TUCTA kuandaa mandamano nchi nzima kupinga bei mpya ya umeme

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Jana TUCTA wamekuja juu na kusema hawaafiki bei mpya ya umeme na kuwa wataitisha maandamano nchi nzima kupinga bei hiyo ambayo itachangia sana kuua soko la ajira na kuwaongezea gharama ya maisha wafanyakazi ambao kipato chao ni kiduchu sana.................

Wafanyakazi nchi nzima kuandamana
Friday, 24 December 2010 21:12 Zaina Malongo


KILIO cha wananchi kupinga kupanda kwa bei ya umeme, sasa kimehamia kwenye moja ya makundi makubwa na yenye nguvu baada ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(Tucta) kuandaa maandamano nchi nzima kupinga bei mpya.
Tayari Chadema imeshatangaza kuandaa maandamano nchi nzima kupinga bei hiyo mpya ya umeme ambayo ni ongezeko la asilimia 18 na ambalo limeshapingwa na wananchi wa kada mbalimbali. Mbali na ongezeko hilo, Tanesco pia imetangaza mgawo wa umeme utakaokuwa wa kuanzia masaa matano hadi 10 kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia jana, uamuzi ambao umetafsiriwa kuwa utaongeza makali ya maisha.

Katibu mkuu wa Tucta, Nicholas Mgaya alisema watafanya maandamano ya amani kupinga kupanda kwa umeme kutokana na athari zake ambazo alisema ni pamoja na kusababisha ugumu wa maisha na umasiki kwa wafanyakazi. "Serikali isipandishe bei ya umeme bali itafute njia nyingine za kuzuia tatizo hilo kutokana na athari kubwa zitakazowalenga wafanyakazi pamoja na kuliweka taifa katika janga la umasikini," alisema Mgaya. Mgaya alisema nchi kama ya Tanzania, ambayo ina vyanzo vya maji kama vile maziwa na mito, ikitumia rasilimali hizo kwa umakini, inaweza kuondoa tatizo la umeme.

"Kama serikali haitachukua tahadhari katika kipindi hiki, hapo baadaye kutakuwa na mwelekeo mbaya hasa kwa wananchi kukosa umeme kabisa," alisema Mgaya. Alisema kamati ya utendaji wa Tucta iliyokutana juzi katika kikao cha kawaida, iliazimia kuwa itoe taarifa kwa serikali ya kupinga kupanda kwa bei ya umeme. Alisema hatua hiyo ni kutokana na kwamba hata bei ya sasa iko juu na hivyo kuwafanya wananchi washindwe kuimudu. " Hivi sasa kuna watu hawatumii baadhi ya vifaa vya umeme kutokana na ukubwa wa bei, je ikipanda tena si watashindwa hata kuwasha taa," alisema.

Takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia 12 ya Watanzania ndio wanaotumia umeme majumbani, lakini kutokana na umuhimu wa nishati hiyo katika uzalishaji, kupanda kwa bei ya umeme kunaweza kusababisha gharama za maisha kupanda.

Tanesco inategemea kuzalisha umeme kutokana na mitambo inayoendeshwa kwa maji, gesi na dizeli.
Akitangaza uamuzi wa kupandisha bei ya umeme, mkurugenzi wa Ewura, Haruna Masebu aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa ongezeko hilo la bei ni chini ya mapendekezo ya Tanesco kwa asilimia 16.1. Kwa mujibu wa Masebu, Tanesco ilipendekeza umeme upande bei kwa asilimia 34.6, lakini baada ya uchambuzi wa kina, mamlaka ilikubali kuruhusu nyongeza ya asilimia 18.5 kwenye nishati hiyo.

Pia alisema pia wameondoa mfumo wa shirika hilo uliokuwa unawapa nafuu wafanyakazi wake kulipia garama za umeme na kwamba kuanzia sasa wafanyakazi hao watalipa gharama hizo kama watumiaji wengine. "Tumeamua kuruhusu ongezeko hilo na kama Tanesco wanadhani gharama zao za uendeshaji zinapanda kwa sababu ya ongezeko la gharama za mafuta ya kuzalishia umeme, wanaweza kujenga hoja na tukabadilisha bei ya mafuta pia," alisema Masebu.

Masebu alisema pia wameiagiza Tanesco kuanza mabadiliko hayo ya bei ndani ya siku 30 na kuwapelekea mkataba ili kujiridhisha kama hautakuwa na madhara kwa watumiaji wa nishati hiyo. Wakati huohuo, Aziza Masoud na Hidaya Omary wanaripoti kuwa serikali inadaiwa kuwapiga danadana na kuwazunguka wananchi kwa kuwatumia kama chambo cha kutatulia matatizo yanayowakabili.

