Tufanye fundraising kuwasaidia waJapan

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
lakini kabla hatujafanya hivyo kwanza hebu tufanye valuation wao wanatusaidia vipi

I can only imagine publicity itakayo generate how people from the poorest country in the world are helping one of the richest in the world

mansemaje?
 
Kutoa ni moyo na si utajiri.Na formula mojawapo ya maisha ,jinsi utuavyo na ndivyo ubarikiwavyo...
Mungu akuongoze unatoa wapi na kwa nia gani...
 
tatizo sisi tunapenda kusaidiwa tu ila hatupendi kusaidia tunaweza kuwapa hata kidogo hicho tulicho nacho kitawasaidia
 
Kama inaweza kupatikana NGO itakayoweza kuratibu litakuwa jambo jema, wenzetu wanahitaji msaada hata huo mdogo utawasaidia. Kwa hiyo kimsingi umetoa wazo zuri, utekelezaji ndio utata.
 
ina maana baada ya maafa haya jamaa watashuka kiuchumi au wataendelea ktk nafasi yao ya sasa? Na je wao wenyewe wanafanya jitihada gani kujisaidia?
 
Nafikiri la msingi hapa si nafasi ya kiuchumi, haya ni maafa yamewapata wenzetu. Nafasi ya kiuchumi inayosemwa is just a position, has nothing to do with this!.

Kama wao wakati wote wamekuwa wakijali tunapokosa chakula na kutuletea mchele tena bure, nafikiri kama binadamu inabidi tuiangalia hali yao katika jicho lingine. Hawa ni watu katika hali ya kawaida wasingehitaji msaada wa mtu yeyote, lakini hapa yamewakuta (sehemu ya jamii yao hawana pa kuishi, hawana chakula, maji, umeme, gas n.k).

So kama kuna anayeweza kuratibu wakati ndio huu, sababu - anayetusaidia wakati wote leo naye ni muhitaji!.
 
Nadhani Japan wanahitaji Msaada wa Nguvu za watu wenye uwezo wa kusaidia katika kujenga kuokoa waliosalia na kutafuta miili ya watu kwa muda huu kwanza.

Hivi Japan wanasaidia wananchi wa Tanzania Au Serikali naomba ufafanuzi... Hawa wafadiri wanaosaidia upitia Serikali mie Siwaafiki kwani hakuna kitu tunachopata.

Watoe misaada kwa wahusika Direct kuliko kupitia mikonono mwa mafisadi
 
lakini kabla hatujafanya hivyo kwanza hebu tufanye valuation wao wanatusaidia vipi

I can only imagine publicity itakayo generate how people from the poorest country in the world are helping one of the richest in the world

mansemaje?

Unafiki huo, mbona ukuanzisha mada ya kuchangia wahanga wa Gongo la Mboto, Kilombero. n.k
 
Hata ukitoa shiling mia moja ni msaada mkubwa sana wa kujali maisha ya watu wengine.
Wazo zuri sana Slidingroof,Lazima utakuwa mwanachama wa CHADEMA
Naunga mkono wazo kwa 1200%
 
Kama inaweza kupatikana NGO itakayoweza kuratibu litakuwa jambo jema, wenzetu wanahitaji msaada hata huo mdogo utawasaidia. Kwa hiyo kimsingi umetoa wazo zuri, utekelezaji ndio utata.

ni kweli kwa wajapani tutakuwa tunakosa fadhira na utu, tukiishia kutoa salaam za rambirambi! hii si tu kutokana na ukubwa wa janga lenyewe bali ukweli kwamba wamekuwa msaada mkubwa sana kwetu.

Kwa jinsi ninavyoona jamaa baada ya kutoa salaam za rambirambi hana tena la zaidi! Napendekeza kama ilivyokwisha ongelewa kwamba kutoa ni moyo na kidogo tutakachoweza kutoa kitakuwa ni msaada mkubwa kwa wenzetu kutokana na hali waliyonayo, CHADEMA watuongoze kuweza kutoa michango hii kwa wenzetu. I hope CHADEMA kunakitengo cha maafa!
 
kama ni pesa.. pia tuangalie uthamani wa Tshs Against JPY! .. inawezekana 100Tsh kwa wenzetu hainunui hata kahawa
 
We sema unataka tuchangie ule wewe.. Japan visenti vyako hana shida navo.. Wewe ukishaoneshwa kuguswa tu na maafa kwa taifa kama lile inatosha.

I lived in japan for 6 years.. Trust me mchango kwa taifa kama letu wataona aibu kupokea

Manake wakituangalia hata umeme hatuna na hatujapata maafa.. Tuchangeni tulipe dowans umeme uwake
 
We sema unataka tuchangie ule wewe.. Japan visenti vyako hana shida navo.. Wewe ukishaoneshwa kuguswa tu na maafa kwa taifa kama lile inatosha.. I lived in japan for 6 years.. Trust me mchango kwa taifa kama letu wataona aibu kupokea.. Manake wakituangalia hata umeme hatuna na hatujapata maafa.. Tuchangeni tulipe dowans umeme uwake

Ama kweli akili ni nywele, kila mtu ana zake!

Naweza kuamini huu usemi walau kwa sasa.. Wajapani wamekumbwa na majanga ambayo binadamu hawezi kuyaelezea kwa lugha ya kawaida.
Lakini wameona jinsi ulimwengu ulivyoduwaa na kupelekea masoko ya hisa kuyumba na kuporomoka ghafla dunia nzima.

Nimefuatilia kwa karibu impact na kwenye mtandao inaonekana tangu juzi wame-pump karibu ya $350,000,000,000 ($350 Bil) kwenye world stock market ili ku-stabilize na kupunguza maafa ya kurudi tena kwenye mdororo wa uchumi wa dunia (world economic recession).

Na kweli leo stock markets zimepanda ghafla dunia nzima!
Tanzania je??!
 
Back
Top Bottom