Tufanye nini ili kupambana na rushwa?

Audax

JF-Expert Member
Mar 4, 2009
442
12
Nimekuwa nikifuatilia historia za nchi mbali mbali kuhusu njia mbali mbali walizotumia na ambazo wanaendelea kutumia ili kupambana na rushwa. Mojawapo ya nchi hizo ni uholanzi. Wanasema hata wao mwanzoni kabla ya uholanzi ya leo rushwa ilitawala. Na mwenye maisha ya chini hakuthaminiwa. Hii ni mojawapo ya hatua walizochukua kama serikali ili kuondoa tatizo hili

1. Kuhakikisha sheria yoyote ile inayotungwa inafuatwa na watu wote bila kujali cheo, dini n.k

2. Ni kufanya utafiti kuhusu maisha ya mwananci wa kawaida-yaani kujua anaweza kutumia shilingi
ngapi kwa mwezi,hii ikiwa ni pamoja na kula, kulala (kodi),kusomesha,kuvaa,kodi za maji,umeme
na mahitaji yote kwa maisha ya kawaida

3. Kupanga viwango vya mishahara kulingana na elimu aliyonayo mtu lakini kwa kuzingatia kuwa
mfanyakazi yeyote ataweza kupata mahitaji yake ya kila cku hasa wale wa kiwango cha chini.

4. Uwiano katika makato yakodi-Kodi inakatwa kulingana na kipatao ulichonazo, bila kujali wewe ni
raisi, waziri,mbunge,mlinzi,wafanyabiashara, etc

5. Kujenga mifumo ya kitaalamu ya kuhakikisha kila mtu analipa kodi bila ya kutokea hata mmoja wa
kukwepa kodi kwa njia yoyote ile.

6. Wakatafuta namna ya kuweka watu waliocommited katika mfumo mzima wa mapato ya nchi, yaani ambao wpo answerable ikitokea mapato yaliyotegemewa hayakupatikana

Na mambo mengine mengi.

Nimeona nitaje baadhi ya series ya mikakati ili nimalizie kwa kusema. Hapa nyumbani Tanzania tunasema kuwapeleka mafisadi mahakamani wafungwe au warudishe mali walichochukua. Mimi kwa upande wangu nahisi hii c njia muafaka ya kumaliza hili tatizo lazima tuliangalie kwa mapana zaidi.

Yaani tuwe na mikakati endelevu ya kupambana na rushwa hata kwa vizazi vijavyo.
Ninachoamini mimi ni kwamba tukisema rushwa-ni matokeo ya matatizo mbalimbali ambayo yanaikumba jamii husika. Swali langu ni je tufanye nini ili na sisi tuondokane na tatizo hili kama c kulitokomeza kabisa?
 
Katika uchaguzi ujao, badilisha uongozi maana huu uliopo ambao umekuwepo kwa miaka nenda rudi rushwa ni mfumo wao wa kujinufaisha hivyo hawawezi kuandaa programme itakayouondoa.
 
MTOA MADA KWANZA KABISA NAOMBA UWE RAFIKI YANGU BILA KUJALI TOFAUTI TULIZONAZO........IWE RANGI,DINI,KABILA,SIMBA/YANGA,TAJIRI/MASKINI,ALIYESOMA/ASIYESOMA........hii vita ni yetu sote...si vita ya klabu ya simba pekee wala si vita ya walalahoi pekee......ni lazima tuungane katika hili.....jamii yetu inahitaji mtu kyjua TAIFA KWANZA MENGINE YAFUATE......! NAOMBA KUCHANGIA.......!MIMI NA WEWE TUBADILIKE......!HAPA NINA MAANA KUWA MIMI NINAYEHITAJI HUDUMA NIACHE KUTOA RUSHWA ILI KPATA HUDUMA HIYO.....NA MIMI PIA KAMA NI MTOA HUDUMA NISIPENDE KUCHUKUA RUSHWA ILI KUMPA MTU HUDUMA....! NIKIANZA MIMI,NA WEWE UKAFUATA NA YULE ...NA YULE...NA YULE.....TUTAPIGA HATUA KUBWA KATIKA MAPAMBANO HAYA....!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom