Kitia
JF-Expert Member
- Dec 2, 2006
- 418
- 74
Hii ina maana kuwa hata magari yaliyozidi miaka mitano ambayo tayari yalikuwepo na kutumika nchini yasiruhusiwe kutumika kwa vile yamekuwa kuukuu? Mimi naona kitu cha kuzingatia hapa ni ubora wa gari, na sio umri, maana gari linaweza likawa na miaka hata mitatu lakini likawa na hitilafu ambazo zinaweza kusababisha ajali.
Tuchukue hadhari kuzuia uagizaji magari makuukuu
2008-10-28 16:20:21
Na Mhariri
Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, akizungumza kwenye uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama mwishoni mwa wiki alisema kwamba serikali inakusudia kuanza utaratibu wa kuzuia magari yenye zaidi ya umri wa miaka mitano kuingizwa nchini.
Katika kauli hiyo, Waziri huo alisema sababu kuu ya serikali kutafakari hatua hizo ni baada ya kugundua kwamba ajali nyingi za magari zinachangiwa kwa kiwango kikubwa na uchakavu wa magari hayo.
Kwa maana hiyo umri wa magari haya kadri unavyokuwa mkubwa ndivyo uwezekano wa kuhusika katika ajali unaongezeka.
Inawezekana kabisa kwamba Waziri Masha anatoa kauli hii kulingana na utafiti uliofanywa na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani.
Kwa maana hiyo ana ushahidi usiotiwa shaka kwamba magari makuukuu yamekuwa chanzo kikubwa cha ajali nchini.
Hata hivyo, tunafikiri serikali inawajibika kutafakari vuzuri na kwa kina zaidi juu ya hatua hizi inazotaka kuchukua kuhusu magari makuukuu.
Tunasema haya kwa sababu tunapotazama uchumi wa taifa hili na watu wake tunajawa na hofu kama kweli ni watu wangapi watakuwa na uwezo wa kununua magari mapya.
Tunasema haya kwa sababu historia inashuhudia ukweli huo, wakati magari makuukuu yalipokuwa yameharamishwa nchini, idadi ya magari ilikuwa ndogo sana.
Uchache wa magari haya kwa kiwango kikubwa ulikwamisha kasi ya maendeleo, matokeo yake ni mrundikano wa watu katika vyombo vya usafiri na hata kukwama kusafirisha mizigo na huduma nyingine.
Ilikuwa ni kawaida kabisa watu kutumia hata malori kusafiri katika maeneo ya mjini, lakini kibaya zaidi upigwaji marufuku wa magari makuukuu wakati huo haukuongeza kasi ya wananchi kujiletea maendeleo yao.
Kwa hali hii basi, tunaamini kwamba hata kama serikali ina kusudio zuri kiasi gani katika kuyaondoa barabarani magari makuukuu, bila kwanza kutafiti kwa kina na kuelewa vizuri uwezo wa Watanzania, hatua hiyo inaweza kuwa ni ya kufifisha maendeleo kuliko kuyaharakisha.
Tunajua, kwamba katika sheria na kanuni za kuagiza magari nchini waagizaji wote wanapashwa kuzingatia viwango.
Kuna vyombo vya ukaguzi wa magari kabla ya kupakiwa melini kutoka kokote katika kona ya dunia hii, lakini pia kuna vyombo vya ukaguzi kabla ya kupakuliwa kutoka melini.
Kote huko uzingatiaji wa viwango, ubora na uwezo wa vyombo hivyo kutembea barabarani unapaswa kuhakikiwa kwa umakini mkubwa.
Swali linalosumbua, ni je, magari yote yanakaguliwa vilivyo na hivyo kuruhusiwa kutembea katika barabara zetu?
Tunathubutu kusema, kama vile tunavyoona bidhaa feki madukani zikiwa zimepitia kwenye bandari au vituo vya forodha katika mipaka yetu zikiwa zimezagaa mitaani, nayo magari makuukuu ambayo hayastahili kugusa barabara zetu, pia hupitia kwenye vituo hivi.
Kwa hali hiyo, kinachochangia magari mabovu kujaa barabarani si suala la uchakavu wake kwa maana ya kuwa ya miaka mingi tangu kutengenezwa, ila ni udhaifu mkubwa katika kudhibiti bidhaa zote zinazoingia nchini.
Kwa hali hiyo basi, kukimbilia kutunga sheria ya kuagiza magari kutoka nje kwa kuweka umri wa miaka mitano haitakuwa tiba ya ajali za barabarani.
Suala la ajali barabarani ni pana, lina mlolongo mrefu; kama vile utoaji wa leseni kwa madereva, uwajibikaji wa trafiki barabarani, lakini kubwa zaidi tabia ya wenye magari ya kutaka kujipatia kipato kikubwa kwa haraka bila kujali usalama kwanza.
Ni kwa hali hii tunafikiri hatua yoyote ya kuharamisha magari yenye zaidi ya miaka mitano kuingia nchini haitapunguza ajali, ila itazidisha umasikini kwa Watanzania.
Kazi ya kudhibiti ubora ipewe kipaumbele kuliko sheria za mkumbo kama hii iliyopendekezwa na Waziri Masha.
* SOURCE: Nipashe