Tuieleweje serikali?

Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
182
Kwa nini serikali haikuonyesha ghadhabu kali kwenye suala la
Richmond?
Ziko wapi ghadhabu za serikali kwa waliohusika na rushwa katika
ununuzi wa rada?
Zipo wapi ghadhabu za serikali kwa ubadhirifu unaofanyika TANROADS?
Ziko wapi ghadhabu za serikali kwenye viongozi wa taasisi
zilizoshindwa kuchunguza kampuni ya Kagoda iliyoiba mabilioni ya pesa
Benki Kuu?
Ziko wapi ghadhabu za serikali kwa upotevu wa mabilioni ya fedha
kwenye halmashauri zetu nchini?
Ziko wapi ghadhabu za serikali kwa waliohusika na mikataba mibovu
kwenye sekta ya madini?
Ziko wapi ghadhabu za serikali kwa wale waliohusika na mkataba wa
uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania?
Serikali inayoghadhabika kwa wananchi wake wanapoomba kuongezewa
maslahi; lakini serikali hiyo hiyo ipo tayari kujadiliana na mafisadi
na kuendelea kushirikiana nao kama ilivyofanya kwa baadhi ya
waliohusika na wizi wa fedha za EPA, Serikali ya aina hiyo haiwezi
kuheshimika na wananchi wake hata kidogo.
 
Back
Top Bottom