makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Wanajamii wa JF,
Mimi huwa napenda sana kusikiliza mashairi ya huyu jamaa anayejiita 'Mjomba' au Mpoto. Kuna shairi huwa analighani kwa kusema,namnukuu,"This country Bwana is very poor", mwisho wa kunukuu. Kwamba haya maneno huwa yanasemwa na viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuongoza na kusimamia Taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo BOT.
Mpoto anamaanisha kwamba viongozi hawa wanawadanganya Wa-bongo kuwa nchi hii ni maskini na fukara ya kutupwa. Lakini wakti huo huo hawa viongozi wanazitumbua fedha mabilioni kwa mabilioni kwa kununulia magari ya bei mbaya na kukarabati majengo ambayo hayana thamani hata ya hayo mabilioni ya ukarabati!!
Mnashangaa ukarabati wa nyumba ya Gavana Ndulu kugharimu Tshs. Bilioni 1??? Mbona Ikulu ya JK huwa inatengewa BILIONI 5 za ukarabati kila mwaka????Nenda pale TANESCO uone kile ambacho Idrisa Rashid amefanya! TANESCO wamekarabati nyumba kwa mabilioni halafu wanataka kujiuzia kwa vimilioni kiduchu!!
Wachunguzi wa mambo na wathaminishaji wa majengo wanadai kwamba hii Bilioni 1 Tshs sawa na Pound sterling kama 500,000 ukiingia nayo katika jiji la Malkia Elizabeth pale Londoni utapata nyumba mbili za nguvu za kununua siyo kupangisha!
Hii ndiyo Tz bwana. Kila mtu akipewa nafasi ni kutafuna fedha kama mchwa kwa kwenda mbele. Nani atakuuliza bwana wewe maana huu ni ulaji unaohusisha mtandao mzima wa mafisadi wale wale wa Chama Twawala-CCM.
Hao mnaosema eti tuna Gavana Makini nawasikitikia sana. Nchi hii haina kiongozi makini hata mmoja katika eneo liwalo lote la kiuongozi. Tutaendelea kushuhudia uoza huohuo ulifanyika wakti wa marehemu Balali na kina Liumba!
Ni wizi mtupu!!!!!
Narudia tena kauli yangu kuwa nchi hii imelaaniwa!