Tuhuma za mh. Lissu dhidi ya majaji zifanyiwe uchunguzi wa kina

Alichosoma Lissu ni malalamiko toka kwa majaji waandamizi

Very true; na Jaji Ramadhani kabla hajastaafu alishampelekea raisi malalamiko haya. Kwenye mkutano (kama sikosei ilikuwa ni siku ya Sheria duniani); raisi alilijibu kisanii katika hotuba yake kwa Majaji, mahakimu etc. Raisi alisema mie naletewa majina- nileteeni majina acheni kulalamika" In other words raisi alitupa lawama kwa mtu anayemletea majina (i guess Jaji Mkuu wa wakati huo-Ramadhani, na washauri wake). Kwakweli alijiaibisha mwenyewe kwasababu; Jaji Mkuu na kamati yake ndio wanaopendekeza majina; na ndio waliopeleka malalamiko. Sasa JK ana walaumu vipi tena? Taarifa zinasema JK anapopata majina huwa anakaa na watu wake nakuyapitia; yale majina ambayo yanaonekana mwiba kwake anaondoa- anaingiza watu wake watakaomlinda at any cost. Same applies to Mahakimu.

Kuna watu ambao JK amewapa ujaji ilihali ni wagonjwa wa muda mrefu. Watu hao hawajaweza kuandika hukumu yeyote toka wameanza kazi. Kuna yule jaji alifariki miezi sita baada ya kuapishwa. Alikuwa mjane, baadhi ya watu wakapeleka maombi kwa raisi awaachie watoto ile nyumba ya serikali mama yao aliyokuwa anaishi kwani ni yatima. Sijui hili lilifikia wapi. Kuna mwingine (namuhifadhi kwani ana ndugu yake huku JF) yeye naye hajaweza kuandika hukumu yeyote toka aapishwe-ni mgonjwa wa muda mrefu sasa. Wote hawa waliapishwa ili waweze kupata benefits za majaji (nyumba, mshahara, matibabu n.k). Kuna waliopewa ujaji baada ya kufanya kazi muda mrefu usalama wa taifa e.g. Retired Jaji Ihema (yeye alianzia usalama wa taifa).Ukweli ni kwamba majaji na mahakimu idadi yao inaonekana ni nyingi lakini watendaji/wenye ujuzi hasa kwenye hiyo fani ni wachache mno, wengine wanasindikiza msafara. Hii ni bubble ambayo itakuja kupasuka vibaya soon or later- hasa wale wajuzi wenyewe watakapostaafu wote.
 
my friend, majaji wangekuwa wameteuliwa kwa vigezo vya ujuzi na kufuata utaratibu sahihi, hakika yake wasingekuwa mambumbumbu namna hiyo. kwa wale wanasheria wanaoenda high court wanajua hili kuwa, kuna majaji kibao ambao kwanza hawana maadili, hawana historia ya maadili huko walikotoka (either kama walikuwa kwenye sector ya AG, mawakili wa kujitegemea au mahakimu). ........wana kiburi hao, kama huamini kaulize wasajili wa mahakama kanda mbalimbali,kwa hawa wanadamu, sina la kusema....hawana maana.

Haha umenikumbusha yule jaji (anatoka maeneo hayo ya senene) alishikana shati na mwenzie wakati wa chai kazini. Kisa mmoja kapeleka umbea kuhusu mwenzie kwa jaji mkuu (wakati huo ni Ramadhani). Yule jaji (sikumbuki jina kama ni Rweyemamu- ameshastaafu sasa lakini) akaanza kujigamba yeye ameshafanya kazi usalama wa taifa hakuna anayemtisha etc etc. Alitoa majigambo kweli mbele ya wenzie.
 
kama tumeshindwa kufata mfano wa jirani zetu Kenya katika mazuri tutaendelea kudidimia,wenzetu wanafanya vetting ya hali ya juu kama judge au hakimu alifanya madudu katika hukumu anawekwa kando sasa cjui kwann sisi kila kitu tunaingiza siasa na maslahi binafsi hii ni mbaya sana kwa mustakabali wa taifa letu tuache ushabiki wa kisiasa ila itatugharimu sana baadae
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom