Tuhuma nzito za ufisadi dhidi ya Mwakyembe pale ATC

Status
Not open for further replies.
mleta mada unasomeka sana, ata kama una ugomvi na Mwakyembe, lakini uliyoelezea yanaingia akilini, kuna viongozi fulani wameshajinyakulia huruma kutoka kwa wanachi, kila utakachoandika kuhusu wao ata kama ukweli itaonekana ni uongo tu, kwa kuwa sijui mpambanaji, dola laki 2 kwa mwezi ni hela nyingi sana, ningependa kuona mchanganua wa mahesabu wanaipataje hiyo dola laki 2 ya kulipa kwa mwezi.
 
Ndugu yangu Msambule, kuna biashara yeyote umeshawahi kuifanya tangu uzaliwe?

Hii biashara yako (ya ATCL) imejaa mapato na wala haionyeshi matumizi (Je, ni kwamba unaficha ukweli wa hasara tarajiwa?). Acha nikusaidie, kwenye usafiri wa anga, asilimia 40 (40%) ya mapato yako yote huenda kwenye mafuta na matengenezo (kwa kila trip!). Kwa hiyo kila trip mwenye ndege anabaki na asilimia 60 (yaani 60%).

Katika hiyo asilimia 60 tunaanza mchanganuo sasa:
- Malipo ya wafanyakazi (hapa tuna maanisha wafanyakazi wote wa ATCL mpaka mfagizi na mlinzi)
- Malipo ya vyakula na vinywaji vya ndani ya ndege (kwa taarifa yenu: soda moja unayokunywa ndani ya ndege, ATCL imeinunua kwa zaidi ya Tsh 2500/-, kama watu hawalifahamu ili nitarudi baadaye kulielezea)
- Kuna tozo ya kiwanja (kila inapotua)
- Kuna tozo ya ma-agent wa ATCL (yaani wakatisha ticket, kwenye bei ya ticket uliyosema sio kwamba hela yote ni ya ATCL, kuna percent ya mawakala (agents).

Sasa katika hiyo asilimia 60 ondoa gharama hizo hapo juu, kisha angalia unabaki na kiasi gani. Then mwisho wa mwezi ufanye hayo malipo yako ya kukodi ndege (yaani USD 200,000)

Halafu mkae mkijua sio kila siku atakuwa na uwezo wa kuruka safari sita (six times) tena kwa kutegemea ndege moja. Lazima kuna siku itakuwa matengenezoni/ ama imeharibika na kutakiwa ku-cancel safari zote sita! Pili hiyo route ina mshindani mkubwa PW (Precision Air) na yeye ameamua kufanya safari ya Kutoka Dar kwenda Mwanza na Kurudi Dar kuwa Tsh 199,000. Kwa maana hii ATCL itaendelea kusubiri abiria wanaokosa nafasi PW, au nae akubali kushusha zaidi bei yake ya Tsh 257,000 (ambapo ni hasara zaidi).

Tatu na mwisho sio kwamba trip zote ATCL itapata abiria 50, kuna wakati atakuwa na abiria 20 tu!! Hii ni kitu cha kawaida sana kwenye biashara ya ndege, na asilogwe ku-cancel safari kwa sababu ya uchache wa abiria, akifanya hivyo basi anajichimbia kaburi kabisa!

Nitarudi tena!

Rudi haraka,mwenzio pamoja na kuegemea upande wa mapato tu,lakini kaweka mahesabu na sio hadithi kama yako,leta mahesabu ya hayo matumizi, nadharia uanazotuwekea hazitusaidii kuujua ukweli wa kile unachotaka tujue, 40% sijui 60% ndiyo nini ? hakuna matumizi ambayo huwa ni 40%. kama ni mafuta itakuwa ...@ litre na mishahara itakuwa TZS au USD,achana na kujificha kwenye %%% yako leta hesabu hapa au kalale ukue
 
Pole kaka kwa hasira hila mikataba ya ndege mara nyingi huwa ni ya masaa ya hewani kwa faida ya mkodishaji (huwa wanapanga masaa kama ulivyoelezea), faida ya mtumiaji hutokana na abiria na bei za trip ya ndege; maana contract zingine zinasema wazi kabisa ndege isisafiri zaidi ya masaa fulani. So it is up to ATC accountants and their marketing teams to know kama kuna biashara hapo au hakuna kutokana na demand and looking at their contract terms in terms of a profitable business venture.

Tatizo hapo sio Mwakyembe, tatizo hapo ni raisi asielewe kuwekeza kwenye baraza la mawaziri wake, huyo Mwakyembe hana background ya business whatsoever, hilo tu lina m-disqualify kushika wizara yeyote ya uchumi especially as important as that one, na ukizingatia kimbele mbele chake na kujifanya mjuaji ni ataboronga tu. Maana hutakuta analizimisha issues ambazo hajui hasara zake for the sake ya kwamba aonekane ameleta ndenge (rahisi kudanganywa kibiashara).

Hawa sio watu wakusema they can come up with an objective and analyse it to find a better solution (pengine ndio sababu hawaoni umuhimu wa ndege mpya na faida zake in the long run), unaweza ukanona Mwakyembe ni tatizo wengine tunaona ni huwezo wake ambao ni dhaifu ndio chanzo. Na tuna sababu zote kwanza he is not a qualified person to run the ministry straight up because of his background kwa maana hiyo we expect uozo anything else would be a success by chance.

Biashara haisomewi, unaiweza au huiwezi,acha ujinga mkuu. isitoshe waziri ni mwanasiasa,wizara imejaa wataalam lukuki,kazi ya waziri ni kuwatumia wataalam ili kufikia malengo yanayotarajiwa,sio lazima waziri awe wa fani fulani ili aweze kutenda yapasayo,mara ngapi wataalam husika wakiwekwa wizara husika wameshindwa kukoga nyoyo za watz ?
 
Nani anaweza sasa? maana nundu alikua mtaalamu hiyo mambo ya ndege! Mnatubabaisha na chuki zenu bwana.ujuaji gani unauzungumzia kuongea uozo hadharani? ulitaka afanye siri kama jando?kwa hali ilivyo tz kila kitu ni bora kiwe hadharani maana hatuwaamini tena viongozi hasa wanaojifanya kufanya vitu kwa vificho kana kwamba eti ndiyo busara na hawana kimbelembele kumbe wanatuibia tu. Sasa mmetumwa kududanganya hapa wala hatuwasikilizi
 
.............Mwakyembe aachwe afanye kazi ... tutaanza kuhoji utendaji wake kuanzia Jan mwakani... maana nayeye anaahadi nyingi alizo toa zinazohitaji utekelezaji
 
Kwakweli sidhani km kuna ukweli hapo,fanya uchunguzi wa kina utupe ushahidi wa kutosha,unless otherwise ni chuki binafsi dhidi ya Mwakyembe.
 
Inawezekana mkuu una hoja katika hili ila Authenticity of your explanations has never been clear!!!
 
Kwangu mimi yote ni sawa tu. Sitamtetea mtu hta mmoja ktk serikali hii. Awe Mwakyembe au Utoh na wengine wote akili ni ile ile.

Mtoa mada anaweza kuwa na hasira zake lakini zikatusaidia kujua yasiyosemwa. Kwani CAG ni mtakatifu? Hayo majumba anayojenga tangu Morogoro hadi Dar hadi Mbeya na Arusha ni mshahara gani huo? Wooote mafisadi tu!
 
Mmmm, wakuu, tuache majungu, Mwakyembe ameweka dira, hata bei za Precion naona kama zimeshuka hivi, i think because of compitetion!

Mkuu umeweka data za ukweli tena za chini lakini kwa hiyo data ATC wana break-even. Umenikuna hapo kwa Precision. Ni kweli precision wanatubamiza sana. Nauli zao ziko juu bila sababu. Unakuta kwenye flight moja abriria mmelipa nauli tofauti bila sababu. Kwa mfano DAR-JRO-DAR kuna TZS422,000 au TZS375,500. Juzi juzi hapa walitangaza nauli ya TZS185,000 kwa route hiyo, the next day ika-shoot to TZS422,000. Kutokuwepo ushindani na Regulator wa Air fare kunatuumiza!
 
Biashara haisomewi, unaiweza au huiwezi,acha ujinga mkuu. isitoshe waziri ni mwanasiasa,wizara imejaa wataalam lukuki,kazi ya waziri ni kuwatumia wataalam ili kufikia malengo yanayotarajiwa,sio lazima waziri awe wa fani fulani ili aweze kutenda yapasayo,mara ngapi wataalam husika wakiwekwa wizara husika wameshindwa kukoga nyoyo za watz ?
Hizo bangi zako huwe ukishavuta unatafuta namna ya kuzikabili na si kuja kutuletea matusi humu ndani na kuongea hovyohovyo tu ilimradi.

Hiyo ndege unajuwa ilikuwa financed kivipi kwa mnunuaji wa kwanza kama walitumia cash or hire-purchase. Point hapo in thirty years time kama kulikuwa na biashara nzuri wameshalipa investments zao na faida juu au wamemaliza malipo na faida juu. Na bado kuendelea kwa mtindo wa faida wanamletea waziri kilaza asiejua kama ndege anaweza nunuwa mpya hata kwa hire-purchase, only he needs to ensure he runs that sector of that ministry as a business.

Tatizo lenu mmezoea sana kuitia hasara serikali ndio sababu za mashirika yetu kwenda hovyohovyo bila ya mipango sahihi ya kibiashara. Hiyo sector ya ndege hipo kwasababu za kibiashara why do we need mitumba kila siku especially kwenye mashirika ya serikali huu ni uhuni tu wa kuleta tender.

Sasa Mwakyembe angekuwa ana background angekuja hakatuelezea business decisions zilizotumika kwa faida yetu in the long run maana hilo dege likizima which wont be long inabidi tukodi lingine na mtu ajichukulie tender lingine na hatuja jenga equity yoyote kwenye hiyo ndege zaidi ya pengine kuwaambia tulipewa nzima tumehiharibu na tulipe wehuoni upuuzi huo.

On the other kama tutachukua za hire-purchase in time tunaweza badilisha tu na kupewa zingine at discounted prices keeping in touch with other airliners and better quality services. Kuna mengi sioni sababu za kukuelezea wewe umeshazoea biashara za dalala unadhani na ndege zinaweza jisimamia hovyohovyo na kuchukua habiria ndio maana huwezi kuona risk zilizopo na strategies zinazo itajika Waziri akiwa kama msimamizi mkuu kama hajui mengi ya hapo surely it is very easy kuongopewa.

Halafu unasema uoni umuhimu wa msimamizi wa hii wizara kuwa na background yoyote ya kibiashara si ndio sababu za haya matatizo yetu yasio hisha huko kwenye mashirika ya umma.
 
Nani anaweza sasa? maana nundu alikua mtaalamu hiyo mambo ya ndege! Mnatubabaisha na chuki zenu bwana.ujuaji gani unauzungumzia kuongea uozo hadharani? ulitaka afanye siri kama jando?kwa hali ilivyo tz kila kitu ni bora kiwe hadharani maana hatuwaamini tena viongozi hasa wanaojifanya kufanya vitu kwa vificho kana kwamba eti ndiyo busara na hawana kimbelembele kumbe wanatuibia tu. Sasa mmetumwa kududanganya hapa wala hatuwasikilizi
kipi alichokiweka hadaharani ambacho kimekufurahisha hivyo mmpaka we uone huyu jamaa anayo busara ya hivyo au unakuwa kama kenge tu kwenye msafara wa mamba.
 
Hizo bangi zako huwe ukishavuta unatafuta namna ya kuzikabili na si kuja kutuletea matusi humu ndani na kuongea hovyohovyo tu ilimradi.

Hiyo ndege unajuwa ilikuwa financed kivipi kwa mnunuaji wa kwanza kama walitumia cash or hire-purchase. Point hapo in thirty years time kama kulikuwa na biashara nzuri wameshalipa investments zao na faida juu au wamemaliza malipo na faida juu. Na bado kuendelea kwa mtindo wa faida wanamletea waziri kilaza asiejua kama ndege anaweza nunuwa mpya hata kwa hire-purchase, only he needs to ensure he runs that sector of that ministry as a business.

Tatizo lenu mmezoea sana kuitia hasara serikali ndio sababu za mashirika yetu kwenda hovyohovyo bila ya mipango sahihi ya kibiashara. Hiyo sector ya ndege hipo kwasababu za kibiashara why do we need mitumba kila siku especially kwenye mashirika ya serikali huu ni uhuni tu wa kuleta tender.

Sasa Mwakyembe angekuwa ana background angekuja hakatuelezea business decisions zilizotumika kwa faida yetu in the long run maana hilo dege likizima which wont be long inabidi tukodi lingine na mtu ajichukulie tender lingine na hatuja jenga equity yoyote kwenye hiyo ndege zaidi ya pengine kuwaambia tulipewa nzima tumehiharibu na tulipe wehuoni upuuzi huo.

On the other kama tutachukua za hire-purchase in time tunaweza badilisha tu na kupewa zingine at discounted prices keeping in touch with other airliners and better quality services. Kuna mengi sioni sababu za kukuelezea wewe umeshazoea biashara za dalala unadhani na ndege zinaweza jisimamia hovyohovyo na kuchukua habiria ndio maana huwezi kuona risk zilizopo na strategies zinazo itajika Waziri akiwa kama msimamizi mkuu kama hajui mengi ya hapo surely it is very easy kuongopewa.

Halafu unasema uoni umuhimu wa msimamizi wa hii wizara kuwa na background yoyote ya kibiashara si ndio sababu za haya matatizo yetu yasio hisha huko kwenye mashirika ya umma.

umetota umebaki kuropoka ropoka tu,ulitaka mkakati uliofikiwa hadi kukodisha ndege hiyo uwekwe hapa JF ? kwa dhamila ya kuwa top poster kwa pumba hizi utaweza.
Swala la ilikuwa financed vipi ni irrelevant hapa,ndege imekodiwa tusubiri matokeo kwani hatuna biz plan ya ATC ambayo tungekuwa tunaikosoa,tatizo wewe kwa nia ya kuwa na post nyingi JF unakuja na utabili ili upate support hapa,nani anasupport up.u.u.zi hapa ?

ungeonyesha strategic plan ya ATC na mapungufu yake ungeweza kuwa na hoja,unabwabwaja tu,hujui mpango makakati wao ukoje na unatekelezwa vipi wewe unauunda board ya ATC kichwani mwako na unajipa UCEO wa ATC kichwani mwako then unaanza kukosoa utekelezaji wa kile usichokijua kwa kutegemea kulinganisha na ndoto zako za mchana, ooh hire purchase or sijui ndoto gani nyingine. Bangi zako zinakuambia haya purchase ndiyo the best option ? watu wengine Mungu awasamehe tu.
Pole kama unaumizwa na utekelezaji wa mipango ya ATC
 
Kaka taratibu

Utafukuza watu JF!

Uchambuzi wa namna hii hautakiwi humu. Lakini potelea mbali

sasa hapo juu umewataja PW...lakini kuna jinamizi lingine linakuja kuwamaliza kabiasa hawa ATC linaitwa FASTJET.

Latest ni kuwa FastJet has reportedly signed up for 2 more Airbus A319 aircraft, configured with 150+ seats in an all economy version na jamaa wanataka within mwaka mmoja wawe na flights 15 na bila kusahau kuwa nauli yao wanasema itakuwa ni usd 20 (of course minus gharama zinginezo lakini I'm sure nauli yao itakuwa much lower than ATC) Sasa hapa ATC watakuwa na lao? Mie naona ATC wataishia kwenda Mafia tuuu. Route ya Nairobi waisahau.

Sasa angalia management ya Fast Jet ikoje? kwanza wameenda kumchukua Bob Bishtom toka EasyJet as COO na kutoka Ryan Air H. Cordan as Chief of Flight Operations, besides the appointment of Kayle Haywood as Regional General Manager (all reporting to CEO Ed Winter). In short hii biashara inayopesa maana hawa waingereza na wa Irish wasingeingia kwa nguvu zote hizi. Haiwezekani Haji Stelios wa Esy Jet avamie African Aviation na kisha aamue kuweka Hub Tanzania na Mwakyembe and Co bado wanaendelea kukodisha ndege ya miaka 32 ambayo ina gharama kubwa sana kui operate. Did I mention yaliyowakuta FLY 540?

Kingine huyu Mwakyembe na mafisadi wa ATC wamesahau kuwa PW wako kitanda kimoja na KQ and they are not there kufanya mchezo bali kutengeneza noti...

Last but not least hawa RwandAir wanampango wa kushusha at least two brand new B787 Dreamliners by about 2015.

Sisi hapa bado tuko humu tunatetea ufisadi na hujuma ya Mwakyembe na wahuni wa ATC.

ungekuwa unabwabwaja huku ukituonesha mpango mkakati wa ATC dhidi ya hao PW na hao wazungu wanaokuzingua hakika hoja yako dhaifu ingepata nguvu,umeweka mikakati ya washindani wa ATC huku ukiwa kimya kwa mikakati ya ATC ambayo utakuwa huijui then wataka kutuingiza mkenge. Pole sana..
 
Hizi allegations hata kama ni za kweli zimekaa kimajungu zaidi kitu amacho kinafanya kuwa ngumu kuzikubali moja kwa moja.

Ungetaka thread yako iwe na mshiko ungeiandika objectively. Too much subjectivity in your thread. For that case, I'm out.

...Dude dwells on majungu!! Inhales & exhales these stuffs irrespective of his extraordinary academic exposure!!
...subjectivity and uncalled for chuki bundled together in a rather very informative subject. Sad!
 
kipi alichokiweka hadaharani ambacho kimekufurahisha hivyo mmpaka we uone huyu jamaa anayo busara ya hivyo au unakuwa kama kenge tu kwenye msafara wa mamba.

eeh sawa hata kama niko kama kenge it is ok lakini yuko sahihi na sisikilizi upumbavu wako! Umetumwa na mafisadi na umezoea kutuibia! hapo unapoteza muda wako hatudanganyiki!
 
hizo bangi zako huwe ukishavuta unatafuta namna ya kuzikabili na si kuja kutuletea matusi humu ndani na kuongea hovyohovyo tu ilimradi.

Hiyo ndege unajuwa ilikuwa financed kivipi kwa mnunuaji wa kwanza kama walitumia cash or hire-purchase. Point hapo in thirty years time kama kulikuwa na biashara nzuri wameshalipa investments zao na faida juu au wamemaliza malipo na faida juu. Na bado kuendelea kwa mtindo wa faida wanamletea waziri kilaza asiejua kama ndege anaweza nunuwa mpya hata kwa hire-purchase, only he needs to ensure he runs that sector of that ministry as a business.

Tatizo lenu mmezoea sana kuitia hasara serikali ndio sababu za mashirika yetu kwenda hovyohovyo bila ya mipango sahihi ya kibiashara. Hiyo sector ya ndege hipo kwasababu za kibiashara why do we need mitumba kila siku especially kwenye mashirika ya serikali huu ni uhuni tu wa kuleta tender.

Sasa mwakyembe angekuwa ana background angekuja hakatuelezea business decisions zilizotumika kwa faida yetu in the long run maana hilo dege likizima which wont be long inabidi tukodi lingine na mtu ajichukulie tender lingine na hatuja jenga equity yoyote kwenye hiyo ndege zaidi ya pengine kuwaambia tulipewa nzima tumehiharibu na tulipe wehuoni upuuzi huo.

On the other kama tutachukua za hire-purchase in time tunaweza badilisha tu na kupewa zingine at discounted prices keeping in touch with other airliners and better quality services. Kuna mengi sioni sababu za kukuelezea wewe umeshazoea biashara za dalala unadhani na ndege zinaweza jisimamia hovyohovyo na kuchukua habiria ndio maana huwezi kuona risk zilizopo na strategies zinazo itajika waziri akiwa kama msimamizi mkuu kama hajui mengi ya hapo surely it is very easy kuongopewa.

Halafu unasema uoni umuhimu wa msimamizi wa hii wizara kuwa na background yoyote ya kibiashara si ndio sababu za haya matatizo yetu yasio hisha huko kwenye mashirika ya umma.

nyie ndiyo majizi mnaifilisi nchi kazi ktunga uongo tu
 
dr-harrison-mwakyembe.jpg

mimi katika vitu vilivyonishinda humu ni mabishani ya nani zaidi kati ya ccm na chadema. Sasa nimeona bora nikufahamisheni mwakyembe ambaye anajisifia kuwa mpinga rushwa mkubwa alivyokuwa fisadi na ushaidi wote nauweka hapa na kama kuna mtu anabisha aendelee.

Kwa kifupi wafuatao wanahusika kwenye huu wizi:

Harrison mwakyembe
management nzima ya atc
bodi ya atc
kamati ya bunge ya mashirika ya umma
external auditors wa atc
ludovick utuoh ambaye ni mkaguzi mkuu wa serikali

tuhuma zenyewe ni kama ifuatavyo:

1. Shirika la ndege la taifa (air tanzania) waliamua kukodisha ndege yenye umri wa miaka 32 aina ya b737-200 iliyozeeka na mbovu kutoka kampuni ya africa kusini inayoitwa star air cargo.

2. Ndege hii ilianza kufanya kazi mwaka 1980 kule uk, na ilikuwa inatumiwa na kampuni inayoitwa british airtours na baada ya hapo ilikodishwa na mashirika zaidi ya 20 ulaya na latin america.

3. Mwakyembe, menejimenti na bodi mpya ya atc walikubali na kupitisha ukodishaji wa hii ndege kwa kiasi cha dola laki 2 (200.000 us dollars) kwa mwezi katika miezi 3 ya awali ya ukodishaji kinyume na ushauri ambao mwakyembe na maswahiba zake wa atc walipewa.

4. Mkataba unaonyesha kuwa itabidi ndege hii itabidi iruke kwa masaa 150 kwa mwezi at a rate of 1.350 us dollars for each hour.

5. Mkataba unaendelea kusema kuwa atc lazima wagharimie gharamza zote za ma crew ambayo iko estimated to be in the region of a further $80 – $100 per day & per individual !

(katika mazingira ya kawaida msomaji utaona gharama ni ndogo lakini ukweli ni kubwa sana uzingatia kuwa ndege yeneyewe inasafiri kwenda sehem 3 tuu yaani kati ya dar es salaam – kilimanjaro – mwanza na hii yoye iko funded na walipakodi wa tanzania).

Sasa ukweli ni kuwa kama kweli mwakyembe & kundi lake wana nia nzuri wasingekubali dili hii ipitishwe kwa kuzingatia kuwa kwanza ndege inge cost less kuikodisha kuliko gharama ambazo hawa mafisadi wamepitisha, na pia hizi gharama za malipo kwa saa ni kubwa mno na hapa ndipo mwakwembe na kundi lake la mafisadi wanakula zaidi kwenye huu mgao.

Suala lingine la kuzingatia hapa ni operating costs ambazo mwakyembe & his crew wa atc ni uhuni mtupu kwani ndege ina miaka 32 na gharama za uendeshaji na hasa za matumizi ya mafuta ni kubwa mno ukilinganisha ndege za kisasa.

Kwa msiojua ni kuwa gharama za mafuta (fuel costs) kwa kawaida zinachukua around 40% ya overall costs lakini kama shirika linatumia ndege za kizamani basi ni wazi kuwa gharama zitaongezeka zaidi. Na uhuni uliofanywa na atc wakishirikiana na wahuni wenzao pale wizarani kwa mwakwembe ni kupiga rangi hizi ndege wakati wakijua wazi kuwa walipa kodi wanataka kujua mikataba iko kwa maslahi ya taifa (national interest).

Moja kati ya maswali ya kujiuliza ni kwa nini mwakyembe na atc walikataa kuchukua ndege kama crj ambazo ni ndogo zaidi lakini zina fly economically lakini pia ni kubwa kiasi kiasi cha kurestart hii biashara ya shirika kama atc. Lakini hii pia ni mfululizo wa uhuni unaoendelea kama ule wa awali wa kukodisha ndege toka kampuni ya arabuni ambayo intugharimu sana sisi walipa kodi kama ile ya uhuni wa awali wa ukodishaji wa airbus.

Sasa huyu mwakyembe ambaye anajifanya ni kinara wa kupiga vita ufisadi anakubali na amepitisha huu uhuni wa atc ambao utamgharimu zaidi mlipa kodi. Huu ni uthibitisho kuwa wanaolack vision si wale wa (pemba + zimbabwe ) pekee lakini mpaka huyu mwanasheria kama mwakyembe ambaye anaendeleza uhuni wa stop gap measures.

Sasa kaeni mkao wa kuona wanaleta maombi ya kutaka wapewe pesa zaidi ili waendelee kula. Na news zilizopo kwenye corridor za atc ni kuwa wana haha kama mbwa mwitu ili warejeshe safari za nairobi na hasa baada ya player mpya chini ya shirika la ndege la kenya (fast jet) kuingia kwenye soko.

Btw

nadhani mnaikumbuka ile ndege ya atc iliyoanguka kule mwanza? Bas ndio model hiyo hiyo aina ya b737-200 kama hii mbovu na iliyozeeka ambayo mwakyembe & his crew wanatuleta.

Uhondo zaidi uko hapa:

air tanzania company limited (atcl) has suspended its contract with the dubai based aviation company, aero vista, that saw the latter lease a boeing 737-500 plane to embark on domestic flights.

captain-milton-lusajo-lazaro.jpg

atcl ceo, captain milton lusajo lazaro

atcl leased a boeing 737- 500 plane with the capacity to carry 108 passengers, which has since then been embarking on the national flag carrier's dar es salaam-kilimanjaro-mwanza routes before launching the dar es salaam-hahaya (comoros) route last month.

The airline's acting chief executive officer, captain milton lazaro, said the company had reached that decision to ensure a win-win situation and sustainability from the contract.

he, however, said the company intends to undertake a contract review with aero vista adding that the company may go in for another company if the two sides do not reach a consensus on the matter.

"we had decided to suspend the contract earlier entered upon with aero-vista in order to ensure compliance with government pre-requisite. We may be able to re-enter a new contract with them after discussions on revision of some clauses that do not favour a sustainable outcome.
4.jpg

"passengers who are holding atcl tickets have been reallocated alternative flights with other carriers and notified accordingly," he said. He added that the national flag carrier will be able to be back on the routes after the completion of the maintenance exercise of its dash-8 q300 plane that is undergoing checks at the julius nyerere international airport in dar es salam.

Captain lazaro said, however, that only its dar es salaam-kilimanjaro-mwanza routes will be temporarily affected by the suspension urging that the airline continue with its three-time weekly flights between dar es salaam and hahaya (comoros).

"we regret the inconveniences that have been caused to our valued customers, we take this opportunity to thank them for their continued support and reassure that, the resumption of these services will take place as soon as possible," he said.

Source daily news.

wakati sisi tuko bize kukodisha ndege za miaka 32 na kutetea ufisadi wa akina mwakyembe & co, rwanda wao wameamua kufanya kweli na kuwa nchi ya kwanza africa kununua ndege 4 aina ya crj900ng ambayo wataalama wanasema kuwa ni the most economical short and medium range jets toka kwa kampuni ya bombadier. (wataalam wa mambo ya ndege watakuambieni ubora wa hizi ndege kulinganisha na mtumba wa atc)

ba-rwandair_delivery_3.jpg

hawa wa nyarwanda ambao tumewashinda kwenye kila kitu (kasoro akili). Kwa sababu wakati sisi tuko bize kusifiana upuuzi wao wameopt kununua state of the art modern aircraft ambayo ina gharama za chini sana kulinganisha na mitumba ya akina mwakyembe & atc lakini pia wao wameunyesha pride ya kununua ndege mpya badala ya kukodisha hizo ndege na hii inawapa sense of ownership na muhimu zaidi inawapa abiria confidence abiria wake wa safari zake za africa na mashariki ya kati

ndege hizi zina dual class configuration ya 7 business class seats kwa mpango wa 2×1 layout na 68 economy class seats katika mpango wa 2x layout, ambayo nadhani ni quite ideal for the short and medium distances ambazo rwanda air inasafiri.

Kwa kuonyesha kuwa hawa wa nyarwanda wako serious, wao hawataki tena mitumba na wanaondoa ndege walizokodisha aina ya dash 8-100 na badala yake wanaweka ngoma iliyokuwa advanced na kubwa zaidi zaidi toka bombadier q400, ambayo kwa sasa zinapatikana kwenye dual class configuration – type ya kwanza ilikuwa delivered kwa ethiopian airlines wiki chache zilizopita

sasa hivi air rwanda inakwenda nchi 14 na wanamipango ya kuongeza frequencies za key destinations zaidi ya 40. Sasa wao hawafkiriii kushindana na atc wao target ni kuwapiku kq. Sisi tuko hapa hatujajua bado kama tanzania ilitokana na pemba na zimbabwe au nchi ya kifikirika.

uongo mtupu na upuuzi!
 
Hii thread imejaa majungu yanayojionesha wazi km si mfanyakazi aliyebanwa na ulaji basi ni mjomba wake maana hawasemi ni nani aje mbadala wa Mwakyembe au Uttoh wao ni lawama tu.
Haya na mm ntaleta lawama MWAKYEMBE FISADI ANAKULA 800/ TRENI YA JIJINI DAR au atokeze mwingine wa Bandari MWAKYEMBE hafai sasa ni lini atapatikana mtu atakekaa mahali bila Lawama au asiye na TUHUMA NZITO?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom