Tuangalie pdf kidogo

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Tuangalie kidogo PDF
Wengi wetu tumekuwa tunatumia Nyaraka zilizo kwenye mfumo wa pdf mara kwa mara ( Portable Document file ) watu wengi wamezoea kutumia program za adobe kama Adobe Reader ambayo kwa sasa kuna ver 9 na Adobe prof ambayo kwa sasa kuna version 9 pia , tofauti ya reader na prof ni kwamba kwenye prof unaweza kubadilisha pdf kwenda word au word kwenda pdf ukiwa kwenye computer yako , wakati reader kazi yake ni kusoma documents za pdf kwa sasa imeongezewa uwezo wa kutafuta maneno maalumu kwenye document Fulani pamoja na mambo mengine mengi tu .

Pamoja na hayo kuna wakati unaweza kupokea document ya PDF ambayo imefungwa , Adobe Prof haiwezi kukuruhusu kuondoa hizo lock ili uweze kuibadilisha kwenda word au excel kinachofanyika ni kutumia programu zingine za kampuni zingine ambazo zinaweza kufanya shuguli hiyo .
Siwezi kutaja hizo program hapa kwa sababu kuna msuguano wa kisheria kuhusu programu hizo haswa kwenye masuala ya hati miliki pale mtu anapoamua kulock document yake halafu wewe ukaondoe lock hiyo uitumie kwenye shuguli zingine nikitaja program moja ni kuhalalisha shuguli za kuunlock .

Hata hivyo kuna watu wengi sana ambao hawana uwezo wa kupata Adobe 9 prof kwa mfano au hata za chini yake kama 6 , 7 na 9 lakini wangependa kuconvert nyaraka zao kwenda pdf au toka pdf kwenda word lakini hii inahusiana zile nyaraka ambazo hazijawa locked .
Nafikiri huko tunapoenda kampuni kubwa za mambo ya program zinaweza sasa kufikiria kupunguza bei ya bidhaa zao kwa nchi ambazo wananchi wake kipato chao ni kidogo ili watu hao waweze kwenda sambamba na wananchi wa dunia nyingine pia hii itapunguza sana utumiaji na uuzaji wa program bandia sehemu mbalimbali
Mipango kama hii imejaribiwa kufanywa na kampuni ya Microsoft kwa kupunguza bei ya baadhi ya program zake ingawa haijatangazwa sana watu waelewe kwamba program Fulani bei zake zimepunguzwa kwa masoko ya ndani .
Kuna program nyingi za bure za kuweza kufanya shuguli hizo moja yao ni primo pdf tembelea www.primopdf.com program hii ni freeware unaweza kudownload na kuingiza kwenye computer yako utaweza kuitumia kwa ajili ya kutengeneza nyaraka za pdf , ukitafuta kwenye mtandao unaweza kupata nyingi zaidi ila hii unaweza kufanya nayo kazi hata kama hauko kwenye mtandao .
Kama hiyo inakushinda kidogo unaweza kutembelea www.pdfonline.com hii ni tovuti ambayo inakuwezesha wewe kuconvert nyaraka kwenda pdf na pdf kwenda word au excel , pamoja na huduma hizo kutolewa bure kwenye tovuti hiyo kuna kitu cha kuangalia hapo .
Ukitaka kwa mfano kubadilisha Word kwenda PDF unatakiwa kuattach nyaraka yako hapo kisha uweke anuani yako ya barua pepe itaconvert na kutumiwa document hiyo kwenye barua pepe yako kwa kitendo cha safari hiyo inawezekana anuani yako ikatumika kwa ajili ya shuguli zingine kwa kuwa umeiandika mwenyewe na watakuwa na uhakika kwamba anuani hiyo inafanya kazi .
Kwahiyo usishangae unapoletewa matangazo ya bidhaa za kampuni zingine ambazo nazo zinatoa huduma ya pdf na matangazo mengine mbalimbali ukashangaa email yako imepatikana wapi ni kwa njia kama hizi hapa hata hivyo unavyoingia na kuacha anuani yako ni kwa kuwa umesoma maelezo ya tovuti husika vya kutosha .
Suala hilo la kuweka anuani za barua pepe sio kwenye tovuti hiyo peke yake hata kwenye tovuti au forum mbalimbali ambazo zinatoa huduma ya kuchat na majadiliano kwa sasa kuna biashara kubwa sana ya kuuza na kununua kundi la anuani za barua pepe kati ya kampuni mbalimbali duniani ingawa hichi kitu kinafanywa ni siri kidogo .
Mimi binafsi nakushauri usitumie email ya ofisi au nyingine ambazo ni za muhimu kwako kuepuka usumbufu ambao unaweza kutokea .
Pia unatakiwa ujue kwamba wasajili wa tovuti nyingi huwa wanahifadhi taarifa za watu wanaotembelea tovuti hizo au kufanya kazi kwenye tovuti hizo kwa ajili ya kazi za mbeleni kwahiyo kama huna uhakika usijaribu .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom