Tubadilishe Jina la Jiji la Arusha : Liitwe Serengeti au Kilimanjaro

Hoja hii inafaa kuipeleka katika Halmashauri ya Manispaa ya Arusha. Madiwani wana uwezo kisheria kubadili majina ya Miji na vitongoji vyao iwapo wataona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

Pamoja na yote sioni mantiki yoyote ya kuita mji wa Arusha.. Kilimanjaro...!

Kibunango,

Hiyo itakuwa hatua ya pili, baada ya wananchi kuikubali hoja kwanza kama ina manufaa, then ndio logistic za Kubadilisha.
 
......Kwa wenyeji wa Arusha ..hili jina lina maana kubwa sana....na ya maana...nakumbuka kuongea na wazee zamani na waliniambia..sema nimesahau..kwa kuwa sikuchukulia umuhimu kwa miaka hiyo..........

wapi MORANI 79...yerrro ..taee njoo elesea iko na maana gani hii jina ati!!!

Kwi kwi kwi.

Challenges, how many tourists are interested with the name "Arusha" and how many are interested with tha name "Kilimanjaro", "Serengeti", "Zanzibar" etc?

Kwa hiyo tunadumilisha mila eehee!!! Haya bwana
 
Tukibadili jina ndio tutapata watalii wengi? Utalii wetu wa ndani ukoje? Nani anafaidika zaidi na utalii huu kwa hivi sasa? Je, utalii sio sawa na mikataba mibovu ya madini?

Don't we need to clean our house first?
 
Kwi kwi kwi.

Challenges, how many tourists are interested with the name "Arusha" and how many are interested with tha name "Kilimanjaro", "Serengeti", "Zanzibar" etc?

Kwa hiyo tunadumilisha mila eehee!!! Haya bwana

Hatutoi majina ya maeneo kwaajili ya kujiuza bali kutambulika/kuenzi wazee maarufu au viongozi. Tunapaswa kutangaza utalii kwa mikakati bora (tujifunze Kenya) kwani tunaweza kubadili jina la Arusha bado kusiwe na impact katika utalii. Mkoa Manyara umepata watalii wangapi baada ya kuitwa MANYARA?

But is good idea.
 
Hiyo halmashuri ya Arusha ndio sababu kuu ya kuufanya mji wa Arusha uendelee kuwa kituko.Na hii ni product ya Lowasa aliyemweka swahiba wake kuwa Mkurugenzi wa huo mji ambaye uwezo wake unatia mashaka. Kwani ni lazima International town kama Ar itawaliwe na Mwarusha ?

Serengeti, Kilimanajaro nk inafahamika kwa contents zake na sio jina. Kilimanjaro ingeweza kuitwa Kichuguu na sifa yake ingebaki pale pale. Contents za Arusha ni poor management na matokeo yake ni uchafu na uhalifu mtupu.Miji kama hii inatakiwa iendeshwe na wataalam wa Urban Management (urban Managers) ambayo ni profession. Sasa ukimweka daktari wa watu kama aliyeko sasa hivi kuwa Director wa jiji si mchangayiko maalum.?
 
Hatutoi majina ya maeneo kwaajili ya kujiuza bali kutambulika/kuenzi wazee maarufu au viongozi. Tunapaswa kutangaza utalii kwa mikakati bora (tujifunze Kenya) kwani tunaweza kubadili jina la Arusha bado kusiwe na impact katika utalii. Mkoa Manyara umepata watalii wangapi baada ya kuitwa MANYARA?

But is good idea.

Manyara ni kitu kidogo kwenye utalii wa Kimataifa,,, lakini Serengeti na Kilimanjaro ni majina makubwa... ingekuwa poa kama unaleta watalii kwenye uwanja wa Kilimanjaro, wanaona Mlima kilimanjaro, wanalala kwenye Mji wa Kilimanjaro... na Mikutano ya kimataifa inafanyika kwenye jiji la Kilimanjaro... jii inaua kabisa contradiction kwamba Kilimanjaro iko wapi?
 
Mabadiliko hayo yote kumkamua mtalii. Mtalii hataleta maendeleo nchi hile.
 
Manyara ni kitu kidogo kwenye utalii wa Kimataifa,,, lakini Serengeti na Kilimanjaro ni majina makubwa... ingekuwa poa kama unaleta watalii kwenye uwanja wa Kilimanjaro, wanaona Mlima kilimanjaro, wanalala kwenye Mji wa Kilimanjaro... na Mikutano ya kimataifa inafanyika kwenye jiji la Kilimanjaro... jii inaua kabisa contradiction kwamba Kilimanjaro iko wapi?

Haya kama jina ni tija wilaya ya Serengeti ina nini cha ajabu?
 
Taabu zote hizo za kubadili majina hazina uzito wowote.

Kama ni shughuli ya 'ku-brand,' basi 'brand' Tanzania. Kenya wanafanya sasa kwa kuunda task force ya kufanya hivyo, na Afrika Kusini walishafanya siku nyingi.

Kenya kuiuza 'Kilimanjaro' kama mlima ulio kwao haikuwalazimu kubadili jina la mji wao wowote kuwa Kilimanjaro!

Jengeni hoteli za kutosha, barabara nzuri ziwepo hadi kwenye vivutio hivyo vya utalii, huduma kwa watalii zipendeze, pawepo na usalama; na promotion ya nguvu ifanyike, watalii wengi tu watakuja.

Ukanda wa pwani wa Kenya ndege zinakuja moja kwa moja toka Ulaya na kuleta watalii huko bila ya lazima kuwapitisha Nairobi kwanza. Sisi wa kwetu wanatua Nairobi kwanza, wakishachoka na huko ndio wanavushwa mpakani, tena na hao waliowauzia hizo 'packages' toka huko kwao - sasa ungetegemea nini kama mtalii asifikirie kuwa bado yupo Kenya wakati anapokwenda kupanda mlima!

Hata matangazo na maandishi tu, wenzetu wa Kenya wanajiuza sana - ukitafuta makara zilizoandikwa kuhusu Maasai Mara kuwa ndiyo iliyopewa hadhi ya 'Wonder of the World' zipo nyingi tu; kwetu ukitafuta Serengeti ambayo ndiyo kwa kiasi kikubwa ilihesabika kuwa 'wonder of the world' utadhani ni Maasai Mara ndiyo namba moja na Serengeti inai-support hiyo Maasai!

Hata kwenye matangazo ya biashara kwa watalii - unakuta Habari inatangaza "Kenya Tanzania" - ulishawahi kujiuliza ni kwa nini imetangazwa hivyo?

Tusipoteze muda mwingi bure kwa kupoteza lengo. Mambo muhimu yanayotakiwa ni kuuza vivutio vyetu vya utalii ambavyo vipo vingi na vizuri zaidi, na kujenga miundombinu inayotakiwa kuwawezesha hao watalii wafurahie utalii wao.
 
..asalaam aleykhum,

..habari za siku kuu kadhaa zilizopita?

..kasheshe, nadhani ungependekeza iitwe meru!
 
Hoja kwa kweli sio kwa ajili ya malumbano... nilisema kwamba mashuleni tumekaririshwa kwamba tutangaze utalii kwa namna fulani... sasa strategy hii niliyotoa kama changamoto ni tofauti na haiko kwenye vitabu moja kwa moja.

Ila bado ukisoma hoja yangu kwa makini (A to G) uta-draw point kwamba kwenye ile A-G kulikuwa na mtiririko wa ku-justify mabadiliko ninayoyaomba bila kuelezea maelezo mengi zaidi. Just go through those points again na nipe specific ipi hailewi logic yake then i can start from there!!!

Solution za Kuikomboa hii nchi mara nyingi hazitakuwa zile popular kama kukamata madini Airport yenye thamani ya mil 150, au kurudisha Bil. 133 za EPA etc... then after that what else... we need vitu endelevu !!! sasa katika kuvitoa hivi kwa kweli vitakuja vingi ambavyo sio popular kama hili langu... lakini eventually people will understand.

Kasheshe,
Ninakubaliana na wewe kabisa kuwa hoja yako haiko kwa ajili ya malumbano, lakini ni vema (kama ulivyogusia hapo awali kuwa ukitaka kutoa maelezo yote itakuwa ni hadithi ndefu) ukatoa maelezo ya kutosha hata kama ni marefu ili uweze kueleweka vizuri zaidi na contributions zetu ziweze kuwa na maana zaidi. Vinginevyo sioni sababu ya kubana maelezo ambayo ni ya kina na unayo!
 
Kasheshe uko sahihi kabisa hii ni sawa kabisa na mtu unaporekebisha vazi lako baada ya kuona umevaa vibaya. Ndugu zetu Wakenya wamebaka mlima wetu na kuutangaza kwamba ni wa Kenya sasa kuna kila haja ya kufanya mabadiliko kwa lengo la kuutangaza mlima Kilimanjaro kwamba ni mali ya Tanzania. Arusha kuitwa Serengeti sioni kama itafaa lakini kuitwa Kilimanjaro hapo ni mwake.
 
Kwa nini mji wa Moshi usiitwe Kilimanjaro? Arusha kuitwa kilimanjaro mmhm naona ni sio mwake kabisa!
 
Back
Top Bottom