Tuhuma za mauaji dhidi ya Dr. Mwakyembe na wenzake

banyimwa

Senior Member
Mar 1, 2011
116
23
Wana JF, pamoja na kwamba ninafahamu kwamba Polisi hufanya kazi zao kwa kuangalia ratiba yao wenyewe na mara nyingi bila shinikizo, ninashawishika kuuliza hatma ya tuhuma zilizotolewa na Dr. Mwakyembe kuhusiana na njama za kumuua yeye pamoja na watanzania wengine sita. Tuhuma hizi zimekabidhiwa Polisi miezi kadhaa sasa lakini mpaka sasa hatupewi hata update kuhusiana na upelelezi ulipofikia na kama kuna ukweli wowote kuhusiana na tuhuma hizo. Basi kama ni za uzushi tuambiwe ili ifahamike kwamba habari hizo zilikuwa ni za kutungwa na ikiwezekana aliyetoa tuhuma achukuliwe hatua.

Kwa kweli kigugumizi hiki, hakitoi taswira nzuri sana kwa kutendaji na uadilifu wa jeshi letu la Polisi na inanikumbusha tuhuma zilizopata kutolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye alishusha tuhuma nzito kuhusiana na njama za Polisi na mfanyabiashara mmoja kumuwekea mihadarati mtoto wa bwana Mengi ili akamatwe na Polisi. Hatujasikia chochote hadi sasa na wale waliotuhumiwa wanazidi kupeta na wengine wanaendelea kushikilia nyadhifa zao. Je ingekuwa tuhuma hizi zimetolewa na kigogo mkubwa serikalini au mfanyabiashara mwingine kama hawa wenye asili ya kiasia hali hii ingejitokeza? Hivi jeshi hili linaangalia usalama wa raia gani?
 
This is probably the lowest point in the discharge of public duties. Precedent iliyokuwa set by the Police and the intelligence services. Watu wao wamekuwa implicated na hii ni mara ya pili (kumbuka lalamiko la Mengi) lakini jinsi wanavyosua sua inaleta picha kana kwamba wakubwa wao wanalijua hili na wanasita kuchukua hatua kwa vile wanahusika.

Hapa yanaibuka maswali kadhaa juu ya dhamira ya Polisi kulinda usalama wa raia na mali zao. Kubwa kati ya maswali hayo ni kwamba: Je, kama watu wakubwa hivi wanawasilisha malalamiko kuhusiana na usalama wao kuwa hatarini na wanapuuzwa, sisi wadogo si itaonekana kama vile ni mdudu tu ametuhumu? Haya hayakutarajiwa kwa jeshi linaloongozwa na mtu makini na mwenye weledi kama Afande Mwema kufanya mambo kama haya. Tunadhani wanatakiwa sasa wajitoe katika ukimya huu ili alinde heshima yake. Vinginevyo ataonekana ametekwa na mafisadi ambao wako all out kuwa-eliminate mahasimu wao.
 
Polisi wamegundua waliotaka kumuua ni wale wanaotufanyia maamuzi watz
 
Wenzagu naona mnashindwa kuijua nchi yenu, kama ccm wanatumia muda mwingi kuchafuana na kugombania msosi wa watu wenye shida. UKWELI NI KWAMBA,
SERIKALI IKIFANYA CHINI JUU BEI ZA MAFUTA ZIKASHUKA,
BARABARA ZIKATENGENEZWA ILI BEI ZA MAZAO YA CHAKULA ZIKASHUKA
WALIMU NA WAFANYAKAZI WA SEKTA YA AFYA WAKABORESHEWA MAFAO YAO, JESHI LA POLISI NALO LIKAKUMBUKWA KWENYE MAFAO NDIKO KUTAKUWA NI KUKONGA NYOYO ZA JAMII NA KUPENDA SERIKALI YAO. HADISI ZA KUJIVUA GAMBA HAZISAIDII KITU NDO MAANA TUNAWAONA WANAO TUKERA NA MALUMBANO YASIYO NA TIJA KIUCHUMI, KWASABABU YA MADARAKA.

HATUSHANGAZWI NA KESI NYINGI KUYEYUKA KWA SABABU YA RUSHWA ILIYOKUWA KITU CHA KAWAIDA KWENYE IDARA ZOTE ZA SERIKALI. MFANO MI NDUGU YANGU ALIUWAWA NA WATU WASIO JULIKANA, LAKINI KUPATA KIBALI CHA MAZISHI, BILA AIBU POLISI (NAHIFADHI JINA LAKE WA KIJITONYAMA) MPAKA APEWE SH. 30,000 NDO ALITOA KIBALI HICHO! ITS A SAD SITUATION.
 
By the way, hivi ile kesi ya mtoto wa Lowassa kumgonga Traffic imeishia wapi?
 
Serikali ya Mafisadi itawezaje kukemea vitendo vya kifisadi?

Sidhani kama comment hiyo ni sahihi. Hapa issue iliyopo ni kwamba kuna ufisadi kati ya baadhi ya wakubwa kwenye vyombo vya dola na watuhumiwa. Serikali siyo ya kifisadi japo kuna watumishi ambao wana chembe za ufisadi na hao ndiyo wanaotukwamisha.
 
Kama kuna watumishi mafisadi ndani ya serilikali na sirikali haichukui hatua dhidi yao basi ujue serika nayo ni fisadi. Kwa sababu wanalindana.
 
Na ya slaa kutegwa vinasa sauti na kamera kwenye chumba chake akiwa bungeni dodoma, wakati wa bunge lililo pita iliishia wapi?
 
Wana JF, pamoja na kwamba ninafahamu kwamba Polisi hufanya kazi zao kwa kuangalia ratiba yao wenyewe na mara nyingi bila shinikizo, ninashawishika kuuliza hatma ya tuhuma zilizotolewa na Dr. Mwakyembe kuhusiana na njama za kumuua yeye pamoja na watanzania wengine sita. Tuhuma hizi zimekabidhiwa Polisi miezi kadhaa sasa lakini mpaka sasa hatupewi hata update kuhusiana na upelelezi ulipofikia na kama kuna ukweli wowote kuhusiana na tuhuma hizo. Basi kama ni za uzushi tuambiwe ili ifahamike kwamba habari hizo zilikuwa ni za kutungwa na ikiwezekana aliyetoa tuhuma achukuliwe hatua.

Kwa kweli kigugumizi hiki, hakitoi taswira nzuri sana kwa kutendaji na uadilifu wa jeshi letu la Polisi na inanikumbusha tuhuma zilizopata kutolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye alishusha tuhuma nzito kuhusiana na njama za Polisi na mfanyabiashara mmoja kumuwekea mihadarati mtoto wa bwana Mengi ili akamatwe na Polisi. Hatujasikia chochote hadi sasa na wale waliotuhumiwa wanazidi kupeta na wengine wanaendelea kushikilia nyadhifa zao. Je ingekuwa tuhuma hizi zimetolewa na kigogo mkubwa serikalini au mfanyabiashara mwingine kama hawa wenye asili ya kiasia hali hii ingejitokeza? Hivi jeshi hili linaangalia usalama wa raia gani?

Mkuu heading ilivyo nikajua kina Dr.Mwakyembe wanakabiliwa na tuhuma za mauaji!
 
hivi mtu anayesoma kwa kutumia cheti cha mwenzake kweli unadhani ana muda wa kufanya upelelezi? NDIO Jeshi letu la Polisi
 
Back
Top Bottom