Tufundishane Ujasiriamali

Discussion in 'Jukwaa La Biashara na Uchumi' started by Sipo, Feb 7, 2010.

 1. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumekuwa na ongezeko la watu wanaotaka kujua ni jinsi gani ya kujiajiri wenyewe, namaanisha kama mtu mmoja au kama kikundi. Naomba tutumie andiko hili hapa kufundishana ni jinsi gani, mbinu zipi, njia zipi tunaweza kutumia katika kujitegemea wenyewe pasipo kutegemea mishahara na kazi za kuajiriwa ambazo kadri dunia inavyosonga mbele ndio jinsi ambavyo kazi hizi zinakwisha.

  Kila mwenye wazo au uzoefu aweke hapa kwa jinsi ajuavyo yeye ilimradi ujumbe ufike kwa jamii kubwa zaidi.


  Asanteni kwa ushirikiano mtakaoutoa

  Wenu
  Sipo
   
 2. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 48
  Moderator naomba utilie mkazo hili na ikiwezekana tukutanisheni na wataalam na walio nautaalam hapa naomba wajitolee; mfano mimi niko tayari kusaidia ama kushauri kwenye upande wa IT na mambo ya Internet cafe
   
 3. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,938
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Bravo!very good idea.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,268
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 48
  Nina uzoefu!

  Nilikuwa kijijini juzi, baba yangu alikuwa na mashine za kusaga kwa miaka mingi, ambazo zimetusomesha sisi.

  Baada ya yeye kuugua na kuhamia Dar 2008 alimwachia mradi huo baba mdogo, ambaye ameshindwa kabisa kuendeleza kazi hiyo, na ameishia kukopa fedha na kuzalisha madeni kila mtaa huko nyumbani.

  Hawezi kulipa bili za umeme,
  Hawezi kufanya maintainance pindi kifaa kikiharibika,
  Hawezi kabisa kuwalipa vijana wanaomsaidia.

  Nadhani hii inasababishwa na ukosefu wa elimu ya ujasiriamali, ambapo angekuwa nayo angejua jinsi ya kupanga bajeti ya mradi, masuala ya uwiano wa mapato na matumizi, na vitu vya namna hiyo.

  Tundiko hili litakuwa la msaada sana kwa wengi, hata kama si members wa hapa, lakini kwa wale tunaoishi nao huko mtaani.
   
 5. M

  Malila JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,047
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 48
  Kitu kizuri wakuu.Hali mtaani si nzuri kwa ujumla hasa kwa ajili za mfumo rasmi. Sector binafsi inakuwa kwa kasi,lakini sehemu kubwa ya sector hiyo inaweza kuja kutawaliwa na wenzetu. Kwa hiyo ni lazima vijana tuanze kuunganisha nguvu ili tujenge misingi na naamini kwa pamoja tunaweza.

  Kitu cha kwanza ninachoweza kuchangia ktk suala la ujasiriamali kwa ujumla, la kwanza ni kujitambua wewe mwenyewe na mazingira yako uliyo nayo ( vipaji,rasilimali,ujuzi,fursa nk). Na la pili ni juhudi ktk kujifunza toka kwa waliofanikiwa na kushirikiana nao.
   
 6. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 48
  Naam natuanze; kulikuwa na mpango wa wajasiriamali wa JF kukutana umeishia wapi?

  Malila ; tunaweza kuanza kuenlist hayo uliyotaja hapo juu? basi fafanua zaidi nini kinahitajika ktk kila nyanja uliyoitaja?
   
 7. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,503
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 38
  Asante Sipo kwa kuileta hoja. Mie ninapenda sana ujasiriamali maana napenda kuanza kujiajiri mapema. Wastaafu wengi wanapata shida sana kwakuanza kujifunza wakiwa tayari hawana kazi, ninauzoefu na hili kwani nimeishaelekeza wawili na ninafuraha wanaendelea vizuri. Mie ninakibiashara changu kwa miaka 3 sasa ambacho kwakweli kinaweza kunipatia mahitaji ya mwezi au tuseme hand to mouth. Ninapenda kutanuka na pia kuinvest tatizo nikifanya hivo ninakula mtaji na inabidi nitoe kwenye salary. Mwenzangu ananiambia kuwa sijui biashara nikasomee enterpreneurship! Ninahitaji account ya biashara, nidhamu ya juu kwenye mtaji etc. Hebu tuelekezane juu ya hili.
   
 8. babalao

  babalao Forum Spammer

  #8
  Feb 8, 2010
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Pia ni mshauri wa biashara, ninatoa ushauri wa biashara na kuendesha mafunzo ya ujasiriamali, kuandaa michanganuo kuombea mikopo benki na misaada kutoka kwa wafadhili. Mwaka 2009 niliwezesha wateja wangu kupata mikopo ya Tshs. milioni 300 toka mabenki mbali mbali, niliendesha mafunzo na kutoa ushauri kwa watu mbali mbali, Kati ya mafunzo ambayo niliyafanya na yakafana ni yale ambayo yaliandaliwa na Mwang'amba Communication na kufanyika Millenium tower, ambapo wawezeshaji tulikuwa mimi( Charles Nazi) James Mwangamba, Eric Shigongo, Martin Kaswahili, Mr Msemwa na Chris Mauki.

  Utafiti nilioufanya nimegundua kwamba watu wengi wanakwama kuendesha biashara zao au kupata maendeleo ya kiuchumi kwa sababu ya kukosa maarifa ya ujasiriamali.Kwa hiyo nimeamua kuwa lengo langu ni kutoa elimu ya ujasiriamali kwa watanzania wote. Kutokana na wito wa mwenzetu natoa ofa kwa Wana JF ambao wako Dar kuwa niko tayali kutoa mafunzo ya ujasiriamali bila malipo yoyote. Nauomba uongozi wa JF usaidie kutafuta ukumbi. Kwa mawasiliano zaidi kwa wanaohitaji kupata mafunzo hayo na uongozi wa JF wanaweza kunipigia simu namba 0755394701. Pia kama una kikundi cha watu ambao wanahitaji kupata mafunzo mnaweza kuniita niko tayali kutoa mafunzo bila malipo mradi mniandalie mahali pa kukutana na muwe idadi isiyokuwa chini ya watu 10.

  CHARLES NAZI
  Mshauri wa biashara na Mtunzi wa kitabu cha Mbinu za biashara
   
 9. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,503
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 38
  Bravo Babalao utatufaa sana jamani. Ngoja tuone kama watapatikana watu, ila hata mie hao 10 naweza watafuta. Ninasubiri wengine wenye nia ntakutafuta lol, asante na ubarikiwe.
   
 10. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,201
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 38
  Baba Joe since unaoneka upo kwenye mood za kutoa ushauri wa bure leo, wacha na wengine tuombe msaada wa ushauri kutoka kwako.

  Hivi mtu anaweza vipi au atumie mbinu gani kuweza attract investors hapo nyumbani, how does he go about raising cash without giving too much shares au what is the maximum loan a bank can offer.
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,047
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 48
  Haya tumeshapewa bure basi tuchangamkie basi nafasi hii. Nikirudi Dar nitakutafuta ili ninyonye machache kt ya mengi uliyo nayo. Asante Baba lao.

  Nyongeza yangu ni hii, ujasiriamali kwa sasa ni kuthubutu kushusha vitu toka kichwani na kuviweka ktk vitendo ili kupitia vitendo ie practical unajiongezea ujasiri na hivyo unasogea mbele.

  Nilipojitambua nilivyo basi nikathubutu kidogo tu na nimeona matokeo.
   
 12. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 48
  Bravo Mkuu!

  Salute!

  Nasi tusiokuwapo Dar tunaweza kuja kushiriki mafunzo hayo; na kama token of apreciation tukajicomit kwa kuchangia gharama za ukumbi! Binafsi sipo Dar; lakini kama mafunzo niya siku kadhaa mfululizo mie naweza kushiriki na pia hapa nakuja na wazo; organization ya JF inaweza ikaandikia BP hii kitu tukapata wafadhili hata kwa hao would be financiers achilia mbali foundations nyingi tu mlizonazo hapo Dar! Ni wazo tu!

  mwito wangu JF leadership mtakuwa mmeanzisha kujenga ile iitwayo corner stone mkiweza kuendesha hii kitu!

  Mubarikiwe!
   
 13. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 36
  Jamani hilii wazoo ni zuri sana na nitamani kuliona linasonga mbele kwa maana ya WALK THE TALK

  Tuhamasike na kusonga mbelee kwa utekelezaji.
  Nashauri kwa hapa dar tukiorganize tutafute sehemu (zipo kumbi mbali mbali za bei nafuu kama kuna yeyote mwenye connection na ukumbi tafadhali kuwa wa kwanza kutuelezaa tuchangishane tayari mtaalamu yupo aweze kutupa somo?

  Jamani INAWEZEKANAA TUSONGE MBELEEE
   
 14. T

  TANURU JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Babalao,

  Hongera kwa kazi yako nzuri. Nashauri pia uongee na TBC ili kuwe na kipindi cha Ujasiriamali kila wiki kwa angalau saa mbili kwa wiki kupitia Televisheni na Radio. Kipindi hiki kinaweza kuwa chini ya JF ila wewe ukawa ndiyo mzungumzaji na muelimishaji mkuu.
   
 15. M

  Malila JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,047
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 48
  Njia nyingine ya kujifunza ni pamoja na kutembelea kazi za wajasiriamali wenzako,hii inaweza kukutia moyo na ari ya kusonga mbele.
   
 16. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 48

  Walau tupate tija kwenye hii nyenzo muhimu ya Taifa letu! senksi sana Tanuru
   
 17. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 2,219
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 48
  wakuu hapa mie nina dokezo la msingi kabsaaa..katika watu 100 wanaoongelea ujasiriamali 99 ni wafanya biashara na 1 ndio mjasiria mali...sasa lazma tujue kuna tofauti ya wafanyabiashara na wajasiriamali.....

  Anayenunua nyanya kariakoo tsh. 100 na kuja kupanga gengeni kwake manzese na kuuza tsh. 120..huyu ni mfanya biashara...sawa na wanaokwenda china/dubai/honkong/thailand....MJASIRIAMALI..huyu anatakiwa awe na jicho la ziada la kuona nafasi/fursa zaidi za kutengeneza pesa..na sio kununua na kuuza tuu...say..mjasiriamali atanunua nyanya kariakoo..atazi-preserve zizioze..kisha atazipack vizuri na kuzitia logo yake kisha ataziuza kempinski..na nyingine atasafirisha kwenda nje ya nchi...zilizoanza kuoza pale kariakoo..mjasiriamali atazinunua na kuzitengeneza sauces mbalimbali na kuuza..

  ANAKUWA ANA-ADD VALUE before selling..na kwa kuadd value anauza/anapata value for money...ni maoni tuu wadau
   
 18. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 374
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Well thought,nicely said.
   
 19. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 48
  Kwa mapoint ka aya; nashauri ubadili jina kwenda I care tih tih tih tih
   
 20. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 2,219
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 48

  kakaaa...sio kivilee kuwa i dont care...sema mambo kama haya ya ujasiriamali yanahitaji kuujua undani wa mafanikio ya wengine kisha uone tofauti ya wasiofanikiwa...ndio maana wafanyabiashara wengi wanaanguka ila wajasiriamali wanaendelea kuishi...UJASIRIAMALI...unahitaji extra senses...creativity in business....an inborn touch of doing things in a different But EFFECTIVE WAY....

  tunayo safari ndefu ya kwenda kuwa wajasiriamali wa kweli..ila tusikate tamaa..tutafika..if at the start somebody can overcome entrepreneu-phobia..she/he stands a great chance of being one of them.....kwa hiyo issue hapa ni ku-overcome uoga wa kuwa mjasiriamali...then unapitia wakati mgumu wa kukomaa kama mjasiriamali kisha unakuwa...soo easier said than...
   
 21. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #21
  Feb 10, 2010
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 1,430
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 38
  Hii imekaa vizuri... Nakubaliana kabisa na "who care?" kuwa mjasirimali lazima asiwe mwoga na awe nauwezo wa kufikiri. Ni lazima uweze ku-connect the dots hakuna ubabaishaji.

  "An enterpreneur is a person who WORK ON a business NOT in it". (Michael Gerber)

  Mfano kama wewe biashara yao ya kuuza chumvi gengeni itasimama endapo utashindwa kuisimamia (mf ukiwa mgonjwa) basi hiyo siyo biashara ya mjasirimali bali ni JOB.

  Biashara ya mjasirimali ina endeshwa kwa mfumo (system) ambao hautegemei mtu fulani bali mfumo wenye kufuata kanuni.

  Mimi binafsi biashara zangu zamtandao (intenert business) zina cashflow hata kama mimi nikiwa nimelala usiku. Nimetengeneza mfumo ambao hautegemei msimamizi wala sehemu ninayo ishi, hata kama nikifa leo hii cashflow itaendelea.

  Jamiiforum ni mfano mzuri wa mfumo was kijasirimali ambao unaingiza pesa kwa kutumia matangazo (contextual advertising) ambapo ukibonyeza tuu hilo tangazo pesa inaingia JF hata kama admin yupo mars.

  Biashara ya mjasirimali lazima iwe scalable ie lazima uweze kuipanua. Fikiria biashara yako kama vie prototype ya nyingi kama hiyo. kwa mfano kama nimefanya research na nimeona kwamba "weightloss" ni niche nzuri na yenye faida basi nitatafuta sub niches nyingi za kuambatanisha main product, mfano losing weight for middle age executives, weight loss for fat husbands, weight loss for women who just had a baby n.k

  Biashara ya mjasirimali inamtengenezea maisha (kiswahili kitamu LOL) huyo anaye miliki siyo kumuibia muda wake kwa kuutumia kuiendesha.

  Just my 2 cents
   
 22. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #22
  Feb 10, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa wale wote wanaoendelea kuchangia mada.
  Kwa mfano mtu mmoja ana kiwanja maeneo ya Bunju na hana uwezo wa kujenga kwa sasa kutokana na ufinyu wa mshahara anaolipwa lakini benki ana shilingi milioni moja. Amekaa na kufikiria kuwa ni bora akafungua kituo cha kufyetulia tofali na kuuza sementi hapo lakini ukumbuke benki ana shilingi milioni moja tu na kazini kwake hawadhamini wafanyakazi kuchukua mikopo benki kwa kutumia jina la kampuni. Na ukumbuke kuwa kuna mahitaji mengi ili kuweza kuanzisha kituo hicho cha kufyetulia tofali mbali na kiwanja ambacho tayari kipo. Mahitaji mengine yanayotakiwa na yeye hana ni kama vile kontena au servant quatre, materials kama sementi, mapipa ya maji, pamoja na wafyetua matofali ambao watahitaji fedha za kuwalipa wakati kazi inaanza pamoja na mahitaji mengine madogo madogo.

  Je hii ni biashara au ujasiriamali kwa mujibu wa maelezo ya Who Cares?
  Je atafanyaje hili aweze kuianzisha kazi hii anayotaka kuanza kuifanya?
   
 23. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #23
  Feb 10, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 5,863
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 48
  Am a farmer cum civil servant . Nafuga nguruwe kwa kwenda mbele, Kuku wa kienyeji, migomba ya kisasa etc. Then nimeajiriwa, nalipwa sh. 280,000 kwa mwezi mzima. Nikiuza mayai napata 300,000. Nikiuza Kitimoto moja tu kwa mwezi napata 200,000-300,000 kuendana na uzito.
  Nikiuza kuku 50 tu kwa mwezi napata 200,000.00. Nyumbani nina mahindi gunia 5 , mchele , na maharage. Mama analima mboga mboga ,na midizi. So cost of foods kwangu ni negligible.
  Nina watoto wawili wa primary school na madogo wawili relatives secondary ya private.
  Ninaendesha pickup na starlet. Ila nina mpango wa kununua lililobora zaidi kifamilia.

  Jumla minimum ni napata 700,000. mazimum 1,500,000.
  Zile 280,000 nawalipa wafanyakazi wawili kila m2 140,000 na wako very happy. Shamba nilinunua eka moja u nusu miaka hiyooo na ndipo nimejenga ikulu yangu. Here I am . Mjasiriamali/ civil servant.
   
 24. K

  Kachoki Senior Member

  #24
  Feb 10, 2010
  Joined: Feb 2, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ubarikiwe sana, naamini wengi tutafaidika nimechukua namba, wanajamii Forum jamani si tungechagua mmoja wetu awe coordinator hapa tujiorodheshe na tuanze darasa mara moja?
   
 25. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #25
  Feb 10, 2010
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,586
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 38
  Kama wewe ni mjasiriamali na umekwama kwenye mbinu za kuendeleza biashara yako, au namna ya kupata mtaji wa kuendeleza, au kuanzisha biashara, fungua web site hizi hapa chini kama unachokitafuta kipo kwao:-

  http://www.bdgtpsf.com/

  au

  http://www.bidnetwork.org/page/87189

  (Kama haifunguki copy & paste kwenye address bar)
   
 26. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #26
  Feb 10, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ningekuwa DSM ningefanya hii kazi lakini kwa sasa niko nje ya jiji. Ambaye anafikiri anaweza kufanya hili please ajitokeze na kutoa mrejesho hapa na kuwa anawasiliana na Babalao moja kwa moja kwa namba ya simu aliyotoa.

  Lakini pia namuomba Babalao kama ana literatures ambazo zinahusiana na mada hii atuorodheshee hapa ili tuweze kuzisoma na kujenga uelewa zaidi.
   
 27. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #27
  Feb 10, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazo ni zuri sana.
  Ila napendekeza kwa wale watu ambao wako tayari kutoa mada mbali mbali kuhusu ujasiriamali ni vyema tukakubaliana kwamba wapewe muda wa kutosha na kuwe na siku maalum ya kuwasilisha ili wadau wote tuweze kujua kwama leo kuna somo ukumbini.
   
 28. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #28
  Feb 10, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,381
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 38
  Huyo ni mjasiriamali. Kitendo cha kugundua kwamba kiwanja ambacho hawezi kukiendeleza kwa sasa kwa kukosa fedha bali anaweza kukitumia kupata fedha kinamweka kwenye kundi la wajasiliamari.

  Mjasiliamari ni mtu anayeweza kuona fursa za kutengeneza pesa pale ambapo wengine hawaoni. Na ndio maana mfano Dar kuna biashara nyingi sana za kuigana. Wafanyabiasha wengi wa Dar (sio wajasiliamari) wana madala dala, hair saloon za kike na kiume (barber shop), baa za kitimoto na bia na migahawa!

  Huyo mwenye kiwanja cha kwake, na mtaji wa shilingi milioni moja tayari ana mtaji mkubwa kuliko anavyofikiria. Tatizo lake anaona kwamba hizo milioni moja ni kidogo sana kwa hiyo hawezi kuanzisha hiyo biashara. Pia ana mawazo ya kwenda kukopa benki.

  Mjasiliamari halisi huwa anaanza na mtaji sifuri na haendekezi mambo ya mikopo. Kama ameweza kujikusanyia shilingi milioni moja kama ''saving'' pamoja na kiwanja bila kukopa, ipo siku atajikuta ana Shs. milioni mia moja na kiwanda cha simenti bila mkopo! Achotakiwa kufanya kuendeleza kanuni zake za kujikusanyia mapato, kujiwekea akiba na kufirikia fursa nyingine za kujiongezea kipato.

  Looser always say it is possible but it is very difficult, where as winners always say it is difficult but it is possible.
   
 29. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #29
  Feb 10, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,120
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 38
  keep it up nakuombea uzidi kufanikiwa zaidi
   
 30. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #30
  Feb 10, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 48
  Kaka asante sana!

  Safari tumeianza na niseme umeianzisha hapa kwa kutupa changamoto na fikra!

  Usichoke mkuu unatufaa wengi!
   

Share This Page