Tuchangie mawazo ya kumkomboa mtanzania

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Haipiti siku moja bila kuona posts za shutuma baina ya vyama - CCM hivi, CDM vile, CUF hivi na vile na posts nyingi katika hizi ni kushutumiana vurugu na udini. Sioni kama posts hizi zinaweza kumsaidia Mtanzania anayeishi kwa shida, mlo mmoja, hana ajira, watoto hawapati elimu ipasavyo, bara bara za vijijini hazipiti, maji na umeme mjini na vijijini shida, rushwa, wizi wa mali za umma na mengine mengi. Hivi shutuma na "hypothesis" za vurugu na udini zitatufikisha wapi?

Kwa nini Great Thinkers hatutoi michango ya "kiujenzi" inayoweza kumsaidia Mtanzania kujikwamua alipo? Sisi kama tunaoumwa na hili, tuna mchango gani?, katika maeneo yetu ya kazi, mtaani, kijijini, kwa marafiki na wanajamii wenzako? Michango yetu hata iwe midogo kiasi gani, kama vile usafi wa mazingira, kupeana miamko na ushauri wa kujiendeleza n.k., ni bora kuliko kuandika mamaia ya kurasa za kushutumiana.

Kwa kuanzia na mimi, nimo katika kutafuta pesa kidogo ili niwakusanye vijana wa kijijini kwangu waanzishe mradi wa matofali ya kuchoma na upandaji miti ya biashara - hasa ya mbao na kuni.

Tanzania itajengwa na ubuifu wa vitendo na sio ubunifu wa majungu.
 
Tudai serikali tatu ,,mfumo huu utamkomboa mtanganyika na tanzania kwa ujumla,,,
 
Back
Top Bottom