Tuhuma nzito za ufisadi dhidi ya Mwakyembe pale ATC

Status
Not open for further replies.
Upuuzi huu ulipelekwa Rwanda wao wakawatimua wale ma middle men sasa cha kujiuliza waliweza vipi kuja Bongo, na kupiga dili na watu kama akina mwakayembe wakakubali ?

its ufisadi tuu hamna cha zaidi.

In a way I feel like ATCL kama vile imekuwa cursed.
Warussian na wachina ni watu wajanja wajanja tuu, hakuna maana kukodi ndege ili ufanye biashara. UFISADI
 
Hizi allegations hata kama ni za kweli zimekaa kimajungu zaidi kitu amacho kinafanya kuwa ngumu kuzikubali moja kwa moja.

Ungetaka thread yako iwe na mshiko ungeiandika objectively. Too much subjectivity in your thread. For that case, I'm out.
 
Enyi wabadhilifu na msiotaka kuwajibika wahanga wa uwajibikaji wa Mwakyembe huko ATC, Bandari na Reli, maumivu yakizidi mumtafute aliyekuwa anawatuma na kuwasponsa. Mimi naunga mkono Mawaziri kama Mwakyembe wanaoonyesha ushujaa wa kuwawajibisha watu kama nyie haijalishi mtamtungia single ngapi zisizouzika.
 
Huyu mleta mada popo kweli, yaani njaa yake anataka kuiambukiza humu ndani? Mwakyembe ni kati ya viongozi wachache wazalendo. Wewe umetumwa
 
Mti wenye matunda mema siku zote huelemewa na mawe. Mwakyembe endelea kukamua Baba. Watanzania tupo nyuma yako na tunakuombea kwa Mungu tena basi tunakuombea kwa yule Mungu wa ukweli na mwenye nguvu, aliyekuwepo, aliyepo na atakayekuwepo; yehova.
 
I don't see any upshot sir. Go back to the drawing board so that you can link your man with the mess. Mess not by bringing others' mess by the way of your own mess.
 
Pole kaka kwa hasira hila mikataba ya ndege mara nyingi huwa ni ya masaa ya hewani kwa faida ya mkodishaji (huwa wanapanga masaa kama ulivyoelezea), faida ya mtumiaji hutokana na abiria na bei za trip ya ndege; maana contract zingine zinasema wazi kabisa ndege isisafiri zaidi ya masaa fulani. So it is up to ATC accountants and their marketing teams to know kama kuna biashara hapo au hakuna kutokana na demand and looking at their contract terms in terms of a profitable business venture.

Tatizo hapo sio Mwakyembe, tatizo hapo ni raisi asielewe kuwekeza kwenye baraza la mawaziri wake, huyo Mwakyembe hana background ya business whatsoever, hilo tu lina m-disqualify kushika wizara yeyote ya uchumi especially as important as that one, na ukizingatia kimbele mbele chake na kujifanya mjuaji ni ataboronga tu. Maana hutakuta analizimisha issues ambazo hajui hasara zake for the sake ya kwamba aonekane ameleta ndenge (rahisi kudanganywa kibiashara).

Hawa sio watu wakusema they can come up with an objective and analyse it to find a better solution (pengine ndio sababu hawaoni umuhimu wa ndege mpya na faida zake in the long run), unaweza ukanona Mwakyembe ni tatizo wengine tunaona ni huwezo wake ambao ni dhaifu ndio chanzo. Na tuna sababu zote kwanza he is not a qualified person to run the ministry straight up because of his background kwa maana hiyo we expect uozo anything else would be a success by chance.
 
mtangulizi wake alikuwa mtaalamu tena wa ndege. aliiweza wizara?

Pole kaka kwa hasira
hila mikataba ya ndege mara nyingi huwa ni ya masaa ya hewani kwa faida
ya mkodishaji (huwa wanapanga masaa kama ulivyoelezea), faida ya
mtumiaji hutokana na abiria na bei za trip ya ndege; maana contract
zingine zinasema wazi kabisa ndege isisafiri zaidi ya masaa fulani. So
it is up to ATC accountants and their marketing teams to know kama kuna
biashara hapo au hakuna kutokana na demand and looking at their contract
terms in terms of a profitable business venture.

Tatizo hapo sio Mwakyembe, tatizo hapo ni raisi asielewe kuwekeza kwenye
baraza la mawaziri wake, huyo Mwakyembe hana background ya business
whatsoever, hilo tu lina m-disqualify kushika wizara yeyote ya uchumi
especially as important as that one, na ukizingatia kimbele mbele chake
na kujifanya mjuaji ni ataboronga tu. Maana hutakuta analizimisha issues
ambazo hajui hasara zake for the sake ya kwamba aonekane ameleta ndenge
(rahisi kudanganywa kibiashara).

Hawa sio watu wakusema they can come up with an objective and analyse it
to find a better solution (pengine ndio sababu hawaoni umuhimu wa ndege
mpya na faida zake in the long run), unaweza ukanona Mwakyembe ni
tatizo wengine tunaona ni huwezo wake ambao ni dhaifu ndio chanzo. Na
tuna sababu zote kwanza he is not a qualified person to run the ministry
straight up because of his background kwa maana hiyo we expect uozo
anything else would be a success by chance.
 
mtanguliizi wake alikuwa mtaalamu tena wa ndege. aliiweza wizara?
Si alifukuzwa kazi au unadhani alionewa?

au kutokana na shairi lake uchwara la 'silent of the lambs/ alilolileta hapa unadhani alikuwa ni mzalendo?

mara ya mwisho EL kwenda UK hata waliokutana nae anadai anaonewa amini usiamini kutokana na siasa za unafiki.
 
Nilitegemea kuona attachment za hiyo mikataba... Blah!! Blah!!! Blah!!!!
 
Ulicho kiitatuhuma nzito kiko wapi? Hapo shirika limejifia miaka hela hakuna afanyaje sasa akae aliangalie minaona unatoa option tu hapo.
 
Sasa hivi Air Rwanda inakwenda nchi 14 na wanamipango ya kuongeza frequencies za key destinations zaidi ya 40. Sasa wao hawafkiriii kushindana na ATC wao target ni kuwapiku KQ. Sisi tuko hapa hatujajua bado kama Tanzania ilitokana na Pemba na Zimbabwe au nchi ya kifikirika.






Hapo tu ndo umenifurahisha
 
dr-harrison-mwakyembe.jpg


mimi katika vitu vilivyonishinda humu ni mabishani ya nani zaidi kati ya ccm na chadema. Sasa nimeona bora nikufahamisheni mwakyembe ambaye anajisifia kuwa mpinga rushwa mkubwa alivyokuwa fisadi na ushaidi wote nauweka hapa na kama kuna mtu anabisha aendelee.


Kwa kifupi wafuatao wanahusika kwenye huu wizi:

Harrison mwakyembe
management nzima ya atc
bodi ya atc
kamati ya bunge ya mashirika ya umma
external auditors wa atc
ludovick utuoh ambaye ni mkaguzi mkuu wa serikali



tuhuma zenyewe ni kama ifuatavyo:

1. Shirika la ndege la taifa (air tanzania) waliamua kukodisha ndege yenye umri wa miaka 32 aina ya b737-200 iliyozeeka na mbovu kutoka kampuni ya africa kusini inayoitwa star air cargo.


2. Ndege hii ilianza kufanya kazi mwaka 1980 kule uk, na ilikuwa inatumiwa na kampuni inayoitwa british airtours na baada ya hapo ilikodishwa na mashirika zaidi ya 20 ulaya na latin america.

3. Mwakyembe, menejimenti na bodi mpya ya atc walikubali na kupitisha ukodishaji wa hii ndege kwa kiasi cha dola laki 2 (200.000 us dollars) kwa mwezi katika miezi 3 ya awali ya ukodishaji kinyume na ushauri ambao mwakyembe na maswahiba zake wa atc walipewa.

4. Mkataba unaonyesha kuwa itabidi ndege hii itabidi iruke kwa masaa 150 kwa mwezi at a rate of 1.350 us dollars for each hour.

5. Mkataba unaendelea kusema kuwa atc lazima wagharimie gharamza zote za ma crew ambayo iko estimated to be in the region of a further $80 – $100 per day & per individual !

(katika mazingira ya kawaida msomaji utaona gharama ni ndogo lakini ukweli ni kubwa sana uzingatia kuwa ndege yeneyewe inasafiri kwenda sehem 3 tuu yaani kati ya dar es salaam – kilimanjaro – mwanza na hii yoye iko funded na walipakodi wa tanzania).

Sasa ukweli ni kuwa kama kweli mwakyembe & kundi lake wana nia nzuri wasingekubali dili hii ipitishwe kwa kuzingatia kuwa kwanza ndege inge cost less kuikodisha kuliko gharama ambazo hawa mafisadi wamepitisha, na pia hizi gharama za malipo kwa saa ni kubwa mno na hapa ndipo mwakwembe na kundi lake la mafisadi wanakula zaidi kwenye huu mgao.

Suala lingine la kuzingatia hapa ni operating costs ambazo mwakyembe & his crew wa atc ni uhuni mtupu kwani ndege ina miaka 32 na gharama za uendeshaji na hasa za matumizi ya mafuta ni kubwa mno ukilinganisha ndege za kisasa.

Kwa msiojua ni kuwa gharama za mafuta (fuel costs) kwa kawaida zinachukua around 40% ya overall costs lakini kama shirika linatumia ndege za kizamani basi ni wazi kuwa gharama zitaongezeka zaidi. Na uhuni uliofanywa na atc wakishirikiana na wahuni wenzao pale wizarani kwa mwakwembe ni kupiga rangi hizi ndege wakati wakijua wazi kuwa walipa kodi wanataka kujua mikataba iko kwa maslahi ya taifa (national interest).

Moja kati ya maswali ya kujiuliza ni kwa nini mwakyembe na atc walikataa kuchukua ndege kama crj ambazo ni ndogo zaidi lakini zina fly economically lakini pia ni kubwa kiasi kiasi cha kurestart hii biashara ya shirika kama atc. Lakini hii pia ni mfululizo wa uhuni unaoendelea kama ule wa awali wa kukodisha ndege toka kampuni ya arabuni ambayo intugharimu sana sisi walipa kodi kama ile ya uhuni wa awali wa ukodishaji wa airbus.

Sasa huyu mwakyembe ambaye anajifanya ni kinara wa kupiga vita ufisadi anakubali na amepitisha huu uhuni wa atc ambao utamgharimu zaidi mlipa kodi. Huu ni uthibitisho kuwa wanaolack vision si wale wa (pemba + zimbabwe ) pekee lakini mpaka huyu mwanasheria kama mwakyembe ambaye anaendeleza uhuni wa stop gap measures.

Sasa kaeni mkao wa kuona wanaleta maombi ya kutaka wapewe pesa zaidi ili waendelee kula. Na news zilizopo kwenye corridor za atc ni kuwa wana haha kama mbwa mwitu ili warejeshe safari za nairobi na hasa baada ya player mpya chini ya shirika la ndege la kenya (fast jet) kuingia kwenye soko.

Btw

nadhani mnaikumbuka ile ndege ya atc iliyoanguka kule mwanza? Bas ndio model hiyo hiyo aina ya b737-200 kama hii mbovu na iliyozeeka ambayo mwakyembe & his crew wanatuleta.


Uhondo zaidi uko hapa:


air tanzania company limited (atcl) has suspended its contract with the dubai based aviation company, aero vista, that saw the latter lease a boeing 737-500 plane to embark on domestic flights.

captain-milton-lusajo-lazaro.jpg


atcl ceo, captain milton lusajo lazaro



atcl leased a boeing 737- 500 plane with the capacity to carry 108 passengers, which has since then been embarking on the national flag carrier’s dar es salaam-kilimanjaro-mwanza routes before launching the dar es salaam-hahaya (comoros) route last month.


The airline’s acting chief executive officer, captain milton lazaro, said the company had reached that decision to ensure a win-win situation and sustainability from the contract.


he, however, said the company intends to undertake a contract review with aero vista adding that the company may go in for another company if the two sides do not reach a consensus on the matter.



“we had decided to suspend the contract earlier entered upon with aero-vista in order to ensure compliance with government pre-requisite. We may be able to re-enter a new contract with them after discussions on revision of some clauses that do not favour a sustainable outcome.
4.jpg


“passengers who are holding atcl tickets have been reallocated alternative flights with other carriers and notified accordingly,” he said. He added that the national flag carrier will be able to be back on the routes after the completion of the maintenance exercise of its dash-8 q300 plane that is undergoing checks at the julius nyerere international airport in dar es salam.


Captain lazaro said, however, that only its dar es salaam-kilimanjaro-mwanza routes will be temporarily affected by the suspension urging that the airline continue with its three-time weekly flights between dar es salaam and hahaya (comoros).


“we regret the inconveniences that have been caused to our valued customers, we take this opportunity to thank them for their continued support and reassure that, the resumption of these services will take place as soon as possible,” he said.

Source daily news.


wakati sisi tuko bize kukodisha ndege za miaka 32 na kutetea ufisadi wa akina mwakyembe & co, rwanda wao wameamua kufanya kweli na kuwa nchi ya kwanza africa kununua ndege 4 aina ya crj900ng ambayo wataalama wanasema kuwa ni the most economical short and medium range jets toka kwa kampuni ya bombadier. (wataalam wa mambo ya ndege watakuambieni ubora wa hizi ndege kulinganisha na mtumba wa atc)

ba-rwandair_delivery_3.jpg


hawa wa nyarwanda ambao tumewashinda kwenye kila kitu (kasoro akili). Kwa sababu wakati sisi tuko bize kusifiana upuuzi wao wameopt kununua state of the art modern aircraft ambayo ina gharama za chini sana kulinganisha na mitumba ya akina mwakyembe & atc lakini pia wao wameunyesha pride ya kununua ndege mpya badala ya kukodisha hizo ndege na hii inawapa sense of ownership na muhimu zaidi inawapa abiria confidence abiria wake wa safari zake za africa na mashariki ya kati

ndege hizi zina dual class configuration ya 7 business class seats kwa mpango wa 2×1 layout na 68 economy class seats katika mpango wa 2x layout, ambayo nadhani ni quite ideal for the short and medium distances ambazo rwanda air inasafiri.

Kwa kuonyesha kuwa hawa wa nyarwanda wako serious, wao hawataki tena mitumba na wanaondoa ndege walizokodisha aina ya dash 8-100 na badala yake wanaweka ngoma iliyokuwa advanced na kubwa zaidi zaidi toka bombadier q400, ambayo kwa sasa zinapatikana kwenye dual class configuration – type ya kwanza ilikuwa delivered kwa ethiopian airlines wiki chache zilizopita

sasa hivi air rwanda inakwenda nchi 14 na wanamipango ya kuongeza frequencies za key destinations zaidi ya 40. Sasa wao hawafkiriii kushindana na atc wao target ni kuwapiku kq. Sisi tuko hapa hatujajua bado kama tanzania ilitokana na pemba na zimbabwe au nchi ya kifikirika.





nenda kajipange ......uzushi mtupu
 
Naona wengi wetu tumechangia kwa hasira because of our 'hero ' Mwakyembe amekosolewa

Sasa wether mtoa mada has malicious(sp) intent against Mwakyembe lakini ameweka pia other factors za kujifunza

Binafsi naona kama serikali ina nia ya dhati ya kufufua shirika la ndege, tungeiga Rwanda walau kununua ndege yetu wenyewe tuioperate hapa nchini kwa faida kubwa sana maana bei za precision japo tumenunua hisa si mchezo, ukiongeza laki 2 ile return ya kilimanjaro ni kama bei ya dar nbi jhb thru KQ

Hivyo pengine tuangalie ni namna gani serikali inaweza kuachana na kukodisha the national carrier
 
Ndugu yangu Msambule, kuna biashara yeyote umeshawahi kuifanya tangu uzaliwe?

Hii biashara yako (ya ATCL) imejaa mapato na wala haionyeshi matumizi (Je, ni kwamba unaficha ukweli wa hasara tarajiwa?). Acha nikusaidie, kwenye usafiri wa anga, asilimia 40 (40%) ya mapato yako yote huenda kwenye mafuta na matengenezo (kwa kila trip!). Kwa hiyo kila trip mwenye ndege anabaki na asilimia 60 (yaani 60%).

Katika hiyo asilimia 60 tunaanza mchanganuo sasa:
- Malipo ya wafanyakazi (hapa tuna maanisha wafanyakazi wote wa ATCL mpaka mfagizi na mlinzi)
- Malipo ya vyakula na vinywaji vya ndani ya ndege (kwa taarifa yenu: soda moja unayokunywa ndani ya ndege, ATCL imeinunua kwa zaidi ya Tsh 2500/-, kama watu hawalifahamu ili nitarudi baadaye kulielezea)
- Kuna tozo ya kiwanja (kila inapotua)
- Kuna tozo ya ma-agent wa ATCL (yaani wakatisha ticket, kwenye bei ya ticket uliyosema sio kwamba hela yote ni ya ATCL, kuna percent ya mawakala (agents).

Sasa katika hiyo asilimia 60 ondoa gharama hizo hapo juu, kisha angalia unabaki na kiasi gani. Then mwisho wa mwezi ufanye hayo malipo yako ya kukodi ndege (yaani USD 200,000)

Halafu mkae mkijua sio kila siku atakuwa na uwezo wa kuruka safari sita (six times) tena kwa kutegemea ndege moja. Lazima kuna siku itakuwa matengenezoni/ ama imeharibika na kutakiwa ku-cancel safari zote sita! Pili hiyo route ina mshindani mkubwa PW (Precision Air) na yeye ameamua kufanya safari ya Kutoka Dar kwenda Mwanza na Kurudi Dar kuwa Tsh 199,000. Kwa maana hii ATCL itaendelea kusubiri abiria wanaokosa nafasi PW, au nae akubali kushusha zaidi bei yake ya Tsh 257,000 (ambapo ni hasara zaidi).

Tatu na mwisho sio kwamba trip zote ATCL itapata abiria 50, kuna wakati atakuwa na abiria 20 tu!! Hii ni kitu cha kawaida sana kwenye biashara ya ndege, na asilogwe ku-cancel safari kwa sababu ya uchache wa abiria, akifanya hivyo basi anajichimbia kaburi kabisa!

Nitarudi tena!

Kama nilivyo sema, hiyo ndege inayotuhumiwa, binafsi nimepanda juzi tu, kaka, hapo kwenye Red, sio kweli kama jamaa wameshusha bei hadi hiyo figure uliobandika, nilikwenda Mlimani city kuuliza, bei niliopewa ya kwenda tu niliambiwa 220,000/= halafu msijaribu kututisha eti kama nimeisha wahi fanya biashara yeyote, kwani wewe umeisha wahi fanya biashara ya ndege?
 
Ufisadi inawezekana upo lakini nakosa imani unapomhusisha Waziri Mwakyembe,CIG,Bunge,ATCL wenyewe..siamani kama wote hao lao moja.!

kwani mwakyembe yeye ni nani? je? yeye n malaika kashuka toka Mbingun, acha hizo bana mtu yeyote anaweza kufanya ufisad hasa ukizingatia kuwa mwakyembe bado hajajitenganisha na lichama la mafisadi. Mwakyembe anaouwezo mkubwa tu wa kufisadi kwa kujua au kwa kuchomekewa ili achafuliwe. mi nafikili ungetuletea kilicho halisi dhidi ya tuhuma inayomkabili ingekua afya badala ya kutaka kutuaminisha kuwa mwakyembe yeye n mzee clean au kwa kua alikua mwenyekiti wa kamati iliyokuwa na majibu yaliyopangwa ya kumlinda JK na chama lao bovu?

kumbuka msemo wa washwahili; Lisemwalo lipo,kama halipo lipo........
 
TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE, INCHI YANGU TANZANIA JINA LAKO NITAMU SANA.: Mwaaah:
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom