Tuhuma za Kukashifu Viongozi: Jinsi Wananchi Wanavyoonewa Bure!!

tk

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
270
6
Mtanzania, Jumamosi Novemba 14, 2009

Aliyewakashifu Mkapa, Mwinyi adhaminiwa

Na Evaline Shayo, TSJ

MKAZI wa Arusha, Anney Anney, anayetuhumiwa kuwakashifu marais Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, amepata dhamana.

Anney, ambaye ni mlemavu wa miguu, alifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Ilala Julai 23, mwaka huu, kwa tuhuma za kuwakashifu marais hao. Dhamana ilikuwa wazi, lakini hakupata wadhamini.

Mwendesha Mashataka, Daniel Juma, mbele ya Hakimu Samwel Maweda, alidai kwamba mtuhumiwa huyo aliwakashifu Mwinyi na Mkapa, huku akimsifia Mwalimu Julius Nyerere.

"Mwinyi aliua Azimio la Arusha, Mkapa aliuza mashirika yetu na nyumba za umma. Wewe unauza ardhi yetu kwa Wazungu na Waarabu pamoja na utu na utaifa wetu. Nyerere alilinda ardhi yetu, utaifa na uzalendo, udumu ujamaa na kujitegemea, lidumu Azimio la Arusha, zidumu fikra za Mwalimu Nyerere." anadaiwa alisema mtuhumiwa huyo.

Mtuhumiwa huyo yuko nje kwa dhamana hadi Novemba 19, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.
 
Maswali ya kujiuliza:

1. Jee kama mwanachi huyu, mlemavu, anashitakiwa kwa hayo aliyoyasema, hivi wana JF wafanyweje maana wanayasema hayo na zaidi ya hayo kila siku.

2. Hivi hawa wanaojiita wanaharakati wako wapi. Hata kumtetea mahakamani wala kumuwekea dhamana hamna?

3. Hapa anashitakiwa Anney Anney au Nyerere?

4. Katika yote aliyoyasema ni lipi la uongo?

5. Mtu kutoa mawazo yake kuhusu anavyoyaona mambo ni kosa?

 
Back
Top Bottom