Tuifute Laana Yetu 31Oct2010

Martinez

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
525
160
Dalili za laana ya Tanzania. Laana inayosababishwa na kushindwa kuitumia fursa ya kupiga kura, kuikomboa nchi:
Dalili ya Kwanza, tuna rasilimali nyingi za utajiri katika dunia hii, mfano madini ya tanzanite hayapatikani popote Duniani, Kuna mbuga za wanyama kama Serengeti ambazo ni za kipekee, utajiri wa Tanzania utajaza vitabu kuutaja, lakini sisi ni kati nchi maskini zaidi Duniani na wajanja wanavuna raslimali hizo huku wakituachia migogoro ya kisiasa na kijamii.
Dalili ya pili, tuna jiografia ya kutegemewa ukanda wa kati na nchi nyingi za kiafrika ukiacha Mito mikubwa na Maziwa, lakini pia tunapaka na bahari ya hindi, na hivyo kuwa na uwezo wa kuwa na bandari kubwa Afrika inayotegemewa na nchi za Rwanda, Burundi, Uganda, Congo drc, Zambia nk huku reli ikitoa mizigo bandarini, lakini cha ajabu ni kuwa Bandarini kutoa mzigo ni kero na usumbufu unaochukua muda mrefu na kukatisha tamaa, bandari ni ya kirasimu huku reli ikiwa imekufa kifo cha mende.
Dalili ya tatu, ni mbuga ya Serengeti, hii imewekwa kuwa ajabu ya saba ya Dunia kutokana na mfumo wa kuhama kwa wanyama wakiwa katika mamilioni, aina kwa aina, makundi kwa makundi, yenye kuvutia na kustaajabisha, isiyokuwepo sehemu yoyote Duniani, huku mfumo wa ecosystem ukionekana dhahiri. Serikali inataka kujenga barabara ya lami inayopita karibu na hoteli inayomilikiwa na JK katikati ya mbuga hii, kwenye njia zinazotumiwa na wanyama wanapohama, hili ni janga. Ni sehemu ngapi hazina barabara Tanzania. Kwanini hapa. Tena kama ni lazima serikali ingeweza kujenga barabara tena kwa gharama nafuu zaidi na umbali mfupi zaidi nje ya mbuga kwenda sehemu hizo hizo. Wazungu wanatushangaa sana. Nenda kwenye www.savetheserengeti.org utaona kwa undani. Ni wazi kuwa mbuga ya Serengeti itapotea katika ramani ya Dunia. Hii pia siyo hujuma, bali ni laana. Kuna dalili nyingi saana za kuthibitisha laana tuliyonayo kama nchi. Laana tuliyoitengeneza wenyewe miaka mitano iliyopita.
Tuone sasa chanzo cha laana hii. Mungu, atukuzwe leo na siku zote, alipoiumba Dunia aliibariki kila sehemu kwa namna yake, kuna wenye utajiri wa mafuta, kuna wenye utajiri wa mazao ya kilimo, maliasili, kuna wenye viwanda, teknolojia n.k, lakini ujue Baraka hizi zote ni fursa, usipozilinda unalaaniwa. Unaweza usiamini kuwa wanyama wa Tanzania wanasafirishwa na kwenda kuanzisha mbuga Ulaya. Sisi tulikuwa na fursa ya kuzilinda, miaka mitano iliyopita. Tumejutia. Fursa itakuja tena 31October2010.
Wafanyakazi, Wakulima, Wafanyabiashara na Wajasiriamali, Mafundi seremala, Walimu na Wanafunzi, Polisi na Wanajeshi, Wanausalama wa taifa, Mashehe na Wachungaji, soote tupige kura kwa lengo la kuikomboa nchi yetu, kwa faida yetu na vizazi vijavyo. Hata kama tunawajibika kwa utawala uliopo, basi siku ya kupiga kura, tuusaliti na kuutosa utawala dhalimu, utawala wa vibaraka. Hiyo ni kwa faida yetu na vizazi vijavyo.
Tupige kura kwa nia ya kuwachagua watu wenye Wito, Sifa na Uwezo wa Kuongoza kwa lengo la kuikomboa nchi. Tupige kura kwa lengo la kuikomboa nchi. Tuepuke kuwachagua vibaraka wa wezi wanaopora utajiri wa nchi yetu, na kubadili sheria kwa manufaa yao na rafiki zao na familia zao.
Shida tunazopata leo ni laana tuliyoichagua miaka mitano iliyopita, maana hatukupiga kura kwa haki, hatukuitumia fursa kuikomboa nchi yetu, tulipiga kura kwa ushabiki, kwa kupewa rushwa ya ahadi za uwongo, fulana na kofia, tukawachagua mafisadi na vibaraka wao, tena kwa kishindo. Hiyo ndio laana tuanayopaswa kuiepuka safari hii.
Ni laana ambayo tuliichagua kwa kuwa hakuna binadamu mwenye haki ya kumtawala binadamu mwenzake bila ridhaa yake. Na ndio maana tunapiga kura. Tulifanya makosa. Laana imetufundisha. Tuiondoe nchi yetu kutoka kwenye laana hii ya kutawaliwa na kundi hatari la mafisadi. Kumpigia kura fisadi kwa vile tu umepatiwa Shati, Khanga, Umekula, umekunywa pombe ni uzuzu. Kumpigia kura mtu asiyefaa kutokana na ushawishi wa fedha na mabango, ni kujiongezea laana. Tupigie kura watu wanaofaa bila kujali vyama vyao
Uchaguzi 2010 ni fursa. Tuitumie kuikomboa nchi yetu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom