Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi!

kwani wikileaks wanakisa gani mpaka wamchukie JK kwa kumtungia uongo.

kwa nini usiitake wikileaks iiombe radhi marekani kwa kuweka taarifa ya uongo (kumsakazia uongo balozi wake) ?

Je ikiwa wikileaks wanatunga kwa nia ya kuigonganisha marekani na Tanzania ni ni ipi hasa faida itakayovuna wikileaks kwenye hii skendo????

Kwa namna IKULU inavyokanusha hata mambo yaliyo na ukweli wa 100% nashawishika kuamini taarifa ya wikileaks
Labda ni mimi sijaelewa malengo ya Pasco kwenye hii thread au ni wewe hujamsoma vizuri.
 
Tuhuma zimelengwa kwa mtu(rais), hakuna haja ya watanzania wote kuonekana wamedhalilishwa!
Ni kweli mtu huyo ni rais wa Watanzania, lakini ni saa ngapi anaFANYA MATENDO FULANI akiwa Mr X, na ni saa ngapi anafanya akiwa rais?...
Kama tendo hili analotuhumiwa kulifanya ni la manufaa kwa taifa basi tujisikie aibu wote, lakini kama ni la personal na familia yake or whatever, then aibu hiyo ni yake milele na hakuna atakayeungana naye kwenye dhalili hiyo...aibebe na wanaomhusu!

Below;Savile row suits

images
 
Alipohongwa suti yeye alitoa nini? Mmmmh sasa kwanini unawataka USA wakanushe? si wao wameshasema ni kweli sasa wajipinge? aaah wapi! tuyaache turudi kwenye maswala ya msingi; umeme, elimu, barabara n.k hayo ya suti labda zilishachakaa saa hizi
 
pasco

hata hilo attachment yako ya proof kuonyesha bi Pile anata kuombwa radhi pia imepikwa na ikulu kutaka kuficha madhambi yenu mnayoyafanya huko ikulu. Kwa kumsafisha bwana wenu.

Ukweli unabakia ukweli mtajitahidi kuuficha lakini tumeshajua kuwa kikwete amehongwa suti na bwana alhadaw.
Subirini bomu jingine liwadondoke mje kumtetea tena hapa jamvini na kukanusha.

100% i do belive on wikileaks cable of secret 100% sidanganyiki na ikulu yenu kusafishana hata mpakane mkorogo mtabakia rangi ile ile na uchafu wenu

 
Suit = suruali + koti +kizibao.,,,,Suit.. hahahahaha !!!

Wanatafuta pakutokea kuwa bosi wao hakuhongwa suti, Duniani kuna mambo kumbe hata wanaume pia wanahongwaga? Hizi za kuhongwa zimenifanya kuanza kujiuliza maswali mengi sana.

Hatari hii :A S 109:
 
Hizi Wikileaks zilikuwa ni internal correspondence kati ya Balozi na Wizara ya Mambo ya Nje ya US. Nyingi ya hizi zilikuwa pia ni Classified au Secret. Walioziandika hawakuwa wanategemea kuwa zingekuja kuletwa kwenye Public Arena..

Hizi taarifa zimetoka nje kwa bahati mbaya. Hakuna haja ya watu waliotajwa kwenye hizo taarifa kukasirika sana. Laiti watu wangejua makampuni yao ya Bima yanavyowasema kwenye internal correspondence, wangezimia.

In conclussion: Itakuwa ni retro-active kama serikali ikiamua kuchukua hatua za kisheria. Hata hii kujibu shutuma haina haja.

In principle, kusoma hizi cables tu ni violation ya privacy ethics. Ni kama umeokota barua ya mtu imefunguliwa ikaachwa kimakosa, watu wenye principles za ethics watamrudishia mwenyewe barua yake bila kuisoma, kwa sababu hawakutakiwa kuisoma.

In reality this is difficult to do because of the nature of the leaks (state entity, not private individual, widespread availability it is hard not to come across them, the lure of strategic interest in understanding how the mighty Americans think etc)

Zaidi ya yote, hata baada ya kuelewa kwamba aliyekuwa violated hapa ni serikali ya Marekani, lakini kwa kuelewa kwamba information zao za ndani ambazo hawajazilinda ipasavyo zimeleta embarassment kwa serikali nyingi kutokana na uzembe wao, Secretary of State Clinton alishaiomba radhi dunia nzima kwa mpigo kutokana na cables hizi.
 
Wanatafuta pakutokea kuwa bosi wao hakuhongwa suti, Duniani kuna mambo kumbe hata wanaume pia wanahongwana? Hizi za kuongwa zimenifanya kuanza kujiuliza maswali mengi sana.

Hatari hii :A S 109:

Tafuta etimology ya neno "hongo" utaona halikuanzia kwa mahusiano ya mapenzi bali kama kodi ya kutumia njia sehemu fulani.Hongo ilitolewa kutoka kwa mgeni mfanyabiashara kwenda kwa chifu.

Hiyo perception yako kwamba hongo ni kwa mapenzi tu iko shallow.
 
Wanabodi,

Kitendo aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini, Michael Ritze cha kupitia mtandao wa Wiki Leaks, kumtuhumu Rais wetu, Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa amehongwa pair 5 za Suti za Savile Row, sio tuu ni cha udhalilishaji wa hali ya juu kwa mkuu wetu wa nchi, bali ni matukano kwa Watanzania kwa ujumla wetu kwani Rais wetu ni kama baba wa familia kwenye nyumba yetu, hawezi baba yetu kudhalilishwa sisi watoto ambao tunaishi kwenye nyumba hii tukakaa kimya.

Kukanusha peke yake hakutoshi, tunataka Marekani imuombe radhi rais Kikwete na Watanzania kwa ujumla kwa kadhia hii ya Wikileaks.

Mara baada ya JF kutundika bandiko la kadhia hii, Ikulu ilikurupuka kutoa taarifa ya kukanusha. Nimesema Ikulu ilikurupuka kukanusha vipengele vya rushwa tuu kwa kukanusha yaliyonukuliwa na JF badala ya kuifuata ile link na kuyakanusha yote yanayohusiana na Tanzania. Kwa vile source mama ipo na tuhuma zinazidi kushuka, ilikuwa ni busara kwa Ikulu kukanusha yote in details once and for all vinvyo na tusubiri kuona ni mangapi Ikulu itakuwa inasafisha kila kukicha.

Mengi yaliyokanushwa na Ikulu, sio yale ya Wiki leaks, bali ya Wiki Leaks yaliyoandikwa JF. Kufuatia kanusho hilo, yule atoa taarifa kwa Balozi wa Marekani, Bi. Lisa Pile, naye ametumiwa sio taarifa ya Wiki Leaks, bali ametumiwa ile thread ya JF ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Matokeo yake, Bi. Pile anakanusha kuwa yeye hajui Kiswahili na wala hakuwahi kukutana na JK hivyo wanamsingizia. Ilitakiwa huyu Bi Lisa atumiwe ile link ya WikiLeaks na sio hiyo ya JF waliomtumia. Alitakiwa akanushe kukutana na balozi wa Marekani au akanushe hakumwambia balozi Ritze kile balozi huyo alichoripoti nchini kwao na kunukuliwa na Wikileaks tujue Balozi ndie muongo hivyo kutupa haki Tanzania kuombwa radhi na JK kutendewa haki sio tuu kwa kuombwa radhi, bali pia kufidiwa kwa madhara aliyoyapata kwa kuchafuliwa reputation yake.

Badala ya kukanusha kilichoandikwa na Wiki Leaks yaani alichoongea na Balozi wa Marekani, hiyu bibie amekanusha hajui Kiswahili na hajawahi kukutana na rais Kikwete wala rais yoyote. Nani kamwambia bibi huyu kuwa kaongea Kiswahili au kakutana na JK?. Hebu soma hilo kanusho hapo chini lenye headline ya thread ya JF!.

Kufuatia kanusho hilo la Bi. Pile, Mmiliki wa Kilimanjaro hotel Albawadry naye ametoa statement ya kanusho akimtetea Bi. Pile kuwa kweli hajui Kiswahili hivyo yote ni uwongo!.

