Hahaha. . Hygea sio nyie wanaume ndo mnapenda kulalia nyama choma na bia alafu wali wa samaki nyumbani mnaona sio kitu? Binafsi nasikitika sana kuona watu wanakimbia vyakula vizuri na fresh vyote tulivyobahatika kuwa navyo alafu wanajaza vitu visivyo vizuri sana kwa afya ya mwili. Yani mimi ningeweza ningekua nakula mboga za majani asubuhi, mchana na jioni. Kitu ambacho wengi hawataki, wao ni nyama, nyama, nyama tuu basi.
Nyie wanaume nanyi kuweni responsible. . .
Kama tatizo ni chakula cha nyumbani hakinogi basi ongea na mkeo aboreshe mapishi yake, omba upikiwe vyakula (vya maana) upendavyo na ujitahidi kuwa hata unatembea kidogo mida ya jioni. Unaweza ukafanya iwe family activity, mama na watoto wote mnaungana. Kama mna kauwanja kenu chezeni hata mpira na watoto wenu.
Sema hayo hapo juu yanahusu yu iwapo wewe ni mtu wa familia, kama hupendi kutumia muda na familia yako endelea tu kujaza nyama/ndizi kavu na ngumu pia machips yaliyojaa mafuta tumboni day in day out. Matokeo yake utayaona soon enough.
Hehehe ndio na somo linahusu, yale nayo ni mazoezi!!
Kimsingi nakubaliana na uliyoongea. Ila na haya mafriji yenu ya siku hizi watu wanalishwa viporo kwa kwenda mbele tu hata majumbani. Wali, maharage, mboga zinapikwa zinakaa wiki nzima kinachofanyika ni kupasha moto tu. Mimi binafsi sioni ubaya wa nyama choma ikiliwa responsibly. Nimekulia kijijini ambapo nyama choma ilikuwa ikiliwa na haikuwahi kuwa sababu ya haya matatizo ya wanaume wa kisasa.
Hilo la kuwaambia kina mama waboreshe mapishi ni "easier said than done". Sio kinamama wote mkiambiwa mboreshe mapishi mnaweza kuelewa kiurahisi. Nakuhakikishia hilo linaweza kuwa chanzo cha mgogoro na unaweza kuambatana na vikwazo vingine kama kununa na usitishwaji wa huduma kuu ya ndoa.