Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi!

Wanabodi,
Leo nimeikumbuka hii, kufuatia thread fulani ya mmoja wa viongozi wa juu wa chama fulani, kualikwa mahali kwenye hoteli ya maana, naye kwenda kwenye mwaliko huo, huku amevaa mavazi rasmi ya chama chake, kulikopelekea kubezwa sana kuwa eti alitakiwa avae suti!, nimeikumbuka hii, kwa sababu, inawezekana kabisa, kiongozi huyu, akawa hana suti?!.

Hebu soma jinsi alivyo bezwa!.


Pasco.
kumbe heshima yangu ilikuwa inapotea bure kabisa!!!!labda ngoja nikumbuke kama ni pasco huyuhuyu niliyewahi kumweshimu ndiye anayeweza kukimbia nje ya mada yake mwenyewe na kwenda kushabikia hoja nyingine mfu kuliko ya kwake,mimi nilitegemea ungemkaripia yule ambaye angeingiza kwenye mada yako maneno kama hayo yaliyokusisimua hadi kujikita kuya promote kama vile ni ya maana kabisa kulingana na mada yako mwenyewe!!!!kweli Mungu ametughadhibikia,anazififisha hata akili zile ndogo tulizozitegemea.
 
Mpaka hapo hujajua tu jamaa anaushabiki wa kivyama? Na anajua anachoshabikia japo hujitangaza a non partisan....

non partisan wapi wakati ni CCM pure, yani anampaka mafuta lowassa utadhani mume wake. Ameanzisha mada halafu anaikimbia kwa kuanza kusema kiongozi wa chama flani, alialikwa mahalh flani, kama sio majungu ninini? Si aseme tu dr. Slaa?
 
hivi mkulu wetu ana suti pea ngapi? si atuwekee risiti hapa tuzione kabla hatujaanza kumtetea. yule balozi nilimpenda sana maana uvasco da gama wake uliwakera hata wazungu wakaona dawa ni kuiweka peupe rushwa ya suti tano na imesaidia siku hizi unaona anazunguka ovyo ovyo?
 
This is dated, but still relevant.

Ninapoanza kusoma tu nataka kutapika.

1. Kama Kikwete baba yako, ni baba yako mwenyewe, wengine tuna baba zetu, na si Kikwete.

2. Swali la muhimu kuliko fake patriotism ni, je, Kikwete alihongwa suti au hakuhongwa? La kuvunda halina ubani, usituletee two bit patriotism kwa kutaka kufunika ukweli. Kama alihongwa suti mwanamme mzima akakubali huo ndo utakuwa ukweli, hata "watoto wake" mkiunda jeshi la kumtetea.

3. Marekani wewe ndio uiombe radhi kwa kusoma barua zake za siri. Waungwana hawasomi barua za siri za wengine.

mkuu ukweli ulishaanikwa na mtandao wa wikileaks hivyo inabaki kama ilivyo kuwa amehongwa suti sio suala la kutoa povu mdomoni hapa
 
Bora hata Mungungo wa Mosovele!!!
Elimu yote hii na kutembea kote huku!!!!! Tukisema Mr Dhaifu..majitu yanakasirika!!
 
JK ameaibisha sana hii nchi wamemuhonga hadi suti utadhani halipwi mshahara
 
Kwa nini kusema ukweli juu ya matendo anayofanya Rais, yanayopendeza na yasiyopendeza, ikiwemo kufungia Magazeti na Vyombo vyote vya Habari ambavyo havimsifii, unadai ni kuisema Nchi vibaya?
Je, Ayubu Rioba wa sasa, anao uwezo wa kuendesha mjadala wa namna hiyo?
Paskali, kusema Nchi inatukanwa na kusingiziwa na Vyombo vya Habari vinavyojitambua, dawa yake ni kuvifuata na kukanusha "huo uongo" kwa kukubali kuongea nao na kuelezea uhalisia.
Hili linawezekana?
Hili nimekuwa nikishauri kwa muda mrefu tuu, lakini halifanyiwi kazi, sijui kwa nini?!.
P
 
Back
Top Bottom