Tuhuma dhidi ya JK zaikoroga CCM

Mlitaka Makamba aseme nini!! Yeye anamtumikia kafiri kwa lengo la kupata mradi. Hana jingine kichwani mwake zaidi ya hilo.
 
Kabla ya kongamano nilikuwa nimejaa na matumaini kwa kijana Nnape Nauye nikaamua kumpigia kura ya maoni kwa ajili ya jimbo la Ukonga. Lakini baada ya kongamano lile nimeghairi. Nimetambua Nnape is just a philosopher/theoretician academician kama Baregu na Dr Azaveri Lwaitama. They are good at criticising only kama mashabiki wa mpira wa Kitanzania ambao wanajiona wao ni bora zaidi ya Maximo. Ukimpa Nnape aongoze hataweza. Mimi nayasema haya from experience. Tunaemjua Jackson Makwetta enzi zake kabla hajawa Mbunge akifundisha IDM. Alikuwa hivi hivi kama akina Baregu na huyu kijana Nnape. Miaka 30 jimboni hata kumuona hawataki. Hilo la kwanza.

La pili nizungumzie kongamano. Hilo kongamano mwanzoni nilifikiri limeitwa kwa ajili ya kuzungumzia mustakabali wa taifa within the context of the changing times and trends ndani ya utandawazi. Ah wapi Bwana kumbe ilikuwa ni mkusanyiko wa wazee ambao walikutana na kulia, kulalamika na kumlaumu kijana JK. Na wakaamua kumchapa Lowasa lakini hawakuwa na ujasiri wa kumtaja hata kwa jina. Basi wangemwalika ahudhurie. Sisi tunaoijua historia ya nchi yetu tunafahamu kuwa hao wazee ndiyo walioweka msingi mbovu wa utawala kiasi kwamba leo akina JK wanahangaika. Mimi ambaye Baba yangu alifanya kazi enzi za Nyerere wakati akina Butiku wakiwa ndiyo Private Secretary wa Rais, tunakumbuka alivyojenga himaya enzi zile. Butiku alikuwa very powerful kuliko hata Katibu Mkuu Kiongozi. Sasa akikumbukia enzi hizo lazima atakuwa nostalgic. Enzi zile zilikuwa za ujima ndiyo maana akina Butiku walimharibia mzee Nyerere mpaka akawa anaitwa Musa na mzee Haambiliki. Au Butiku amesahau jinsi alivyokuwa anapendelea watu wa kabila la kutoka Musoma ndiyo maana akina Warioba wakainukia. Enzi zile watu wa Musoma wakiitwa true Northerners. Kama hutoki huko hupewi cheo cha maana hata. Butiku amesahau hilo.

Enzi zile hazikuwa kama leo ambapo nchi imebadilika kiteknolojia kwa hiyo huwezi ukategemea JK afanane na Nyerere au Mwinyi. Akitaka kufanana hivyo mnamtaka awe Dikteta? Jk anasoma alama za nyakati na anajua anachopaswa kufanya. Tanzania ya leo yule Prosper Mbena au kabla yake Jairo hawawezi kuwa powerful kama alivyokuwa Butiku. Jamani Butiku ndiyo aliekuwa anawapa watu vyeo. Muulizeni Mhe. Kitine alivyopanda kutoka kuwa Major kule chuo cha Monduli na kufikia cheo cha Mkurugenzi
Mkuu wa Usalama wa Taifa. Badala ya kufanya kazi cheo kikampanda kichwani akawa anatembeza ubabe na starehe tu. Siku zile Radio moja TRD, Magazeti mawili Daily News la Serikali na Uhuru/Mzalendo la CCM. Kwa hiyo upuuzi wao ukawa hauandikwi. Isipokuwa zilikuwa zinadumishwa fikra za Mwenyekiti wa CCM.

Tanzania ya leo haiwezi kurudi huko. Na hao wazee watulie waandike vitabu na wale pensheni zao. Wakijiingiza kwenye uharakati wa siasa pensheni zao zitaliwa na madalali wa kisiasa ambao wako wengi siku hizi. Tanzania ya leo ni ya dotcom. Wawaachie akina Nnape, Masha,Serukamba, Vita Kawawa, Mnyika, Mbowe na kizazi cha akina JK na Lowasa ndiyo wawe wana kongamano kwa nia ya kuipeleka nchi mbele.

Hebu angalia wale wazee kwenye kongamano lile. They were all spent forces.
 
Ranting! Wewe umeongelea nyakati mbili tofauti kabisa; the cold war era and the globalization era. Nyerere amewaachia Nchi mwaka 1985, now it is over 25 years. He rules 24 years and you had the rest. Mpwayukaji wewe. Hebu dhihirisha kuwa Wenye vyeo walikuwa wote Musoma au Northerners?

Factor ya Nyerere haiwezi ky-affect Nchi for all times. Nyerere kashika ubongo wako usifanye kazi?

Kikwete has all the means open to change this country, he has failed the people. He can on the banner of YOUNG MAN, with kasi, nguvu i can't even remember; now he is lost on the way!

For your information in case this if this same guy (JMK) had sent you to write this, tell him it is the sign of the times, the ace is with us and we are just waiting to throw it. Lile Kongamanno ni kama initial warning there are many coming!!
 
Mangula, ambaye alishika nafasi ya katibu mkuu wa CCM kwa kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa serikali ya awamu ya tatu, alitahadharisha kuwa iwapo mambo hayo hayatarekebishwa kwa haraka na kwa kipaumbele kinachostahili, taifa litaelekea pabaya zaidi.

"Utawala wa sasa umetofautiana na tawala nyingine kwa
kupungukiwa na mambo matatu ya msingi ambayo ni ubinafsi, kufanyika maamuzi kabla ya kuelimisha wananchi pamoja na kutokuwepo kwa wigo mpana wa majadiliano kuhusu masuala mbalimbali ya mustakabali wa taifa," alisema Mangula.

Mangula alisema hali hiyo imesababishwa na watu wengi wanaopewa uongozi kutokuwa sifa za kuongoza na kwamba wamepata nafasi hizo kwa njia za urafiki.

"Hata utaratibu mzima wa kuwapata viongozi wanaostahili kwa sifa haupo, badala yake mambo yanafanywa kwa urafiki," alisema Mangula ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu. Akifafanua hoja zake hizo, Mangula alisema katika utawala wa sasa ubinafsi ndio umeonekana kuchukua kipaumbele katika kutatua mambo muhimu ya kitaifa.

Mangula aliweka bayana kwamba katika utawala uliopita ubinafsi haukupewa nafasi kwa kuwa kabla kiongozi hajazungumzia jambo lolote, alilazimika kupata mawazo ya chama tawala na wanachama kuhusu anachotaka kuzungumza. Aliongeza kwamba kutotumika kwa mfumo huo ndio sababu ya kupishana kwa kauli za viongozi kunakoendelea kutamba kwenye safu za mbele za vyombo vya habari kwa sasa.

"
Tabia ya kutaka kuonekana kuwa wewe ni bora kuliko mwingine ipo, ndio maana leo viongozi, tena wa kutoka chama kimoja, wanapishana kauli kuhusu jambo moja," alifafanua.

Akizungumzia kufanyika kwa maamuzi kabla ya kuwaelimisha wananchi, Mangula alisema hilo ni tatizo linaloendelea kulalamikiwa na Watanzania.

Mangula alisema katika utawala uliopita watu walielimishwa kwanza kabla ya kufikiwa kwa maamuzi.

"Utaratibu wa kuelimisha kwanza kabla ya kufikiwa kwa maamuzi ndio uliokuwa ukitumika, lakini hali sasa inaonekana kuwa tofauti," aliongeza.


Kuhusu kutokuwepo kwa wigo mpana wa majadiliano katika masuala ya kitaifa, Mangula alisema hiyo inatokana na viongozi wachache waliopewa dhamana na wananchi kuamini kuwa mawazo yao yanajitosheleza.

Hoja za Mangula, ambaye kwa sasa anajishughulisha na masuala ya kilimo, zinashabihiana na zile zilizowahi kutolewa na mawaziri wakuu wawili wastaafu, Dk Salim Ahmed Salim na Jaji Joseph Warioba kuhusu mustakabali wa taifa.


Source: Mwanachi
 
Waandishi wa habari hawajui kuandika ripoti ya darasa la nne kwa kutumia Who, what, when, why, how

Article nzima haionyeshi Mang'ula (I believe it is not Mangula) ameongea wapi na lini. Kwenye Nyerere Foundation? Nyumbani kwake? Kilabuni? lini?

Hiki kinaweza kuonekana kama kitu kidogo lakini kinaweza kubeba perspective kubwa na kuinform watu pamoja na kuwapa timeline.

Think about it, article nzima haina "when" and "where"

Mambo ya darasa la nne haya!
 
Huyu naye atakuja Makamba ampe vidonge vyake. Badala ya kusikiliza ujumbe wanatizama pua ya aliyetoa hoja.
 
Mtu akiniambia kuwa kabla JK hajawa rais aliwahi kufanya nini mpaka wa tz mkaona anawafaa kuwa rais wenu, nitawaelewa! Otherwise mkubali matokeo maana ndio price yakufanya maamuzi makubwa bila kufikiria sana! Watanzania walidanganywa na kampeni za redet (mkandara) na bbc swahili (tido muhando)! Poleni bandugu!
 
M/kiti hana vision katibu ndio huyo Makamba, mzee wa taarab what do you expect? gabage in gabage out! Ni sawa na average tennis player anapojaribu kucheza na pro kama serena williams, udhaifu utakuwa wazi mwanzoni tu! Sasa Makamba and co its high time to refer to mwl JKN statement ...kuongoza nchi si suala la kukimbilia, hebu ona sasa rais anadhalilishwa hadharani alafu bila aibu unamtetea, lisemwalo lipo mzee makamba thats the reality just accept!
 
Back
Top Bottom