Tuchukue tahadhari na magazeti ya Habari Corporation

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,599
3,673
Siku zote magazeti yanayochapishwa na kampuni ya Habari Corporation chini ya mhariri mtendaji muhingo rweyemamu yamekuwa yakiandika habari zenye kutia shaka ile dhana ya weledi katika taaluma ya habari.

Ukitizama trend ya kinachoandikwa sasa hivi baada ya Dr. Slaa kuchukua fomu ya kuomba kugombea Urais kupitia CHADEMA, wanamuhusisha Slaa na Kanisa Katoliki na Wakristu, angalia rai ya jana na pia mtanzania kwa nyakati mbalimbali, na tunashangaa serikali imekaa kimya kwa uchochezi huu unaofanywa na Habari corporation kwa kuwaaminisha watu siasa chafu zenye mwelekeo wa udini, other wise tunataka kuamini serikali ndio imewatuma hawa wehu wa HC.
Ni vema sasa tukachukua tahadhari na makanjanja hawa wasiokuwa na aibu na wasioitakia mema Tanzania.
nawasilisha.
 
umenena. lkn tunaambiwa cuf ni waislam, ukisema hivyo ndani ay jf utaungwa mkono 100% na wachangiaji wakiwemo wanaojulikana kama chadema dam. lkn sasa kijiba kimegeuka kimeingia mguu mwengine na mwiba mwengine , malalamiko yamekuwa makubwa. jitahidi sana kuelimisha wananchi wanweaza kuelewa baada ya miaka 100 ijayo

Two wrongs do not make a right
 
mkuu ukisikia siasa mchezo mchafu ndio huo, hiyo ipo sana obama aliitwa gaidi lakini akapeta.
hata ukisoma tz daima usitegemee kukuta mazuri ya vyama vingine zaidi ya chadema
 
mzee umenena, lkn CUF wanaambiwa ni chama cha kiislam hamna aliepiga kelele isipokuwa cuf wenyewe. lkn humu humu ndani ya jf unaposema cuf wadini utaungwa mkono 100% na wachingiaji, sasa kijiba kimegeuka kimekuwa huko. papatueni mnaweza watu wakakusikilizeni lkn labda miaka 100 ijayo

Malaria Sugu: Jukwaa hili la JF ni tofauti yna magazeti yaliyoandikishwa kwa kufuata sheria na maadili. Humu ndani unaweza kusema chochote na sijasikia Mkuchika akitaka kuifungia JF. lakini yuko tayari kuyafungia magazeti ya Kubenea na Mengi, lakini siyo ya Rostam. Hapo ndiyo wengi tunajuliza!

MS -- Usichanganye mada tafadhali. Wewe endelea tu kumponda Dr Slaa kwa ukristo wake humu ndani lya JF lakini magazetini unaweza kupambana na kesi za libel, iwapo Mkuchika atalisamehe gazeti kulifungia. Jaribu kuandika gazetini unayoandika humu ndani uone!!!!!!
 
umenena. lkn tunaambiwa cuf ni waislam, ukisema hivyo ndani ay jf utaungwa mkono 100% na wachangiaji wakiwemo wanaojulikana kama chadema dam...


kwa hiyo msingi wa uchochezi wa kidini wa HC dhidi ya dr slaa ni kwa sababu cuf wameambiwa ni wa dini fulani? ama kweli jf imejaa hoja za sokoni (market place arguments) na ni hizo hizo zinazoleta uchochezi kwa wenye fikra sahihi.
 
Back
Top Bottom