairi yenye kuhamasisha kupigana bila

kufikiri....."

Unajua kipande hiki nimekitoa wapi??

Usiendekeze ujinga huu wa kuwa mwepesi kuchukia mtu, kuamua, kupigana bila kufikiri.

.
 
Maendeleo gani yapo zanzibar Zomba??? Mnabalozi Ngapi Duniani?? Rais wenu Anatambuliwa na Umoja wa Mataifa??, Je wimbo wa Taifa ni Upi?
 
Udini uko wapi hapo? au ni uongo Zanzibar sio zaidi ya 98% Waislaam? mseme nyinyi tukisema sisi udini, wakati nyinyi ndio wadini wakubwa na mnachuki kila mnapoona neno Uislaam au Waislaam roho zenu zinawauma. Zanzibar 98% ni Waislaam kwa hiyo huwezi kwenda wewe na uchungaji wako ukawapangie wafunguwe hoteli za mitaani mwezi wa Ramadhan. Waislaam wana vigezo vyao vya Hoteli na Restaurants zipi zifunguliwe mwezi wa Ramadhan na kwa namna gani, kwani katika Uislaam kuna vigezo vya wasioweza kufunga kwa wakati huo, kama wagonjwa, wazee, watoto, wasafiri, wanawake walio kwenye siku zao. Wote hao wana ruksa ya kula mchana lakini kwa vigezo vyake, sio kwa kuwa wameruhusiwa basi wakae nje wale waziwazi.

Usomeni Uislaam muuelewe, umekuja kuwaokoa katika kufuru za kuabudu binaadam wenzenu kwa kuwafanya ndio miungu yenu. Uislaam haukulazimishi wewe uyafate mambo ya Waislaam na wala wewe usiwalazimishe Waislaam wafate utakavyo wewe.

Wacha kumsikiliza huyo mchungaji aliyekosa umaarufu kwa siasa safi anarukia kujitafutia umaarufu dini ya Wazanzibari, zote chuki kwa kuwa chadema hawana kiti hata ch akuombea maji Zanzibar.

Anajuwa akiuleta udini kwa Wazanzibari Waislaam wote wa bara na pwani hatutakaa kimya na ndicho anachokitaka kujitafutia umaarufu lakini hajui kuwa anazidi kukishindilia msumari chama chake kinachofata siasa za Kikristo kikisaidiwa na CDU ya Ujerumani.

Kaona Zitto hampati ki udini sasa anawachokoza Waislaam wa wa Zanzibar, asiwachezee Waislaam, akichokoza Muislaam mmoja ajuwe kachokoza Waislaam wote, amuulize Mwinyi, alizabwa kibao hadharani kwa kushadidia zinaa na kondom.

Na yeye asituletee udini wake. Atuwache Waislaam kama tulivyo. Amuulize Zena Kawawa, umesahau au hujui yaliyomkuta au Mrema, mpaka leo hana hamu ya kuwataja Waislaam. Acheze na kanisa na Wakristo asicheze na Muislaam au Uislaam, hatutamvumilia.

Hivi mna wabunge wangapi kutoka Zanzibar? kwi kwi kwi teh teh teh!

Penye red, maajabu ya dunia!!

Soma tena kipande hiki cha Msigwa niambie udini wake uko katika neno lipi??

"Siku ya ijumaa ya tarehe 20.7.2012 waziri wa Sheria na katiba mh. Abubakary Khamis alihutubia taifa la Zanzibar kupitia vyombo ya ZBc-TV na ZBc radio ,akiwataka wananchi wote wanoishi Zanzibar ,kuheshimu mfungo wa ramadhani ,na Alitoa maelekezo kwa vyombo vya dola, kuwa kamata wale wote watakaokutwa wanakula mchana. Kwa kile alichokiita kuwashawishi waliofunga. Pia alipiga marufuku migahawa yote kufunguliwa na kutoa huduma ya chakula na chai kwa wateja wakati wa asubuhi na mchana, isipokuwa usiku tu, Kama vile Hitoshi waziri huyu aliviagiza vyombo vya dola, kuwa kamata wale wote watakaovaa nguo fupi, hasa wanawake za kuwatamanisha wanaume. Katiba ya ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inasema Kila mtu anayohaki ya kuamini dini anayotaka ,na swala la katiba ni la muungano ,katika Majibu yake waziri mkuu alinishitua sana kwa kile alichodai Zanzibar kuna waislamu wengi hivyo tamko Hilo ni halali japo ni kuikanyaga katiba, na kwa Bahati mbaya radio nyingi za dini ya kiislamu zimenishambulia na kukimbilia swala la nguo fupi,baadala ya hoja ya msingi ya Uhuru wa kuabudu ,mwislamu akiwa mmoja katika kundi la wakristo 1000 lazima haki yake ya kiimani ilindwe na kuheshimiwa,hivyo hivyo kwa mkristo,tusijaribu kupotoshwa na watu wasiotaka kufikiri,waziri mkuu amelipotosha taifa.baadala ya kutukana na jaziba jibu hoja ya kikatiba,Mbona tanga,mtwara ,lindi ambako kuna waislamu wengi amri hiyo haijatolewa, double standard............"
 
Hii ndio taabu ya kuwa na mapadri, wachungaji na makatekista kwenye chama. Akili zao ni kupambana na uislamu.
Mpendwa jadili hoja wacha kujidhalilisha kiasi hiki. Upadre au ukatekista wangu unahusiana nini na hoja zangu? Au unadhani kuwa mkristo au mwislamu ni kufa kwenye ubongo? Iwapo mojawapo ya dini hizo zinaua uwezo wa mtu binafsi kuwa na utashi sahihi na kuwa na reason, basi huko ni kufuata mkumbo na si kuelewa hoja. Jadilini alichosema Pinda, rebuttle ya Msigwa na si uchungaji wa Msigwa. Angeuliza swali hilo Zitto ungesemaje?
 
Back
Top Bottom