Naibu katibu mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alitoa kauli hiyo baada ya Tanesco kutangaza mgawo wa umeme kwenye mikoa yote iliyounganishwa kwenye gridi ya taifa. Akizungumza na Mwananchi jana, Mtatiro alisema tatizo la hilo linatokana na serikali kutotafuta vyanzo vipya vya kuzalisha umeme na badala yake kuendelea kutumia vile vilivyoanzishwa enzi za Mwalimu Julius Nyerere. "Tatizo la umeme haliwezi kuisha nchi hii hata baada ya miaka 1,000 kutokana na serikali iliyo madarakani kushindwa kutafuta vyanzo vya umeme vya ukweli. Hivi sasa tunaendelea kutumia vyanzo vya Mwalimu Nyerere ambavyo kwa sasa haviwezi kukidhi mahitaji yaliyopo," alisema Mtatiro.

Alisema kulingana na mahitaji, serikali ilipaswa kutafuta vyanzo mbadala vya kuzalisha umeme badala ya kuingia kwenye mikataba aliyoiita ya kifisadi kama wa Dowans. Alisema bei ya nishati ya umeme imepanda kwa 18 asilimia wakati kipato cha Mtanzania kipo palepale, kitu alichosema kinaonyesha dalili za kupanda kwa gharama za maisha. "Walisubiri uchaguzi upite ndio wameanza kuleta matatizo yao. Kipindi kile cha uchaguzi waliogopa kusema haya kwa kuwa wananchi wasingekubali kuwachagua na hii hali haiwezi kuvumilika," alisema Mtatiro. Alisema nchi isiyoweza kuzalisha umeme wa kutosha haiwezi kuwa na viwanda, hivyo watu hawawezi kupata ajira. Naye mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba alisema suala la mgawo wa umeme limetokana na ufisadi.

"Hakuna mpango wala mkakati wowote wa kumaliza tatizo la umeme nchini, bali ufisadi ndio umejaa na utaimaliza Tanesco," alisema Lipumba. "Sioni mwanga wowote mbele ya tanuri linalofuka moshi, kwa hiyo utatuzi wa tatizo hili utabakia historia na siasa za mdomoni." Alisema kuwa kila mwaka mahitaji ya umeme yanaongezeka kwa asilimia 15 na kuhitaji megawati 200 au 300 kati ya zile mia 800 zilizopo sasa. Naye Prof Haji Semboja kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaamu (Udsm) alisema ukosefu wa sera na taaluma ya kutatua tazizo ndio kikwazo kikubwa kinachokwamisha upatikanaji wa suluhisho.

Aliongeza kusema: "Sekta mbalimbali zitaathirika na mgawo huu kwa kuwa hazitaweza kuzalisha na hivyo kusababisha kurudi nyuma kwa uchumi wetu." Alisema viwanda vidogovidogo na wananchi wa kawaida ndio wataathirika zaidi ukilinganisha na wale wenye viwanda vikubwa. Mafanyabiashara wa nguo katika soko la Kariakoo jijini, Ashirafu Jumaa alisema itawalazimu kuongeza gharama za uendeshaji wa biashara zao kwani wanapaswa kutumia jenereta ili kuepukana na joto na mwanga hafifu kwenye maduka yao. "Mgawo tumeusikia na sisi hatuwezi kufunga biashara zetu... kikubwa tutakachokifanya ni kuingia gharama za kununua jenereta ili tuendelee na shughuli zetu," alisema Jumaa.

Ijumaa, mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Francis Kiwanga alipinga ongezeko hilo akisema bei hiyo mpya ni mzigo kwa mtanzania wa kawaida. Kiwanga alishauri Watanzania waandamane kupinga Tanesco kuendelea kuongeza bei ya umeme wakati huduma zake ni mbovu. Alisema kupandishwa kwa gharama za umeme kila kukicha, kunachangiwa na mikataba mibovu ambayo shirika hilo limekuwa likiingia.
 
Wafanyakazi na Wakulima wa nchi hii wanaposema jambo, sote tunatulia tulii na kuwasikiliza kwa kila nukta.

CHADEMA + Wafanyakazi Tanzania + Vyuo Vikuu kwenye maandamano ongezeko bei ya umeme kweli sasa mambo mazito na hapo madai ya uchakachuaji umeya bado, mmmhhh!

Kweli kutawala watu WAPENDE WASIPENDE ni kazi kubwa kweli kweli katika nchi.
 
Hivi Mungu haoni tunavyoteseka? Shuka Bwana shuka....

Kuiba kura za watu ni mzigo mzigo mkubwa huo!!! Nchi haiwezi ikatulia mpaka ukawarudishie chao kiungwana tu. Hii miaka mitano ni miaka ya shida tupu!!!!
 
wtz tuamke bilakujali itikadi vyama panapohusumasilai ya taifa izuluma kuibiwa havitaisha iwapo hatutaonyeshamshikamano
 
Nadhani tucta wangeitisha mgomo wa wafanyakazi nchi nzima kwa muda usiojulikana kupinga suala hili,pia wangeunganisha na madai ya maslahi bora.
 
Back
Top Bottom