Kwa vile chanzo cha uwongo wote huu ni taarifa ya Balozi wa Marekani kipindi hicho, Bw. Michael Ritz, Serikali ya Tanzania, kupitia njia za kidplomasia,
1. Kwanza Lisa Pile apelekewa taarifa rasmi za Wikileaks na akanushe hayo aliyomweleza balozi wa Marekani maana Pile ndie chanzo kilichonukuliwa na balozi. Hiyo taarifa ya Pile kukanusha kilichoandikwa Jf ni nothing.
2. Waziri Membe kupitia njia za Kidiplomasia, kuulazimisha ubalozi wa Marekani nchini, Kukanusha taarifa hizo za aliyekuwa balozi wake nchini si za kweli bali ni uzushi wa aliyekuwa balozi wake hivyo kumuomba radhi JK na Watanzania kwa jumla.
3.Balozi Michael Ritz popote alipo, ama athibitishe alichoandoka ndicho alichoambiwa na Pile, au akiri kuwa kuwa yeye hakuzungumza hayo na Bi. Pile bali ndiye mzushi aliteutunga uwongo ule hivyo kumuomba rasmi radhi JK na kumpa JK fursa ya kudai fidia na Watanzania tutapoozwa kidogo japo kwa chochote kitu.
4. Wasaidizi wa Rais JK, kuanzia Ikulu mpaka chini, kunapotokea rais kuchafuliwa, muwe mstari wa mbele kumsafisha na kuilinda hadhi na heshima yake instantl na promptly mapema kadri iwezekanavyo, na sio kusubiri mpaka Mtandao wa JF uweke hadharani ndipo mkurupuke na kujibu tuhuma za JF ambazo ni nusu nusu, jibuni tuhuma za Wiki Leaks!.

Mbona ni mengi, mabaya, machafu, ya kudhalilisha na kutia aibu yamesemwa na Wiki Leaks nanyi mko kimya tuu bila kukanusha lolote, kitendo cha kuibuka na kukanusha hili la hongo kwa JK pekeyake, huku sio kukanusha proper, ni kujikomba komba kwa rais muonekane nanyi mko kazini!

JF ilipoziweka tuhuma zile, iliwawekea mpaka link ya Wiki Leaks, kilichowafanya msifungue hiyo link na kukanusha tuhuma zote moja baada ya nyingine ni nini, hadi kuwapelekea waarabu tuhuma za Kiswahili na Mtoa habari Bi. Pile kupelekewa taarifa ya JF ya kiswahili badala ya kumpa taartifa halisi ya Wiki Leaks?!.

Kwa vile kwenye ile link ya Wikileaks kuna tuhuma lukuki mle, kuanzia ile ya Hosea, itakuwa ni busara na kuwatendea haki Watanzania, sasa kama mtaingia kazini rasmi, na kuanza kupangua tuhuma moja baada ya nyingine kwa, vinginevyo usafishaji huu wa tuhuma za rais peke yake, utaishia kugeuka ni 'Funika Kombe, Mwanaharamu Haramu Apite!'...wenye akili zao watakuwa wameisha pepeta kujua pumba ni zipi na mchele ni upi, na badala ya kumsafisha rais wetu, mnajikuta ndio kwanza mnazidi kumpaka ....!.

Wito kwa Wana jf wenzangu kwenye issues kubwa kama hizi, zinazomhusu kiongozi wetu mkuu wa nchi, nawasihi sana, tuache mambo ya mizaha. Tuhuma hizi ni mzito na very serious, tunapozijadili, naombeni sana tuwe serious accordingly na kutumia lugha za Staha kwa Viongozi wetu.

Rias Jakaya Kikwete ni rais wa nchi yetu, yeye sio tuu ndiye mtu mwenye jina la JK, bali yeye ndie mkuu wa taasisi ya urais, ambayo ndio taasisi yenye hadhi na heshima kuliko taasisi zote hivyo inastahili heshima yake.

JK ndiye rais wetu, uwe ulimchagua, ua hukumchagua, uwe unamkubali au haumkubali, yeye ndiye rais wetu na ni rais wa wote hata hao alioshindana nao, this is not debateble fact ni hard fact. Naomba awe addressed kwa heshima stahiki.

Mode: For the sake of this thread, naomba muimoderate effectivel na kama mko busy sana naomba nipewe u-mode kwa muda only for the sake of this thread ili post zozote za kipuuzi puuzi zenye lugha isiyo na staha, nizifutilie mbali, ili zisichafue lengu, madhumuni na maudhui ya mjadala kwenye thread hii kwa maslahi ya taifa.

Wasalaam.

Pasco.

Kumbe kuandika kote ni kuomba Kazi JF ya u-Mode ili upate Nafasi ya Kumsafisha vizuri Bosi wako na kutu-delete-a Habari zetu nzuri.

Kwa taarifa yako hupewi Kazi hapa Jf bakia huko huko Usalama wa Taifa Kazi yenu ni kuficha madhambi ya Wakubwa wenu na kuramba ramba miguu ya CCM. Siku zenu zinahisabika
 
Mimi mtanzania niitwaye Tata sihitaji kuombwa msamaha na marekani wala wikileaks. Ninachohitaji kujua ni kwa nini huyu Mwarabu alipewa Kilimanjaro Hotel badala ya Reginald Mengi & Co? Kwanini Mengi alipotuhumu kuwa kuna mchezo mchafu umetumika kumuengua kwenye mchakato wa kuipata hotel serikali, kupitia kwa Mr Masilingi aliyekuwa waziri wa utawala bora wakati huo, ilimtishia kumshughulikia kwa kutumia nguvu za dola? Nadhani ni wakati muafaka kwa Mengi kuweka wazi alimaanisha nini alipoituhumu serikali kucheza mchezo mchafu.
 
Pasco,
Tumesikia na kusoma kanusho la Ikulu, tumesoma pia kanusho la Lisa na la Al Bawardy; bado hatujasikia kutoka kwa Balozi Retzer, huenda kasingiziwa. Suala la Tanzania kuombwa au kutoombwa radhi lifikiriwe baada ya hapo.

........Ukweli unauma eeeeeeh???
 
Pasco,
Tumesikia na kusoma kanusho la Ikulu, tumesoma pia kanusho la Lisa na la Al Bawardy; bado hatujasikia kutoka kwa Balozi Retzer, huenda kasingiziwa. Suala la Tanzania kuombwa au kutoombwa radhi lifikiriwe baada ya hapo.

........Ukweli unauma eeeeeeh???

Wamarekani wangeweza kukwambia Tanzania nawote wanaosoma Wikileaks cables, cable za mawasiliano yao (Wamarekani) ya siri ndio wanaotakiwa kuwaomba radhi Wamarekani kwa kusoma cables zao za siri bila idhini yao.

Lakini hawakusema hivyo, Hillary Clinton alishaomba radhi. Na unlike Kapuya who was "apologising repeatedly" to the US embassy, wenyewe wanaweza kusema hawawezi kuomba radhi mara mbili mbili.
 
Pasco kama umeshindwa kuandika jina la balozi wa Marekani tu kwa umakini tutegemee vipi kwamba uchambuzi wako una makini?
 
msiturudishe katika ujamaa, kama BABA ametukanwa kwanini amtume house boy(salva) kukanusha skendo mbele ya watoto? tunamtaka yeye na si house boy hivyo marekani hawana haja ya kutuomba msamaha kwanza document zenyewe ni confidential hawakuwa na lengo la kumpaka matope rais, lakini kumbuka waswahili usema lisemwalo lipo.
 
Sioni kwa nini tunajaribu kutetea tabia ya kawaida kwa raisi wetu. Nchi yetu anaiuza kama karanga. Kuhongwa ni neno linapatikana ndani ya dictionary. ili lifanyiwe matumizi ni lazima mtu mmoja akubali kupewa kitu na mwingine kwa faida inayotazamiwa baadaye. Hata hivyo safari za raisi wetu nje ni za nini kama si za kwenda kuomba nguo za kuvaa. Sioni faida yoyote tokana na ziara zake za kila siku ,kwa nchi na wananchi waliochoka na rushwa wizi na kila aina ya ahadi hewa za papo kwa papo.
 
Pasco nakubaliana na wewe kuwa waandishi wa ikulu na watetezi wa rais wasikurupuke katika kujibu hoja bali wazichunguze kwa undani na umakini.
Jambo la kuombwa msamaha sikubaliani nalo.Aliyetuzalilisha si marekani bali rais wetu.
Kama mzazi alilewa akajikojolea ukisikia anasemwa mtaani usiwashambulie wanaomsema;jaribu kumrekebisha huyo mzazi wako.
 
.......................Sasa kama kaongwa sisi tufanyaje? Mimi naona nzuri tu,tena kama yapo mengine wayaweke hapa...sasa kama mwenyewe alikubali kuongwa alidhani itakuwaje? Yeye alipokuwa anasema kauli kama hizi alimaanisha nini...?

...Wasichana wanaopata mimba ni kiereere chao....
...Wanaopata Ukimwi ni kujitakia.........

Na yeye kuongwa suti ni kujitakia na kiereere chake..........................ngoja akinywee.
 
Back
Top Bottom