TUCTA ni dhaifu inahitaji kufutwa

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
kumekuwa na ongezeko kubwa la migogoro kati ya wafanyakazi na serikali.
Haiingii akilini kuona kila sekta ya wafanyakazi ikiingia kwenye mgogoro na serikali huku TUCTA ambayo ndio mwamvuli wa vyama vyote vya wafanyakazi wakiwa kimya.hii inamaanisha hakuna mawasiliano kati ya TUCTA na vyama vya wafanyakazi.hakuna haja ya kuwakata wafanyakazi fedha zao huku matakwa yao hayaelezwi au kusimamiwa na TUCTA.nashauri TUCTA ivunjwe na kubakia na mashirikisho ya kisekta ya wafanyakazi.
 
  • Thanks
Reactions: PPM
Nadhani kikwazo cha uimara wa TUCTA ni raisi wake bw. Omar Jumaa.
Huyu mtu mimi sielewi aliwezaje kuchaguliwa kwa mara nyengine.
 
Naunga mkono hoja TUCTA wanatuyeyusha yani naona wapo kimyaaaaa sanaaaa wakati hili swala halipo mahakani.
 
TUCTA na TALGU ni wasaliti wa wafanyakazi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
TUCTA na TALGU ni wasaliti wa wafanyakazi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

Hamna jamani sie TUCTA mbinu zetu hazitekelezeki tufanyeje tupeni ushauri......kama serikali kubwa yaani wananchi wote lkn haya hapa chini hayayakutekelezeka sie tutawezaje?

Kufikisha mahakamani mafisadni na kuwafirisi -haitekelezeke tunawaomba warudishe walivyoiba
Kuinyanyua taifa stars kwa serikali kumlipia kocha mbrazil- haikutekelezeka
Mishahara kima cha chini kwa wafanyakazi-madai hayatekelezeki
Haya basi madaktari tuu-madai hayatekelezeki
Kummaliza kiongozi wa madai ya madaktari-mbinu hazitekelezeki
Haya basi walimu tuu madai yao-madai hayatekelezeki
 
kuna haja ya kila chama kumove kivyake

hata mimi naamini hivyo,TUGHE imeshindwa kuwatetea madaktari kwa kuwa ni chama cha watumishi wa serikali kuu akiwemo rama mzee wa mabwepande.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Nilikuwa nafikiria kitu kama hicho leo. Namna pekee ya kuweza kufanya mgomo wenye matokeo kwa serikali ni ule utakaoitishwa na TUCTA. Lakini kama na wenyewe ni "mbayuwayu" na wanaogopa "kukamatwa" watafanya nini na wao wakizuiwa na mahakama kugoma? Kimsingi, JUWATA ilikuwa na nguvu zaidi kulikua TUCTA!
 
TUCTA ya leo inasubiri sherehe za mei mosi kuomba nyongeza ya maslahi.wanatumia mbinu ile ile wakitegemea matokeo tofauti.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Nilikuwa nafikiria kitu kama hicho leo. Namna pekee ya kuweza kufanya mgomo wenye matokeo kwa serikali ni ule utakaoitishwa na TUCTA. Lakini kama na wenyewe ni "mbayuwayu" na wanaogopa "kukamatwa" watafanya nini na wao wakizuiwa na mahakama kugoma? Kimsingi, JUWATA ilikuwa na nguvu zaidi kulikua TUCTA!
nashangaa sana kuona chama cha wafanyakazi kimedharauliwa namna hii wakati wana nguvu ya kuamua uongozi wa nchi uende kwa nani.ni kweli wafanyakazi tumekuwa mbayuwayu mbele ya serikali.hata mahakama ilitakiwa kujua ni sehemu ya TUCTA.
 
Mgaya alianza vizuri kumbe alikua anasaka kiti tu saiv kakipata loh bure kabisaaaa....ila walimu wamejitahidi sema mahakama zetu hizi chovu zilizojaa rushwa zimeingilia kama kawaidaila je zitaingilia hata kufundisha darasanai?~~!!
 
Back
Top Bottom