Tuienzi vipi siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mwl. Nyerere?

POMPO

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
6,690
2,400
WanaJF,

Ni miaka 13 toka Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere atutoke, Alizaliwa tarehe 13 Aprili, 1922. Alifariki dunia 14 Oktoba, 1999,
daima atakumbukwa kuwa:

Ndiye rais wa kwanza wa Tanzania aliiongoza Tanzania toka mwaka 1961 hadi mwaka 1985.

Anakumbukwa na watanzania kuwa ndiye mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea.

Anakumbukwa na watanzania hasa kwa kujenga umoja na amani kwa Taifa na utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa taifa katika vitani dhidi Idi Amin.

Anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu.Pia ataendelea kukumbukwa na waafrika kote barani hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.

Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiyari baada ya kutawala kwa muda mrefu. Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo.

WanaJF,najua kukutana ilishakuwa ni story,

Alikuwa na mapungufu alikuwa na mafanikio: JE TUIEZI VIPI SIKU YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MWL. NYERERE?

Na miaka 13 Taifa bila Mwalimu Nyerere?
 
Mimi kwangu nikisoma kitabu cha Mwembechai Killing, bado sioni haja ya Kumuenzi baba wa taifa
 
Baadhi ya nukuu zake

1.Tuwaogope kama UKOMA,wale wote wenye tamaa za kwenda ikulu! ikulu kuna nini au kuna biashara gani
2.CCM sio baba yangu wala mama yangu
3.Dhambi ya ubaguzi haishi itaendelee tuu! sisi wazanzibar nyie watanganyika! Mkitengena itakuwa sisi wapemba nyie waunguja
4.Wewe Edward......ni kijana mdogo sana na umejilimbikizia mali sana! Hufai kuwa rais.
5.Na wewe ****** muda wako bado subili(alimaanisha hawezi kutawala nchi)
 
Tumshukuru kwa yakwake aliyo tufanyia kwa kadiri ya uwezowake then tuyasahau kabisa aliyofanya na sisi tufanye yetu zaidi yake kwani ni ukweli usio pingika MAGEUZI YA KWELI HAYATO LETWA NA KIONGOZI ALIYE ZALIWA KABLA YA UHURU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom