Tuition Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Tuisheni ninayozungumzia ni wanachuo wa chuo kikuu cha dar es salaam, sehemu ya mlimani yaani "watoto wa mkandala" nenda changanyikeni kituo cha daladala cha bondeni, iliza madarasa wanayosomea wanachuo utaoneshwa. Madarasa yanajaa kama tution za mkandawile enzi zile

watoaji/mtoaji wa hiyo twisheni ni akina nani?
 
Tuisheni ninayozungumzia ni wanachuo wa chuo kikuu cha dar es salaam, sehemu ya mlimani yaani "watoto wa mkandala" nenda changanyikeni kituo cha daladala cha bondeni, iliza madarasa wanayosomea wanachuo utaoneshwa. Madarasa yanajaa kama tution za mkandawile enzi zile

I hope ni kujaa kwa madarasa ndo unakufananisha na tuisheni za mkandawile....

maana hata lecture theatres udsm ni za shida sasa hizi tuisheni zinapataje space pale au wanafanyia majumba 21?

Sasa hapo ndo kama wale kina sie kwisha habari yetu, ya kula mtihani haya ya kulimlipa mhazili?
 
Hii story nasita kuiamini. Aliyeileta angetakiwa kuwa wazi na kuelezea ni wanafunzi wa Kitivo gani hao waliokuwa wakitoka kwenye hiyo tuisheni.Nnavyofahamu UD hamna kitu kama hiki na hakitatokea angalau kwa siku za karibuni.
 
huyu pengine aliona watu wanatoka kanisani, wameshika bibilia mkononi yeye akazani wanatoka tushen. misa nyengine zinajaa watu bana!. si mchezo!
 
Inategemea unaongelea levo gani brother kilemi. researcher ndiye nadhani anatakiwa ajitafutie mwenyewe vitu gani asome na kwa staili ipi. Kwa mwanafunzi (pupil au student) hata awe wa PhD anatakiwa apate mwongozo na msaada wa mwalimu wake (tuisheni)

maswali kumi kivipi, sijakuelewa point yako. kutunga mtihani mrahisi hilo sio tatizo la twisheni bw.kilemi, huo ni uzembe wa mtungaji mwenyewe.

bw.kilemi pupil na student wote wanasaka elimu. tofauti ni level tu ya elimu wanayoitafuta.

"Tuition" ina maana tofauti ndugu Piper: kwa vyuo vya elimu ya juu ni mwongozo kama ulivyosema, ili mwanafunzi aelewe nini cha kufanya!!
kwa maana ambayo nafikiri ni ya mtoa mada pia, ni Ni masomo ya ziada, yaani baada ya kuelekezwa darasani, hukumwelewa mwalimu, hivyo umamlipa huyo mwalimu fedha ili akufundishe baadae wewe mwenyewe, au kama mpo wengi mnachanga!!

Maswali kumi kalika elimu ni recomended sample for measuring Instructional performance!!

Pupil na student ni sawa kabisa, ni level za elimu:
tofauti ni Pupil anahitaji msaada wa mwalimu for 80%, Student yeye anahitaji just 40%
 
Sishangai kamat toka kindergatten anasoma tuisheni then ata chuo ni mwendo wa tuisheni tuu.
Ni jambo la ajabu chuo tuisheni wakati kuna lecture then seminar bado matutorial assistants wapo kwa maelezo zaidi aibu hiii.
Huo kwanza ni uvivu wa kusoma vitabu kabisaa!
 
Ili kutoumiza moyo wangu nimeamua kuamini kwamba hao watoto wa chuo kikuu walikuwa wanatoka kwenye tutorial na si tuition. Labda wameshindwa kujua tofauti, na hivi wamezoea neno "tuition" kwenye lower levels walikotoka.

Uwii. Kwishnei
 
mmh naomba niikope hii faraja yako uliyojipa Injinia!!!
 
Ili kutoumiza moyo wangu nimeamua kuamini kwamba hao watoto wa chuo kikuu walikuwa wanatoka kwenye tutorial na si tuition. Labda wameshindwa kujua tofauti, na hivi wamezoea neno "tuition" kwenye lower levels walikotoka.

Uwii. Kwishnei

Many thanks Injinia......! Watu hupenda sana kudandia gari kwa mbele na kuanza kudiscuss issues kabla ya kujua ukweli halisi ni upi!

Tutorial /Tuition Univeversity ndio mahala pake.....sasa na nashangaa watu mnashangaa hapa tu kisa mmekariri kuwa TUITION hutumika kumaanisha masomo ya ziada baada ya kutoka darasani in case mwanafunzi hajaelewa au hakucover topics fulani kwa malipo ya ziada! Hii ni applicable kwa shule za msingi, Chekechea & Secondary (O & Alevel)!

Tuition /tutorial anayosema hapa mwanafunzi halipii extra money, akisha lipa ada inatosha......! Please don't confuse things! Kuanzia mtoa mamda mpaka wa changiaji wamechanganya mambo hapa!

Sorry Mkuu Mabuba unaweza kutuambia unaelimu ya level gani na umesoma vyuo gani?(option). Naoana uelewa wako ni mdogo sana kuhusu mfumo wa vyuo vikuu!
 
Sikia Bwana,
Haya mambo si Bongo peke yake tu. Kwa M7 walianza siku nyingi na tunawasifia wagraduate wengi kuliko sisi. Tulitaka idadi, compromise yake ni poor quality.

Wenzetu hapo jirani hata Desertation hawaandiki, kama unazo wapo waliomaliza zamani wasio na ajira rasmi wanakuuzia na unafaulu vilevile. Lugha kwao si tatizo, hivyo hata wakienda kwenye interview wanababatiza ajira. Suala la job performance ndilo huwasumbua, lakini kwa kuwa ni malobist hutumia ujanja kudumu kwenye kazi hatimaye mambo yanajipa.

Twende hivyo hivyo tu tutafika; walau tuwe na matapeli walioenda shule kuliko waliopo Samora na Posta.

Wala sitanii mjomba.
 
Jamani isiwe kweli jamani.Sasa hii tuition kama ipo ni kwa ajili ya kufaulu mitihani?this is crazy why mwalimu huyo huyo anaetunga mtihani then atoe tuition huko si kuwapa majibu wachache ya mitihani yake atakayotoa?
 
Lengo lake (pre entry) ni kuwasaidia wanafunzi wa kike katika kozi za sayansi na injinia, ili angalau taifa liweze kuwa na wataalam wa kike katika fani hizo. Kwa kweli imesaidia sana, kwani kuna wanafunzi wengi wa kike katika kozi hizo kwa sasa. Na wengi wao wanafanya vizuri.

Haijasaidia hii kitu imezalisaha Viwango duni ( VD), nimesoma nao Uhandisi mkuu ilikiwa ikitokea wamepewa mtihani na wao wakaona ni mgumu basi jioni wanaitisha mkutano wa Principle then Lecture anaambiwa atunge mtihani FAIR, hii imeharibu sana it was politically motivated ( Lengo ni lili lile kuwa na IDADI kuwa ya wahitimi wa Kike bila kuangalia ubora wao)

Sasa ukipeleka watu wa namna hii Uhandisi ni lazima watafute watu mtaani wa Kuwa solvia Madesa
 
Tunakushukuru mtoa mada hii kwa kuileta hapa jamvini ili wanataaluma wenzako (walimu) waweze kutoa michango yao mbalimbali kwamba tatizo la tuition ninini? ikizingatiwa kwamba hapo kabla haya mambo hayakuwepo na bado kiwango cha uzamivu naamini kilikuwa kizuri kuliko ilivyo sasa.

Kwa haraka haraka nadhani tuition ni matokeo ya wanafunzi kutopata muda wa kutosha ili kuhudhuria masomo, walimu kutotumia ipasavyo muda uliopangwa kwa lecture na badala yake kufanya mambo yao kutokana na kazi yenyewe (taaluma ya ualimu) kutothaminiwa na mwajiri mkuu (serikali). Yote mawili au uwezo mdogo wa wanafunzi na walimu na hivyo kuchukua muda mrefu kufidia vitu ambavyo mwanafunzi alitakiwa awe anafahamu kabla ya kuwa katika level hiyo ki elimu.

Mwisho kabisa, ni bahati mbaya kwamba tuition imeshakuwa utamaduni.utashangaa kwamba mzazi ana mpeleka mwanafunzi tuition kwa ajili ya pre std one. Kama taifa tuone jinsi hali ilivyo mbaya ki elimu.
 
Ili kutoumiza moyo wangu nimeamua kuamini kwamba hao watoto wa chuo kikuu walikuwa wanatoka kwenye tutorial na si tuition. Labda wameshindwa kujua tofauti, na hivi wamezoea neno "tuition" kwenye lower levels walikotoka.

Uwii. Kwishnei

Mkuu Injinia, kama ingekua ni Tutorial za kawaida na si hizi tuisheni tulizo zoea basi kungekua hakuna haja ya kuleta hii mada hapa. Mwandishi wa andiko hili anaoneshwa kushangazwa, hivyo basi ina maana ni kuwa alidhani hawa walikua wanatoka tuisheni sawa tu na wanafunzi wa Secondary watokavyo pale Perfect Vision ubungo.
 
Tunakushukuru mtoa mada hii kwa kuileta hapa jamvini ili wanataaluma wenzako (walimu) waweze kutoa michango yao mbalimbali kwamba tatizo la tuition ninini? ikizingatiwa kwamba hapo kabla haya mambo hayakuwepo na bado kiwango cha uzamivu naamini kilikuwa kizuri kuliko ilivyo sasa.

Kwa haraka haraka nadhani tuition ni matokeo ya wanafunzi kutopata muda wa kutosha ili kuhudhuria masomo, walimu kutotumia ipasavyo muda uliopangwa kwa lecture na badala yake kufanya mambo yao kutokana na kazi yenyewe (taaluma ya ualimu) kutothaminiwa na mwajiri mkuu (serikali). Yote mawili au uwezo mdogo wa wanafunzi na walimu na hivyo kuchukua muda mrefu kufidia vitu ambavyo mwanafunzi alitakiwa awe anafahamu kabla ya kuwa katika level hiyo ki elimu.

Mwisho kabisa, ni bahati mbaya kwamba tuition imeshakuwa utamaduni.utashangaa kwamba mzazi ana mpeleka mwanafunzi tuition kwa ajili ya pre std one. Kama taifa tuone jinsi hali ilivyo mbaya ki elimu.

Mkuu hili tatizo lina misingi yake, na litakuwa kubwa sana pale Kata Schools zitakapoanza kupeleka watu Chuo

Kuna mzee mmoja alishtakiwa kwa kukataa kumpeleka mwanae aliyefaulu Sekondari, akajitetea kwamba hawezi kumlipia ada mtu ambaye hata jina lake hajui kunadika, Dogo kaitwa mahakamani anaambiwa aandike jina lake Hawezi, basi mdingi akashinda kesim sasa fikiria mtu kama huyu aende kukata shule ya Uhandisi kweli si ni lazima atatafuta tuition tu
 
Mkuu Injinia, kama ingekua ni Tutorial za kawaida na si hizi tuisheni tulizo zoea basi kungekua hakuna haja ya kuleta hii mada hapa. Mwandishi wa andiko hili anaoneshwa kushangazwa, hivyo basi ina maana ni kuwa alidhani hawa walikua wanatoka tuisheni sawa tu na wanafunzi wa Secondary watokavyo pale Perfect Vision ubungo.

After all Tutorial Mtaani?
 
hao ni vilaza wanaitwa vidu pale coet...yani ni project ya mama mkapa kuwainua wanawake kwenye masomo ya sayansi, wanalipiwa ada mpaka accomodation na tuisheni ili kuwabust.

vidu kirefu chake ni viwango duni.

Nakataa kabisa kuwaita VIDU. Nataka nifahamu hilo kundi kubwa na wengine katika daladala na vi a.k.a chenge walikuwa ni wanawake/mabinti tu?

Ikumbukwe kuwa mitihani ya vidato vya nne na sita inavuja sana miaka ya karibuni hadi leo. Imagine mtu kuanzia form iv anaibiwa mitihani halafu akifika chuo kikuu unafikiri mashine/mitambo itakamata kweli??? Ndiyo maana wakimaliza wakija maofisini ukimwambia akuandikie hata minutes za kikao ni sifuri kabisa, sembuse meaningful reports(progress reports). Tumechoka maofisini huku.

Tutakubaliana kuwa aliyekuwa anapata nafasi ya kuingia chuo miaka mingi iliyopita alikuwa na sifa za kufaulu bila kuibia mitihani na ukimaliza chuo kazi unamudu bila shida!!! Leo hii thubutu technical work uwape baadhi ya graduates wa chuo uone mambo!!! Labda customer care ambayo hata asiye na degree anaweza!!!! Poor Tanzania.

Jana gazeti limetoa majina ya watahiniwa watarajiwa wa vyuo vya ualimu na kidato cha sita ambao vyeti vyao vya kujiandikisha (form iv na form vi kwa waalimu) vilishatumika huko nyuma na watahiniwa wengine!!! Sasa niambieni udanganyifu huu si ndiyo sehemu ya hizo tution??? Itabidi mtu apate tuition kwa kuwa aliingia na div one kali mlimani ya kuibia mtihani au fake certificate halafu leo anafeli na pengine ata disco, sasa aibu yote atapeleka wapi zaidi ya kukazana na tuition kulazimisha nyota zipande??

Kwa upande mwingine, namba ya wanachuo ni kubwa sana, mazingira ya kusomea na lectures ni duni mno. Imagine Nkrumah Hall linabeba kiasi gani wakati wa lecture?? Na waalimu nao wamechoshwa maana hata kusahisiha mitihani ni kero. Ndiyo maana nasikia eti siku hizi kuna mitihani ya multiple choices chuo kikuuu? Kulaleki!!! Hapo kuna kutumia akili na kufikiria critically kweli?? Hapo utampata graduates mwenye the best or better analytical skills? Tulizoea watu wa Sociology kipindi chetu ndiyo walikuwa wanapewa maswali wanasoma (kama 10) il watumie references mbalimbali na yanatoka katika mtihani wao. Tulikuwa tunawacheka sana!!!!

Bottom line the education system and its quality are in the intensive Care Unit(I.C.U). Poleni wana vyuo na watanzania, hasa wajukuu zangu sijui wao wataikuta hali ni vipi maana kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya Tanzania.
 
Mkuu ilikuwa ni Tution au Tutorial?labda haukusikia vizuri,wanafunzi wa Udsm hawana muda wa kwenda Tution wakati Madesa yapo!!!
 
Kwanza kabisa napenda kujahamisha wanajf kuwa mimi ni mwalimu mwenye shahada ya uzamili jamii katika elimu, shahada ya elimu katika elimu ya watu wazima zote hizi kutoka chuo kikuu cha Dar es es Salaam, pia nina stashada ya elimu kutoka chuo cha ualimu korogwe ninauzoefu wa kufundisha miaka sekondari maika 7. Napenda kusema kuwa jina la Mabuba ni jina langu halisi na sio jina kivuli.

Naweza kutofautisha kati ya Tutorial na tuition. Hapa ninachozungumzia ni TUITION. Labda wanajf tujadili ukweli (issue) kuliko mtu. Tution ile inafundishwa na wanafunzi waliomaliza udsm, somo ni uchumi, kila mtu hulipa shilingi za kitanzania 500/= kwa kipindi. Mimi nadhani wote wanaotetea ni waathirika wa tuition.

Jamani tuition za aina hii hazijengi taifa. Hebu fuatilia wanafunzi wengi waliosoma tuition, utakuta hajuikujenga hoja, ni mtu wa kuelewa maswali kuliko dhana ya jambo. Wanakariri kuliko kuelewa. Pia wajf kuna vitabu TUITION yaani vile vya maswali na majibu, vitabu hivi kwa sasa ndio vianaongoza kwa mauzo ya vitabu.

Tujadiliane ukweli kuliko kuukimbia, tutatue tatizo
 
Back
Top Bottom