Tuitazame upya nafasi ya Katibu Mkuu CHADEMA

MBELWA Germano

Mkuu,

Haya uliyoandika umeandika vizuri isipokuwa mtu asipokuwa makini hawezi kugundua kosa. Hivi uliona wapi watu wanabadilisha makamnda katikati ya Vita?

Dr. Slaa na Freeman Mbowe wanafanya kazi nzuri so far. Kinachohitajika ni kuendelea kuwa focused. Kuna watu wachache sasa wanatumia kisingizio cha DEMOKRASIA kuhujumu harakati na dhima kuu ya CHADEMA. Tunachopaswa ni kuungana kuwapinga maadui wa nje na ndani

Vijana chadema tusimame kidete, tusikubali kutolewa katika malengo ya msingi kwa maslahi binafsi ya watu
 
Last edited by a moderator:
Huu sio wakati wa Party Supremacy, Makuzi yoyote ya kidemokrasia lazima yaambatane na changamoto, Dr. yupo well contented hivyo anaweza sana kutafsiri kwa ufanisi zaidi Mabadiliko ambao CDM wanasimamia, kamwe usiogope neno DEMOKRASIA, sasa ni wakati wa kufanya SIASA na sio HARAKATI.

Nafasi ya ukatibu haitaji sana political figure, bali strategy maker, na hivi ndio tutajenga CDM imara zaidi.
Kwa hiyo chadema hadi leo unasema inafanya harakati?
Ofcourse makuzi ya demokrasia ni lazima yaambatane na changamoto lakini inapotokea katika line ya makuzi ya demokrasia baadhi ya watu wana-attack pillars za chama hicho hicho kinachotakiwa kulea demokrasia na kuandaa hata succession plan nzuri unahisi nini?Damage....!
 
mabadiliko ni muhmu sana popote pale hata China walikuwa wakimuona MAO kama Mungu wao na waliamini hakuna kama MAO lakn leo hii unaweza kuona RAISI waliyenae sasa amefanya makubwa zaidi kwa kuendeleza alichofanya MAO kwahyo cha msing ni mabadilko ndan ya CHADEMA kwa kuangalia hyo nafas unampa nan na sio mtu km ZANA ZA KILIMO (ZZK)

Nadhani nasindwa kupata point yako! Mabadiliko ya uongozi hayafanywi tu kwakuwa tunadhani bali ni kwa mahitaji. Pale tunapoyahitaji tutafanya. Kwa sasa sioni mahitaji ya mabadiliko ya kiuongozi!
 
Nafasi ya katibu mkuu inapaswa kushikwa na Doctor Slaa kwa sababu ni nafasi ya mtu mwenye taaluma.

Kwanza kabla ya yote alikuwa Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, hii siyo kazi ndogo kuwa katibu mkuu hivyo maoni yangu ni kwamba bado Slaa aemdelee kuwa katibu.

Kuhusu mgombea kuwa na nguvu sidhani kama ili kuwa na nguvu ni lazima uwe mwenyekiti? Jibu ni hapana.

Chama kinatakiwa kumpendekeza mtu yoyote kuwania uraisi siyo lazima awe mwenyekiti au mtendaji,

Mbona nchi nyingi hufanya hivyo.

We need strategy maker...Kamwe usigope demokrasia,changamoto ni kielelezo cha imani kubwa ya kifikra kukabiliana na mahitaji ya nyakati na juu na changamoto ndio linajengeka neno MABADILIKO. Hivyo tusiogope MABADILIKO.
 
Sijui usultani utaisha lini kwenye vyama vya upinzani.kila chaguzi uwa wagombea wale wale mpaka wafukuzwe kwenye chama ndio anaingia mwingine.
 
Katibu ndiye mtendaji mkuu (executive) wewe unakuja na mawazo kuwa aache kufanya anayofanya kwa kuwa anawanyima usingizi, pole sana ataendelea kutenda kazi mpaka kieleweke na mkimbe nchi.

Mnaleta mawazo ya kuchagua kati ya katibu mkuu na Zitto hebu tazama kura alizopata. Hampati kitu lengo lenu ni kuleta kutokuelewana ili kasi ya mabadiliko ipungue, haipungui bali ndiyo inaongezeka.
 
Mimi naona Zitto aoe kwanza ili tujue tabia ya huyu mwanamke ndio apewe nafasi ya kugombea. Naona wake wamekua na sauti siku hizi. Mbowe amepasi lakini Slaa amefeli.
 
Mkuu,

Haya uliyoandika umeandika vizuri isipokuwa mtu asipokuwa makini hawezi kugundua kosa.Hivi uliona wapi watu wanabadilisha makamnda katikati ya Vita?

Dr.Slaa na Freeman Mbowe wanafanya kazi nzuri so far.Kinachohitajika ni kuendelea kuwa focused.Kuna watu wachache sasa wanatumia kisingizio cha DEMOKRASIA kuhujumu harakati na dhima kuu ya CHADEMA.Tunachopaswa ni kuungana kuwapinga maadui wa nje na ndani

Vijana chadema tusimame kidete,tusikubali kut9olewa katika malengo ya msingi kwa maslahi binafsi ya watu

Nadhani bado hujaelewa vizuri mantiki ya hoja yangu...kamwe usikubali kuishi kwa hisia bila kujua uhalisia, hoja yangu haipo kisiasa kama baadhi ya wengi mnavyodhani bali ipo kimkakati zaidi, kwa miaka mingi tumeishi kwa mazoea na monopolization ya CCM kwenye ulingo wa siasa kwa muda mrefu umetuathiri kifikra na kudhani hatuwezi kufanya kitu nje ya mazoea...

Siasa haiwahusu wanasiasa pekee bali inamhusu kila mmoja katika jamii yetu hivyo lazima tujifunze kuwekeza kwenye siasa za akili na kutumia maarifa zaidi na kamwe tusilewe na mafanikio ya sasa bado ipo kazi kubwa mbele yetu, haitoshi kuhubiri MABADILIKO bila kutafsri mabadiliko yenyewe, haitoshi kusema Peoplessssss bila kutafsiri malengo unazosimamia.
 
Dr.Slaa ndio mtu sahihi kwa sasa.

Hujatoa hoja msingi; ukokimagamba mgamba

1. Hujaangalia sustainability ya mafanikio kama mabadiliko unayoyataka yata sustain mafanikio..

2. Ni taratibu za chama baada ya tathmini kuona mwelekeo mpya uendeje kwa raslimali gani.

3. Ungepeleka maoni hayo kupitia tawi lako kama unaona yana msingi
 
Ongeauchok

...kamwe usikubali kuishi kwa hisia bila kujua uhalisia, hoja yangu haipo kisiasa kama baadhi ya wengi mnavyodhani bali ipo kimkakati zaidi, kwa miaka mingi tumeishi kwa mazoea na monopolization ya CCM kwenye ulingo wa siasa kwa muda mrefu umetuathiri kifikra na kudhani hatuwezi kufanya kitu nje ya mazoea...

We need strategy maker ambaye si lazima awe political figure. Na kamwe tusijaribu kupotosha mada kwa kumuhusisha Zitto....
 
Last edited by a moderator:
Tuko front-line TUNAPAMBANA kutoa elimu ya uraia kwa wanainchi hoja yako isubiri muda Huu si muda wake nakushauri vaakombati jiunge na si huku vijijini kuendeleza M4C nyumba kwa nyumba, shina hadi shina, mtaa hadi mtaa na kijiji mpaka kijiji!

Nawatahadharisha Wapenda UKOMBOZI M4C imewapa kiwewe watawala kwa sasa wanatumia mbinu nyingi ikibidi kuzua mijadala hasi
 
Kwahiyo Zitto awe katibu mkuu pale au sio.

Hapana zito nadhani itakuwa ni vizuri akikaa pembeni kwanza kwasababu wanachama tumeanza kupoteza imani naye kwamba hana misimamo asije kukiangusha chama, maana amekwisha wahi kusema hataki Siasa anataka kufundisha lakini cha ajabu bado tunamuona yupo kwenye Siasa wewe huoni kwamba ni mbabaishaji?

Na imani ya wanachadema ilishuka zaidi dhidi yake hasa baada ya Mwanahalisi kuandika mawasiliano yake na Usalama wa Taifa ambao wanaumiza vichwa kila siku watakiua vp chama hivyo wenye akili timamu tunajua huyu mtu ni kweli hataki siasa anataka aue chama then akafundishe.

Habari za mwanahalisi zilikuwa kweli kwasababu hakuwahi kuzikana kwa dhati.

Chonde chonde wanachadema tusije tukasahau ubabaishaji wa Zitto
 
Dr Slaa na team yake kwa sasa performance yake hakuna katibu mkuu wa chama chochote cha siasa hapa Tz kinaweza kumfikia kura zimeongezeka, wanachama up, wabunge up, madiwani up, matawi up na wanawake up.

Kumbuka siku za awali mikutano ya cdm wamama walikuwa hawaendi.

Namba unayo bip haipatikani jaribu baadae
 
Hujatoa hoja msingi; ukokimagamba mgamba

1. Hujaangalia sustainability ya mafanikio kama mabadiliko unayoyataka yata sustain mafanikio..

2. Ni taratibu za chama baada ya tathmini kuona mwelekeo mpya uendeje kwa raslimali gani.

3. Ungepeleka maoni hayo kupitia tawi lako kama unaona yana msingi

Jifunze kufikirisha akili...
 
Dr Wilbroad Slaa hakuwahi kutamka hata mara moja kwamba atagombea urais uchaguzi ujao. Ni kumuonea kumlisha hayo maneno kwani Dr Slaa si mtu wa hovyo kupindisha taratibu za chama na kujitangaza leo eti atagombea urais miaka 3 ijayo. Hilo linafanywa tu na mtu mwenye hila chafu kuchafua upepo ndani ya chama.

hapo kwa red, kwani mpaka aseme?
 
Back
Top Bottom