Baadhi yetu tulisoma na kuisikia ripoti ya Dr Mwakyembe kuwa kundi la Al-shabab toka Somalia likishirikiana na Wahalifu sugu wa hapa kwetu Tanzania, limekodiwa na baadhi ya wanasiasa kwa ajili ya kuwaua baadhi ya viongozi hapa nchini kama Dr Slaa, Prof Mwandosya, Anne Kilango, Bernad Membe na Mfanyabiashara maarufu Reginald Mengi pamoja na yeye mwenyewe Dr Harison Mwakyembe، zile ni tuhuma nzito sana maana ziligusa Serikali, Uhamiaji, Polisi, Usalama wa Taifa,viongozi wa serikali, watu binafsi na rasilimali za Taifa,
Je? Serikali inayotawala na vyombo vyake waliamua kumpigia magoti baada ya kuona mpango wao umevujishwa?
Walifanya nini wakati watuhumiwa wanajulikana majina yao na walipokuwapo hapa nchini pamoja na wenyeji wao? Je kwa
hali hii haitaonekana serikali iko likizo na haina Mtawala?
Serikali isingepaswa itoe tamko kama ni kweli au ni uzushi ili aliyetoa uzushi akamatwe kwa kuhatarisha usalama wa Taifa? Hii inadhihirisha ndani ya serikali kila mtu ana jeshi lake na usalama wake wa Taifa! Hili halina ubishi. Ufalme umegawanyika tayari:
Nataka mchango wenu Great thinkers maana najua mnajua mambo mengi pia: