tubadilike

Kilambi

Member
Apr 3, 2009
94
18
habari ya siku nyingi wana jf

naandika huku nikiwa na donge moyoni linalonifanya niseme...i wish i knew..
yes..i wish ni msemo wa kujuta na ndivyo ilivyo.. nimeoa kwa muda mrefu na kwa kipindi kirefu nimekuwa sio muaminifu katika ndoa yangu, kuoa kwangu hakukuwahi kuwa na tofauti na bachelor yeyote asiyejiheshimu, nimefanya hivyo kwa kificho kiasi kwamba imekuwa vigumu mtu kunishtukia including my lovely wife, nimekaa nimetafakari na kugundua kuwa hakuna lolote jipya zaidi ya kuingiza kipato cha familia kwenye uzinzi na kutumia akili nyingi katika kujificha ili kuendeleza uzinzi tu, kila nilikokuwa napita nikiangalia nyuma my wife ana vitu vya ziada mbali tuuu,nimeamua sasa baaasi,natulia na mke wangu tuu na familia yangu, sitaki tena!offcource sikuwahi kumuudhi na nimekuwa nikifarijika mno ninapokuwa nae na pia hajawahi kunihisi, nashindwa kuelewa sijui ni pepo au nini kilikuwa kikinipeleka huko, heei..usijeanza kujiuliza nini kimenikumba,niko safi kimwili na kifya.sasa hapa napata taabu kwa wale niliokuwa nawafuata hawanielewi kabisa kuhusu maamuzi yangu,yes i messed up lakini sasa nahitaji kubadilika, naona kama nimekuwa huru zaidi siku hizi kwani sina tena haja ya kufichaficha simu,akili yangu pia imekuwa na muda mwingi zaidi wa kufikiria mambo ya kimaendeleo zaidi....
wewe je?!
 
Hufichi fichi simu, hivyo vimeo vyenzako vimekuelewa?
Nahisi umekiona cha moto huko!
Au kipato kimepungua,
Au umekuwa mkubwa sasa!

All in all hongera kwa maamuzi yako.
Usirudi tena ulikotoka, nyie ndo mnaozibia wanaotafuta wa kuoa wasipate.
 
hongera kwa kulielewa hilo.hakuna aliekuwa mkamilifu.muombe msamaha mke wako,ila usimwambie sababu ya kumuomba msamaha.yasije yakazuka mengine.akikuuliza msamaha wa nini,wewe mwambie najihisi sikuwa the best husband kwako,mke wangu wewe ni mvumilivu nakupenda na nitazidi kukupenda,make it up kwa uliyomkosea kwa kumfanyia chochote kizuri.bora umegutuka mapema.kuna wengine huwa hawapendi kubadilika
 
Wengi wamefanya makosa mengi kwenye ndoa zao, cha muhimu ni kujiuliza walifikia stage kama yako, sasa hivi unajielewa, unajijua, ulikuwa umepotea na sasa ni kama umezaliwa upya, nakushauri endelea na moyo huohuo usibadilike tena.......kucheat ni kubaya sana hasa unapokuwa na family kipindi kile unakuwa hata hauko huru na simu yako ikiita riho inakupaa utadhani nini sijui, kuoga unaogopa....mhhh muombe Mungu akusaidie kwa hili mwenyewe hautaweza, vishawishi ni vingi sana
 
Kilambi i really hope your words are genuine...

Hongera saana kwa kutambua makosa/madhaifu yako na kutaka kuyafanyia kazi..
Hata hivyo inabidi uwe makini saana na furaha yako, sababu wewe ni mwanaume
naamini kua you understand more than me jinsi ilivyo ngumu mwanaume kubadilika his
true self... NDIO unasema kua umeacha, inatakiwa pia utafakari kitu gani kimekufanya uje
katika uamuzi huo... ukitambua na kukubali hio ndo sababu then utajua jinsi gani daima
ubaki faithfull kwa mkeo (yaani usishawishike tena...),
umuhimu wa wewe kujua sababu ni kwamba itasadia saana katika kudumisha malengo yako.

Sababu ambazo zina possibility kubwa wewe kurudia...
  • Umefumaniwa but ukaponyoka.. (ina maana usha ona kabisa kua jambo baya kama kupigwa kama mwizi lingekukumba au mkeo kujua)
  • Mwanamke ulompenda nje ya ndo kakutenda..(ina maana unaona bora tu ubaki na wife kuliko tapeli mwingine..)
  • Hali ya fedha imebadilika for the worse.. (aidha labda kazi umeachishwa/posho sitishwa/umebadili kazi n.k)
  • Na nyingine nyiiingi.
Sababu ambazo possibility ya kutorudia...
  • You have fallen in love with your wife na kugundua she is the best.
  • Umepima afya inspite your ukipanga na carelessness umekuta afya ni nzuri.. Yaani no STDs
  • Umejitambua na ghafla kuhisi umekua mtu mzima na inatakiwa utulie...
BUT what ever the factors nakuombea saana uweze simamia uamuzi wako for inapendeza saana watu wanapokua waaminifu dhidi ya each other.
 
No one can screw your life, unless you gave them the screw driver!-by Gaga
mimi napenda uelewe hii sentence......na wote wanaopenda matatizo kama huko ulikochomoka-muombe mungu wako sana akulinde.Kwani shetani ananjia nyingi...unaweza okoka hiyo usipokuwa na mungu karibu waweza ukatumbukia kwenye balaa jingine....mweke mungu mbele katika maisha yako mapya.
 
No one can screw your life, unless you gave them the screw driver!-by Gaga
mimi napenda uelewe hii sentence......na wote wanaopenda matatizo kama huko ulikochomoka-muombe mungu wako sana akulinde.Kwani shetani ananjia nyingi...unaweza okoka hiyo usipokuwa na mungu karibu waweza ukatumbukia kwenye balaa jingine....mweke mungu mbele katika maisha yako mapya.
Heshima zote zimwendee Mwanajamii1
 
Duuu.. yamekusibu yapi mkubwa huko duniani? manake katika hali ya kawaida ni aghalabu sana kwa mwanaume kuamua tu hivi hivi kuuacha uzinzi na kumgeukia wife.. Hongera sana.. Usiache kusali maana shetani hatoacha kukujaribu kama usipokuwa makini.
 
pamoja na ukweli kuwa watakupopoa mawe wakitoka huko mafichoni walipo,ww ni mjanja coz umejistukia b4 hujastukiwa. hongera. Neema ya Mungu ina nguvu,nahisi maombi ya mkeo yamejibiwa. blv me, a woman knows, yaani ukiwa unamcheat anajua,sema hajui jina,sura wala mahali pa tukio.ila kujua moyoni tunajua,galz will back me up. uzuri tuna hekima,tunawaombea na kuwangojea mzinduke usingizini.
 
Kwanza hongera sana kwa kujitambua kuwa ulikuwa omepotea na sasa umepatikana
Hamna kitu kizuri kama kuwa mwaminifu kwa familia yako utakuwa na furaha amani na
siku zote mambo yako yataenda vizuri. Hivi mnajua ni kwanini hata makazini au kwenye
biashara wanaume/wanawake ambao wanacheat hawaendelei?sababu ya vilio vya
maumivu vya wenzao.Mwombe mungu akusaidie nawewe uwe na nia hiyo hiyo coz
ulichokuwa unapata kule ni kile kile kilichopo nyumbani hamna tofauti utofauti ni kuwa
ya nje unagharamia zaidi kuliko ya nyumbani
 
Hongera sana mpendwa kwa uamuzi ulioufikia muombe sana mungu akuepushe na hilo pepo ulilokuwa nalo na umshukuru sana kwa kukuonesha kuwa hukuwa sahihi wengine huwa wanakuja kuzinduka huku pamekwisha kucha
 
Nyama ile ile mabucha tofauti! Mti uleule mbao tofauti! Kitumbua kilekile wapishi tofati! Hakuna jipya chini ya jua yote ni ubatili mtupu ni sawa nakujilisha upepo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom